The Icebreaker
JF-Expert Member
- Feb 11, 2018
- 18,159
- 51,091
Hivi amesha apishwa tayari?
Pongezi kwa CCM kwa ukomavu wa kisiasa, hongera ACT kwa kukubali kwamba maendeleo hayana chama.
Tuliwaasa sana ndugu zetu kwamba hakuna upinzani Tanzania ila kuna wachumia tumbo na vibaraka wakatukatalia, ila nadhani sasa wataelewa.
Mungu ibariki Tanzania
Zanzibar hamuhitaji siasa za kuuwana wala kuandamana, lakini wakati wa uchaguzi lazima muuwawe ili ccm wakae madarakani! Sasa sijui ni kuuana kupi unakuoongelea.
Ninachokiona mimi ni kujaribu kurudi kwenye siasa za maridhiano na utulivu ambazo zilikuwa na matunda mengi tuu. Wanyonge waliweza kuendelea na shughuli zao za kawaida na pia iliweka mazingira ya uchaguzi wa utulivu kwa uchaguzi ujao/2015.
Kukaa nje kutaendeleza purukushani na waznz wataishi kwa miaka 5 ijayo kwa mkiki bila ya sababu yoyote. Nadhani hii ni faida moja kubwa kuliko hizo nyengine.
Ni Baadhi tu ya watu na sio Chadema kama unavyosema, Juzi juzi Tu umetoka kulialia eti kina Mdee wamepigwa pesa usoni halafu unasema Chadema, taja mtu na sio chamaHapo ndo nasema chama cha upinzani tanzania ni chadema tuuuu
Nope haina maana hio sheikh. Fikiria hivi ni sawa na kuwa jela halafu ukagoma kula wakati ukijua mlinzi wa magereza hajui hata maana ya haki za binadamu. Pengine anakuombea dua ufe apate aendelee na shughuli zake nyengine! Sasa ni kheri ule tuu huo ugali kama hauna sumu basi sawa na unavuta muda ukitarajia msaada na kudra za M.Mungu.Kwahiyo kwa maneno marahisi ili wazanzibari washiishi kwa amani ni lazima ccm iwatale kwa shuruti?
Nope haina maana hio sheikh. Fikiria hivi ni sawa na kuwa jela halafu ukagoma kula wakati ukijua mlinzi wa magereza hajui hata maana ya haki za binadamu. Pengine anakuombea dua ufe apate aendelee na shughuli zake nyengine! Sasa ni kheri ule tuu huo ugali kama hauna sumu basi sawa na unavuta muda ukitarajia msaada na kudra za M.Mungu.
Hebu nitajie faida moja ya kugoma na kususa itakayopatikana ?
1995, 2015 ni mifano ya kugoma. Ilipatikana iyo haki ? Nadhani mazingira ya 2020 yalikuwa mabaya zaidi, bora tungeshiriki na kujaribu kujenga umoja toka 2015 hadi 2020 basi tungelikuwa wamoja na pengine kusingekuwa na hata nzi alieumizwa.Kugoma na kususa ni kulazimisha haki kutendeka. Sasa unategemea upate haki kwa kushirikiana na anayepora haki yako, hapo utatoboa?
Sasa kama mlikuwa hamataki kuteseka, kwanini kuwasumbua CCM wakati wanawapa raha?Pia hatuna haja ya kuteseka bila ya sababu za msingi wakati tukiwa safarini.