Ombi kwa waishio marekani

masssaiboi

JF-Expert Member
Feb 10, 2009
636
132
Wanajf mnaoishi USA naomba maoni yenu.
Mie nipo TZ ila mke wangu anaishi US na nimefanikiwa viza ili nije nimjoin . Tatizo ni kuwa nimepata kazi ya prof bongo na nategemea mshahara wa kama 3million, sasa nipeni maoni yenu kama ni ww ungechagua kazi au kwenda US.
Nmeishi Euro kama miaka sita hivi nimerudi recently baada ya kuchoka, hivyo najua nn kitatokea nkienda US. Wife kazi zake ni hizo hizo wanazofanya wageni na mara nyingi analalamika kuchoka kwani analala hm nights 3 tu siku zingine ni kazi 24 hrs.
Naomba maono yenu esp kutoka kwa watu waliotoka bongo miaka au siku za karibuni.
Ahsante
 
Duh pole sana ndugu kwa kuwa njia panda. Uisache kazi yako ya sasa coz huwezi jua kama USA utapata kazi nzuri au la. Kukaa ugenini bila kazi utakuwa frustrated sana. Fanya hiyo kzi yako ya bongo then after 6 month omba ruhusa ucheki zali USA, ukipata kazi nzuri states, milion tatu za kibongo sio ishu.

NB:Kuzeekea ughaibuni siukushauri, kama umri umeenda bora ubaki bongo FANYA HIYO KAZI, kama wewe bado kijana then u may try usa.
 
Mie nipo bongo na nimepata viza ya kumjoin wife US, ila pia nimepata kazi ya prof na malipo ni kama 3mil.
Hivyo naombeni ushauri wenu kama nije US au nipige job bongo, ningependa kusikia kutoka kwa watu waliokuwa bongo recently.
Nimekaa Euro mpaka karibuni hivyo najua mikiki ya life na wife kazi zake ni hizo hizo za wahamiaji.
 
Huko USA umeshapata kazi au ndio utaenda kubangaiza? Anyway yote yanategemea na wewe unajali nini kati ya career, familia, uzalendo kwa nchi yako, na mengine mengi.
 
Mkuu.
Wife akiiona hii msg basi atakupiga red card au atauwasha moto. Au una uhakika sio member hapa JF?
Vizuri ungeshauriana na yeye na mukakubaliana. Wife anaweza kuwa mshauri mzuri tu.

Priority yako au yenu wewe na wife ni nini?
Halafu, long distance relationship ni mtihani mkuu.
 
Huko USA umeshapata kazi au ndio utaenda kubangaiza? Anyway yote yanategemea na wewe unajali nini kati ya career, familia, uzalendo kwa nchi yako, na mengine mengi.

Kazi ni mpaka nifike ndio nitafute na priority kwangu ni kazi kwani bila job hata familia inasambaratika.
 
mkuu

Hapa umejipa jibu mwenyewe sasa unatafuta ushauri gani tena?
Kama wife ukimwelewesha hilo basi hatatia ngumu. Lakini kuna haki za mke na mume hayo jee umeyafikiria?

Ndio niliposema kuwa long distance relationships ni mtihani mgumu.
 
Duuh mi natamani hata hiyo ya mil 3 nakosa wewe unataka uikache!!! Kama vp niunganishe na hoyo prof. Ni PM nijue kama naweza kuifanya. Samahani kwa kuchangia ingawa sipo USA, ila nimevutiwa na mshahara uliotaja. Tuwasiliane mkuu kama itawezekana.
 
sijui marekani kukoje,ila sikushauri uiache kazi yako ya milion 3 kwa box la marekani...no waay baki hapo hapo bongo.:decision:
 
Wanajf mnaoishi USA naomba maoni yenu.
Mie nipo TZ ila mke wangu anaishi US na nimefanikiwa viza ili nije nimjoin . Tatizo ni kuwa nimepata kazi ya prof bongo na nategemea mshahara wa kama 3million, sasa nipeni maoni yenu kama ni ww ungechagua kazi au kwenda US.
Nmeishi Euro kama miaka sita hivi nimerudi recently baada ya kuchoka, hivyo najua nn kitatokea nkienda US. Wife kazi zake ni hizo hizo wanazofanya wageni na mara nyingi analalamika kuchoka kwani analala hm nights 3 tu siku zingine ni kazi 24 hrs.
Naomba maono yenu esp kutoka kwa watu waliotoka bongo miaka au siku za karibuni.
Ahsante

Hapo kwenye RED hakuna nchi inayoitwa euro, pili inaonekana hauna plan na maisha yako mwenyewe sasa itakuwa vigumu mtu mwingine kukupa ushauri, tatu haujasema kama Marekani umeshapata kazi au ukifika ndio utafute kazi. ila ni kichaa tu peke yake ambaye anaweza akakuamini eti kwa msoto huu mtu ulipwe millioni tatu halafu uache kazi uende kuishi utumwani, i don't buy this story.
 
I Love JF! Nice Week end Buddy
 
Mimi napaona kwenye atlas tu ila nakushauri ufanye hiyo kazi hapa ujenge mazingira wife arudi.
Analalamika nini mtu anakwao bwana.
Tz hata kama huna kitu huwezi kulala nja.
 
Hapo kwenye RED hakuna nchi inayoitwa euro, pili inaonekana hauna plan na maisha yako mwenyewe sasa itakuwa vigumu mtu mwingine kukupa ushauri, tatu haujasema kama Marekani umeshapata kazi au ukifika ndio utafute kazi. ila ni kichaa tu peke yake ambaye anaweza akakuamini eti kwa msoto huu mtu ulipwe millioni tatu halafu uache kazi uende kuishi utumwani, i don't buy this story.

Euro is short 4 europe, sikutaka kuwa specific so as to hide my ID. Pia nimesema ndio tu nimepata visa so huwezi omba kazi mpaka uwe ndani ya US.
Ni case ya ukweli so if you dont trust just dont comment, na it was meant 4 US residents only
 
Nasisitiza hakuna nchi inaitwa europe, kutaja kama ulikuwa UK. Holand, German, Spain, France n.k hakuwezi kukutambulisha ki namna yeyote ile sababu ni Watanzania wengi sana wameishi na wanaendelea kuishi kwenye nchi hizo. na kama unataka mawazo ya watanzania waliopo U.S,A labda ungeomba tukupe blogu zao, humu JF hawaingii watu wajingajinga.
 
Nasisitiza hakuna nchi inaitwa europe, kutaja kama ulikuwa UK. Holand, German, Spain, France n.k hakuwezi kukutambulisha ki namna yeyote ili sababu ni Watanzania wengi sana wameishi na wanaendelea kuishi kwenye nchi hizo. na kama unataka mawazo ya watanzania waliopo U.S,A labda ungeomba tukupe blogu zao, humu JF hawaingii watu wajingajinga.

Mkuu jamaa leo unaye!
 
Mzee nakushauri usiache kazi ya hako kamshara Bongo cozi hapa u may make more than that for nothing! Mimi binafsi hata nikiapa kazi Bongo ya m1.5 narudi nyumbani maisha hapa ni mzigo mbaya sana!!!!!!!!!!
 
Nasisitiza hakuna nchi inaitwa europe, kutaja kama ulikuwa UK. Holand, German, Spain, France n.k hakuwezi kukutambulisha ki namna yeyote ile sababu ni Watanzania wengi sana wameishi na wanaendelea kuishi kwenye nchi hizo. na kama unataka mawazo ya watanzania waliopo U.S,A labda ungeomba tukupe blogu zao, humu JF hawaingii watu wajingajinga.

VP walikubania visa nn!!!???
Nipe blogs basi
 
Nasisitiza hakuna nchi inaitwa europe, kutaja kama ulikuwa UK. Holand, German, Spain, France n.k hakuwezi kukutambulisha ki namna yeyote ile sababu ni Watanzania wengi sana wameishi na wanaendelea kuishi kwenye nchi hizo. na kama unataka mawazo ya watanzania waliopo U.S,A labda ungeomba tukupe blogu zao, humu JF hawaingii watu wajingajinga.

Matola bana muwie radhi mwenzio hajasema nchi ya Euro rudi usome vizuri bana acha kumsumbua ni vizuri ukamwelimisha. Mimi nimemwelewa hakutaka kuwa specific kutaja jina la nchi ndio maana amesema ameishi Europe. It could be any country in Europe ni sawa na kusema North America sio kwamba ni Marekani tu ni pamoja na Canada sasa kipi ambacho hujaelewa hapo mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
ndio tu nimepata visa so huwezi omba kazi mpaka uwe ndani ya US.

Ni visa ya aina gani hiyo? kwasababu si zote unaweza kupata
SSN, kama ni ile ya DV then poa tuu lakini kama ni zile
nyingine ni bora uairishe kwa sasa.

Naelewa unataka pia kuwa karibu na mkeo lakini hujasema
amekua US kwa muda gani au aliendaje endaje US?. Usije
acha kazi ukakuta mkeo ameshaendelea na maisha yake
ukaja kudata.
 
Mhm, hii thread naona kama ni ya kutafutia njaa tu, ifike saa mbili tukale.
Maoni yangu tu jamani.... Eh, nimesahau, samahanini kwa kuchangia ingawa nipo Mtogole.
 
Back
Top Bottom