Rais Dkt. Mwinyi amteua Maalim Seif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,805
11,964
20201206_224741.jpg

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Maalim Seif Shariff Hamad, kuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar kuanzia leo Disemba 06, 2020.

=====

Taarifa kwa vyombo vya Habari

Kwa kuzingatia matakwa ya Kifungu cha 9(3) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984,kinachosema kwamba “Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utakuwa na Umoja wa Kitaifa na utendaji wa kazi zake utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa kwa umoja nchini na lengo la kufikia demokrasia”.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 6 Disemba, 2020

IMG_20201206_225612_855.jpg
 
Pongezi kwa CCM kwa ukomavu wa kisiasa, hongera ACT kwa kukubali kwamba maendeleo hayana chama.

Tuliwaasa sana ndugu zetu kwamba hakuna upinzani Tanzania ila kuna wachumia tumbo na vibaraka wakatukatalia, ila nadhani sasa wataelewa.

images (10).jpeg
Mungu ibariki Tanzania
 
Yaani mwezi ndio kwanza umeisha. Kwa ndugu zangu Waislam wanasema hata 40 bado haijaisha! Nikiwa mkubwa sitaki kuwa mwanasiasa. Kilimo kinatosha, na ufugaji wa samaki.

Kwa hiyo na wale alio wahamasisha KUANDAMANA na wakaishia KUPATA ULEMAVU/KUPOTEZA NDUGU na wengine wakafikia hatua ya KUFILISIKA.

Mzee anawaachaje kuwapunguzia machungu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom