Ombi kwa waishio marekani

Ombi kwa waishio marekani

Huku usije unaweza pata hata mil 10 lakini matumizi ni makubwa mno. Kwa bongo mil 3 ni nyingi mno, nakushauri mrudishe mkeo bongo. Huku usa vishawishi ni vingi na watu watambandua mkeo. Fimbo ya mbali haiui nyoka massaboi
 
Kwanza unatakiwa uwe na malengo! ni nini kilichompeleka mkeo Merekani wakati wewe unaishi Tanzania?

Kama ni ujana na ma-adventure, ntakuelewa.

Maisha ya Merekani ni tofauti na maisha ya kwetu. Unaweza ukapata kazi ukalipwa vizuri, lakini, Jee, fedha ndio kila kitu?

Hivi mkeo kuwa mbali nawe kwa sababu tu za kipato! huoni kuwa hapo kuna tatizo, anaweza akabamizwa huko na wewe ukabamiza huku! hapo kuna faida?

Kuna rafiki yangu, alimpeleka mkewe mkewe kutafuta maisha kama miaka kumi iliyopita, bahati nzuri au mbaya, yule dada sasa ana watoto wawili, wa nje ya ndoa.

Kuna sababu maalumu za kumpeleka mtu nje ya kwao. Kama kusoma au matibabu na hata maisha lakini, utazame maisha yako ya sasa na unategemea yepi huko uendako?

Kuna dada mmoja namjuwa alikwenda Merekani, kama miaka mitatu sasa, lakini huyu alikwenda na malengo. Aliondoka hapa ni muathirika wa HIV, kenda kule sasa anapata tiba namba moja. Wanawajali sana wenye maambukizi, matibabu ni first class kwa wenye virusi. Huyu halaumiki kwa kwenda huko. Si unajuwa hapa tunavyo nyanyapaa wagonjwa?

Kama unaenda popote pale, uwe na malengo! la sivyo, mrudishe mkeo muhangaike hapa bongo yetu, bado kuna opportunities nyingi sana. Usiwasikilize Chadema, watakupoteza.
Majimshindo, nimeguswa sana na hayo niliyo ya bold, its more or less na yaliyonikuta mimi binafsi, thanks God, nomore regret because we both managed to go on with our new lives!.
 
Pasco kama hutajali naomba nieleweshe maana ya......watoto wawili (boy & girl)......asante
Sorry Preta hayo ni mambo ya pre-formation za mobile. Nilimaanisha tulipata watoto wawili kwenye ndoa yetu, japo saa hizi tuna jumla ya watoto 8!.
 
Dunina Mwalimu
Nchi ya marekani ni nchi ngumu sana kuliko zote duniani kwa masuala ya visa vya familia, ndo unaona watu wanaishi miaka nenda rudi wakati familia zao ziko walikotoka.
Ukitaka kwenda Marekani kwa maisha we nenda tu, lakini kama waenda kwa masuala ya kiuchumi jaribu kuwa na malengo ya muda mfupi na hivyo utakamia na kubana matumizi ili urudi kujijenga bongo vinginevyo utakachochuma utawarudishia wenyewe.

Kwa wajanja wanapiga box kwa miaka kama 11-12 hivi na hapo social security imekamilika na anarudi bongo kwani atakapofikia umri wa miaka 62 ana uhakika wa pensheni ya $$$ kwa bongo inalipa kama umepata uraia utapaswa uingie Marekani kila miaka 5, lakini kama huna uraia utatakiwa uwe unaingia marekani mara 2 kwa mwaka, kitu ambacho ni usumbufu.

Ajira ni ngumu sana kama utapendelea kuishi katika miji mikubwa kwa sababu ya impact of demand and supply. Miji midogo demand ya employment inaridhisha kuliko miji mikubwa. Miji midogo tatizo huduma nyingi hasa usafiri ni kujitegemea. Ajira nyingi kwa siku hizi zinawapa nafasi zaidi vijana, kama umri wako ni zaidi ya 35 basi vema kama una kazi nzuri bongo, uwe unaitembelea tu familia yako Marekani.

Gharama ya maisha Marekani ni kubwa sana na kama ingekuwa hivyo Bongo tungewanyonga viongozi wa serikali. Ndio maana tunasema kwa wenye mtazamo wa kiuchumi bora kuwa na malengo ya muda mfupi utajikaza kubana matumizi na maraha ukafanye ukishasetirika bongo, vinginevyo ukiona ufaidi mazuri yote Marekani, itafikia wakati mahesabu ya tiketi ya kurudia bongo yanakatishatamaa na pengine hujaandaa mazingira ya kuishi bongo na pengine tofauti ya uliowaacha bongo na wewe uliyeko majuu itakukatisha tamaa uatamua kuzamia.

Umeshauriwa mengi ya kutosha sasa wewe unaamua vipi? Waacha kibarua bongo na kumfuata mkeo aliyeko Marekani ili nawe ukaanze kuhangaika kutafuta kazi au wabaki bongo na kumwita mkeo arudi kuungana nawe bongo?

Swali lingine ilikuwaje wewe uende Europe na Mkeo aende Marekani, kwa nini wote msingeenda bara moja?
 
Siasa ndio zinatuongoza ama kwenye maamuzi mazuri ama kwenye maamuzi mabovu, na ndio kwa sasa zinachukuwa misingi muhimu ya maamuzi yetu. Kwa hiyo ni ushauri wa bure, Chadema watampoteza akiwasikiliza ushauri wao. Si unaona jinsi wanavyo danganya hovyo wananchi na wengi kwa matatizo waliyokuwa nayo huwasikiliza kama misukule. Badala ya kuwahamasisha wafanye kazi kwa bidii, wao wanawadanganya kuwa tukiitowa CCM madarakani sisi tutawapa mnachokitaka! Duhh, halafu kwa nini nisimshauri asiwasikilizw ushauri wao?

Yaani hata ukiingiliwa kinyume na maumbile ni siasa hizo ndio zimekuelekeza huko? basi pole maana tunawajuwa vizuri mpaka wanaowaharibu.
 
naishi Arusha,mji mtamu sana ukiwa na mil 3 kila ukizungusha macho utakuwa unamwomba mungu asikuchukue mapema hata kama uko hoi kwa UKIMWI
 
kwa ushauri wangu ndugu yangu ingawa sipo USA ila nipo umangani huku karibia na jua.kama unapata mil3 kwa bongo nakushauri ubaki bongo ufanye kazi na uweke na vitega uchumi.Kwa 3m ni hela nzuri sana una uwezo wa kusave 2m kwa kila mwezi na ni hela nzuri hata ukiomba mkopo kama una business plan una uwezo wa kukopa mil 70.Kumfuata wife haina tija sina unaweza kwenda walau mara moja kila baada ya miezi 6.Kukaa USA ni vema pia ila kwenye nchi za watu mara nyingi matumizi ni makubwa na pia savings inakuwa ndogo.Chagua mwenyewe kwenda kuishi na wife ilihali ukirudi bongo huna hata cha maana.wazungu wajanja sana wanakulipa vizuri lakini wanahakikisha hela yote utaitumia kwao.Imagine unapokea $6000 kwa mwezi lakini unabakiza tu $500 hivi kwa mwezi kama savings.Mshahara wako wa bongo ni sawa na waziri ndugu yangu au majaji ww upo kwenye class ya juu kabisa sasa huko USA cha zaidi ni nn huko? labda uniambie utaenda kusoma lakini uwe umeshafanya kazi na upewe ruhusa ya kusoma na mwajiri wako ili ukimaliza urudi pale pale.


upo umangani, msalime mawarid
 
hahaaa hahaaa jamani!
post inasema "kwa waishio marekani"
dah kazi kweli...
 
Nadhani umetumia muda mwingi sana kunielimisha mimi kuhusu europe, bahati mbaya usichokijuwa mimi katika shenghen countries sijafika Norway, Belgium, luxernborg na France tu. na sikuwahi kupiga box mtoni, all was vacasion trips. na hapa ninapotambaa na keybord nina mailage za kutosha za kusafiri bure kwenye kadi yangu ya swiss air.

:wink2:
 
Wanajf mnaoishi USA naomba maoni yenu.
Mie nipo TZ ila mke wangu anaishi US na nimefanikiwa viza ili nije nimjoin . Tatizo ni kuwa nimepata kazi ya prof bongo na nategemea mshahara wa kama 3million, sasa nipeni maoni yenu kama ni ww ungechagua kazi au kwenda US.
Nmeishi Euro kama miaka sita hivi nimerudi recently baada ya kuchoka, hivyo najua nn kitatokea nkienda US. Wife kazi zake ni hizo hizo wanazofanya wageni na mara nyingi analalamika kuchoka kwani analala hm nights 3 tu siku zingine ni kazi 24 hrs.
Naomba maono yenu esp kutoka kwa watu waliotoka bongo miaka au siku za karibuni.
Ahsante

There is A BIG Difference between carer & JOB!...

JOB You can find anytime.. but if you have to choose between your carer & wife... F* It ii go after money! wife asubiri mambo yatakaa fresh..na kama huko states kazi yenyewe ni ya kubangaiza baki bongo.. life la mbelembele sometimes stress
 
Need I say more? Wenzangu wamemaliza yote!


. . . Uamuzi ni wako . . .
 
Umeshauriwa mengi ya kutosha sasa wewe unaamua vipi? Waacha kibarua bongo na kumfuata mkeo aliyeko Marekani ili nawe ukaanze kuhangaika kutafuta kazi au wabaki bongo na kumwita mkeo arudi kuungana nawe bongo?

Swali lingine ilikuwaje wewe uende Europe na Mkeo aende Marekani, kwa nini wote msingeenda bara moja?

Brother Candid Scope, kila siku nakukumbushaga "ukiwa muongo, basi hifadhi na kumbukumbu"
Sasa waona ulivyoyaboronga!
Ni Mchawi ama Malaika ndiyo awezae kukaa two continents at the same times!
Niko kitafsida zaidi ktk comments yangu! Hii kick si direct, ni indirect!
Na imani umenipata.
 
Last edited by a moderator:
Umeshauriwa mengi ya kutosha sasa wewe unaamua vipi? Waacha kibarua bongo na kumfuata mkeo aliyeko Marekani ili nawe ukaanze kuhangaika kutafuta kazi au wabaki bongo na kumwita mkeo arudi kuungana nawe bongo?

Swali lingine ilikuwaje wewe uende Europe na Mkeo aende Marekani, kwa nini wote msingeenda bara moja?

Brother Candid Scope, kila siku nakukumbushaga "ukiwa muongo, basi hifadhi na kumbukumbu"
Sasa waona ulivyoyaboronga!
Ni Mchawi ama Malaika ndiyo awezae kukaa two continents at the same times!
Niko kitafsida zaidi ktk comments yangu! Hii kick si direct, ni indirect!
Na imani umenipata.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom