Rais Dkt. Mwinyi ahimiza nidhamu, uadilifu na mshikamano

Rais Dkt. Mwinyi ahimiza nidhamu, uadilifu na mshikamano

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amehimiza suala la nidhamu, maadili, uwajibikaji, uadilifu, mshikamano, umoja na upendo baina ya viongozi na watendaji wa Serikali katika kutenda haki kwa wananchi.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo katika Kongamano la Kiimani kwa Viongozi na Watendaji Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na kuratibiwa na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar ukumbi wa Idrissa Abdul-Wakil Kikwajuni, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 6 Aprili, 2024.

Aidha Rais Dkt. Mwinyi amesema suala la nidhamu sio kwa Majeshi peke yake ni suala la utumishi wa umma mzima.

Kwa upande mwingine Rais Dkt. Mwinyi amesema ili kuwepo uwajibikaji, maadili na nidhamu jambo kubwa ni kuwa na hofu ya Mungu na kuchunga ahadi zinazotolewa ili kutekeleza wajibu kwa uadilifu.

Rais Dk. Mwinyi amesema kongamano lijalo waalikwe Wenza wa viongozi na watendaji wa Serikali ili wapate kujifunza mada zinazotolewa na Masheikh na Wahadhiri.

Vilevile Rais Dk. Mwinyi amesema kodi ndiyo inayoendesha Serikali kwa kutekeleza huduma mbalimbali za kijamii, Suala la kulipa kodi ni halali.

IMG-20240406-WA0038.jpg
IMG-20240406-WA0029.jpg
IMG-20240406-WA0035.jpg
IMG-20240406-WA0037.jpg
IMG-20240406-WA0041.jpg
IMG-20240406-WA0039.jpg
IMG-20240406-WA0036.jpg
IMG-20240406-WA0033.jpg
IMG-20240406-WA0030.jpg
IMG-20240406-WA0031.jpg
IMG-20240406-WA0032.jpg
IMG-20240406-WA0034.jpg
 
Ya nchi za watu hayo,binafsi hayanihusumi natafuta ya Tanganyika
 
Back
Top Bottom