Rais Samia: Uchaguzi utakuwa huru na wa haki

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987

View: https://www.youtube.com/watch?v=st-YFWzMvWQ
f025966e-7796-45af-bd98-b39e4d3ff111.jpg



RAIS SAMIA: UCHAGUZI UTAKUWA HURU NA WA HAKI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema haki, demokrasia, sheria na utawala bora utadumishwa kwa watu wote wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Rais Samia amesema hayo leo katika sherehe za mwaka mpya 2024 (Diplomatic Sherry Party) kwa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa zilizofanyika Ikulu.

Aidha, Rais Samia amesema ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, Kikosi Kazi huru cha kupitia na kushauri mageuzi muhimu katika mfumo wa siasa kiliundwa ambapo kiliwasilisha ripoti yake mwaka 2023.

Rais Samia pia amesema mapendekezo mengi ya Kikosi Kazi yaliyopokelewa na serikali na wadau wote yalihusu kuongeza uwazi katika michakato ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.

Vile vile, Rais Samia amesema masuala machache hayakupokelewa moja kwa moja ambayo yalikuwa kinyume na katiba hivyo yanaweza kuchukuliwa wakati wa mchakato wa marekebisho ya katiba.

Rais Samia amesema serikali itaendeleza ushirikiano na balozi hizo kwa mujibu wa katiba, tunu za kitaifa, usawa, umoja na mshikamano wa kitaifa huku akiwataka mabalozi hao kutokuingilia uchaguzi na kuzingatia mila, kanuni na maadili ya kidiplomasia.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema Tanzania inasikitishwa na vita vinavyoendelea Palestina na kusababisha mauaji ya watoto na raia wasio na hatia na inaunga mkono usuluhishi kati ya Palestina na Israeli kwa kutoa wito wa kusitishwa mapigano na kupatiwa misaada ya kibinadamu.


a1abb3d7-ea68-4842-b35f-402731a58767.jpg

ee417eb8-d158-4079-abc6-18fa12361ff5.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party), Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Februari, 2024.

b87f87eb-b7a1-4cb6-9dfa-0354586f1751.jpg

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party), Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Februari, 2024.

e8248827-c859-4b43-9521-51d5c3f13259.jpg

77a6bd09-8285-4faa-848c-fe34dcda444c.jpg

4e8ba3c8-e872-41d5-ba6a-8b14c8a383c8.jpg

d2fc4a23-8030-4878-9a2a-989af58f54b3.jpg

Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania wakiwa pamoja na baadhi ya Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa kwenye Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party), Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Februari, 2024.

17d1ac21-1dc6-4f5e-aa3b-8887e956cb58.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party), Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Februari, 2024.
==============================

The President of the United Republic of Tanzania, Samia Suluhu Hassan, has affirmed that justice, democracy, the rule of law, and good governance will be upheld for all during the upcoming Local Government Elections scheduled for this year.

President Samia made these remarks during the New Year's celebrations for 2024 (Diplomatic Sherry Party) with ambassadors representing their respective countries in Tanzania and international organizations, held at the State House.

Furthermore, President Samia emphasized that to ensure a free and fair election, an independent Task Force was established to review and propose crucial reforms in the political system, which presented its report in 2023. She also mentioned that many recommendations from the Task Force, accepted by the government and stakeholders, focused on enhancing transparency in the election processes, including the appointment of the Chairman of the Election Commission.

President Samia noted that a few issues, which were contrary to the constitution, were not directly accepted and might be considered during the constitutional amendment process. Furthermore, the government will continue collaboration with the ambassadors in accordance with the constitution, national values, equality, unity, and national solidarity, urging them not to interfere in the election process and to adhere to diplomatic customs, principles, and ethics.
 
Tanzania inasikitishwa na vita vinavyoendelea Palestina na kusababisha mauaji ya watoto na raia wasio na hatia
 
Tanzania inasikitishwa na vita vinavyoendelea Palestina na kusababisha mauaji ya watoto na raia wasio na hatia
Hii ndo point niliyoiona nyingine zote sijui mambo ya uteuzi wa mwenyekiti wa tume Mimi hayanihusu kama ambavyo teuzi nyingine hazinihusu
 
19de031d-eabc-40b4-b6a7-8d7b229b7fc3.jpg


Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema haki, demokrasia, sheria na utawala bora utadumishwa kwa Watu wote wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Rais Samia amesema hayo leo katika sherehe za mwaka mpya 2024 (Diplomatic Sherry Party) kwa Mabalozi wanaoziwakilisha Nchi zao hapa chini pamoja na Wawakilishi wa mashirika ya kimataifa zilizofanyika Ikulu, pia amesema ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, Kikosi Kazi huru cha kupitia na kushauri mageuzi muhimu katika mfumo wa siasa kiliundwa ambapo kiliwasilisha ripoti yake mwaka 2023.

Rais Samia pia amesema mapendekezo mengi ya Kikosi Kazi yaliyopokelewa na serikali na wadau wote yalihusu kuongeza uwazi katika michakato ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na amesema masuala machache hayakupokelewa moja kwa moja ambayo yalikuwa kinyume na katiba hivyo yanaweza kuchukuliwa wakati wa mchakato wa marekebisho ya katiba.

Rais Samia amesema Serikali itaendeleza ushirikiano na balozi hizo kwa mujibu wa katiba, tunu za kitaifa, usawa, umoja na mshikamano wa kitaifa huku akiwataka mabalozi hao kutokuingilia uchaguzi na kuzingatia mila, kanuni na maadili ya kidiplomasia.
 
Ilikuwa Sherry kweli kweli.

Nakiri, nimeanza kumuelewa Rais Wangu Mh. Samia Suluhu Hassan.
 
Tanzania hakuna uchaguzi, Bali Kuna maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura.
Wewe hata ukiwa ni mgombea pekee jimbo lolote lile, huchaguliki.

Una makasiriko sana leo, vipi, ni kwasababu ya Wasafi?
 
Sitting arrangement haiko comfortable kabisa, wamebanana. Wangeweka roundtables!
 
Back
Top Bottom