Rais Samia: Ukanda wetu wa Bahari kuu ni mkubwa sana, tunafikiria kujenga Bandari nyingine ya uvuvi Bagamoyo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka Jiwe la Msingi Mradi wa Bandari ya Uvuvi - Kilwa Masoko leo tarehe 19 Septemba, 2023.


Rais Samia amewasisitiza wananchi waliopata boti za mkopo nafuu kwenye Bandari ya Uvuvi, Kilwa Masoko kurejesha mikopo hiyo kwa uaminifu, kuzitunza pamoja na kuzitumia vizuri bila uwepo wa migogoro.

"Tunafikiria kupokea meli nyingi sana za kimataifa katika nchi yetu Tanzania kwa kuwa ukanda wetu wa bahari kuu ni mkubwa sana, tunafikiria pia kujenga bandari nyingine ya uvuvi pale Bagamoyo" amesema Rais Samia.

Kilwa ina historia kongwe, ilifanya biadshara enzi hizo, na tunaambiwa karne ya 11 ilikuwa na safaru yake. Ndo maana Serikali tumeamua kumimina fedha ili wana Kilwa mrudi mlikotoka.

Kuhusu kuadimika kwa samaki kwenye maeneno ya karibu ya bahari, Rais Samia amewashauri waache kutumia baruti kwenye kuvua kwani baadae hata bahari kubwa itakosa samaki.
 
Back
Top Bottom