Mobhare Matinyi - Mpiganaji mpya wa Rais Samia kwenye ulingo wa habari na mawasiliano

kevylameck

Member
Nov 3, 2013
18
19
0C68C40C-74AF-4AC1-AB70-301688436F63.jpeg

Na Kevin Lameck

Kama ipo sehemu ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amepatia katika teuzi zake za karibuni, bhasi miongoni mwake ni uteuzi wa sasa wa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Gerson Msigwa.

Bwana Mobhare Matinyi, Mkuu wa wilaya ya Temeke ameteuliwa kuwa Msemaji mkuu wa serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari - Maelezo.

Kabla ya kuwa Mkuu wa Wilaya mwezi wa saba mwaka huu, Mwanahabari huyu kitaaluma, alikuwa akitumika kwenye jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika maarufu kama SADC.

Muda mfupi kabla ya uteuzi huu, wiki iliyopita, nikiri kuwa nilibahatika kuzungumza naye kupitia kipindi chetu cha runinga kiitwacho #TheBantu sambamba na mazungumzo mafupi baada ya kipindi.

Bahati iliyoje kuwa tuligusia pia kuhusu sehemu muhimu ya mawasiliano na mahusiano ya umma kwa serikali ya Rais Samia na namna ilivyo muhimu katika kujenga picha na sifa nzuri ya serikali.

Nitasema machache kumuhusu ili kuchagiza maoni yangu ya awali kuhusu ubora na uzuri wa uteuzi huu wa Bwana Matinyi.

Mosi, Mh. Matinyi ana exposure ya juu sana ambayo ni nadra kuikuta kwa viongozi wengi wa sasa. Nafasi alizopita awali kuanzia kwenye uandishi wa habari, Uhariri mkuu wa magazeti kadhaa na kwenye jumuiya za kimataifa kumemfanya kuwa na utashi,m na mwenye kujaa maarifa na taarifa nyingi zilizomjengea upekee wa aina yake.

Pili; Mh. Matinyi ana uelewa mpana kuhusu siasa za ndani ya nchi, za jumuiya za kimataifa pamoja na hadhira yake kwa ujumla. Suala hili litampa wakati mzuri kuwa msaada kwa Rais na Chama chake katika kushauri na kuupasha umma taarifa zenye kujitosheleza katika urari wa habari na mawasiliano ya umma.

Tatu; Mh Matinyi ni mzungumzaji mzuri sana. Anajua kupangilia na kuumba maneno vyema akiongozwa na hekima ya kufahamu cha kusema na kisemwe wakati gani.

Nne;Mh Matinyi ni msikilizaji mzuri sana wa maoni ya watu. Kwa takribani muda wote niliokuwa naye alielekeza masikio yake zaidi kwangu kusikiliza na kujaribu kupata mtazamo na maoni mbalimbali na kutamani kusikia ninavyoyaangalia mambo.

Mwisho,Niliuona uwezo wake pia mkubwa katika nidhamu na kufuatilia masuala mbalimbali yahusuyo kazi yake. Sio kiongozi wa kukaa ofisini. Wingi wa taarifa alizonazo kuhusu wilaya yake kwa miezi mitatu tu aliyotumika kama Mkuu wa Wilaya ulitosha kuonesha namna ambavyo si kiongozi wa kupokea taarifa tu ofisini.

Kwa muda wa miezi mitatu ya uDC ameiacha Temeke ikiwa kinara wa usafi miongoni mwa wilaya tano za Dar es salaam,Amefanikiwa kuhuisha data za kodi kwa wafanyabiashara wote wa Temeke, amewezesha pia ongezeko la makusanyo ya kodi na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.

Aidha Mobhare aliwezesha mpangilio mzuri wa wafanya biashara wadogo maarufu kama Machinga , bila ya kutumia nguvu na hatukumsikia popote akilumbana na wahusika ama waathirika wa mageuzi mbalimbali huko wilayani Temeke.

Msingi wake mkubwa umekuwa ni kutoa elimu ya ufahamu kwa wananchi na kuacha wahusika wajiongoze na kujiiamulie mambo yao katika namna nzuri kulingana na matakwa ya serikali.

Kila la Kheri Comrade Matinyi Mobhare.

🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
Miezi mitatu,ameleta mabadiliko wilaya ya Temeke? Wakati Wana Temeke wenyewe hatumfahamu au hawajawahi kufanya mikutano mbalimbali kusikiliza changamoto za wananchi.Kuhusu maduhuli, Mkuu wa wilaya alihusika vipi? Siyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke ndiyo ameweka mifumo mizuri ya kukusanya mapato,kwa maana hicho kipindi cha miezi mitatu alikuwa anajifunza mifumo na kazi mpya ya ukuu wilaya.
Wewe Mleta hoja kuongea naye kwenye kipindi chako Cha The Bantu kwa muda huo huo mfupi umeshahitimisha kuwa ni msikivu,ana weledi,uchaguzi bora kuwahi kutokea kwa awamu ya sita nk.
Tuwe tunaweka akiba ya maneno,ili hata kesho akishindwa ku-deliver kwa namna moja au nyingine isiwe tabu.Aidha tuache kupamba Sana na kuwasemea wengine,kwa maana baada ya kufanya kipindi chako,sina uhakika kama ulifuatilia na kuwahoji wananchi ili ku-balance stori yako.
Inawezekana na nakubaliana na wengine kuwa Matinyi Ni team player,na wana Temeke,tumemkosa DC ambaye alikuwa na maono ya kuipeleka mbalimbali Temeke kwa kushirikiana na viongozi wenzake na sisi wananchi
 
Msingi wake mkubwa umekuwa ni kutoa elimu ya ufahamu kwa wananchi na kuacha wahusika wajiongoze na kujiiamulie mambo yao katika namna nzuri kulingana na matakwa ya serikali.
Too much exaggeration.

Anaweza kuwa na baadhi ya sifa ulizotunga, lakini umfanya habari yako yote iwe kama unampigia kampeni,...yale yale ya "uchawa" kila tunapogeuka!

Ni kama vile tayari unategeshea buyu la asali kwa mataraji ya baadae.
 
View attachment 2769067

Na Kevin Lameck

Kama ipo sehemu ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amepatia katika teuzi zake za karibuni, bhasi miongoni mwake ni uteuzi wa sasa wa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Gerson Msigwa.

Bwana Mobhare Matinyi, Mkuu wa wilaya ya Temeke ameteuliwa kuwa Msemaji mkuu wa serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari - Maelezo.

Kabla ya kuwa Mkuu wa Wilaya mwezi wa saba mwaka huu, Mwanahabari huyu kitaaluma, alikuwa akitumika kwenye jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika maarufu kama SADC.

Muda mfupi kabla ya uteuzi huu, wiki iliyopita, nikiri kuwa nilibahatika kuzungumza naye kupitia kipindi chetu cha runinga kiitwacho #TheBantu sambamba na mazungumzo mafupi baada ya kipindi.

Bahati iliyoje kuwa tuligusia pia kuhusu sehemu muhimu ya mawasiliano na mahusiano ya umma kwa serikali ya Rais Samia na namna ilivyo muhimu katika kujenga picha na sifa nzuri ya serikali.

Nitasema machache kumuhusu ili kuchagiza maoni yangu ya awali kuhusu ubora na uzuri wa uteuzi huu wa Bwana Matinyi.

Mosi, Mh. Matinyi ana exposure ya juu sana ambayo ni nadra kuikuta kwa viongozi wengi wa sasa. Nafasi alizopita awali kuanzia kwenye uandishi wa habari, Uhariri mkuu wa magazeti kadhaa na kwenye jumuiya za kimataifa kumemfanya kuwa na utashi,m na mwenye kujaa maarifa na taarifa nyingi zilizomjengea upekee wa aina yake.

Pili; Mh. Matinyi ana uelewa mpana kuhusu siasa za ndani ya nchi, za jumuiya za kimataifa pamoja na hadhira yake kwa ujumla. Suala hili litampa wakati mzuri kuwa msaada kwa Rais na Chama chake katika kushauri na kuupasha umma taarifa zenye kujitosheleza katika urari wa habari na mawasiliano ya umma.

Tatu; Mh Matinyi ni mzungumzaji mzuri sana. Anajua kupangilia na kuumba maneno vyema akiongozwa na hekima ya kufahamu cha kusema na kisemwe wakati gani.

Nne;Mh Matinyi ni msikilizaji mzuri sana wa maoni ya watu. Kwa takribani muda wote niliokuwa naye alielekeza masikio yake zaidi kwangu kusikiliza na kujaribu kupata mtazamo na maoni mbalimbali na kutamani kusikia ninavyoyaangalia mambo.

Mwisho,Niliuona uwezo wake pia mkubwa katika nidhamu na kufuatilia masuala mbalimbali yahusuyo kazi yake. Sio kiongozi wa kukaa ofisini. Wingi wa taarifa alizonazo kuhusu wilaya yake kwa miezi mitatu tu aliyotumika kama Mkuu wa Wilaya ulitosha kuonesha namna ambavyo si kiongozi wa kupokea taarifa tu ofisini.

Kwa muda wa miezi mitatu ya uDC ameiacha Temeke ikiwa kinara wa usafi miongoni mwa wilaya tano za Dar es salaam,Amefanikiwa kuhuisha data za kodi kwa wafanyabiashara wote wa Temeke, amewezesha pia ongezeko la makusanyo ya kodi na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.

Aidha Mobhare aliwezesha mpangilio mzuri wa wafanya biashara wadogo maarufu kama Machinga , bila ya kutumia nguvu na hatukumsikia popote akilumbana na wahusika ama waathirika wa mageuzi mbalimbali huko wilayani Temeke.

Msingi wake mkubwa umekuwa ni kutoa elimu ya ufahamu kwa wananchi na kuacha wahusika wajiongoze na kujiiamulie mambo yao katika namna nzuri kulingana na matakwa ya serikali.

Kila la Kheri Comrade Matinyi Mobhare.

🇹🇿🇹🇿🇹🇿
Ukimsifu mgema tembo hulitia maji wacha kupiga mayowe wacha.........
 
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ungeweka takwimu basi...kaongeza Kodi kiwango gani?kabla ya hapo ilikuwaje?
Umesema Temeke ndo kunaongoza Kwa usafi ? Mbagala including??
Kwani Mbagala siyo Temeke? Mbagala ni Tarafa na Jimbo ndani ya Wilaya ya Temeke
 
Back
Top Bottom