DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,143
Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, ametangaza kibali maalumu cha mwaka mmoja cha kuruhusu marekebisho ya taarifa za usajili ambazo zilikwama kutokana na kukinzana na taratibu za uthibitishaji, ikiwemo matumizi ya nyaraka za kughushi na taarifa za uongo.
Kibali hicho, kilichoanza kutumika Oktoba 2025, kinahusu makundi manne: waathirika wa vyeti vya kughushi katika ajira za Serikali, watu waliotumia majina ya wengine kupata vyeti vya elimu, waliotoa taarifa za uongo wakati wa usajili wa NIDA, na raia wa Tanzania waliojisajili kama wakimbizi.
Wananchi walio kwenye makundi hayo wanatakiwa kufika ofisi za NIDA wakiwa na nyaraka sahihi. Kaji amesisitiza kuwa ni maombi yatakayokidhi vigezo pekee ndiyo yatakayokubaliwa, na muda wa kibali hicho hautaongezwa.