Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 887
- 774
Kuna jambo ambalo tunapaswa kulisema kwa uwazi kabisa bila kuficha ukweli.
Inasikitisha kuona uongozi wa juu wa nchi ukipambana usiku na mchana kutafuta suluhisho la matatizo ya wananchi Rais akisimamia utekelezaji wa miradi Serikali ikitenga fedha mawaziri wakizunguka kusimamia majukumu yao
halafu mwisho wa siku baadhi ya watumishi waliokabidhiwa jukumu la kutekeleza sera hizo wanakuwa ndio chanzo cha malalamiko ya wananchi.
Je tunatambua uzito wa nafasi tuliyopewa?
Rais anaweza kuwa na maono mazuri sana.
Serikali inaweza kutenga mabilioni kwa ajili ya hospitali dawa vifaa tiba na huduma nyingine muhimu.
Lakini fedha hizo zikifika kwenye maeneo ya utekelezaji zinahitaji watu wenye dhamira ya kweli.
Zinahitaji watumishi wanaoona kazi zao kama wajibu kwa taifa na si kama sehemu ya kwenda kusubiri mwisho wa mwezi.
Hasa katika sekta ya afya uzembe hauwezi kutazamwa kama kosa dogo.
Hapa tunazungumzia maisha ya watu.
Mwananchi anapoingia hospitalini akiwa na maumivu haji kuomba hisani anakuja kupata huduma ambayo ni haki yake.
Anahitaji kupokelewa kwa utu kusikilizwa kwa heshima na kuhudumiwa kwa weledi.
Lakini nini kinatokea pale mtumishi anapokuwa kikwazo?
Mwananchi anayenyanyaswa au anayepuuzwa haondoki akisema“Nimekosewa na mtumishi fulani” Mara nyingi anaondoka akisema “Serikali imeshindwa”
Hapo ndipo tunapaswa kuelewa uzito wa matendo yetu.
Kosa la mtu mmoja linaweza kuharibu taswira ya taasisi nzima na uzembe wa watumishi wachache unaweza kufunika kazi kubwa inayofanywa na Serikali.
Hii ndiyo mianya tunayosema.
Mianya ambayo wapotoshaji wanaweza kuitumia kusema hakuna kinachofanyika
wakati ukweli ni kwamba rasilimali zimepelekwa miundombinu imejengwa na mipango imewekwa lakini utekelezaji katika baadhi ya maeneo unakwama kwa sababu ya uzembe na tamaa kutowajibika au kukosekana kwa moyo wa huduma.
Tujiulize kwa uaminifu Rais awe afanye nini zaidi kama kila hatua ya maendeleo inahitaji mtu mwingine kuharibu kwa kutotimiza wajibu wake?
Rais au waziri hawezi kusimama kwenye kila mapokezi ya hospitali🙌.
Hawezi kukaa kwenye kila chumba cha wagonjwa.
Hawezi kusimamia kila dawa inayotolewa wala kufuatilia kila mtumishi kila dakika.
Ndiyo maana Serikali ina mfumo wa watumishi na viongozi katika ngazi mbalimbali.
Kila mmoja amepewa dhamana.
Kwa hiyo kuwa mtumishi wa umma si kupata ajira tu ni kubeba dhamana ya maisha na ustawi wa wananchi.
Tunahitaji kubadilisha namna tunavyoitazama kazi yetu.
Uzalendo wa kweli haupimwi kwa maneno mengi bali kwa namna unavyotekeleza wajibu wako.
Kama wewe ni daktari muuguzi mtumishi wa mapokezi mtoa dawa au kiongozi wa taasisi ya afya sehemu ya uzalendo wako inaonekana kwenye namna unavyomthamini mwananchi.
Usimchelewesha bila sababu Usimdhalilishe Usimpuuze Usimfanye ajisikie kama anaomba favor.
Kwa sababu huyo mwananchi ndiye sababu ya wewe kuwepo katika nafasi hiyo.
Kuna tofauti kubwa kati ya kufanya kazi na kutumikia taifa.
Mtu anaweza kufika kazini kila siku lakini asiwe anatimiza wajibu wake kwa moyo.
Anaweza kusaini mahudhurio lakini huduma zikabaki duni.
Anaweza kuwa na cheo lakini asiwe na uwajibikaji.
Taifa halijengwi na viongozi wa juu pekee.
Taifa linajengwa na kila mtu anayetekeleza wajibu wake kwa uaminifu katika nafasi aliyopo.
Ndiyo maana wakati mwingine tunapaswa kuacha kulaumu uongozi wa juu kwa kila tatizo na kuanza kuangalia Je sisi tuliopo kwenye mstari wa utekelezaji tunatimiza wajibu wetu?
✍️Haiwezekani Rais na Serikali yake wapambane kutafuta fedha kujenga miundombinu kupeleka vifaa na kuboresha mazingira ya kazi halafu baadhi yetu tunageuka kuwa kikwazo cha wananchi kupata matokeo ya juhudi hizo.
Hii si haki kwa wananchi
Si haki kwa Serikali Wala si haki kwa taifa.
Watumishi wa umma tunapaswa kuelewa kuwa kila tunapofanya uzembe tunatoa nafasi kwa wananchi kupoteza imani na mfumo mzima.
Kila tunaposhindwa kuwajibika tunaharibu hata kazi nzuri inayofanywa mahali pengine.
Tunahitaji uwajibikaji wa kweli.
Tunahitaji viongozi wasimamie watumishi wao kwa haki na uthabiti.
Tunahitaji watumishi wazuri watambuliwe na kutiwa moyo.
Lakini pale ambapo kuna uzembe wa makusudi kutowajibika au tabia zinazowaumiza wananchi hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na taratibu.
Uzalendo hauwezi kuwa mzigo wa Rais na viongozi wa juu pekee .
Kila mmoja wetu ana sehemu yake.
Kuanzia ofisi ndogo kabisa kituo cha afya hospitali shule na taasisi nyingine za ummahapo ndipo mwananchi hukutana moja kwa moja na Serikali yake.
Sisi watumishi ndiyo sura ya Serikali mbele ya wananchi.
Tukiwa wema wenye heshima na uwajibikaj wananchi wataiona Serikali yenye kujali.
Tukiwa wazembe wenye dharau na wasiowajibika wananchi wataona Serikali kupitia makosa yetu.
Kwa hiyo kabla hatujasema “Serikali imefanya nini?” tujiulize pia
MIMI NILIYEPEWA DHAMANA NIMEFANYA NINI?
JE NIMEKUWA SEHEMU YA SULUHISHO AU SEHEMU YA TATIZO?
JE NINASAIDIA KUJENGA IMANI YA WANANCHI KWA SERIKALI AU NINAIHARIBU KWA MATENDO YANGU?
Rais anaweza kuonyesha njia.
Serikali inaweza kuweka sera na kuleta rasilimali
Lakini mafanikio ya taifa yanategemea mikono ya wale wanaotekeleza majukumu hayo kila siku usiku na mchana.