Angalia jinsi Kagame anavyoionesha duniani kuwa nchi yake ina watu wenye akili, elimu na uwezo mkubwa wa kufikiri kushinda waisrael

6 Pack

JF-Expert Member
Apr 17, 2022
1,827
4,076
Niaje waungwana,

Leo nimeamua nije na ukweli ambao baadhi ya ndugu zetu wayahudi wa bonyokwa, tangibovu, kiembe mbuzi na buza hawaujui. Hii ni kwa sababu wale wachache wenye kuujua huu ukweli hawataki kuusikia popote, u kuuzungumzia kwa mtu yoyote.

Kwanza naomba nianze na Rwanda ya leo inayoongozwa na jemedari Paul Kagame kutoka kabila la watutsi walio wengi serikalini, na wenye maamuzi ya mwisho ya nchi hiyo, japo nafahamu kuwa nchi hiyo ina makabila mengine kama vile wahutu na watwa.

Historia inasema, mnamo miaka ya 60 kuelekea 70, ulifanyika msako nchini Rwanda, kwa lengo la kuwaangamiza wanyarwanda wote wenye asili ya kitutsi. Hali hiyo ya msako ilipelekea maelfu ya watutsi kukimbilia sehem mbali mbali za dunia hii, lakini wengi wao walikimbilia katika nchi jirani za Tanzania, Burundi, Congo na Uganda. Watutsi walipokuwa huko kambini waliishi maisha ya shida na ya mateso makubwa sana (hapa watu waliowahi kuishi kambini watakuwa wamenielewa).

Baada ya mateso ya muda mrefu wakiwa nje ya nchi yao, ikabidi jumuia ya kimataifa ikaingilia kati ili kuangalia uwezekano wa watutsi hao warudi katika nchi yao wakaishi maisha yale yale ya kawaida wanayoishi wanyarwanda wenzao (wahutu na watwa). Mpaka hapo hakuna aliekuwa anajua kwamba kurudi kwao kungekuwa ni kwa usalama kweli au ni mtego wameweka au kuwekewa.

Mwaka 94 (miaka 30 tu iliyopita) makubaliano yakafanyika ili watutsi wale waliokuwa nje waanze kuingia nchini kwao kwa makubaliano maalum ya kulindwa na umoja wa mataifa ili wasidhuriwe kwanza. Na wakati huo kuna baadhi ambao sio politicians walikuwa wameshaanza kuingia. Wakati juhudi za kimataifa zikiendelea kufanyika huko Arusha kwa kuwaandalia hao watutsi mahali watapofikia wale watakaoletwa. Ghafla aliekuwa raisi wa nchi hiyo ambae ndo alikuwa anatoka kufanya mazungumzo ya kuwataharishia wageni wake makazi akatunguliwa akiwa angani.

Bwana wee, kilichofuatia kila mtu anakijua, mauaji ya kimbari yakaanzishwa dhidi ya watutsi. Ilianza chinja chinja, kwa aliehusika na asiehusika, aliekuwepo katika mission ya mauaji na asiekuwepo, wakubwa kwa wadogo, wanawake kwa wanaume, wazee kwa vijana. Yani watutsi walichinjwa kama mbuzi wa machinjioni huku dunia ikiangalia tu kinachoendelea. Lakini kama wazee wetu walivyosema kuwa "kila muosha na yeye ataoshwa". Ghafla hali ikabadilika, wachinjaji (wahutu) wakageuka kuwa wachinjwaji. Kimbembe hadi wakajikuta wako Congo wote, mji na nchi wamewaachia watutsi.

Watutsi walipoingia waliikuta nchi inanuka harufu za maiti zilizooza mitaani, umasikini wa kutupwa, miji michafu nk. Wanyarwanda wakaanza kuijenga nchi yao taratibu huku wakijifunza baadhi ya mambo kutoka kwa majirani zao ikiwemo Tanzania, Uganda, Kenya na hata nchi za magharibi.

Leo hii tunavyoongea ni miaka 30 tu toka waipindue serikali ya kihutu, lakini hatua ya maendeleo iliyochukuliwa ni kubwa mno ukilinganisha na nchi zingine ambazo hazikuwahi kukumbana na vita vya aina yoyote toka uhuru. Rwanda ya leo ina jeshi lake imara, ina silaha zake imara inanunua kutoka nje, ina uchumi mzuri kwa kiasi fulan. Japokuwa nchi hiyo haina rasilimali zozote za maana na pia imetoka vitani miaka 30 tu iliyopita, plus imezungukwa na maadui watupu ukiitoa tu Tanzania na kidogo Uganda, lakini kamwe, hautosikia kuwa Kagame anailinda nchi yake kupitia msaada wa kijeshi wa Marekani, Ufaransa au Russia. Kagame ana maadui wengi kuanzia wa nchi zilizomzunguka hadi kwa makundi fulan ya waasi, lakini kamwe hautomsikia analia lia eti mataifa makubwa yaje yamsaidie kupambana na maadui waliomzunguka.

Ngurunziza aliwahi kumjambisha Kagame kwa kumtumia vikundi vya waasi vikafanye maangamizi katika ardhi ya Rwanda, wale waasi walichokutana nacho huko Rwanda, kimewafanya wengine waliokuwa wanataka na wao waingie ku take advantage wachenji mipango yao. Leo hakuna tena muasi anaetaka kuthubutu kwenda kuvamia ardhi ya Rwanda. Wengi wanaishia kupiga zogo, na mikwara ya hapa na pale huko katika misitu ya Congo, Burundi nk. Hakuna mwenye hamu hata ya kusogelea mpaka, achilia mbali kuvamia nchi. Tshesekedi ashawahi kuchimba mkwara kwa kutumia videge vyake visivyokuwa na rubani, Rwanda yenyewe bila kuhitaji msaada wa Marekani wala Ufaransa, alivishusha videge vile alaf akawapa askari wa Congo wampelekee bosi wao wakamuoneshe kuwa silaha alizokuwa nazo si lolo si chochote, Tshesekedi alivyoona vile akafyata, hadi leo hajarudi kupeleka ndege wala mwanajeshi hata mmoja mpakani. Rwanda chini ya raisi Kagame ina viongozi wasomi ambao hawapendi kuona nchi yao inashindwa kujiendesha yenyewe, wamepambana wenyewe bila msaada wa nchi yoyote kutatua changamoto zao kubwa na ndogo.

Tukija kwa Israel, nayo ni kama Rwanda. Walikimbizwa katika nchi yao na kwenda kuishi Uhamishoni. Nao pia waka face mauaji ya kimbari kama wanyarwanda huko Ujerumani. Japo haijulikani kama walikufa wayahudi wote, na kina Netanyahu (wazungu) wakavishwa uyahudi wa mchongo kwa masilahi ya wazungu wenzao pale Mashariki ya kati. Kina Netanyahu wakaletwa na kupachikwa pale wakiambiwa eti ndio kwao. Anyway hilo sio tatizo.

Tatizo ni kwamba inakuaje nchi ambayo imeanzishwa miaka zaidi ya 75 iliyopita mpaka leo inashindwa kujiendesha yenyewe. Yani pamoja na kutumia media kuipamba sijui Mosad sijui upuuzi gani, lakini bado tunauona ukweli kuwa nchi hii inapata misaada ya kijeshi, silaha na hata bajeti ya nchi kutoka nje. Mbona wanashindwa hata na wanyarwanda ambao wameamu kuishi kwa kujitegemea.

Kama maadui hatari hata Rwanda anao na ana deal nao mwenyewe, so inakuaje Israel nayo ishindwe ku deal nao yenyewe? Yani hata Hamas kikundi cha vijana wasiokuwa na uwezo wa kutengeneza hata gwanda za jeshi ni wa kuwaombea msaada wa kijeshi kutoka Marekani, Uingereza na Ujerumani ili upambane nao kweli?

Yani vijana wasiokuwa hata na kifaru ni wa kuwaendea kwenye vita na midege ya kivita, mivifaru na manuari za kivita kweli?

Ama kweli tumshukuru mtu alieleta utandawazi na simu za internet. Maana zimetusaidia kujua mengi tuliokuwa hatuyajui. Tulikuwa tunadanganywa mengi kuhusu taifa hilo kiasi ya kwamba tulifikiri labda nchi hii imefunikwa na mbingu ya chuma ambacho hakiwezi kuruhusu chochote kibaya kuingia ndani. Lakini kumbe ni taifa la hovyo la wanaoishi kwa kulia lia na kutegemea msaada wa nchi zingine. Tena hili la kulia lia na kutegemea msaada wa nchi zingine linaonekana ndio utamaduni na asili yao, maana hata yule raisi wa Ukraine ambae ana asili ya kiyahudi na yeye kila siku analia lia ili asaidiwe kupewa silaha na fedha 😂😂😂.

Kwangu mimi Kagame na serikali yake ni watu makini na wenye akili mara mia moja zaidi ya Netanyahu na genge lake la mashoga huko Israel.

Hata hili shambulizi la Iran, waisrael washukuru Mungu nchi takriban 7 zilifanya juhudi usiku na mchana kuzuia mashambulizi yale. Laiti kama wangeachwa kama Rwanda wajitetee wenyewe, leo hii Netanyahu na wahuni wenzake wangekuwa wamefukiwa vifusini.
 
Niaje waungwana,

Leo nimeamua nije na ukweli ambao baadhi ya ndugu zetu wayahudi wa bonyokwa, tangibovu, kiembe mbuzi na buza hawaujui. Hii ni kwa sababu wale wachache wenye kuujua huu ukweli hawataki kuusikia popote, u kuuzungumzia kwa mtu yoyote.
SIJASOMA MAANA I KNOW NI HAYO HAYO YA UCHAWA, RWANDA INAIZIDI ISRALE?
 
Niaje waungwana,

Leo nimeamua nije na ukweli ambao baadhi ya ndugu zetu wayahudi wa bonyokwa, tangibovu, kiembe mbuzi na buza hawaujui. Hii ni kwa sababu wale wachache wenye kuujua huu ukweli hawataki kuusikia popote, u kuuzungumzia kwa mtu yoyote.
Hivi mna chuki gani israel kila kukicha mmedanganywa nini kwenye dini yenu kuhusu israel mbona kama ni mauaji ya waislamu yamefanywa na assad wa syria mbona saudia arabia imeua waislamu wengi wa yemen kwani wapalestina ni nani?
 
Hivi mna chuki gani israel kila kukicha mmedanganywa nini kwenye dini yenu kuhusu israel mbona kama ni mauaji ya waislamu yamefanywa na assad wa syria mbona saudia arabia imeua waislamu wengi wa yemen kwani wapalestina ni nani?
Hakuna sehemu iliyotajwa dini. Afrika Kusini asilimia 99 ni wakristo wa madhehebu mbali mbali akiwemo hayati Desmond Tutu. Lakini wanaichukia Israel kwa matendo yake machafu zaidi ya wewe unavyowachukia waislam.
 
ila waislamu israel itawatoa roho yaani mnatafuta kila namna ya kujifariji
Huo mda uliotumia kuandika uzi wote huo ungetumia kufanya mambo yako ya msingi
Afrika kusini asilimia 99 ni wakristo wa madhehebu mbali mbali akiwemo hayati Desmond Tutu, lakini wanaichukia Israel zaidi ya vile wewe unavyowachukia waislam.

Hapo sijamtaja hayati baba wa Taifa mkatoliki original. Hivyo sio kila anaeipinga Israel ni muislam au anaeunga mkono unyama wa Israel ni mkristo. Acha kukariri maana post haikutaja dini ya mtu.
 
Afrika kusini asilimia 99 ni wakristo wa wa madhehebu mbali mbali akiwemo hayati Desmond Tutu, lakini wanaichukia Israel zaidi ya vile wewe unavyowachukia waislam.

Hapo sijamtaja hayati baba wa Taifa mkatoliki original.
Hao wanataka usawa ni tofauti na waislamu hawataki taifa la israel liwepo huo ndo utafauti

Mwaka 1947 mpango wa nchi mbili uliopendekezwa na UN israel waliikubali ila waarabu na waislamu waliukataa
Wakapigana vita israel ikawashinda ndo mwanzo mwa israel kuanza kuyakalia maeneo ya west bank kimabavu

Waislamu na waarabu walianza kukubali kinafki two state solution baada ya kushindwa vita vya 1967
 
Hao wanataka usawa ni tofauti na waislamu hawataki taifa la israel liwepo huo ndo utafauti

Mwaka 1947 mpango wa nchi mbili uliopendekezwa na UN israel waliikubali ila waarabu na waislamu waliukataa
Wakapigana vita israel ikawashinda ndo mwanzo mwa israel kuanza kuyakalia maeneo ya west bank kimabavu

Waislamu na waarabu walianza kukubali kinafki two state solution baada ya kushindwa vita vya 1967
Ndio maana nikasema tuwashukuru watu walioleta sim na mitandaoni, maana vimetusaidia kuujua ukweli. Hayo ya mpango wa nchi mbili mwaka 47 umeyasikia tu kutoka kwa walioamua kuegemea upande wa Israel. Mimi na wewe hatukuwepo na wala hatukuona kupitia media yoyote kipindi hicho, so tutaamini vp?

Mbona leo mimi na wewe tupo, sim zipo na media zipo zinazoonesha kuwa Netanyahu na Israel yake wanapinga uwepo wa mataifa mawili.

Ni mara ngapi toka mzozo wa Hamas uanze Marekani anaishauri Israel ikubali mpango wa nchi mbili ili liwe suluhisho la kudumu, lakini Netanyahu na Israel yake wanakataa? Wewe hujawahi kuisoma hiyo news? Maana hizo habar za mwaka 47 tumehadithiwa tu, hakuna anaejua kama ni kweli au porojo, lakini hii ya sasa tunashuhudia jinsi nchi za magharibi zinaibembeleza Israel ikubali suluhisho la mataifa mawili, lakini Israel ikakataa. So hiki ulichoandika hapa hakina mashiko yoyote, ni propaganda kama zilivyo propaganda zingine za Israel.

Hata hivyo mada haizungumzii swala la waarab, mada inazungumzia namna wanyarwanda wamefanikiwa kutengeneza system ya kujitegemea wenyewe bila kuhitaji msaada wa kijeshi wala silaha kutoka kwa nchi yoyote, licha ya nchi hiyo kuzungukwa na maadui lukuki. Sasa kwanini Israel taifa la Mungu lenyewe lishindwe kujitegemea?
 
Hivi hapo Rwanda ukiacha Kigali kuna jiji lingine zuri na tajiri
Sizungumzii utajiri wa mji mkuu, nazungumzia uwezo wa Rwanda kujilinda yenyewe na sio kulindwa na nchi za magharibi kama vile Israel.
 
SIJASOMA MAANA I KNOW NI HAYO HAYO YA UCHAWA, RWANDA INAIZIDI ISRALE?
Rwanda inaishinda Israel kijeshi, kwa sababu Rwanda inapambana na maadui zake yenyewe. Ila Israel inapambana na maadui zake kwa kupitia msaada wa Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujeruman na nchi zingine za magharibi.
 
Back
Top Bottom