Orodha ya Watumishi wenye vyeti vya Kughushi...

Orodha ya Watumishi wenye vyeti vya Kughushi...

Utakapojua mmoja wa waanga ni mama yako au baba yako sijui utasemaje ..
Dogo wazazi wangu walistaafu utumishi wa umma back miaka ya 90 mwanzoni na sina ndugu mbabaishaji kwenye elimu alitaka kufanya hivyo mdogo wangu 2001 baada ya several attempts za CSEE tulimkanya vibaya lakini baada ya kurudia mara 4 alipasua na yupo Kilimo Uyole pale anakula mshahara,forgery ni mwiko na kama wewe ni muumini hakuna dini inaruhusu huo uhuni wa kufoji wakati wenzio wanasotea hicho cheti.Tuache uhuni kwenye mambo ya msingi, hawa ndo wale wanawaandikia wagonjwa dozi sumu.Bad.
 
Mbona nimeona pale manyara kunamwasibu kabisa kasombwa usiangalie mkoa mmoja ukatoa hitimisho.
 
Hii ndiyo orodha ya watumishi 9000 ya watumishi wenye vyeti feki. Je ni sahihi kuwafukuza kazi ukizingatia mchango walioutoa kwa miaka hiyo waliyoitimikia serikali? Hakuna njia nyingine yoyote inayoweza kufanywa bila kuwafukuza?

Karibuni wadau.
Tuwekee naya serikali kuu, BTW kunaorodha nyingine nimeona mwalimu wangu wa chuo kikuu yumo , ngoja nikae kimya
 
aliyesoma kweli ndo apate ajira hawa wengine wote ni makanjanja wamesababisha wengine kukosa ajira acha watumbuliwe ,vyeo vingine ni vya kisiasa na inafamika toka zamani sema cc watz tulio wengi c wafualiaji wa mambo nani asiyejua kuwa mkuu wa mkoa/wilaya ,wazri,mbunge nk inatakiwa tu ajue kusoma na kuandika tu,
 
Baada ya Rais Magufuli kusema majina ya watumishi walioghushi vyeti yaanikwe; sasa yamewekwa hadharani.

Orodha ni hii hapa
mkuu vipi orodha ya wale tulio pewa muda hadi tarehe 15 Mei kuwasiliaha vile ambavyo hatukuviwasilisha
 
Pongeza basi hata kwa juhudi zilizofanyika basi aseee.....umenikumbusha usemi mmoja kua Watu hata wakikuona unaogelea watasema unawatimulia vumbi.
Mkuu ni kitu kizuri ila kisingebagua...
 
Ngoja nisubiri kesho udaku zaidi, tutawajua tu
Wakuu habarini za majukumu.

Nimefatilia baadhi ya watu wengi walio na vyeti feki ni walinzi, madereva, wahudumu wa masjala, ma typist, na wafagiaji. Watu hawa wengi kazi zao hazihitaji elimu ukifananisha na kama ilivyo kwa walimu, sekta Afya na zingine zenye mfanano wa hivyo.

Kwa nini isiwepo exemptions kwa walinzi, wahudumu wa huduma zote, kwani tayari kazi zao zinafanyika tu kwa uzoefu, na ndizo zinahitaji zaidi kujua kusoma na kuandika ukifananisha na viongozi wa kisiasa kwenye serikali ambao wana mishahara mikubwa.

Mishahara ya hawa wahudumu kwa ujumla ni midogo sana, mfano kwenye mshahara wa RC au DC kwa mwezi hawa wahudumu wanaingia kuanzia 15 @ kila mhudumu wastani wa Tsh. 250,000/=

Mbona hawa maboss wenyewe kama Wakurugenzi, wakuu wa Idara na vitengo ni kweli wote wana vyeti halisi? Hakuna mtu aliefoji kweli? Mbona mi kuna fulani na fulani nawajua, lakini hawapo kwenye list.
 
Back
Top Bottom