Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Baada ya kumteua kisha kuthibitishwa na Bunge mwishoni mwa wiki, leo asubuhi Rais John Magufuli atamwapisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Majaliwa ataapishwa ili kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa kipindi cha pili ikiwa ni siku tatu baada ya Bunge kumthibitisha.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo, Rodney Thadeus amesema Majaliwa ataapishwa leo asubuhi Ikulu ya Chamwino.


=========


4:13 Asubuhi: Kassim Majaliwa ameapa na kuweka sahihi kwenye hati za kiapo kwa waziri mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma. Baada ya hapo waziri mkuu amekula kiapo cha uaminifu kilichoongozwa na Jaji mkuu.

Philip Mpango: Hotuba yako ya kufungua bunge la 12 ilikuwa hotuba ya karne, ni muongozo thabiti wa sisi wateule wako jinsi ambavyo tutende kazi kutekeleza matarajio ya wananchi wa Tanzania. Nikuahidi nitasimamia nidhamu ya watumishi ya wizara uliyonikabidhi na tasasisi zilizo chini yake, uzembe, wizi na ubadhilifu wa fedha za Umma, hilo nitalitilia kipaumbele cha juu, kwenye miradi ya maendeleo bado kuna tatizo kubwa, bado tunaibiwa.

Hawa wazembe maadam umenipa kisu, watupishe mapema kwa sababu huo mzigo mkubwa sana kwa hiyo watupishe tutende kazi nchi yetu isonge mbele.

Prof. Palamaganda Kabudi: Kazi ya wizara yetu sasa, itaendelea kuimarisha mahusiano mazuri na nchi zote kubwa na ndogo ili taswira ya Tanzania na sauti ya Tanzania iendelee kusikika, tumefanya hivyo ulivyokuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika mashariki, SADC na tutafanya hivyo miezi sita ambapo Tanzania tumechaguliwa kuwa mwenyekiti wa nchi za Afrika, Pacific na Caribbean.

JAJI MKUU(Ibrahim Juma): Kwanza nawapongeza kwa kupata madaraka na mamlaka kutoka kwa wananchi, pili kupata Imani ya mheshimiwa Rais kuwapa wadhifa na madaraka ya kuwa mawaziri.

Madaraka makubwa na mamlaka mliyopewa yana lengo moja tu, ustawi wa wananchi, si yenu binafsi lakini mtayatumia namna gani kuleta ustawi.

Ukiangalia utangulizi wa katiba ya Marekani, katiba yao imedumu kwa miaka 231 hadi leo. Wao utangulizi unasema bado wanatafuta 'The perfect union' Bado wanatafuta nchi iliyokamilika.

Sisi umri wa umri wa Jamhuri yetu, tulipata uhuru miaka 59 iliyopita, tumeungana miaka 56 iliyopita vilevile bado tunatafuta perfect union. Sasa viongozi kazi zetu ni kujaribu kufikia hiyo perfect union an mwalimu Nyerere mwaka 1962 alitukumbusha hakuna katiba ambayo imekamilika wakati wote, katiba inakamilika wakati viongozi wanaitafuta katika hali ya ukamilifu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema katika nafasi yake ya uwaziri kwa awamu hii ya pili ataanza kushughulika na bei ya saruji iliyopanda kiasi cha kulalamikiwa.

Katika hotuba yake baada ya kuapishwa amesema amewapa wakuu wa mikoa muda hadi Novemba 20 saa nne asubuhi wawe wamekwenda kwenye viwanda na kwa mawakala wa saruji kujua kwa nini bei ya saruji imepanda.

Amesema upandaji wa bei ya saruji hauna sababu ya msingi kuwa serikali haijaongeza kodi na miundombinu ipo na waliohitaji gesi waliwapelekea, pia makaa ya mawe yapo mengi.

Hivyo atahitaji maelezo ya kupanda kwa bei ya saruji kutoka kwa wakuu wa mikoa ambao nao walikuwepo katika sherehe za kuapishwa kwa Waziri Mkuu

Samia Suluhu: Sisi ulioturudisha kwa Imani kubwa, haikuwa rahisi kivile. Tulipoanza nawe ilikuwa ngumu, hukua unatuona, tulikuwa tunalia kila siku. ukimkuta Mpango anasema na uprofessa wote huu naambiwa hivi na hivi, ukija kwangu nasema hee mwaka huu lakini na kina Kassim wote hawa. Lakini uliendelea kutunyoosha mheshimiwa, mheshimiwa tumenyooka. Miaka miwili ya kwanza tulinyooka, wa kwanza tulinyooka, wa pili ilikuwa tunateleza, miaka mitatu iliyobaki tukachapa kazi kwelikweli mpaka ukapata Imani na sisi.

Nasubiri baraza la mawaziri tutakaloliteua, sisi tutakusaidia kazi sasa. Wewe fikiria mengine makubwa lakini sisi tuliotangulizwa tayari wana uwezo wa kunyoosha wengine kama alivyosema Mpango, kama alivyosema Kabudi.

RAIS MAGUFULI: Sikutaka kuteua haraka haraka na mimi ningeomba waheshimiwa wabunge presha mzishushe kwa sababu kazi tuliyoomba ni ubunge wala sio uwaziri.

Nafasi za mawaziri na manaibu waziri haziwezi zikafika 30, sasa katika watu 350, hata ungekuwa wewe unateua ungepata shida kubwa, sasa inabidi kucheki jina kwa jina, factors nyingi na nyingine unazitafuta ili umtoe kwa sababu haiwezekani ukawa na wabunge katika mkoa mmoja wakawa hata watano, hiyo nayo ni factor, lazima pawepo na division.

Hawa wawili sio kwamba ni maarufu sana kuliko waliobaki, miaka ya nyuma niliwateua hawakuwa na majimbo na niliwaambia waende kwenye majimbo au waende walikotoka. Lakini nikaona kwa kuwa nitachelewa kidogo kuwa na baraza la mawaziri na ninyi wabunge lazima mlipwe mishahara, lazima mlipwe posho zenu na lazima tutafute fedha za kuwalipa wafanyakazi mishahara, lazima tuwe na waziri wa fedha kwa sababu fedha tutazihitaji, haziwezi kusubiri miezi yote mitatu, minne.

Mpango ametutoa katika dimbwi la nchi masikini na kuwa nchi ya uchumi wa kati, nikasema basi ngoja nimrudishe, ndio maana nimemrudisha.

Kwenye wizara ya mambo ya nje nako hatuwezi tukakosa mtu wa kutusemea, tukaendelea kutukanwa, watu wanatengeneza majambo yao hayapati majibu kwa sababu nchi yetu nayo haiwezi ikaishi kwenye 'isolation'. Ndio maana nikasema huyu kwa kuwa alimudu kazi yake, ngoja aendelee kuwa waziri wa mambo ya nje, wapo wengi waliomudu nafasi zao lakini nikaona nijiridhishe kwanza.

Wasaidizi wangu walishaniletea ushauri, unajua wizara ya Ulinzi na mambo ya ndani ungefanya hivyo hivyo wala sikuwajibu kwa sababu sio lazima uwe na waziri wa Ulinzi. CDF akiwa na tatizo anataka kupigana wala haendi kwa waziri wa Ulinzi, anakwenda kwa Rais ambae ndie kamanda mkuu.

Ukiangalia hizi nafasi za waziri mkuu, maana yake ni nafasi ambazo hazina guarantee, nilikuwa naangalia kwenye vyombo vya habari na wengine wakishangilia, wakisema mheshimiwa Kassim sasa amepata miaka mingine mitano kana kwamba nimeshawaambia atakaa miaka mitano na wakazi wa Lindi nikasikia wengine wanafurahia na wengine wanajipongeza mahali fulani kwamba tumepata waziri mkuu kusini Kassim tena miaka mitano mingine.

Nataka niwaambie waheshimiwa wabunge na nataka nimwambie mheshimiwa Kassim na watanzania, kazi ya uwaziri mkuu haina guarantee na nilitaka nilizungumze hili mheshimiwa waziri mkuu aelewe, itategemea na perfomance yake kwa hio tumuombee kwamba angalau afikie kwenye rekodi ya mheshimiwa Sumaye.

Anayoyasema mheshimiwa makamu wa Rais ni kweli, mkichekeana hamuwezi mkafika, sijui ufike unasema makamu wa Rais umependeza, umevaa nguo gani, ushungi wako unapendeza wakati miradi ya maji inalala, wakati barabara hazitengenezwi, ni kumvurumisha tu, nenda huko ndio ulieomba hiyo kazi.

Sasa lugha za namna hiyo hawajazizoea watu lakini mzoee zoee kidogo. Namshukuru makamu wa Rais amezoea, waziri mkuu amezoea na wale niliowachagua karibu wote walizoea na mimi nafikiri nilikuwa natimiza wajibu wangu kwa watanzania hasa wanyonge.

Kwa hiyo namshukuru makamu wa Rais amelisema hili, ni kweli, mimi diplomacy sijui. Mimi najua mbili jumlisha na mbili ni nne au mbili na mbili ni tano ukitoa moja, basi. Na tumeenda hivyo na matokeo yake nafikiri ndio haya na ndio maana kwenye kampeni niliwapanga hawahwa watatu pamoja na wajumbe wa 'cental comitee' kwa sababu ndio waliotekeleza ilani ya uchaguzi.
 
The first ceremonial PM in Tanzania. Anafokewa kama mtoto. Utasikia "na wewe hebu maliza hiyo hotuba yako, vinginevyo nitakukatisha"

Au "nilikuwa nakisubiri na wewe uungane nao, ningewafuta wabunge wote wa Kusini"

Au "ningewapiga mashangazi zako".

Hivi PM unatukanwa on camera halafu upo tu?
 
Baada ya kumteua kisha kuthibitishwa na Bunge mwishoni mwa wiki, leo asubuhi Rais John Magufuli atamwapisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Majaliwa ataapishwa ili kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa kipindi cha pili ikiwa ni siku tatu baada ya Bunge kumthibitisha.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo, Rodney Thadeus amesema Majaliwa ataapishwa leo asubuhi Ikulu ya Chamwino.
Nafasi ya Waziri Mkuu kikatiba ana takiwa awe mbunge wa jimbo. Ila Majaliwa ni mbunge wa viti maalum. Hapo imekaaje?
 
Bado najiuliza kwanini PM alipita bila kupigwa ubunge!? Kwanini wapinzani wake walitekwa!? Kama ni kosa kugombea na mwenye maamlaka kwanini mbinu za uungwana zisitumike kama kubadili katiba kuondoa dhuluma ya kikatiba?
 
Back
Top Bottom