Ombi kwa waishio marekani

hongera sana kwa yote mkuu but pole sana kwa kuingia katika dilemma ila utapewa ushauri mwisho wa yote usikilize moyo wako tu!
 
Nasisitiza hakuna nchi inaitwa europe, kutaja kama ulikuwa UK. Holand, German, Spain, France n.k hakuwezi kukutambulisha ki namna yeyote ile sababu ni Watanzania wengi sana wameishi na wanaendelea kuishi kwenye nchi hizo. na kama unataka mawazo ya watanzania waliopo U.S,A labda ungeomba tukupe blogu zao, humu JF hawaingii watu wajingajinga.
mkuu mbona unang'ang'ania nchi ya europe yeye kasema aliishi europe sasa hapo huelewi nini? kwani haiwezekani kuishi europe au afrika au asia?
 
Nasisitiza hakuna nchi inaitwa europe, kutaja kama ulikuwa UK. Holand, German, Spain, France n.k hakuwezi kukutambulisha ki namna yeyote ile sababu ni Watanzania wengi sana wameishi na wanaendelea kuishi kwenye nchi hizo. na kama unataka mawazo ya watanzania waliopo U.S,A labda ungeomba tukupe blogu zao, humu JF hawaingii watu wajingajinga.


Unamshambuli kwa vile kasema Euro, mbona humshambulii hajataja sehemu anayokwenda marekani? Zote Europe na Marekani ni general names za mkusanyiko wa nchi mbalimbali (nadhani Marekani ni muungano wa federal states).

Samahani kama nitakuwa nimekosea.

Kwa upande mwingine, unamaanisha watanzania wanaoishi marekani wenye blogu ni wajingawajinga?
 
Ni Visa ya aina gani na mke ana muda gani USA? Kama ni Green Card basi wee kaa kaa bongo mpaka mke akishaweka mizizi ndio uende la sivyo mtachemsha wote wawili mkiwa hamna kazi za maana. Ila kama mke ana work visa, student visa etc etc halafu wewe unakuja na K3 bora ukae huko huko uwe unakuja kumsalimu tu. Siku hizi USA kwa wageni sio easy na kama kazi mke anayofanya haina health Insurance God forbidden muugue mtafilisika sana tu (sijui ni state gani yupo) lakini states nyingi siku hizi hazina hela hivyo hiyo fund ya kutibu bure imepunguzwa sana kwa wasio na health insurance halafu adding your are a foreigner!!! Utakua guinea pig tu huku bila health insurance siku hizi. Mahali popote siku hizi ni heri uende as a student (na siku hizi nasikia hawatoi ss kwa student visas anymore) au kama umelost kweli bongo na unataka kujaribu mahali pengine lakini uwe at least below 25 yrs old. Unemployment is still above 9% sijui unajua hilo? Kwa hiyo kupata professional job na degree ya nchi nyingine ni next to nothing. Wee una professional job bongo halafu unataka kuiacha? Njoo utembee uone situation zilivyo then ukiona it's better here then it is okay kwa vile kama ulishaenda hata kuchukua visa means uishaset your mind to go kwa hiyo hamna mtu atakushauri ukaelewa lakini kama unasema umeshaishi Europe sasa sioni kwanini iwe vigumu kuelewa? Ulichokikimbia Europe ndio hicho hicho kitakukimbiza USA if you don't have determination hamna mahali ni rahisi kuishi ulimwengu huu. Ni juhudi zako na your goals ndio will lead you to your destination...
 
Wanajf mnaoishi USA naomba maoni yenu.
Mie nipo TZ ila mke wangu anaishi US na nimefanikiwa viza ili nije nimjoin . Tatizo ni kuwa nimepata kazi ya prof bongo na nategemea mshahara wa kama 3million, sasa nipeni maoni yenu kama ni ww ungechagua kazi au kwenda US.
Nmeishi Euro kama miaka sita hivi nimerudi recently baada ya kuchoka, hivyo najua nn kitatokea nkienda US. Wife kazi zake ni hizo hizo wanazofanya wageni na mara nyingi analalamika kuchoka kwani analala hm nights 3 tu siku zingine ni kazi 24 hrs.
Naomba maono yenu esp kutoka kwa watu waliotoka bongo miaka au siku za karibuni.
Njoo huku likizo! Kamwe usiache kazi ya 3mil,huku hamna kitu unless you are in your teens and early twenties,otherwise ni utumwa tu!nipo huku miaka 15,maziwa na keki kila asubuhi,mayai ubwete!..misosi mvua na easy tu! bali umeme,cable and other bills ndio kazi.ni vigumu ku save! kama una mke poa,ila hiyo kazi nimeimind,usiiache!.....mpeleleze sana mkeo,huku misosi na winter watu tunalambana sana! but that depend on a person.
Halafu kama umezoea kupewa ujiko,huku utajisikia vibaya kwani elimu ya Africa japo ni kali,huku wanaona kama shule ya kata tu!.tunapiga box na wanaubalozi wetu,mainjinia wa UDA,watu wa masters kibao lakini wanabeba boksi kama hawana akili nzuri,ila kama wewe ni mhindi na umeelimika,umewini.
Other than that,ni kama europe tu but with a lot of Gangstaz!
 
Nakushauri lakini wewe ndio wa mwisho katika hili.
Mshahara 3Mil. na unakaa Bongo, yaani ukiachia hiyo nafasi ...
Muulize mkeo, yeye anafanya kazi huku USA? Na analipwa kiasi gani kwa saa na kwa wiki?
Mkeo anaishi state gani, analipia nyumba kwa mwezi kiasi gani na ana bills nyingi (cabletv/home phone/ cell phone/internet, nk.) ni kiasi gani?
Tafadhali usi-convert in Tshs.
Kwakifupi, ni afadhali mkeo arudi bongo kuliko wewe uje USA.
Unauhakika utapata kazi USA na ni kazi gani na itachukua muda gani hadi hapo utakapo pata kazi?
Kama mkeo ni Lawyer, doctor ni sawa kabisa lakini kama ni mwanafunzi au anaishi tuu USA... Tshs 3mil in TZA, go for it.
Naishi USA.
 
Mkuu.
Wife akiiona hii msg basi atakupiga red card au atauwasha moto. Au una uhakika sio member hapa JF?
Vizuri ungeshauriana na yeye na mukakubaliana. Wife anaweza kuwa mshauri mzuri tu.

Priority yako au yenu wewe na wife ni nini?
Halafu, long distance relationship ni mtihani mkuu.

Kweli kabisa.
USA ya sasa sio kama enzi zile. Inategemea mkeo anafanya shughuli gani hapa USA.
Lawyer, doctor or else! Kama ni mchapa kazi tuu, basi mshauriane vizuri ili aweze kurudi bongo na kuishi pamoja.
 
Kazi ni mpaka nifike ndio nitafute na priority kwangu ni kazi kwani bila job hata familia inasambaratika.

Unafikiria kutafuta kazi ya namna gani?
Ni lazima upate Social Security number, driving license and work permit ndio upate kazi ya maana. Huu utakuwa ni mtiani mkubwa kama mambo yako hayatakaa sawa.
Pray about this please and pray for your wife.
 
thanx people, mke wangu ni US citizen na amekuwa huko over 10yrs.

10 years citizen bado anafanya kazi za kinyemela???? ...Mhhhhh what went wrong? Kabla hujaja mshauri arudi shule. Akimaliza shule na kupata kazi ndio uje la sivyo mtaishia devorce tu. We have seen a lot....Na pia hata kama utakuja na visa ambayo itakuruhus kufanya kazi labda uwe na network nzuri au field/career yako iko very juice kwa vile sasa hivi kazi zote za professional zimehamia China. Kama umezoea kubeba brief case huko na kufunguliwa milango ya gari utakua depress sana tu huku. Huku uje mdogo utablend vizuri na maisha ya huku. Ukija mtu mzima ni kujiengezea pressure tu.
 
Nasisitiza hakuna nchi inaitwa europe, kutaja kama ulikuwa UK. Holand, German, Spain, France n.k hakuwezi kukutambulisha ki namna yeyote ile sababu ni Watanzania wengi sana wameishi na wanaendelea kuishi kwenye nchi hizo. na kama unataka mawazo ya watanzania waliopo U.S,A labda ungeomba tukupe blogu zao, humu JF hawaingii watu wajingajinga.

kuuliza ni kosa siku hizi? kwa majibu yako ya kijinga nahisi na wewe ni mjinga uliyekosea njia uko JF!!!!
 
thanx people, mke wangu ni US citizen na amekuwa huko over 10yrs.

Kama mkeo ni US citizen basi anaweza kukaa nje ya US muda wowote anaotaka bila shinikizo lolote. Na kwasababu umesema anakazi ya box kwanini asije bongo mjenge familia halafu muwe mnakwenda US kutembea tuu?

Nasema hivyo kwasababu kama anapiga box zaidi ya 16hrs (double) inamaana yeye hulala masaa machache. Hayo siyo maisha ndugu, yanaleta frustration sana na kama na wewe ukiwa upo upo (wakati yeye anafanya kazi) halafu mambo yako yasiende vizuri mtaanza kugombana kwasababu ataona unamwelemea.
 
ingawa me ni wa mwanza bt nakushauri ujibakie hapa hapa bongo yetu , ungemtafutia mkeo kazi aje akae hapa hapa tz afanye kazi, tena km analalamika anachoka na kuwa bzy na kazi za kubeba mabox kila cku kwann asirudi huku?, hiyo kaz ya mil3 wenzio tunaitafuta hatuipati
 
mhh nnavyotamani kwenda majuu,sina tu wa kunialika japo nkatembee wiki ntagharamia mwenyewe kila kitu:rain:
 
ingawa me ni wa mwanza ... hiyo kaz ya mil3 wenzio tunaitafuta hatuipati
wewe unatafuta hiyo kazi ya mil 3, mwenzio ana ambitions kubwa zaidi, usishauri based on your own vision-less outlook.

Isitoshe, anataka ushauri wa waliopo Marekani, wewe ni wa Mwanza!
 
kwa ushauri wangu ndugu yangu ingawa sipo USA ila nipo umangani huku karibia na jua.kama unapata mil3 kwa bongo nakushauri ubaki bongo ufanye kazi na uweke na vitega uchumi.Kwa 3m ni hela nzuri sana una uwezo wa kusave 2m kwa kila mwezi na ni hela nzuri hata ukiomba mkopo kama una business plan una uwezo wa kukopa mil 70.Kumfuata wife haina tija sina unaweza kwenda walau mara moja kila baada ya miezi 6.Kukaa USA ni vema pia ila kwenye nchi za watu mara nyingi matumizi ni makubwa na pia savings inakuwa ndogo.Chagua mwenyewe kwenda kuishi na wife ilihali ukirudi bongo huna hata cha maana.wazungu wajanja sana wanakulipa vizuri lakini wanahakikisha hela yote utaitumia kwao.Imagine unapokea $6000 kwa mwezi lakini unabakiza tu $500 hivi kwa mwezi kama savings.Mshahara wako wa bongo ni sawa na waziri ndugu yangu au majaji ww upo kwenye class ya juu kabisa sasa huko USA cha zaidi ni nn huko? labda uniambie utaenda kusoma lakini uwe umeshafanya kazi na upewe ruhusa ya kusoma na mwajiri wako ili ukimaliza urudi pale pale.
 
Back
Top Bottom