SankaraBoukaka
JF-Expert Member
- Jul 2, 2019
- 910
- 1,394
Du!.. Baada ya kuupiga mwingi naona kajipiga OWN GOAL...
Msomi wa kiwango cha kimataifa wa Tanzania, Profesa Shivji ameshangazwa na kitendo cha wafanya biashara kuchaguliwa kuongoza taasisi za umma.
Shivji anasema sekta ya umma haiwezi kuchangamana na sekta binafsi.
Sisi wengine tumeshangazwa na uteuzi wa wafanya biashara na watu wenye maslahi binafsi kwenye bodi ya TANESCO. Yule mama Balozi ndie mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Rex Attorneys ambao wanaiwakilisha Dowans na Symbion kwenye kesi ambazo TANESCO inashitakiwa na hayo makampuni halafu anateuliwa kuwa board member.
"Pamoja na kushirikiana na sekta binafsi, huwezi kuwaingiza wafanyabiashara jikoni wakupikie chakula cha umma!
Sekta ya umma na sekta binafsi hazilinganiki. Ni kweli huwezi kuendesha biashara kama idara ya serikali; pia ni kweli huwezi kuendesha serikali kama kitengo cha biashara."
Unaweza kusoma mwenyewe hapa.
View attachment 1954110
Angalao huko anaguswa hata kwa kuhojiwa, hapa kwetu utaweza! Thubutuu!Sawa nimekuelewa lakini si kwa kuirejea afrika kusini. Niirejee nchi ambayo fisadi Zuma anafungwa miezi 15?!!! Utofauti uko wapi na kutofungwa?
Akili umekosa ndio nachoweza kusemaNaomba nielimishwe kidogo, hilo lipo katika katiba au ni mawazo binafsi ya Shivji? Yule Trump aliyekuwa Rais wa Marekani ana biashara dunia nzima, Vipi nchi iliathirika na ubiashara wake au ya kule nisiyahusishe na huku kwetu wenye nyeusi ngozi?
Mbowe ni mfanyabiashara na aliwahi kugombea uraisi, vipi km angepata Prof Shivji angekuja na maoni haya pia?!!
Siku utasikia azam hawalipi bill za umeme ndio hapo tutapojua kuwa sisi ni washamba wa waarabuTatizo nilionalo mimi ni huko kuingiza watu ambao ama tayari wanasemwa semwa kwa kutilia shaka uadilifu wao au wale ambao kutokana na mgongano wa kimaslahi wanaweza kuleta ushawishi kwa bodi na menejimenti ili kupata upendeleo kwenye taasisi zao binafsi.
Wanazoziongoza lakini suala la shirika kujiendesha kibiashara mbona hata wakati wa Magufuli tuliambiwa shirika sasa linajiendesha kibiashara na kudaiwa kwamba sasa shirika halipokei tena ruzuku toka serikalini au ilikuwa changa la macho ili kumpamba mzee wa misifa?
Na katiba mpya unayoongelea wewe ni ipi?You could be right. Tatizo kubwa la utendaji wa mashirika ya umma Tanzania halitokani sana na incompetence ya watendaji wala BOD. Bali ni viongozi wa kisiasa wenye hulka ya ufisadi. Power sekta imeteseka sana na hili. Ni juzi tu tumetoka “kufunika” suala la Tegeta Escrow (ambalo suspected top villains ndio hao hao). Ndio maana wamehakikisha hakuna kesi mahakamani. Zipo scandals nyingine zilivyofunikwa hivyo hivyo.
Hata uweke private sekta yote kwenye mgt na BOD ya TANESCO kama viongozi wa juu kisiasa wamelenga kufanya yao kama walivyofanya kupitia IPTL sahau habari ya ufanisi. Hapa, baadhi ya wateule kwenye hiyo BOD wanatia shaka mapema kwamba wana conflict of interest.
Labda pengine tusihangaike sana na hilo. Tupiganie kwanza katiba itakayodhibiti mikono ya wanasiasa kuingilia moja kwa moja shughuli za utendaji za mashirika ya umma na kutengeneza mazingira ya “state capture” ili kufanikisha ufisadi mkubwa.
Mbona ilishawahi kutokea hapohapo Tanesco? Kuna Bosi mmoja make wake ndiye aliyekuwa anapewa Tender mbalimbali hapo kwenye Shirika. Na ilifanyiwa kazi. Hii inaitwa "Conflict of interest". Ni kosa kubwa. Ni sawa na Uhujumu uchumi.Naomba nielimishwe kidogo, hilo lipo katika katiba au ni mawazo binafsi ya Shivji? Yule Trump aliyekuwa Rais wa Marekani ana biashara dunia nzima, Vipi nchi iliathirika na ubiashara wake au ya kule nisiyahusishe na huku kwetu wenye nyeusi ngozi?
Mbowe ni mfanyabiashara na aliwahi kugombea uraisi, vipi km angepata Prof Shivji angekuja na maoni haya pia?!!
I mean "Mke wake"Mbona ilishawahi kutokea hapohapo Tanesco? Kuna Bosi mmoja make wake ndiye aliyekuwa anapewa Tender mbalimbali hapo kwenye Shirika. Na ilifanyiwa kazi. Hii inaitwa "Conflict of interest". Ni kosa kubwa. Ni sawa na Uhujumu uchumi.
Hahaha nani nao mkuu?Dawa ni kuwapiga risasi mbwa hawa.
Ewe mfuasi wa jiwe hebu tulia dawa ikuingieHuyu bibi huwa hata hausiki kwenye teuzi, yeye kazi yake ni kusaini tu, nadhani ingekuwa vyema angejiuzulu kabisa maana hakuna kitu cha maana anafanya
Imesambaratushwa vibaya mnoHivi Sukuma gengi bado ipo ?
Umemjibu vyema huyo oya oyaWewe pia hapa na ujinga wako! Balozi ana law firm ambayo inatetea kampuni zinazoishitaki Tanesco, huyo mama huoni kuwa katika Bodi ya tanesco si sahihi? Je, vetting imefanyika Sawa? Au kwa vile walimwajiri Ridiwani Kikwete wakati huo
Msomi wa kiwango cha kimataifa wa Tanzania, Profesa Shivji ameshangazwa na kitendo cha wafanya biashara kuchaguliwa kuongoza taasisi za umma.
Shivji anasema sekta ya umma haiwezi kuchangamana na sekta binafsi.
Sisi wengine tumeshangazwa na uteuzi wa wafanya biashara na watu wenye maslahi binafsi kwenye bodi ya TANESCO. Yule mama Balozi ndie mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Rex Attorneys ambao wanaiwakilisha Dowans na Symbion kwenye kesi ambazo TANESCO inashitakiwa na hayo makampuni halafu anateuliwa kuwa board member.
"Pamoja na kushirikiana na sekta binafsi, huwezi kuwaingiza wafanyabiashara jikoni wakupikie chakula cha umma!
Sekta ya umma na sekta binafsi hazilinganiki. Ni kweli huwezi kuendesha biashara kama idara ya serikali; pia ni kweli huwezi kuendesha serikali kama kitengo cha biashara."
Unaweza kusoma mwenyewe hapa.
View attachment 1954110
Mkuu kwani hujui Trump ana kesi ya kukwepa kulipa kodi,alitumia cheo cha uraisi kukwepa kulipa kodi kibao na aliposhtukiwa akayaka ang'ang'anie madarakani ili apate kinga ya kutopelekwa mahakamani. Unapoteua mtu kama mtoto wa Bakhresa kwenye bodi ya Tanesco maana yake makampuni yake yaanzae kupata upendeleo maalumu,pia unapomteua aliyekuwa wakili wa kampuni za kitapeli zilizoinyonya Tanesco maana yake nini huyu February ni mpigaji wa juu kwa juu, sasa tunaona team ya wapigaji wakirudi kwa nguvu,Shivji yupo sahihi.Naomba nielimishwe kidogo, hilo lipo katika katiba au ni mawazo binafsi ya Shivji? Yule Trump aliyekuwa Rais wa Marekani ana biashara dunia nzima, Vipi nchi iliathirika na ubiashara wake au ya kule nisiyahusishe na huku kwetu wenye nyeusi ngozi?
Mbowe ni mfanyabiashara na aliwahi kugombea uraisi, vipi km angepata Prof Shivji angekuja na maoni haya pia?!!
Kubwa na la msingi, Ilani ya chama.... nchi inaongozwa na sera za CCM tuzingatie hilo.
Mwigulu kwenye nishati?Teuzi zinafanywa na akina Mwigulu Nchemba