Orodha ya Watumishi wenye vyeti vya Kughushi...

Orodha ya Watumishi wenye vyeti vya Kughushi...

~~~>>>Kuwa mpinzani sio kupinga kila kitu.... Mengine jarbuni kutumia akili zenu...

~~>>>Vijana wa Chadema badala ya kupanua akili nyie mnapanua vidole.. Mwisho mtapanua na makalio....
 
haahahaha.........huwaga na wao wanazingua..???
nimeyaona duu ni mekuta dgo aliyepiga zero o level anatamba na kazi yake leo katumbuliwa dah nampa pole na yupo hapa jf ohoo baba mtu mzito ziro bongo...
 
Kuna mtu nimesoma nae olevel ameonewa alimaliza mwaka mmoja mbele yangu yaani roho inaniuma sana Nina uhakika hajafoji sijui namsaidiaje?
Mnachotakiwa kujua ni hili. Unaweza kuwa ulisoma mwenyewe na jina ni lako lakini matokeo ya kwenye cheti sio yako. Hilo wengi hamjui.
 
Wakuu habarini za majukumu.

Nimefatilia baadhi ya watu wengi walio na vyeti feki ni walinzi, madereva, wahudumu wa masjala, ma typist, na wafagiaji. Watu hawa wengi kazi zao hazihitaji elimu ukifananisha na kama ilivyo kwa walimu, sekta Afya na zingine zenye mfanano wa hivyo.

Kwa nini isiwepo exemptions kwa walinzi, wahudumu wa huduma zote, kwani tayari kazi zao zinafanyika tu kwa uzoefu, na ndizo zinahitaji zaidi kujua kusoma na kuandika ukifananisha na viongozi wa kisiasa kwenye serikali ambao wana mishahara mikubwa.

Mishahara ya hawa wahudumu kwa ujumla ni midogo sana, mfano kwenye mshahara wa RC au DC kwa mwezi hawa wahudumu wanaingia kuanzia 15 @ kila mhudumu wastani wa Tsh. 250,000/=

Mbona hawa maboss wenyewe kama Wakurugenzi, wakuu wa Idara na vitengo ni kweli wote wana vyeti halisi? Hakuna mtu aliefoji kweli? Mbona mi kuna fulani na fulani nawajua, lakini hawapo kwenye list.
Una uhakika na ulichokiandika?
 
Miaka 7 ilopita, baada ya kufaulu digrii yangu ya pili, niliomba kazi na kufanyiwa usaili. Majina 5 tuliingia round ya pili ya usaili, wawili wakapata kuajiliwa, mimi na jamaa wengine tukakosa hiyo nafasi.

Niliamua kujiajili kwa kilimo na biashara ndogo ndogo, sikutaka tena fedheha ya kuomba kazi.

Leo nimebaki mdomo wazi! Aliyekuwa anaongoza jopo la usaili, pamoja na hao jamaa tulofanyanao usaili wakapata ajira, wamekumbwa na fagio la vyeti feki.

Poleni, na karibuni kitaa muonje maisha bila mshahara na posho za safari. Maisha bila kukomaa hata mia huioni.
 
Hapo kwa mikopo ndo pagumu, au ile bima ya mikopo ita compasate?? ngoja wataalam waje watufafanulie.
Ni loan insurance lakini pia baadhi ya Taasisi husecure mikopo yao na pensheni. Nadhani na huko patafungwa.
 
Kuna mtu nimesoma nae olevel ameonewa alimaliza mwaka mmoja mbele yangu yaani roho inaniuma sana Nina uhakika hajafoji sijui namsaidiaje?
Kusoma nae O level sio tatizo, inawezekana alitengeneza cheti kingine feki chenye majina yake hayo hayo ila kikabadilishwa matokeo na kuwa mazuri zaidi ya aliyopata.
 
Kwanza hiyo list mm siiamini sana naona kama kuna sample tu majina mengi ni hewa pia (yaani hayana wenyewe) maana nmechunguza nimekuta 90% ya watumishi hao ni walimu na manurse afu sehemu zilzoguswa ni manispaa, miji wilaya na mikoa sjaona majna ya board kama TRA, TANESCO, CDA etc au wote hawa ni wateuliwa?
Musa Kuna list nyingine ya wafanyakazi wa Serikali Kuu.
 
Nauza vyangu Original, nipate tu pesa ya mtaji.

Kuna haja gani ya kuwa navyo huku sina kazi, alietayari kununua ani PM
Mkuu itabidi tutengeneze tangazo la biashara redioni na kwenye luninga.

Mimi pia vyeti vyangu vinaoza kabatini, ngoma original zote ziko powa, kutoka std 7 hadi Masters. Havina kazi na wala sitegemei tena kuvitumia.

Kilimo cha vitunguu na biashara ndogo ndogo haihitaji vyeti. Watoe pesa tuwaachie makaratasi.
 
Nimegundua vetting nchi hii ni bosheni tu ya kuwapatia watu ulaji au vetting huenda inafanywa kujua tu kwamba mtumishi huyu ni CHADEMA supporter au sio, Haiwezekani mkuu wa Idara ambaye tunaambiwa lazima apitie vetting kuthibitishwa hicho cheo naye jina lake linatokea kwenye wenye vyeti fake!

Kasikilize hotuba zao tena, acha kujiambia yasiyo.
 
Binafsi nimeona jina langu,na sijawahi kufanya kazi serikalini wala kumpa mtu vyeti vyangu
Inawezekana majina yamefanana tu. inawezekana ukawa ni wewe, vyeti vyako vimetumika bila kujua.

Hizi sehemu za kupigia copies ndio chanzo kikubwa cha watu kuchukua vyeti vya wengine.

Vizuri wangeweka na index number za O level.
 
Kuna watu wengi wameumia katika hili lakini wapo waliomizwa zaidi kwa muda mrefu kutokana na watu hawa.
Ushauri wangu ni kwamba, serikali ilazimishe Taasisi zote na mashirika ya dini ambayo hupokea ruzuku zake, kuhakiki watumishi wao. Hapa ninamaanisha sifa kuu ya ajira kwenye utumishi wenye mahusiano na pesa za serikali iwe ni uhalisia wa wafanyakazi. Hii ni hospital na vyuo vikuu vyote binafsi vinavyopokea pesa za serikali.
Ni maumivu lakini nchi lazima tuisafishe.
 
Mambo zenu wanaJF.

Zimwi la vyeti fake ndo habari ya mujini mujini Dsm na duniani kote. Hapa Dsm, ukipanda daladala au ukienda bar ,swala la vyeti fake limegusa familia nyingi sana hapa nchini.

Kuna ambao wameona watoto wao, ndugu zao, rafiki zao, waume/wake zao, wazazi wao nk na sasa habari imeshavuja.
Sasa basi, tutegemee maofisi kupwaya watu siku za karibuni. Na pia watu kubaki majumbani kulea watoto na vijukuu.

Umejisikiaje baada ya kuona mtu unayemfahamu kwenye orodha ya watumishi hewa?

Binafsi sijaona mtu ninayemfahamu.
Hiyo orodha iko wapi? Japo hainogi kwa kutowahusisha viongozi wa kisiasa
 
Back
Top Bottom