Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,906
Msomi wa kiwango cha kimataifa wa Tanzania, Profesa Shivji ameshangazwa na kitendo cha wafanya biashara kuchaguliwa kuongoza taasisi za umma.

Shivji anasema sekta ya umma haiwezi kuchangamana na sekta binafsi.

Sisi wengine tumeshangazwa na uteuzi wa wafanya biashara na watu wenye maslahi binafsi kwenye bodi ya TANESCO. Yule mama Balozi ndie mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Rex Attorneys ambao wanaiwakilisha Dowans na Symbion kwenye kesi ambazo TANESCO inashitakiwa na hayo makampuni halafu anateuliwa kuwa board member.

"Pamoja na kushirikiana na sekta binafsi, huwezi kuwaingiza wafanyabiashara jikoni wakupikie chakula cha umma!
Sekta ya umma na sekta binafsi hazilinganiki. Ni kweli huwezi kuendesha biashara kama idara ya serikali; pia ni kweli huwezi kuendesha serikali kama kitengo cha biashara."

Unaweza kusoma mwenyewe hapa.

907E480A-99DD-4807-9CA7-989901068575.jpeg


 
Leo nimesikia kwenye mkutano wa viongozi wa TANESCO na waziri kwamba shirika lijiendeshe kibiashara.

Unajiuliza, tanesco msingi wa uanzilishwaji wake ilikua ni nini, quality service delivery ama profit oriented?

Kama waziri anataka Tanesco ijiendeshe kibiashara, itakuwa ngumu watu kuunganishiwa umeme. Ndio maana serikali ilikuja na hoja ya 27000 kwa kila mtu ili kuongeza uunganishwaji kwenye umeme.

Waziri kwa unafiki mkubwa anasema sasa shirika liko mikono salama, utafikiri waliokuwepo wote walikua wezi. Huu ni udhalilishaji.

 
Naomba nielimishwe kidogo, hilo lipo katika katiba au ni mawazo binafsi ya Shivji? Yule Trump aliyekuwa Rais wa Marekani ana biashara dunia nzima, Vipi nchi iliathirika na ubiashara wake au ya kule nisiyahusishe na huku kwetu wenye nyeusi ngozi?

Mbowe ni mfanyabiashara na aliwahi kugombea uraisi, vipi km angepata Prof Shivji angekuja na maoni haya pia?!!
 
Tatizo nilionalo mimi ni huko kuingiza watu ambao ama tayari wanasemwa semwa kwa kutilia shaka uadilifu wao au wale ambao kutokana na mgongano wa kimaslahi wanaweza kuleta ushawishi kwa bodi na menejimenti ili kupata upendeleo kwenye taasisi zao binafsi wanazoziongoza.
Lakini suala la shirika kujiendesha kibiashara mbona hata wakati wa Magufuli tuliambiwa shirika sasa linajiendesha kibiashara na kudaiwa kwamba sasa shirika halipokei tena ruzuku toka serikalini au ilikuwa changa la macho ili kumpamba mzee wa misifa?
 
Naomba nielimishwe kidogo, hilo lipo katika katiba au ni mawazo binafsi ya shivji? Yule trump aliyekuwa rais wa marekani ana biashara dunia nzima...
Ukiingia kwenye siasa biashara zako unakabidhi watu wengine na serikali ukifanya biashara na biashara zako lazima itangazwe ili watu wengine waweze ku scrutinise kama kuna upendeleo wa aina yoyote au ni biashara tu kama nyingine
 
Ukiingia kwenye siasa biashara zako unakabidhi watu wengine na serikali ukifanya biashara na biashara zako lazima itangazwe ili watu wengine waweze ku scrutinise kama kuna upendeleo wa aina yoyote au ni biashara tu kama nyingine
Ahsante, sasa tubaki tunalaumu tu haraka haraka au tuone kwanza kama biashara zao wamekabidhisha kwa watu wengine?!!
 
Tatizo nilionalo mimi ni huko kuingiza watu ambao ama tayari wanasemwa semwa kwa kutilia shaka uadilifu wao au wale ambao kutokana na mgongano...
Ulikuwa ni uongo, Tanesco ni dili japo WAnapata hasara kubwa kila mwaka billions, lakini katika ulaji kwa maana ya manunuzi Kuna pesa nyingi mno, entity zinazoongoza kwa zabuni za pesa mingi nchi hii NI
1. Tanroad
2.Taneaco
3.REA
SASA KAMA UKIWEZA KUCONTROL HIZO 2, 3 UKAWEKA WATU WAKO ULAJI NJE NJE, MAKAMBA NI BIG BRAIN
 
Ukiingia kwenye siasa biashara zako unakabidhi watu wengine na serikali ukifanya biashara na biashara zako lazima itangazwe ili watu wengine waweze ku scrutinise kama kuna upendeleo wa aina yoyote au ni biashara tu kama nyingine
Wakati wa Kikwete walidai wanataka kutunga sheria inayoelekeza hivyo lakini hadi anaondoka hiyo sheria haikuwahi kupatikana na hadi Magufuli anafariki haikuwepo sheria hiyo, kwahiyo hicho unachokisema hakipo kisheria mambo yanajiendea tu.
 
Back
Top Bottom