Ombi kwa waishio marekani

Ombi kwa waishio marekani

Wanajf mnaoishi USA naomba maoni yenu.
Mie nipo TZ ila mke wangu anaishi US na nimefanikiwa viza ili nije nimjoin . Tatizo ni kuwa nimepata kazi ya prof bongo na nategemea mshahara wa kama 3million, sasa nipeni maoni yenu kama ni ww ungechagua kazi au kwenda US.
Nmeishi Euro kama miaka sita hivi nimerudi recently baada ya kuchoka, hivyo najua nn kitatokea nkienda US. Wife kazi zake ni hizo hizo wanazofanya wageni na mara nyingi analalamika kuchoka kwani analala hm nights 3 tu siku zingine ni kazi 24 hrs.
Naomba maono yenu esp kutoka kwa watu waliotoka bongo miaka au siku za karibuni.
Ahsante
Wewe njoo huku tupige box bana. Bila risk huwezi kufanikiwa katika dunia ya leo, kwani Tsh 3M nini bana. Ila ukae ukijua huku hakuna misheni town wala town kisomo~kila mtu anaishi kwa jasho lake. Welcome to the land of opportunity brother!.
 
Kati ya ushauri uliopewa umeambiwa uangalie na umri wako ikiwa utaaamua kutimkia huko. Inavyoonesha upo juu ya 30. Binafsi sikushauri.
Maisha ughaibuni ni magumu sana. Utakuwa unafanyakazi klipa madeni tu, miaka inaenda. Tahamaki umekuwa mzee, ngvu zimeisha, hela huna, majuu hakukaliki nyumbani hakurudiki. Kwa kuwa umeshakaa Europe sin ahaja ya kukuhadithia, umeshayaona. Hakuna maisha bali utumwa. Mwambie Lady afunge virago arejee bongo. Kama utaenda wewe nenda kwa matembezi kucheki ustaarabu.

Katikati ya miaka ya 90 mdogo wangu alitaka kupoteza kama milioni 10 kuja Europe, bila ya kujua kama atarejeshwa, kama atapata kazi au vipi. Nikamshauri hiyo hela aitumie kwa kufanya biashara hata ya mkaa. Alikubali, akanunua Landrover 2º hand akawa anapiga mzigo kuleta bidhaa mjini. Sasa anajiendesha vyema. Ukweli ni kuwa hata adui yangu simshauri aende ughaibuni ikiwa hana profession kati ya zilizotajwa. Bakia Bongo Mkuu.
 
Nadhani umetumia muda mwingi sana kunielimisha mimi kuhusu europe, bahati mbaya usichokijuwa mimi katika shenghen countries sijafika Norway, Belgium, luxernborg na France tu. na sikuwahi kupiga box mtoni, all was vacasion trips. na hapa ninapotambaa na keybord nina mailage za kutosha za kusafiri bure kwenye kadi yangu ya swiss air.

Ngoja waanze ku-Gaddafi Tanzania.
 
mhh nnavyotamani kwenda majuu,sina tu wa kunialika japo nkatembee wiki ntagharamia mwenyewe kila kitu:rain:

Shosti, believe you me ................................you are not missing anything! I remember when I was young, nilikuwa nawachefua wazazi na habari za majuu, to an extent that one day mazee was like "find pple to adopt", but after going there hata sikuna kikubwa ni nini!
 
jamani ...! kupiga box maana yake nini .... ? samahani kwa usumbufu
 
Massai boy,
Hali uliyonayo ni mtihani mkubwa kwako na familia yako. Naomba nikupe ushuhuda wa true life experience yangu ili yasikukute yaliyonikuta.

Mimi na wife tulioana bongo tukabahatika kupata watoto wawili (boy & girl). Wote tulikuwa na kazi zetu za vipato vya wastani na tulimanage life ya bongo.

Tulihamia UK kujaribu maisha. Kusema ukweli japo tulimake money lakini tulikuwa kama watumwa!. Hata nafasi ya kuifurahia ndoa ilikuwa issue!.

Wife akapata shule US , Tukarudi Bongo tukaprocess US visa tukahamia US (Maryland). Kwa vile yeye ndio alikuwa na shule, yeye ndie alipata kazi, mimi nikageuka yaya na mume wa nyumbani!, Hivyo ukimjoin wife jiandae kwa lolote hata ikibidi kujikuta wewe ndio ushinda nyumbani na watoto!.

Maisha hayo yanishinda hivyo tukakubaliana na wife, yeye abaki US na mimi nirudi bongo na watoto akimaliza shule atapata kazi nzuri tutamjoin na kuendeleza familia.

Nilifungasha na kujirudia bongo na watoto na yeye alibaki US. Huku bongo mimi nilipata kazi ile ile mahali pengine na life iliendekea huku yeye akituma fedha za maendeleo.

Unfortunately long distance relationship doesn't work well with damu moto, both sides!. hivyo baada ya miaka miwili nilimvisit wife, niliyo yasikia kuhusu yeye niliyasikia na yeye pia aliyasiki ya kuhusu mimi. Nilimvisit tena baada ya miaka miwili mingine by then shule kamaliza na kazi nzuri kapata, ila kilichofuata ni historia tuu!. Tulishindwana kila mtu kivyake at the expense of our family in search of greener pasture. We now just good friends yeye akiendelea na maisha yake US nami nikiishi Bongo!.

Hiyo kabla hujapoteza kazi yako nzuri bongo, jiulize priority zenu za maisha for now ni nini. Kama ni kujenga familia based on love na malezi ya baba na mama kwa watoto wenu, sucrifice everything, join your wife mjenge familia mkiwa pamoja!.

Kama lengo lenu ni ku make money hiyo M. 3 kwa mwezi kwa bongo is not nothing!, CRDB unakopesheka mara 36 na kulipa deni ndani ya 72 instalments!. Hivyo hapo ulipo unaweza kuchukua mkopo wa M.100 plus na kufanyia maendeleo hapa hapa bongo huku wife naye akituma mchango wake huku mkitembeleana mwaka hadi mwaka.

Uamuzi wa busara ni wewe na mkeo muongee kwa kina what do you really need out of your lives huku ukisikiliza 'listern to your heart'. The voices within itakuambia the right thing to do. Maisha sio pesa, kazi nzuri, nyumba nzuri na gari zuri la kutembelea. Its more than that, don't rush to decide something now ukaishia to regret for the rest of your lives!.
 
Pasco kama hutajali naomba nieleweshe maana ya......watoto wawili (boy &girl)......asante
 
Mie nipo bongo na nimepata viza ya kumjoin wife US, ila pia nimepata kazi ya prof na malipo ni kama 3mil.
Hivyo naombeni ushauri wenu kama nije US au nipige job bongo, ningependa kusikia kutoka kwa watu waliokuwa bongo recently.
Nimekaa Euro mpaka karibuni hivyo najua mikiki ya life na wife kazi zake ni hizo hizo za wahamiaji.

Masssaiboi: Mimi nafanya kazi Marekani na pia nipo na familia huku, maisha si rahisi kama unavyofikiria. Mshahara wa M3 bongo ni bora sana na unaweza kusave. Mimi hapa niko mguu mmoja ndani mmoja nje namalizia MBA ikiisha na nikiweza kupata kazi nyumbani naludi mjomba.. Huwa nawaza kama nitapata kazi ya hata 2.5m kwa mwezi naludi zangu bongo kabisa bila kugeuka. Pesa siyo kila kitu huku. Na pia najua wazi wife atakubaliana na ww ubaki bongo kuliko kuja huku. Fanya kazi ya bongo na uwe unakuja kumtambelea. Kama inawezekana na mama ameenda shule shule mtafutie kazi Tanzania mkichanganya mishahara yenu maisha yenu yatakuwa bomba. Unaweza kuni PM kama utahitaji maelezo ya ziada.
 
Kwanza unatakiwa uwe na malengo! ni nini kilichompeleka mkeo Merekani wakati wewe unaishi Tanzania?

Kama ni ujana na ma-adventure, ntakuelewa.

Maisha ya Merekani ni tofauti na maisha ya kwetu. Unaweza ukapata kazi ukalipwa vizuri, lakini, Jee, fedha ndio kila kitu?

Hivi mkeo kuwa mbali nawe kwa sababu tu za kipato! huoni kuwa hapo kuna tatizo, anaweza akabamizwa huko na wewe ukabamiza huku! hapo kuna faida?

Kuna rafiki yangu, alimpeleka mkewe mkewe kutafuta maisha kama miaka kumi iliyopita, bahati nzuri au mbaya, yule dada sasa ana watoto wawili, wa nje ya ndoa.

Kuna sababu maalumu za kumpeleka mtu nje ya kwao. Kama kusoma au matibabu na hata maisha lakini, utazame maisha yako ya sasa na unategemea yepi huko uendako?

Kuna dada mmoja namjuwa alikwenda Merekani, kama miaka mitatu sasa, lakini huyu alikwenda na malengo. Aliondoka hapa ni muathirika wa HIV, kenda kule sasa anapata tiba namba moja. Wanawajali sana wenye maambukizi, matibabu ni first class kwa wenye virusi. Huyu halaumiki kwa kwenda huko. Si unajuwa hapa tunavyo nyanyapaa wagonjwa?

Kama unaenda popote pale, uwe na malengo! la sivyo, mrudishe mkeo muhangaike hapa bongo yetu, bado kuna opportunities nyingi sana. Usiwasikilize Chadema, watakupoteza.
 
Jamani nina rafiki yangu yuko kwenye serious relationship na hubby wake to be anaishi na kupiga box warehouse marekani. Kama ilivyosituation ya Mmasai kwenye thread hii, mdada huyu ni senior lecturer ktk university, bado kama two to three years awe Prof.

Mchumba wa binti anamshauri bint aache kazi amfuate mumewe huko no-mans'-land. Mdada's age ni 37. Mkaka ni 42 na anasema hawezi kumanage long distance relationship, ila mke anataka na anahesitate atachekwa akirudi bongo kumfuata mke. Bint na eanataka vyote mume na career.

Je the very same ushauri mnampa kaka mmasai hapa unaaply kwa mdada pia?
 
mkuu hii imekujaje kujaje tena hapa?.......ameomba ushauri kuhusu Chadema au kuhusu wanaoishi Marekani?

Siasa ndio zinatuongoza ama kwenye maamuzi mazuri ama kwenye maamuzi mabovu, na ndio kwa sasa zinachukuwa misingi muhimu ya maamuzi yetu. Kwa hiyo ni ushauri wa bure, Chadema watampoteza akiwasikiliza ushauri wao. Si unaona jinsi wanavyo danganya hovyo wananchi na wengi kwa matatizo waliyokuwa nayo huwasikiliza kama misukule. Badala ya kuwahamasisha wafanye kazi kwa bidii, wao wanawadanganya kuwa tukiitowa CCM madarakani sisi tutawapa mnachokitaka! Duhh, halafu kwa nini nisimshauri asiwasikilizw ushauri wao?
 
Siasa ndio zinatuongoza ama kwenye maamuzi mazuri ama kwenye maamuzi mabovu, na ndio kwa sasa zinachukuwa misingi muhimu ya maamuzi yetu. Kwa hiyo ni ushauri wa bure, Chadema watampoteza akiwasikiliza ushauri wao. Si unaona jinsi wanavyo danganya hovyo wananchi na wengi kwa matatizo waliyokuwa nayo huwasikiliza kama misukule. Badala ya kuwahamasisha wafanye kazi kwa bidii, wao wanawadanganya kuwa tukiitowa CCM madarakani sisi tutawapa mnachokitaka! Duhh, halafu kwa nini nisimshauri asiwasikilizw ushauri wao?

na kama massaiboi anafuata sera muozo za CCM akaona hazimfai.....amechoka na ufisadi wao na wizi....utamshauri nini?
 
Shosti, believe you me ................................you are not missing anything! I remember when I was young, nilikuwa nawachefua wazazi na habari za majuu, to an extent that one day mazee was like "find pple to adopt", but after going there hata sikuna kikubwa ni nini!

mhh kweli au unanitania,nnavyotamani sijui kwanini au kuchoka tu na kero za ccm na magiza:wink2:
 
i really doubt kama kweli umekaa euro zone kwa miaka 6, swali lako ni kama mtu ambaye amekaa bongo mda wote
 
i really doubt kama kweli umekaa euro zone kwa miaka 6, swali lako ni kama mtu ambaye amekaa bongo mda wote

umemshtukia eeh............

Well, massaiboi.......nyumbani ni nyumbani.....its always the best kuwa nyumbani na kuwa na kipato cha uhakika kitakacho kuwezesha kuanzisha miradi yako..........
Kuhusu maisha........binafsi naamini........maisha ni popote pale ulimwenguni (wengine tumeishi Sudan na hata Afghanistan)........ili mradi unachanga karata zako vizuri kama unavyoshauriwa hapo juu na wanaJF.......pia inategemea sana na juhudi zako za ku-create aina ya miradi itakayokuondoa ktk akili ya KUAJIRIWA............
 
Ndg, mie ni mtu mzima na nimewahi kuishi hizo nchi zilizoendelea zaidi ya miaka 15, nikaamua kurudi home.

1. Hizo nchi zina frustrate sana hata km una career yako utaratibu wa kuingia ktk system ni mgumu sana.
2. Km mkeo nafanya kazi za kawaida tu bora wewe ujijenge hapa bongo utafanikiwa kuliko kuenda kufanya hizo kazi za kawaida tu, of course utapata pesa nyingi, ila hautakuwa na raha nazo, kodi kubwa na life is very expensive asikudanganye mtu.
Utapokea pesa nyingi lakini yote inarudi serikalini kwa kodi za kufa mtu.

Hapa bongo kwa mshahara uliotaja si mbaya sana na ukijishughulisha zaidi utapata zaidi ya hizo.

ushauri wangu, Ungetulia hapa achana na ndoto za ulaya kabisa zitakuharibia future, maana ukizeeka utatamani urudi bongo kuliko kukaa nyumba za wazee ulaya na itakuwa too late.

Jijenge hapa bongo na umrudishe mkeo maana ukienda ulaya huna pesa unaweza kukuta mambo magumu na kuna jamaa wa pesa huko wataweza hata kumrubuni mkeo mkakosana.

East and West Home is Best!
 
Hivi Tanzania hakuna frustration za maisha? Hivi Tanzania maisha ni rahisi zaidi kuliko nchi zilizoendelea?
 
Dunina Mwalimu
Nchi ya marekani ni nchi ngumu sana kuliko zote duniani kwa masuala ya visa vya familia, ndo unaona watu wanaishi miaka nenda rudi wakati familia zao ziko walikotoka.
Ukitaka kwenda Marekani kwa maisha we nenda tu, lakini kama waenda kwa masuala ya kiuchumi jaribu kuwa na malengo ya muda mfupi na hivyo utakamia na kubana matumizi ili urudi kujijenga bongo vinginevyo utakachochuma utawarudishia wenyewe.

Kwa wajanja wanapiga box kwa miaka kama 11-12 hivi na hapo social security imekamilika na anarudi bongo kwani atakapofikia umri wa miaka 62 ana uhakika wa pensheni ya $$$ kwa bongo inalipa kama umepata uraia utapaswa uingie Marekani kila miaka 5, lakini kama huna uraia utatakiwa uwe unaingia marekani mara 2 kwa mwaka, kitu ambacho ni usumbufu.

Ajira ni ngumu sana kama utapendelea kuishi katika miji mikubwa kwa sababu ya impact of demand and supply. Miji midogo demand ya employment inaridhisha kuliko miji mikubwa. Miji midogo tatizo huduma nyingi hasa usafiri ni kujitegemea. Ajira nyingi kwa siku hizi zinawapa nafasi zaidi vijana, kama umri wako ni zaidi ya 35 basi vema kama una kazi nzuri bongo, uwe unaitembelea tu familia yako Marekani.

Gharama ya maisha Marekani ni kubwa sana na kama ingekuwa hivyo Bongo tungewanyonga viongozi wa serikali. Ndio maana tunasema kwa wenye mtazamo wa kiuchumi bora kuwa na malengo ya muda mfupi utajikaza kubana matumizi na maraha ukafanye ukishasetirika bongo, vinginevyo ukiona ufaidi mazuri yote Marekani, itafikia wakati mahesabu ya tiketi ya kurudia bongo yanakatishatamaa na pengine hujaandaa mazingira ya kuishi bongo na pengine tofauti ya uliowaacha bongo na wewe uliyeko majuu itakukatisha tamaa uatamua kuzamia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom