KWELI Paul Kagame alihudumu kwenye Jeshi la Uganda na kufikia cheo cha Mkuu wa Usalama wa Jeshi

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Baada ya kauli ya CDF wa Tanzania Jenerali Mkunda kusema kuwa 'Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi' imenifikirisha sana nikakumbuka nilishawahi kusikia tetesi kuwa Paul Kagame wakati akiwa mkimbizi nchini Uganda, aliwahi kuhudumu kwenye jeshi la nchi hiyo na mpaka kufikia cheo cha Mkuu wa usalama wa Jeshi Uganda.

Mpaka sasa tunaona jinsi Kagame anavyoisumbua Uganda labda kutokana na ukweli kuwa anaijua nje ndani.

Kagame.png

Je, ni kweli Paul Kagame aliweza kuaminiwa na kupewa cheo nyeti kwenye Jeshi la Uganda?
 
Tunachokijua
Paul Kagame, Rais wa sasa wa Rwanda alizaliwa Gitarama, katikati mwa Rwanda, Oktoba 23, 1957, katika familia ya Watutsi. Mwaka 1959, mauaji ya Watutsi yaliyofanywa na Wahutu yalipoanza, familia ya Paul Kagame ilikimbilia Uganda pamoja na maelfu ya Watutsi ili kuokoa maisha yao.

Mwaka 1979, akiwa na umri wa miaka ishirini na miwili, Kagame alijiunga na kundi la National Resistance Army (NRA), lililokuwa linaongozwa na Yoweri Museveni, wanamgambo waliokuwa wanaoungwa mkono na Marekani kupigana na dikteta wa Uganda wa miaka ile, Idi Amin Dada.

Mwaka 1986, NRA ilimpindua Obote na Museveni akawa Rais na kumteua Mkuu wa Mkuu wa Idara ya Ujasusi ya Ulinzi ya Uganda.

"Kwa miongo kadhaa, Kagame na Museveni walipigana bega kwa bega, na kumwangusha dikteta wa Uganda, Milton Obote kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1986 na kumwangusha Mobutu Seko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 1997. Kagame, ambaye alipata mafunzo ya ujasusi nchini Tanzania, akawa mkuu wa ujasusi wa Museveni na msiri wa karibu. Kwa upande wake, Museveni alisaidia kuinuka kwa Kagame madarakani, na kuwaingiza wakimbizi wa Rwanda ambao hatimaye waliunda Rwanda Patriotic Front. Kwa kuungwa mkono na Museveni, Kagame aliivamia Rwanda, na kumaliza mauaji ya kimbari ya 1994", wanaandika Council on Foreign Relation.

Mnamo 1990, baada ya kuhudhuria kambi ya mafunzo ya kijeshi ya Merika huko Fort Leavenworth, Kansas, Kagame alianza kutawala katika nchi yake ya asili ya Rwanda na Oktoba 1, 1990, Front Patriotique Rwandais (FPR), iliyojumuisha Watutsi wengi walio uhamishoni, na kuundwa katika miaka ya 1980, walianza kushambulia miji ya mpakani mwa Rwanda. Oktoba 2, kiongozi wa FPR Fred Rwigema alikufa vitani na Rais Museveni akamteua Kagame kama kiongozi mpya wa FPR.

Kati ya 1991 na 1993, Kagame aliongoza FRP katika mazungumzo huko Arusha, Tanzania ili kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Rwanda. Mwaka 1994, hata hivyo, baada ya kifo cha Rais wa Rwanda Juvénal Habyarimana katika ajali ya ndege, mauaji ya halaiki yalianza ambapo takriban watu milioni moja waliuawa wakati wa mauaji hayo.
Paul Kagame alikulia katika kambi ya wakimbizi ya Nshurungerezi iliyoko Uganda.

Lakini baadae akiwa na rafiki yake Fred Rwigyema walijiunga na FRONASA ambalo lilikuwa ni kundi la waasi la Uganda lilokuwa na makazi yake Tanzania na liloongozwa na mzee Yoweri Kaguta Museveni.

FRONASA walipewa hadhi ya ukimbizi nchini Tanzania na serikali ya Tanzania na Yoweri Museven amesoma chuo kikuu cha Dar-es-salaam.

Kulipoibuka vita ya Tanzania na Iddi Amin mwaka 1979, mzee Kagame na rafiki yake Fred Rwigyema waliungana na wapiganaji wa FRONASA chini ya Museveni kumuondoa Iddi Amin.

Hapo ndipo Paul Kagame alifanya kazi za uchambuzi wa kijasusi (intelligence analyst) kwa serikali na majeshi ya Tanzania na aliongoza kazi maalum ziloratibiwa na kusimamiwa na marehemu brigedia (baadae luteni jenerali) Imran Kombe.

Mzee Paul Kagame amesoma na kupata mafunzo ya kijeshi kutoka katika chuo cha kijeshi cha CGSC cha nchini Marekani.
 
Paul Kagame alikulia katika kambi ya wakimbizi ya Nshurungerezi iliyoko Uganda.

Lakini baadae akiwa na rafiki yake Fred Rwigyema walijiunga na FRONASA ambalo lilikuwa ni kundi la waasi la Uganda lilokuwa na makazi yake Tanzania na liloongozwa na mzee Yoweri Kaguta Museveni.

FRONASA walipewa hadhi ya ukimbizi nchini Tanzania na serikali ya Tanzania na Yoweri Museven amesoma chuo kikuu cha Dar-es-salaam.

Kulipoibuka vita ya Tanzania na Iddi Amin mwaka 1979, mzee Kagame na rafiki yake mzee Fred Rwigyema waliungana na wapiganaji wa FRONASA chini ya Museveni kumuondoa Iddi Amin.

Kagame na vita vya Kagera ni juisi ya pilipili
 
Mwaka 1979 Kagame alikuwa na umri gani?
 
Baadae Lin wakati vita vya idi Amin..mwaka huo?
Alikuta watu wako kazini tayari,
Fred Rwigema ndiye alikua front,Salim Saleh,Sam kaka,na wengineo hao ndio waliingia mazima na makamanda kama Samson Mande ndio aliikamata Kampala.
Ye hakuwepo,alikutana nao washamaliza kumkimbiza Amin wanaelekea njiani Chigali.
Fred ndo alikua na kikosi kizima,akalimwa shaba ya kisogo na wenzie hao hao,wakasonga mbele.
Pk ndio akashika Mpini.
Hao wote wamekulia hapo bongo Upanga,na waliondokea hapo kulianzisha huko.
 
Inaonekana huko ndani kuna mambo hayajakaa sawa......

Hili suala la uraia linaweza kuacha kovu kubwa kwa taifa
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom