Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Tumemsikia wenyewe hivi Leo, wakati akimwapisha waziri mpya wa sheria na Katiba, Mwigulu Nchemba, katika mengineyo aliyoongolea Rais, ni kuhusu hatua iliyochukuliwa na wabunge wa Chadema, ambao wameamua kujifanyia "self isolation" kwa ajili ya kile walichokiita wenyewe kuwa ni hofu ya usalama wao na wa wenzao wa CCM, kutokana na ugonjwa wa corona, unaotingisha dunia hivi sasa na kuwa siyo busara kuendelea na vikao hivyo, wakati wabunge wote wakiwa hawajapimwa afya zao kubaini wale walioambukizwa ugonjwa huo na hivyo wafanyiwe katantini.
Jambo lililonistua ni pale nilipomsikia Mheshimiwa Rais akieleza kuwa amemwagiza Spika wa Bunge, ili asiwalipe.posho hizo wabunge wote wa Chadema, kwa siku zote ambazo hawatukuwepo Bungeni!
Ndipo hapo nikaanza kujiuliza, hivi mhimili wa Bunge si unaendeshwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo uko huru kufanya maamuzi yake?
Kwa utawala bora unaojali "power separation" hilo jambo haliwezi kujitokeza hata kidogo
Ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania, kuna mihimili 3, ambayo ni serikali, inayoongozwa na yeye Rais, mhimili wa Bunge, ambao unaongozwa na Spika na mhimili wa mahakama, ambao unaongozwa na Jaji Mkuu.
Ndani ya Katiba hiyo hiyo, inaitaka mihimili hiyo mitatu, ifanye kazi kwa Uhuru, katika kile kinachoitwa "check and balance" ambapo haitakiwi mhimili mmoja uingilie shughuli za mhimili mwingine.
Tunachojiuliza wananchi, hivi kama tumemsikia wenyewe wakati akilihutubia Taifa, akiuingilia mhimili wa Bunge, tutajuaje kama hauingilii pia katika utendaji wake, mhimili wa mahakama?
Ndipo hapo ninapojiuliza, hivi Rais Magufuli amepata wapi mamlaka, hadi kumpa kiburi cha kuongea hadharani kuwa atauagiza mhimili wa Bunge, upige STOP malipo yoyote ya posho, ambayo wabunge wa Chadema walistahili kupewa_ wakati akijua fika kuwa mamlaka hayo anayo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania?
Ninawakaribisha wachangiaji wa aina yoyote ile, ili tuidadavue mada hii muhimu mno kwa mustakabali wa Taifa letu