Orodha ya Watumishi wenye vyeti vya Kughushi...

Orodha ya Watumishi wenye vyeti vya Kughushi...

Kwa walioonewa hata mimi nawahurumia,Ila wale watumishi hewa wakaanze maisha kama yale waliokuwa wanatunyanyasa sisi tuliokuwa tunahangaika na vyeti vyetu.
 
Huko kwenye majeshi nusu yao wana vyeti siyo vyao na ndio maana malaika kafanya double standard katika hili, na huko kwa wanasiasa ni balaa tu. JPM zoezi hili la uhakiki wa vyeti feki limekosa uhalali kwa wengine kuwapendelea
Nimieona orodha wengine walishastafuu kitambo.
 
Kiswahili kikae vizuri hao hatuwezi kuita watumishi hewa, labda tuseme watumishi wasio na sifa kitaaluma! Lakini ni vyema pia kila mmoja akacheki jina lake usije kuwa unaangalia kama fulani yumo ama hayumo kumbe nawe umo, waliofanya kazi hiyo ni binadamu.
Mtumishi hewa yeye sifa yake ni ipi mkuu?
 
Tafadhali waziri utakapowatangaza wahusika wa vyeti feki gazetini tuwekee na picha zao.Hii itasaidia kupunguza utapeli mtaani, ahsante!
 
Tafadhali waziri utakapowatangaza wahusika wa vyeti feki gazetini tuwekee na picha zao.Hii itasaidia kupunguza utapeli mtaani, ahsante!
acha roho mbaya kama ya shetani, ufe na ushetani wako, ufeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Msichanganye mambo.Iko hivi mwengine O level au A level wamesoma ila sifa za kuingilia vyuo walikuwa hawana.Wamefanya magumashi ya short cut ili kupata professional ya kitu.Hivyo kusoma naye sio hoja ya msingi sana kwani sio kila uliyesoma naye alifika hapo ulipokutana naye kihalali.Kwani Bashite UD amesoma na wangapi?
 
Mi kuna Dada mmoja tumefahamiana ni afisa kilimo wilaya Fulani Ana level ya diploma alikuwa anampenda sana magufuli anadai ndiyo kiongozi anayefaa kwa misimamo yake na wala hayumbishwi anafanya anachokiamini..Nilimwambia unampenda magu sababu hayajakupata yaliyowapata wanaomchukia nikamsihi utawala huu bora mtu ukanyamaza maana lolote linaweza kutokea.

Sasa jina lake limetoka kwenye list ya vyeti feki na mbaya zaidi yupo chuoni anajiendeleza sasa sijui ataendelea kumpenda hivyo hivyo .sijampigia hata simu naona aibu ntamwambia nn
 
Duh afu walikuwa wanasema watu wa dini flani hawajasoma lakini nikiangalia hyo orodha napatwa mshangao
 
Ni vyema na nafasi zao/cheo zingeliwekwa ili iwe rahisi kwa wadau/wananchi kufahamu kwa kuwa inaweza kuleta usumbufu katika utoaji huduma.
 
Binafsi nimeona jina langu,na sijawahi kufanya kazi serikalini wala kumpa mtu vyeti vyangu
Pia na mimi nimeliona langu huko butiama na sikuwahi kuajiriwa popote dah! Yani majina yangu yote kama yalivyo[emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Back
Top Bottom