ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,051
- 49,734
Bwana Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Samia ni mfano wa kupigwa na kinara wa utekelezwaji wa Ilani.
My Take
Samia amemwaga mabilioni Nchi nzima Kila sekta haijawahi tokea Kwa Rais yeyote kabla yake tena Kwa mda mfupi sana.
====
Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kassim Majaliwa, amesema Rais Samia Suluhu Hassan ni kinara katika utekelezaji ilani ya chama hicho.
Aliyasema hayo juzi wakati wa mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Kavuu uliofanyika katika Shule ya Sekondari Mizengo Pinda, Halmashauri ya Mpimbwe, Wilaya ya Mlele, mkoani Katavi.
"Ni ukweli usiopingika kuwa Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais na Mwenyekiti wa chama chetu amekuwa kielelezo cha mafanikio makubwa yanayofikiwa na nchi yetu kwa sasa," alisema.
Majaliwa alisema kuwa tangu Rais Samia ashike madaraka hayo, ameendelea kutekeleza miradi yote ya kimkakati kama ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 ilivyoelekeza.
"Dk. Samia ameendelea kusimamia utekelezaji ilani ya CCM ikiwamo upatikanaji huduma za afya kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa, kanda na rufani," alisema.
Waziri Mkuu alisema pamoja na mafanikio mengine, Rais Samia ameimarisha diplomasia ya kiuchumi na nchi mbalimbali sambamba na kukuza utalii, lugha ya Kiswahili na masoko ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi.
"Taifa hili, chini ya serikali za CCM tuna uwezo mkubwa wa kujitegemea na kujiletea maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii.
Nipashe