Balozi wa Tanzania aliyevurunda nchi ya SADC ni nani? Rais Samia apangua mabalozi akiwepo mmoja kutoka SADC

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,819
18,558
Katika hali isiyokuwa ya kawaida rais Samia ameeleza kupokea ombi kutoka kwa mmoja wa marais wa nchi za SADC akimwomba rais Samia ambadilishe balozi wa Tanzania aliyeko nchini “kwake” kutokana na utendaji wake mbovu.

“Nilishakutana na Rais mwenzangu ndani ya nchi za kiafrika, ndani ya Sadc, akaniambia nimbadilishie balozi, akisema uliyeniletea hata kazini haendi, mikutano hashiriki, yupo yupo tu, hatuelewi, Tanzania hatujawazoea hivyo, sasa labda umbadilishe, nikamwambia nimekusikia,” amesema Rais Samia .

Rais aliyasena hayo jana tatehe 16 August alipokuwa akiwaapisha mabalozi wapya ikulu.

Taarifa zilizopatikana leo tarehe 17 August zinaeleza rais Samia amefanya mabadiliko katika balozi tatu moja kati ya hizo ni ubalozi uliopo nchi ya SADC.

Je ni balozi yupi huyo aliyeombwa kumtangua? Soma habari hiyo hapa chini.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amewapangia vituo vya kazi mabalozi watatu na kumbadilishia kituo cha kazi Balozi Mbelwa Kairuki aliyekuwa China ambaye sasa anakwenda Uingereza akichukua nafasi ya Dk Asha-rose Migiro aliyemaliza mkataba wake.

Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu usiku wa kuamkia leo Alhamisi Agosti 17, 2023 ikiwa ni saa chache tangu Rais Samia awaapishe mabalozi wapya huku akizungumzia suala la utendaji usioridhisha wa baadhi ya wanadiplomasia hao.

Katika mabadiliko hayo, waliopangiwa vituo vya kazi ni pamoja na Balozi Khamis Mussa Omar anayekwenda China akichukua nafasi ya Kairuki ambaye amehamishiwa London, Uingereza.

Rais Samia amempangia kituo cha kazi Balozi Ceaser Waitara kwenda Namibia akichukua nafasi ya Dk Modestus Kipilimba ambaye amestaafu.

Mwingine ni Balozi Bernard Kibesse aliyepangiwa kuiwakilisha Tanzania nchini Kenya, akichukua nafasi ya Balozi John Simbachawene ambaye amehamishiwa Kampala, Uganda.
 
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ni Jumuiya ya Kiuchumi yenye nchi wanachama 16;
Angola,
Botswana,
Comoro,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
Eswatini,
Lesotho,
Madagascar,
Malawi,
Mauritius,
Msumbiji,
Namibia,
Shelisheli,
Afrika Kusini,

needless to say
Jamhuri ya Muungano Tanzania,

Zambia

.... na Zimbabwe

Tuwekeeni hao mabalozi waliopo huko sasa, SSH keshaanika....Mmoja wao hakidhi matakwa au ana mapungufu....'aah' in SSH voice
 
Sasa kama anateua kwa kufata ukada, u ccm uchawa, anategemea atapata watu wa maana? Ubalozi, imekuwa ni sehemu ya kutoa zawadi kwa walioshindwa ubunge, makada, machawa, sycophants,
Zamani hii kazi walikuwa wanapewa mashushu, academic Ian's, waliobobea kwenye nafasi, zao,
Sasa hv watu wanaperekwa ili wakazeekee huko, mtu kama IjP Siro, unampa ubalozi, ili akafanye nini cha maana, Jeshi, LA polisi lilimshinda, unapeleka vijana wasiojua chochote zaidi ya, uchawa na uccm tu,
Salim Ahmed Salim, aliteuliwa kuwa balozi, nchini Misri akiwa kijana wa form six tu, sasa, hawa,wa sasa, richa ya, kuwa, na shahada lakini vichwani ni bure kabisa.
 
Back
Top Bottom