vipik2
JF-Expert Member
- Nov 24, 2011
- 2,803
- 2,185
Leo nimesikia kwenye mkutano wa viongozi wa TANESCO na waziri kwamba shirika lijiendeshe kibiashara.
Unajiuliza, tanesco msingi wa uanzilishwaji wake ilikua ni nini, quality service delivery ama profit oriented?
Kama waziri anataka Tanesco ijiendeshe kibiashara, itakuwa ngumu watu kuunganishiwa umeme. Ndio maana serikali ilikuja na hoja ya 27000 kwa kila mtu ili kuongeza uunganishwaji kwenye umeme.
Waziri kwa unafiki mkubwa anasema sasa shirika liko mikono salama, utafikiri waliokuwepo wote walikua wezi. Huu ni udhalilishaji.
Usiumize akili yako wee unganisha dots awamu ya nne, kashfa ya Dowans, Singasingaa na mzee Ruge na mwisho chambua kila mmoja upate background za kila Boss pale TANESCO finally utaniambia tujitayarishe kwa Dowans nyingine au maumivu poa kwenye uchaguzi wa 2025