Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,362
- 13,001
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Mabalozi Wateule Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.
RAIS SAMIA: MAFUNZO YA UBALOZI YASIWE YA JUMLAJUMLA
Rais Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Mabalozi Wateule Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, leo 16 Agosti, 2023 amesema mafunzo ya Mabalozi yawe yanaendana na maeneo wanayopangiwa kwa kuwa mahitaji hayapo sawa.
RAIS SAMIA: RAIS MWENZANGU ALINIAMBIA NIMBADILISHE BALOZI
Akiwaapisha Mabalozi Wateule Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma, Agosti 16, 2023, Rais Samia Suluhu Hassan amesema “Katika Nchi nyingine Mabalozi wetu sijui niseme hawajui wanachokifanya, wapo tu, nilikutana na Rais mwenzangu ndani ya #SADC akaniambia nimbadilishie Balozi kwa kuwa aliyepo kazini haendi na mikutano hashiriki.”
Amesisitiza baadhi ya Mabalozi hawatoi ripoti muhimu katika maeneo yao, ndio maana aliunde Kamati ya kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ili kubaini mambo kadhaa ikiwemo kasoro, mazuri na ugawaji wa Mabalozi.
RAIS SAMIA AWATAKA MABALOZI KUFUATILIA HATI ZA MAKUBALIANO ZILIZOSAINIWA
Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo wakati akiwaapisha Mabalozi Wateule Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Amesema “Mnapokwenda angalieni tumesaini nao kitu gani na vimefikia hatua zipi, mnapopeleka Hati za Utambulisho mkikaa na Rais au Mfalme wa Nchi husika zungumzeni mawili matatu ambayo yametekelezwa au yapo njiani.”
RAIS SAMIA: WIZARA ZOTE ZIFUNGIWE MTANDAO NA VIONGOZI TUWE NA ‘PASSWORD’
Akitoa mfano amesema Wizara ya Mambo ya Nje iwe na ubao wa mtandaoni unaoonesha Mikataba, Hati za Makubaliano na mengine yote yanayoendelea kisha Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Katibu Mkuu Kiongozi wawe na Neno Siri (password) ili waweze kusoma na kujua kinachoendelea.