Orodha ya Watumishi wenye vyeti vya Kughushi...

Orodha ya Watumishi wenye vyeti vya Kughushi...

Binafsi nilivyo hua naamini katika kila mtu kupata haki yake kwa kadri inavyostahili.
Kama ulifoji cheti, kufanya kazi kwa miaka 25 hakufanyi kile cheti kiwe halisi. Kwa sababu hata kuipata hiyo kazi ya miaka 25 ulitumia cheti feki.

Kinachoniacha hoi ni maamuzi ya wizara ya kuamua kua hiko kikombe kiwapate baadhi ya watumishi huku wengine wakisemwa kua siyo watumishi.
Ni shida.
 
ishu sio kumaliza mbele yako o level..je kama alikula zero cheti alikitoa wapi..na what if kafoji cha form six?
Si hivyo tu kuna baadhi vyeti ni halali kabisa isipokuwa matokeo ameyachezea
Mfano kama
Civics alikuwa na D then akagushi somo moja kwenye cheti chake yaani akabadilisha
Ikasomeka CIVICS B
Tayali cheti kimeshaharibika hivyo
Umegushi cheti
Bila shaka hao mnaowatetea kwa kuwajua na kwa kusoma nao huenda wamefanya mchezo huo
Huko nako ni kugushi cheti
 
View attachment 502470
Watumishi wa umma wapo 570,000, kwa nini wakaguliwe 400,035 hawa wengine waachwe? tuna taka orodha ya JWTZ, Polisi, JKT na Magereza.
Huko kwenye majeshi nusu yao wana vyeti siyo vyao na ndio maana malaika kafanya double standard katika hili, na huko kwa wanasiasa ni balaa tu. JPM zoezi hili la uhakiki wa vyeti feki limekosa uhalali kwa wengine kuwapendelea
 
Dah,kwa ofisi yetu wameondoka watu watatu..very sad
 
Hivi watapata stahiki zao kama pensheni na malupu lupu mengineyo..maana unakuta kuna mtu alikuwa na pension ya ya milion 100 nikusema itaota mbawa..mwenye ufahamu atufahamishe
 
Mambo zenu wanaJF.

Zimwi la vyeti fake ndo habari ya mujini mujini Dsm na duniani kote. Hapa Dsm, ukipanda daladala au ukienda bar ,swala la vyeti fake limegusa familia nyingi sana hapa nchini.

Kuna ambao wameona watoto wao, ndugu zao, rafiki zao, waume/wake zao, wazazi wao nk na sasa habari imeshavuja.
Sasa basi, tutegemee maofisi kupwaya watu siku za karibuni. Na pia watu kubaki majumbani kulea watoto na vijukuu.

Umejisikiaje baada ya kuona mtu unayemfahamu kwenye orodha ya watumishi hewa?

Binafsi sijaona mtu ninayemfahamu.


Baada ya wiki mbili Kamba za katani zitakosekana madukani maana nishaona watu wanazinunua kwa wingi na tetesi zinasema kwamba wengi watajitundika vitanzi kuondokana na haibu.
 
RAS ina maana REGIONAL ADMINSTRATIVE SECRETARY yani watumishi walio chini ya Katibu Mkuu wa Mkoa
 
Hivi watapata stahiki zao kama pensheni na malupu lupu mengineyo..maana unakuta kuna mtu alikuwa na pension ya ya milion 100 nikusema itaota mbawa..mwenye ufahamu atufahamishe


Mwizi/kibaka ana haki mkuu? Haki yao wale ni kupelekwa mahakamani kusomewa mashitaka na kuswekwa tu, hakuna Zaidi ya hapo. Magufuli ndiyo rais asikudanganye mtu.
 
Serikali haiwezi kuingia gharama kuajiri wazee kama wewe...miaka mitano huna ajira na bado unasubiri ajira,si ndo ninyi mkiajiriwa mnashinda kupiga umbeya ofisini???
utakuwa na vyeti feki
 
Nacho omba n msaada nn cha kufanya au nianze na hatua IPI maana kwel nmeonewa hata nlio soma nao wanapga simu hawaamin wanacho kiona.
 
Kuna mtu nimesoma nae olevel ameonewa alimaliza mwaka mmoja mbele yangu yaani roho inaniuma sana Nina uhakika hajafoji sijui namsaidiaje?
Wewe umsaidie yeye hawezi? Kwamba wewe una unauhakika na uchungu kuliko mwenyewe?
 
Kuna wengine kunaa makosa ya logistics tu,kwa mfano kuna dad namfahamu amefanya mtihani kidto cha pili mara mbili,na kisha kufaulu na kwenda kusoma...six,kisha chuo..lakini alichkosea ni majina ya mwisho kwenye acount ya mshahara kutofautina nayaliyopo kwenye cheti si nae yumoooo...daaa lkn cheti sio cha kugushi maskiiiiniiiiii
Acha uongo wewe mbona wengi sana majina ya akaunti zao wamekosea ila sio fake? Huyo lazima kuna cheti amechakachua
 
ishu sio kumaliza mbele yako o level..je kama alikula zero cheti alikitoa wapi..na what if kafoji cha form six?
Ni kweli..wapo waliobadili matokeo badala ya kuwa na four cheti kinaonekana ana division three
 
Mambo zenu wanaJF.

Zimwi la vyeti fake ndo habari ya mujini mujini Dsm na duniani kote. Hapa Dsm, ukipanda daladala au ukienda bar ,swala la vyeti fake limegusa familia nyingi sana hapa nchini.

Kuna ambao wameona watoto wao, ndugu zao, rafiki zao, waume/wake zao, wazazi wao nk na sasa habari imeshavuja.
Sasa basi, tutegemee maofisi kupwaya watu siku za karibuni. Na pia watu kubaki majumbani kulea watoto na vijukuu.

Umejisikiaje baada ya kuona mtu unayemfahamu kwenye orodha ya watumishi hewa?

Binafsi sijaona mtu ninayemfahamu.
Watumishi hewa na Watumishi wenye Vyeti feki ni viwili tofauti
 
Katika orodha ya majina ya walioghushi vyeti iliyowekwa, ingewekwa pia na aina ya cheti kilichoghushiwa kama ni kidato cha nne, sita, degree, master ama PhD.
Kuna watu wana PhD feki kabisa yawezekana majina yao yapo kwenye orodha kutokana na kuwa na PhD feki lakini haijabainishwa kama ufeki wa vyeti vyake ni PhD yake!
...Mamlaka iliyotia hayo majina iongezee na aina ya cheti kilichoghushiwa!
 
~~~>>>Kuwa mpinzani sio kupinga kila kitu.... Mengine jarbuni kutumia akili zenu...

~~>>>Vijana wa Chadema badala ya kupanua akili nyie mnapanua vidole.. Mwisho mtapanua na makalio....
 
Back
Top Bottom