Mambo zenu wanaJF.
Zimwi la vyeti fake ndo habari ya mujini mujini Dsm na duniani kote. Hapa Dsm, ukipanda daladala au ukienda bar ,swala la vyeti fake limegusa familia nyingi sana hapa nchini.
Kuna ambao wameona watoto wao, ndugu zao, rafiki zao, waume/wake zao, wazazi wao nk na sasa habari imeshavuja.
Sasa basi, tutegemee maofisi kupwaya watu siku za karibuni. Na pia watu kubaki majumbani kulea watoto na vijukuu.
Umejisikiaje baada ya kuona mtu unayemfahamu kwenye orodha ya watumishi hewa?
Binafsi sijaona mtu ninayemfahamu.