Vifaranga kwa maelfu vyachomwa moto awamu ya sita! uchokozi kwa Rais Samia

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
602
1,407
VIFARANGA KWA MAELFU VYACHOMWA MOTO AWAMU YA SITA! UCHOKOZI WA RAIS SAMIA!

1.0 Utangulizi

1) Rais Samia Suluhu Hassan alimkashifu Hayati John Pombe Magufuli hadharani kwa eti kuchoma moto vifaranga. Mbaya zaidi, hii ilitokea mbele ya mgeni, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.

2) Ndio maana tunasubiria kwa hamu kubwa kusikia kauli ya Rais Samia kuhusu haya maelfu ya vifaranga vinavyochomwa moto ndani ya awamu ya sita. Awamu ya Rais Samia Suluhu Hassan, mlinzi wa vifaranga.

3) Nimeongelea pia hii tabia ya Serikali ya awamu ya sita kumgeuza Hayati Magufuli a "punching bag" ("mnyonge wao" wa kumshughulikia kwa "mipasho", "madongo", "mateke" na "ngumi" kila kukicha). Nimemshauri Rais Samia:

a) Aanze Mwaka Mpya 2023 kwa kumsahau Magufuli, iwapo hana mazuri ya kumkumbuka nayo.
b) Kinachoendelea hakipendezi wengi, hata ambao walikuwa hawampendi Rais Magufuli wanashangaa, wanakereka na kujiuliza: "Kulikoni kila kukicha kupambana na marehemu?!"

4) Nimetoa maoni na ushauri wangu, bila kusahau kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa:

a) Mapambano ya kuendesha nchi, na kwa
b) Uchokozi wake na ujasiri wa kuthuhutu kuwatukana wanasheria wa Tanzania kwamba wanashindwa kesi za nje ya nchi kwa sababu eti hawajui Kiingereza.

5) Nimeshangaa wasomi na wataalam wa Bongo wameufyata kimyaaa, hakuna anayekohoa wala kujikuna.

a) Hata TLS (Chama cha Wanasheria wa Tanganyika) wameufyata.
b) Viongozi wa upinzani (pamoja na wanaharakati na wanahabari) ndio mmhuuu, wako bize wanafakamia asali ya mama Samia na peremende za mabeberu.

2.0 Rais Samia Amshambulia Tena Hayati Magufuli

1) Rais Samia alipoingia madarakani, baada ya Kifo cha Rais Magufuli, alianza kazi ya urais kwa maneno yafuatayo:

a) Mimi na Magufuli ni kitu kimoja, huwezi kututenganisha.
b) Viatu vya Magufuli havinitoshi, ni vikubwa sana kwangu. Wachora katuni nao wakamuunga mkono kwa vifijo.

2) Baada ya muda si mrefu, Rais Samia akaanza kumrushia madongo na kumdhihaki Rais Magufuli kwa mafumbo na mipasho. Mfano: "Mimi sitafoka kwa sauti bali kwa kalamu. Rais sio lazima ufokefoke."

3) Baadae kidogo, Rais Samia akaanza kumshambulia Rais Magufuli waziwazi (sio kila siku lakini kila alipopata upenyo).

a) Haraka sana, Serikali nzima ikaanza kushirikiana na wapinzani, wanaharakati pamoja na wanahabari rafiki, kuimba wimbo mmoja trying to distort and destroy the Legacy of President John Pombe Magufuli.

b) They started conducting "character assassination". Wakaunda usharika wa chuki kwa marehemu. Uchuro mtupu!

c) Rais Samia akaanza kubadilisha maamuzi mbalimbali ya Rais Magufuli. Mfano: Serikali ya Rais Samia ikaanza kuwarudisha kazini kwa mbwembwe na kuwalipa wale wote walioachishwa kazi kwa kugundulika kutumia vyeti feki.

d) Hii ni pamoja na wale walioapata ajira Serikalini kwa udanganyifu na kwa kutumia vyeti na majina ya watu wengine, ambalo ni kosa la jinai. Ni wazi kitendo hiki kina mchango hasi katika ujenzi wa maadili na utawala wa sheria nchini. Bahati mbaya, inaelekea Rais Samia alisahau kujiuliza (na hakuna aliyemkumbusha!): "Hivi tunawafundisha nini watoto, wajukuu na vijana wetu?! Hivi tunaifundisha nini jamii?!"

e) Rais Samia akaanza kuwaachia huru wote/wengi waliokuwa na kesi za uhujumu uchumi.

f) Ikawa si siri tena kwamba awamu ya sita inapambana na awamu ya tano, mapambano yakiongozwa na Rais Samia mwenyewe! CCM vs CCM!

g) Hili limewagawanya sana Watanzania, ambao wengi wao bado wako msibani na wala hawaelewi vizuri nini hasa kimekatiza uhai wa Rais wao mpendwa. Kwa namna fulani, sinema ya "Royal Tour" nayo ikatuchanganya zaidi wananchi... (na labda dunia nzima)! Mungu akipenda, ntaandika makala nyingine kuhusu Royal Tour.

4) Wema Hudumu Milele!

a) Kama ilivyo kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, wabaya wa Magufuli wameshindwa kabisa kumfuta toka mioyoni mwa Watanzania.

b) Mitandaoni tumekuwa tunakutana na ushuhuda toka kwa watu mbalimbali wakisema (mfano): "Mimi nilikuwa simpendi Rais Magufuli akiwa hai, na nilisherehekea hata kifo chake, lakini nimekuja kutambua kwamba nilikosea sana. Tanzania hatutakuja kupata Rais mzuri kama Magufuli! Naomba Mungu anisamehe, namuomba Magufuli anisamehe huko aliko!"

c) Ni wazi idadi ya wapenzi na mashabiki wa Magufuli imeongezeka badala ya kupungua. Kila Magufuli akitukanwa au kusimangwa hadharani, wao wanaongezeka, na hasira zao zinaongezeka!

d) Sababu?! Watu wanajionea wenyewe hali halisi na wanakumbuka vizuri Rais Magufuli alifanya makubwa kiasi gani na aliendeshaje nchi. Wanakumbuka mema mengi aliyowafanyia Watanzania. Watu wanashuhudia sinema ya bure ya undumilakuwili na usaliti unaoendelea bila haya!

5) Siku ya siku, Rais Samia Suluhu Hassan alimrushia madongo Hayati John Pombe Magufuli eti kwa kuchoma moto vifaranga.

6) Rais Samia hakumtaja Magufuli kwa jina lakini ilikuwa wazi kabisa kwamba anamnyooshea kidole mwenzie ambaye tayari alikuwa kwenye pumziko la milele, akiwa hawezi tena kujitetea.

7) Nilishangaa na kuhuzunika sana maana Rais Samia alimshambulia Rais Magufuli mbele ya Rais Uhuru Kenyatta! Kwa maoni yangu, hapo nchi yetu ilifedheheshwa kimataifa!

8) Nijuavyo, vile vifaranga vilivyochomwa moto na maafisa wa Serikali ya awamu ya tano (ambayo Rais Samia alikuwa Makamu wa Rais na msaidizi Na.1 wa Rais Magufuli) kama namna ya:

a) Kuzuia magonjwa yatokanayo na vifaranga/ndege ambavyo viliingizwa nchini kinyume cha Sheria za Nchi (na bila kufuata taratibu za kimataifa za afya na magonjwa ya mifugo).

b) Kama "tit for tat" kujibu mapigo na kuwashikisha adabu Serikali ya Kenya ambao tulikuwa kwenye vita nao ya kibiashara! Kabla ya hapo Kenya walikuwa wamezuia mahindi yetu yasiingie Kenya. Serikali ya Kenya walikuwa wamezuia pia malori yetu mengi pale mpakani Namanga (bila kujali yamebeba bidhaa gani na bidhaa hizo zinaelekea wapi)!

c) Kulinda soko la ndani.
d) Kulinda afya na uhai wa Watanzania.
e) Kama sehemu ya usalama wa taifa.

9) Tafadhali rejea hiyo video clip ya Rais Samia akiendesha moja ya mapambano dhidi ya Serikali ya awamu ya tano.

10) Naomba nimnukuu Rais Samia:

"Biashara yetu na Kenya ilikuwa ngumu sana. Ngumu sana. Fika vifaranga pale mipakani pale makaratasi hayasemi vizuri vimetoka wapi haisemi vizuri, kunapitwa vifungu vya sheria as if sheria is everything. No, no, no, sheria hairuhusu. Solution? Hata hatuogopi dhambi, choma hivyo vifaranga. Mmesahau, tumejisahau, kwamba vifaranga navyo ni viumbe vya Mungu, sio? Walikuwa na life, tukachoma."

11) Wote tunajua Rais Magufuli alikuwa muumini mzuri wa Mungu na aliishi kwa hofu ya Mungu. Ndio maana kujaribu kumchonganisha Rais Magufuli na Mwenyezi Mungu is a punch below the belt.

12) Mbaya zaidi, haipendezi Rais wa nchi kuwahubiria wananchi wake umuhimu wa kuvunja sheria za nchi!

3.0 Taifa Lafedheheshwa

1) Rais Samia ana haki ya kikatiba (kama mwananchi mwingine yeyote) kuongea anachotaka ili mradi havunji Katiba na sheria za nchi!

a) Lakini Katiba hiyohiyo inatambua pia haki za binadamu.
b) Ndio maana ni kosa kisheria mtu yeyote kumtukana mtu mwingine yeyote (hata marehemu!) hadharani.

2) Hata kwa utamaduni wetu sisi Watanganyika hii si sawa!

a) Si sahihi Rais mmoja kumnyamba Rais mwingine (tena mtangulizi wake ambaye hayuko duniani!) mbele ya Rais wa nchi nyingine.
b) Si sawa kabisa.

3) Ni sawa na ndugu kukaa kikao kimoja na majirani kumkashifu baba yenu au mama yenu, mjomba wenu au shangazi yenu!

a) Ni uchuro mkubwa.
b) Ni ujuha kama si laana.
c) Si sahihi, si haki.

4) Ndio maana najiuliza:

a) Rais Uhuru Kenyatta alikuwa Rafiki wa Magufuli na alikuwa anapenda kumuita Rais Magufuli "kaka yangu" au "ndugu yangu".
b) Je, siku ile Rais Uhuru Kenyatta alijisikiaje maana alikuwa amekaa pembeni ya Rais Samia?!
c) Hivi hili tukio halikuwa kituko cha kimataifa kweli?!

5) Hivi wanaposhuhudia matukio ya ajabu/aibu kama haya, viongozi, ndugu na marafiki zetu waliokuwa wanamheshimu na kumkubali sana Rais Magufuli wanajisikiaje?! Wanaelewaje haya yanayoendelea nchini kwetu?! Mfano:

a) Rais Yoweri Museveni wa Uganda.
b) Rais Paul Kagame wa Rwanda.
c) Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi.
d) Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji.
e) Rais Felix Tshisekedi wa Congo DRC.
f) Rais Lazarus Chakwera wa Malawi.
g) Rais Hage Geingob wa Namibia.
h) Raila Odinga wa Kenya.
i) Rais Xi Jinping wa China.
j) Na wengine.

6) Najiuliza sana:

a) Hivi Rais Magufuli alimkosea nini hasa Rais Samia hadi awe na chuki nae kubwa kiasi hiki?!

b) Hivi bila Rais John Pombe Magufuli, Samia Suluhu Hassan angekuwa Rais wa Tanzania kweli?!

7) Hivi iwapo Rais Samia, Mzee Yusuph Makamba, Nape Nnauye, Peter wa Royal Tour na wengine wanathubutu "kumshughulikia" Hayati Magufuli kwa kiasi hiki hadharani, wanapokuwa faragha, wanaenda mbali kiasi gani?!

8) Nimejikuta nakumbuka zile audio clips za wale jamaa waliomsaliti Rais Magufuli.

9) Ajabu, karibu wote wametunukiwa nafasi za matawi ya juu ndani ya Serikali ya awamu ya sita!

10) Dah! Naona mengine tumuachie Mungu!

4.0 Vifaranga zaidi ya 50,000 Vyachomwa Moto Awamu ya Sita

1) Mwaka 2022 tumeuaga na taarifa kwamba zaidi ya vifaranga 50,000 vimechomwa moto katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita.

2) Tafadhali rejea hiyo video clip toka taarifa ya habari ya ITV ikionyesha picha za huzuni za kuchomwa moto hawa "viumbe wa Mungu wasio na hatia", huku mwekezaji, Bi. Faye Crane, akilalamika jinsi Serikali "ilivyomuacha solemba" kama mwekezaji. Bi. Crane anasema kufuatia Wito wa Serikali kuongeza uzalishaji wa vifaranga, kampuni ya Kibo Poultry inazalisha vifaranga 200,000 kwa wiki.

3) ITV wanasema:

"Vifaranga vya kuku wa nyama na mayai zaidi ya 50,000 vimeteketezwa kwa moto mkoani Kilimanjaro, baada ya kukosa soko, kufuatia vifaranga wanaoingizwa nchini toka nje kuathiri soko la ndani"!

4) Hivi Serikali inamjibuje huyu mwekezaji, na wengine kama yeye?!

5) Ndio maana wananchi wenye kumbukumbu za madongo aliyotupiwa Rais Magufuli tunasubiria kwa hamu kauli ya Rais Samia kuhusu kuchomwa moto kwa vifaranga hivi ndani ya awamu yake.

6) Sijui familia ya Rais Magufuli itaombwa radhi kwa madongo aliyorushiwa mpendwa wao?!

7) Sitashangaa iwapo, kama kawa, itatafutwa namna ya kuitupia lawama vita ya Ukraine kwa vifo vya vifaranga hawa zaidi ya 50,000 (na labda wengine zaidi watakaolazimika kuchomwa kwa kukosa soko)!

5.0 Vifaranga 62,730 toka Ubelgiji Vyakamatwa Uwanja wa Ndege

1) Vifaranga vya kuku wa mayai 62,730 vimekamatwa Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam vikiwa vinaingizwa nchini toka Ubelgiji, kinyume cha sheria za nchi.

2) Serikali imetoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari, kupitia Profesa Hazron E. Nongwa, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

3) Tafadhali rejea hiyo video clip na hiyo taarifa kwa vyombo vya habari.

4) Nawapongeza sana mamlaka husika pamoja na maafisa wa uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kwa kusimamia sheria.

5) Bahati mbaya, kusimamia sheria ni moja ya mambo yanayoelekea kumkera sana Rais Samia!

6.0 Taarifa ya Serikali

Naomba ninukuu sehemu ya taarifa ya Serikali:

1) "Tarehe 22.12.2022 saa nne usiku Wakaguzi wa Mifugo na Mazao yake walio katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) walikamata vifaranga wa kuku wa mayai 62,730 mali ya Kampuni ya Phoenix Farms Limited ya Mkuranga, vilivyofikishwa uwanjani hapo vikitokea nchini Ubeligiji bila kuwa na vibali vya kuingiza nchini vifaranga (Import Permit) pamoja na cheti cha afya (Animal Health Certificate)."

2) "Vifaranga hivyo viko katika makasha (crates) 697 na stakabadhi ya mauziano (invoice) ya mzigo inaonyesha vina gharama ya shilingi 200,262,706 ambazo ni sawa na Euro 80,828.80 (Cost of Insurance and Freight - CIF)."

3) "Mkurugenzi wa Kampuni pamoja na Wakala wa Mmiliki wa vifaranga (Clearing Agent) walikiri kutokuwa na kibali hicho hivyo kuwa amevunja Sheria ya Magonjwa ya Wanyama Sura ya 157 na Kanuni ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Wanyama na Mazao yake ya GN Na.28/2007."

4) "Kulingana na Kifungu cha 54(2) cha Sheria ya Magonjwa ya Wanyama Sura ya 156 kinakataza kuingiza nchini Mifugo na Mazao yake bila kuwa na kibali nanukuu: 'No person shall bring or cause or permit allow to be brought into the country any animal product, contrary to any order or regulation prescribing the introduction of animal products into the country or without animal products inspected and certified in the prescribed manner.' Hivyo kwa kitendo cha Kampuni ya Phoenix Farms kutaka kuingiza nchini vifaranga wa kuku wa mayai 62,730 ni kukiuka Sheria."

5) "Aidha Kanuni ya 26 ya Kanuni za Udhibiti wa Usafirishaji wa Wanyama na Mazao yake ya GN 28/2007 inabainisha kuwa, 'ikiwa wanyama au mazao ya wanyama yatafika nchini bila kibali na cheti cha afya ya wanyama au mazao ya wanyama husika nchini. In the event, of any animal or animal products intended for importation arriving without the certificate required as aforesaid, an inspector shall refuse to allow such animal or animal products to enter Tanzania...'."

6) "Hivyo, kutokana na tafsiri ya vifungu hivyo viwili hapo juu, vifaranga wa kuku wa mayai 62,730 walioletwa na Kampuni ya Felix Farms Limited waliopo Uwanja wa Julius Nyerere International Airport (JNIA) upande wa mizigo (cargo) wamezuiliwa kuingia nchini kwa kuwa ni mzigo hatarishi."

7) "Aidha Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeutaka Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Tawi la Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam kuielekeza Kampuni ya Phoenix Farms Limited kuvirudisha vifaranga hivyo nchini Ubeligiji kwa sababu wanaweza kuhatarisha usalama wa kuku nchini. Vilevile Mkurugenzi wa Kampuni ya Phoenix Farms Limited ameelekezwa kuviondosha vifaranga hivyo kutoka maeneo ya uwanja wa ndege na kuvirudisha alikovitoa."

8) Licha ya taarifa hii ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (taarifa ya Serikali) kuwa na makosa mengi, ujumbe umeeleweka. Nashangaa tu kwamba:

a) Jina la Mkurugenzi wa Kampuni ya Phoenix Farms Limited limefanywa siri! Hivi ni kwa nini?!

b) Serikali haijaipa "deadline" Kampuni ya Phoenix Farms Limited ya kuondoa vifaranga hivyo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam (JNIA) na kuvirudisha Ubelgiji vilikotoka.

c) Taarifa ya Serikali haiko wazi nini kitatokea iwapo vifaranga vitaanza kufa.

d) Taarifa ya Serikali haijaweka wazi lini Serikali italazimika kuingilia kati na kuhakikisha vifaranga hivi vinachomwa moto haraka ili kulinda afya na maisha ya Watanzania, pamoja na kuku na mifugo mingine nchini. Kuna taarifa ya kitaalam ambayo inasema vifaranga hivi vitakufa kwa kukosa chakula baada ya masaa 72 toka viwasili nchini. Sijui ukweli ukoje...?!

9) Nashangaa inakuwaje taarifa ya Serikali kuwa na makosa mengi kiasi hiki!

10) Kwa uelewa wangu mdogo, baada ya kufa, vifaranga hivi 62,730 vinageuka hatarishi zaidi maradufu. Ndio sababu ya kulazimika kuvichoma moto kwa mujibu wa sheria za nchi na protokali za kimataifa za usalama na afya ya mifugo na binadamu.

7.0 Maswali ya Kizushi!

Kwa unyenyekevu mkubwa, heshima na taadhima, naomba kuuliza:

1) Rais Samia anajisikiaje?!

2) Je, kimoyomoyo, hajutii kauli tata na madongo aliyomrushia Rais Magufuli kwa eti "kuua vifaranga visivyo na hatia"?! Je, Rais Samia haoni umuhimu wa kutoa ufafanuzi kuhusu kuchomwa moto kwa vifaranga ndani ya awamu ya sita?!

3) Wananchi tungependa kujua iwapo jumla ya vifaranga vilivyochomwa moto ndani ya awamu ya sita ni:

a) 50,000
b) 112,730 au
c) Zaidi ya 112,730.

4) Hivi Rais Samia hajisikii vibaya kumbagaza na kumdharirisha Hayati Magufuli hadharani, tena mbele ya mgeni wetu, Rais Uhuru Kenyatta?!

5) Je, Serikali ina ufafanuzi gani maana wananchi wamekuja juu mitandaoni!

a) Wananchi wanahoji: iweje juzijuzi vichomwe moto vifaranga zaidi ya 50,000 kwa kukosa soko, halafu leo viingizwe Vifaranga 62,730 toka Ulaya?!

b) Mbona haiingii akilini?!
c) Nini hasa kinaendelea?!

6) Hivi kipaumbele ni kulinda maisha na afya ya Watanzania au uhai wa vifaranga vilivyoingizwa nchini kinyume cha sheria za nchi (na ambavyo hatuna uhakika iwapo havina magonjwa hatarishi)?!

7) Hivi kweli Rais Samia anasimamia kauli yake ya (sio nukuu ya neno kwa neno): "Sheria kitu gani bana!" aliyoitoa wakati anamnyamba Rais Magufuli?!

8) Kwa nini tunajenga nchi ambayo inakuwa kama kufuata sheria ni "kosa la jinai" na kuvunja Sheria ndio poa?! Nchi ambayo wanaosimamia sheria wanashughulikiwa na kuadhibiwa na wahalifu, wanaovunja sheria, ndio wanaopeta 24/7?!

9) Je, hivi vifaranga 62,730 viliisharudishwa kwao Ubelgiji na vilirudishwa tarehe ngapi?! Hivi Serikali ya Ubelgiji ilikubalije kupokea mzigo wa vifaranga vilivyokufa?!

10) Je, hivi vifaranga 62,730 vimeishachomwa moto na vilichomwa moto lini na vilichomewa wapi exactly?!

11) Je, maelekezo ya Rais Samia (kuhusu kutochoma moto vifaranga vya Mungu na kutong'ang'ania kufuata "sheria maana sheria sio kila kitu"!) yametekelezwaje katika sakata hili la vifaranga 62,730 toka Ubelgiji?!

8.0 Ushauri wa Bure

Kwa unyenyekevu mkubwa, heshima na taadhima, naomba kushauri:

1) Rais Samia na Serikali yake waanze Mwaka Mpya 2023 na ukurasa mpya na waachane kabisa na Hayati John Pombe Magufuli (hasa pale ambapo wanaona hawana neno zuri kwake)!

a) Najua "Mzimu wa Magufuli" unaweza kuwa unawahangaisha wengi, lakini nadhani itamsaidia sana Rais Samia kujenga jina lake kwa nguvu zake, kwa kupambana kujenga nchi badala ya kujaribu kumbomoa bosi wake aliyempa kazi. Ni vema Rais Samia akatoa maelekezo haya kwa chama chake, kwa Serikali yake na kwa wateule na watendaji wake... waache kabisa usaliti na unafiki!

b) Serikali ingeangalia, iwapo itaona inafaa, umuhimu wa kumuomba radhi Hayati Magufuli kwa kumdharirishwa na kumbagaza. Nimeshauri Serikali ndiyo iombe radhi maana nimeona kumshauri Rais aombe radhi inaweza kuwa ni kama kumvunjia heshima. Sina uhakika!

c) Maombi rasmi ya msamaha yanaweza kukabidhiwa kwa familia ya Rais Magufuli (kupitia kwa mjane wa Magufuli, Mama Janeth Magufuli).

d) Ndio uungwana maana hakuna Bin Adam asiyekosea.

e) Ingawa Rais Samia ana haki ya kikatiba ya kumsema vibaya Rais Magufuli (au mtu yeyote yule asiyempenda), iwapo anaona inafaa, aepuke kumsema vibaya Rais Mstaafu yeyote wa nchi hii mbele ya Rais wa nchi nyingine. Kwa kweli haipendezi.

2) Hakika haipendezi Rais kumfokea au kumtukana Waziri wa Serikali yake mbele ya Rais wa Nchi nyingine. Rais Samia akumbuke ahadi yake kwa Watanzania.

a) Siwezi kusahau jinsi Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda, alivyofurumushwa hadharani na kutukanwa "Tusi la Nonsense" mbele ya Rais Yoweri Museveni.

b) Nahisi kuna wajanja walimtia Rais Samia utambi kwa malengo maalum. Labda kilikuwa kinatafutwa kiti cha Profesa Adolf Mkenda (ambaye sasa kahamishiwa Wizara ya Elimu na nafasi yake kuchukuliwa na Hussein Bashe). Nawaza tu!

c) Vyovyote vilivyo, nadhani Rais Samia aliteleza kumtukana Waziri wake wa Kilimo mbele ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda. Mbele ya wageni toka nchi nyingine. Tena "kosa" la Waziri Mkenda likiwa ni kulinda na kusimamia maslahi ya taifa!

3) Nimekumbuka na tukio la hivi karibuni ambapo Rais Samia aliwatukana wanasheria wa Tanzania kwa kuwaambia Serikali inashindwa kesi nyingi za "International Arbitration" kwa sababu wanasheria wa Tanzania/Serikali hawajui Kiingereza!

a) Kilichonishangaza sio kauli hii ya Rais Samia bali mahali alipoitolea.

b) Rais Samia aliwatukana wanasheria wa Tanzania mbele ya wanasheria wenzao wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maana Rais Samia alikabiribishwa kwenye mkutano wao wa pamoja.

c) Ingawa mimi sio mwanasheria, tukio hili liliniuma sana maana wanasheria wa Tanzania walitukanwa sio tu mbele ya "dunia nzima", bali mbele ya Wakenya ambao huwa wanapenda sana kutukashifu waziwazi kwamba: "Watanzania hawajui Kiingereza, wanaongea na kuandika broken English".

d) Halafu anakuja Rais wetu anawapa "zawadi ya ushahidi"! Sasa Wakenya na wengine watakuwa wanasema: "Mnabisha nini wakati hata Rais wenu aliwafurumusha hadharani kwa kuingizia nchi yenu hasara kubwa kwa kutojua Kiingereza?!"

e) Katika muktadha huu, ndio utaelewa vizuri kwa nini Rais Samia aliteleza sana kuwakashifu wanasheria wetu hadharani mbele ya wageni wanaotudharau (hata kama alilosema lina ukweli fulani)! Ndio yaleyale yaliyofanywa na MC Kipilipili akiwa Kenya kwenye Churchill Show! (Ingawa Kipilipili ni wa kumsamehe na kumuelimisha tu maana nadhani uelewa wake ni mdogo! Hakika hakujua atendalo!)

4) Najiuliza!

a) Hivi Rais Samia ana uhakika gani kwamba Serikali inashindwa kesi za kimataifa kwa sababu wanasheria wa Tanzania hawajui Kiingereza?!

b) Kama kweli wanasheria wa Serikali hawajui Kiingereza, kwa nini Serikali inaajiri Wanasheria wasiojua Kiingereza?! Kwa nini Serikali haiajiri Wanasheria wanaojua Kiingereza?!

c) Sasa hizi kesi za ndani ya nchi zinazoendeshwa kwa Kiswahili, mbona Serikali huwa inashindwa?! Ushahidi: Kauli ya Rais Samia mwenyewe kwamba Serikali inashindwa kesi nyingi kwa kukosa ushahidi.

5) Kwa msingi huu, kwa nini Rais Samia aliwashambulia wanasheria wa Tanzania kwa hoja dhaifu?! Au huu ndio Uchokozi wa Rais Samia?!

6) Nimeshangaa tu kuona wafuatao wako kimya:

a) Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
b) TLS (Chama cha Wanasheria wa Tanganyika).
c) Wanasheria maarufu kama Profesa Issa Shivji, Profesa Harrison Mwakyembe, Jenerali Ulimwengu, Palamagamba Kabudi, Fatma Karume, Tundu Lissu, n.k.
d) Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma.
e) Jaji Joseph Sinde Warioba.
f) Wanahabari.
g) Wanaharakati.
h) Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda.

Nilitegemea walau baadhi yao watoe kauli ya kuunga mkono, kupinga au kutetea.

7) Inaelekea Rais Samia kawashika pabaya!

8) Vifaranga!

a) Rais Samia atoe tamko rasmi kuhusu hii kashfa ya vifaranga zaidi ya 50,000 kuchomwa moto kwa kukosa soko. Na kuhusu hatma ya vifaranga 62,730 toka Ubelgiji.

b) Serikali isipotezee kuhusu hii kashfa ya vifaranga.

c) Serikali imjibu Bi. Faye Crane.

d) Serikali iweke wazi tatizo ni nini na imechukua hatua gani kulitatua kwa faida ya nchi, wafanyabiashara (wa vifaranga, mayai na kuku), wafugaji wa kuku, wawekezaji na walaji.

e) Serikali ituambie wananchi imechukua hatua gani kuhakikisha kwamba vifaranga havitaendelea kuingizwa nchini kinyemera (na kinyume na sheria) ambayo ni hatari kubwa kwa afya za Watanzania na usalama wa taifa. Aidha ni hujuma kwa nchi kibiashara.

f) Serikali ituambie wananchi imechukua hatua gani kuwasaidia wafugaji na wafanyabiashara wa vifaranga, kuku na mayai nchini. Na kulinda soko letu na uchumi wetu.

9.0 Sheria ni Sehemu ya Utawala Bora

1) Nina mashaka makubwa iwapo utawala/uongozi bora unawezekana katika nchi ambayo haiheshimu sheria.

a) Maendeleo ya kweli yanapatikanaje katika nchi ambayo kauli ya Rais ndiyo kama sheria.

b) Kauli au matakwa ya Rais yakipingana na sheria, inabidi sheria ipindishwe au kubadilishwa kabisa. Nakumbuka jinsi Rais Samia alivyomwamuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali achukue hatua za haraka kubadili Sheria ya Manunuzi maana inamkwamisha.

2) Msingi wa taasisi imara ni utawala/uongozi wa sheria, na sio "utawala wa Rais"!

a) Moja ya changamoto zinazoikabili nchi yetu ni kuwa na taasisi dhaifu lakini Rais mwenye mamlaka makubwa kupita kiasi.

b) Tunasahau kwamba Rais ni Bin Adam kama Bin Adam wengine, mwenye mihemko yake inayotegemea Jua na Mwezi!

c) Moja ya hoja nzito kuhusu umuhimu wa kupata Katiba Mpya Tanzania ni umuhimu (urgency) wa, pamoja na mambo mengine, kupunguza mamlaka ya Rais ambayo ni makubwa mno kupita kiasi. Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alitutahadharisha kuhusu hili miaka kama 37 iliyopita (wakati anatangaza uamuzi wake wa kung'atuka)!

3) Kosa si kufanya kosa, kosa ni kurudia kosa!

a) Miaka 61 ya Uhuru tumetwanga sana maji kwenye kinu.

b) Hakika nchi yetu inahitaji Mwelekeo Mpya. Inanikumbusha ule usemi: "No wind will serve a boat without a port of destination"! Kwa sasa, inaelekea mwelekeo wa nchi umo kwenye briefcases za wawekezaji! Mwekezaji kutoka Oman (kwa mfano) akitaka hekta 30,000 za kulima paparachichi anakatiwa "fastafasta"! Na mtendaji mkuu wa taasisi husika ukisuasua, unatumbuliwa, anawekwa mtendaji mkuu mwingine wa kuharakisha utekelezaji wa maelekezo au matakwa ya Rais!

c) Tuheshimu Katiba, sheria na kanuni.

d) Tuuheshimu na kuulinda utamaduni wetu maana yajayo, mmhuuu...!! Tusisahau kwamba utamaduni ni kioo cha uhai na utashi wa taifa!

e) Kutawala kwa malengo, mapambano na mapambio ya "miaka mitano mitano" hakujengi nchi, bali kunadumisha hadaa na kukata tamaa.

f) Kamwe Tanzania haiwezi kuendelea kwa kutegemea Wazungu (na Weupe wengine). Maendeleo ya Tanzania yataletwa na Watanzania wenyewe (kwa rasilimali zao, ardhi yao, juhudi na maarifa). Maendeleo ya Tanzania hayawezi kuletwa na Wazungu/Mabeberu!

g) Kamwe Afrika haiwezi kuendelea kwa kutegemea Wazungu/Mabeberu. Afrika itaendelea kwa kujitegemea yenyewe.

h) Faida ya "mikopo" na "misaada" ya Wazungu ni kulinda na kuneemesha tawala dharimu na mafisadi wa Afrika wanaolinda maslahi ya Wazungu na Mabeberu. Viongozi na watawala dharimu wanaowawezesha Wazungu (na Weupe wengine) kuendelea kutuibia.

i) Hakika maendeleo ya Afrika hayawezi kuletwa na mamluki.

4) Watanzania sasa tunajua kwa uhakika zaidi kwamba viongozi wa Afrika ambao ni imara na hawakubali kuuza nchi au uhuru wake kwa Mabeberu (au kuruhusu uporaji wa rasilimali za taifa) huuawa! Tafadhali rejea kitabu kiitwacho: "Confessions Of An Economic Hit Man" by John Perkins.

5) Kama Uongozi wa nchi yetu ungeheshimu sheria tulizotunga wenyewe:

a) Tusingekuwa tunaongelea "kashfa ya vifaranga".
b) Tusingekuwa tunarushiwa ajenda za kiki na kusahaulishana mambo muhimu kila kukicha.

6) Nadhani hata Mwenyezi Mungu anajiuliza:

a) "Hivi unawezaje kuthamini Maisha ya vifaranga (ambao unasema ni "viumbe wa Mungu") kuliko maisha na heshima ya Hayati Magufuli (ambaye pia ni kiumbe wa Mungu)?!
b) Hivi unawezaje kuthamini maisha ya vifaranga kuliko maisha na afya za Watanzania, ambao wewe ndiye Rais wao?! How?!"

7) Mjane wa Magufuli aonewe huruma, na asiendelee kuumizwa kama alivyoumizwa na Mzee Yusuph Makamba siku ile huku akitamba na kumkufuru Mungu kwamba eti "wema hawafi..."!

a) Mzee Makamba alitoa mifano ya "Immortal Beings" wawili: Jakaya Mrisho Kikwete (Rais Mstaafu) na Abdulrahman Kinana (Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara)!
b) Kufuru iliyopitiliza!

8) Na kama, labda, mna bifu zenu na Rais Magufuli (ambazo sisi Wananchi hatujizui wala hazituhusu!) wote mnaohusika mumuombe Mungu awasaidie jinsi ya kuzitatua. Please don't continue treating President Magufuli as a punching bag because he isn't!

9) Moja ya uharibifu mkubwa wa kinachoendelea ni kuwaumiza Watanzania kwa kuchochea migawanyiko nchini (polarisation of the country), ambayo ni hatari kubwa sana kwa usalama na amani ya nchi yetu pendwa Tanzania!

a) Narudia! Ni hatari kubwa kuliko maelezo.
b) Usharika wa chuki kwa marehemu unaipeleka nchi pabaya.

10) Mheshimiwa Rais!

Kwa unyenyekevu mkubwa, heshima na taadhima, naomba nikushauri usijiamini kupita kiasi kwa sababu tu leo walamba asali na waotamani asali wote umewaweka mkobani!

a) Kuna siku wanaweza kulambishwa asali tamu zaidi (au peremende za chokoleti!) wakakutosa Mama! Hatuombei!

b) Si unakumbuka Baba wa Taifa (Mwalimu Julius Kambarage Nyerere) aliwaita jina gani?! Mimi sithubutu kulirudia!

c) Kufanikiwa kuweka mkobani media, viongozi (wakuu) wa upinzani (CHADEMA, ACT Wazalendo na wengine!), viongozi wengine, wanaharakati na baadhi ya wasomi/wataalam (watetea chochote) si ishara ya ushindi maana wote hao wana ajenda zao! Wamejitoa ufahamu na kujigeuza kituko na aibu ya kitaifa kukidhi maslahi yao, njaa zao, uchumiatumbo wao, unafiki wao na usaliti wao!

d) Bahati nzuri, kila kukicha wananchi wengi zaidi wanaendelea kuwastukia. Watanganyika sio mafala!

e) Na usisahau kwamba mamluki hawako upinzani tu, hata CCM wako wengi tu! Kumbuka pia kwamba kila palipo na puppets, nyuma yao kuna puppet masters! After all, wote si mnategemea funds from the same source/basket...?! Na wote tunajua kwamba: It is the one who pays the piper that chooses the tune! Ndio maana hapo juu nimekitaja kitabu kiitwacho: "Confessions Of An Economic Hit Man" by John Perkins.

f) Naililia nchi yangu!

11) Usharika wa Chuki kwa Marehemu!

a) Usharika wa Chuki kwa Marehemu ni usharika wa mashaka!
b) Usharika wa 2025, uchumiatumbo, asali na peremende za mabeberu hauwezi kuivusha nchi. Labda kuiuza nchi!
c) Ni Usharika wa "nguvu ya soda". Haudumu ng'o!

12) Tafadhali rejea makala zangu "Sura Mbili za Tundu Lissu" (16.02.2019) na "Kilio cha Mpemba" (19.09.2022). Tafadhali rejea pia kitabu cha Baba wa Taifa kiitwacho: "Tujisahihishe".

10.0 Hitimisho

1) Licha ya yote niliyosema hapo juu, sina budi kumpa pongezi nyingi sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutochoka kupambana. Ni wazi kuongoza nchi yetu ni mapambano makubwa sana kuliko sisi tulio huku mtaani/chini tunavyodhani.

2) Namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa uchokozi wake mzuri (ingawa unaokera sana!) kwa wasomi na wataalam wa Tanzania. Nilivyomuelewa mimi, Rais Samia amewataja wanasheria kama mfano tu wa mapungufu na changamoto kubwa tulizo nazo (baadhi ya) wasomi na wataalam wa Bongo.

3) Mapungufu haya ni pamoja na:

a) Uwezo mdogo. (Incompetence)
b) Kutojua vizuri Kiingereza.
c) Kutojua vizuri Kiswahili.
d) Kutawaliwa na hujuma, rushwa, wizi na ufisadi. (Corruption)
e) Kuendekeza/kuingiza siasa kwenye kazi za kitaalam.
f) Kutojiamini na unafiki.
g) Kuabudu Wazungu.
h) Kiburi. (Arrogance)
i) Kutokuwa na uzalendo.
j) Viwango duni.
k) Kufanya karibu kila kitu kwa "mazoea" na kwa "staili la bora liende". Wasomi na wataalam wengi kukubuhu katika copy-and-paste.
l) Kutokuwa makini. (Lack of seriousness)

4) Mimi BJC namuunga mkono Rais Samia katika uchokozi wake huu iwapo anamaanisha hivyo nikivyodhani na anakubali kwamba changamoto hii si ya wanasheria peke yao, bali pia:

a) Viongozi wa mihimili yote mitatu (yaani Serikali, Bunge na Mahakama).
b) Viongozi wa kisiasa.
c) Wanahabari.
d) Wanaharakati.
e) Walimu na wanafunzi wao (at all levels).
f) Wasomi na wataalam wa fani zote nchini.

5) Mfano mzuri ni hiyo taarifa ya serikali (kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi). Hii taarifa ina makosa mengi! Kwa Unyenyekevu mkubwa, heshima na taadhima, najiuliza:

a) Profesa (ambaye pia ni Mkurugenzi) alikubalije taarifa muhimu ya Serikali itolewe na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikiwa na makosa yote haya?!
b) Napata tabu kuamini kwamba Profesa aliisoma kwa makini taarifa hii, akaona iko sawa na akaidhinisha itolewe hivyo ilivyo!

6) Huu ungekuwa mwanzo mzuri sana wa kujadiliana kuhusu "Uchokozi wa Rais Samia"!

7) Naomba nichangie Uchokozi wa Rais Samia kwa kukumbushia:

a) Ripoti ya Kamati ya Mwakyembe Kuhusu wanafunzi wengi kufeli Shule ya Sheria (Law School). Ningependa kuisoma Ripoti ya Mwakyembe kwa makini. Usikute Uchokozi wa Rais Samia umeegemea huko...!
b) Makala yangu ya tarehe 10.10.2022 yenye Kichwa: "Siamini Kwamba Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini Hawajui Kusoma na Kuandika".

8) Kunogesha Uchokozi wa Rais Samia ningechomekea pia:

a) Ujuha wa Mtu Mweusi.

b) Kujiongopea kwamba Wazungu na Weupe wengine ndio watakaotuletea maendeleo (kupitia "mikopo" na "misaada" inayoharibu nchi na kutunyang'anya Uhuru wetu).

c) Nchi kutoendeshwa kwa misingi ya utawala wa sheria/Katiba, bali kwa "busara" na "mihemko" ya Rais.

d) Nchi kukumbatia ufisadi/mafisadi pamoja na "hadaa za miaka mitano mitano". Kusilimishana kwa asali, tende na harua!

e) Taasisi dhaifu.

9) Hilo ndilo "Gunia la Baadhi ya Madudu" yanayoihangaisha nchi yetu!

10) Nimemkumbuka Mchungaji Christopher Mtikila...!

11) HAPPY NEW YEAR 2023!!

12) MUNGU IBARIKI TANZANIA!

BJC. DSM. 06.01.2023. 2023hrs.
 
Nakanusha!!!
Huyu ni mbaya wa aliyeshika remote kwenye hii cenema
 
Punguza uzi.. tuna soma kitu kile kile kinajirudia ..inachosha kusoma. Summarize buana,
Ni uzi wa mtu huwezi kuupunguza nimeuwasilisha kama alivyoundika na kuusambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii
 
Kwa kukujibu tu.
Ni kweli kabisa Makamba alikuwa sahihi kusema kuwa wema hawafi. Alichokosea ni kutokamilisha sentensi ya maneno ambayo naamini aliyasikia mahali ila hakuyasikia kwa ukamilifu...
Yesu akasema, yeye aniaminiye mimi (mtu mwema), hatakufa, ajapokufa, atakuwa anaishi.
Hii ina maana kama 'huyo mtu wako' naye alikuwa mtu mwema (kwa viwango vilivyowekwa na Bwana Yesu, na sio kwa viwango vilivyowekwa na wana propaganda), basi naye atakuwa anaishi sawa sawa na maandiko katika Biblia.
Screenshot_20230109-185316.jpg
 
Kwa kukujibu tu.
Ni kweli kabisa Makamba alikuwa sahihi kusema kuwa wema hawafi. Alichokosea ni kutokamilisha sentensi ya maneno ambayo naamini aliyasikia mahali ila hakuyasikia kwa ukamilifu...
Yesu akasema, yeye aniaminiye mimi (mtu mwema), hatakufa, ajapokufa, atakuwa anaishi.
Hii ina maana kama 'huyo mtu wako' naye alikuwa mtu mwema (kwa viwango vilivyowekwa na Bwana Yesu, basi naye atakuwa anaishi sawa sawa na maandiko katika Biblia.View attachment 2475304
Unatukosea sana wasoma maandiko.

Umeamua kufanya upotoshaji kabisa wa neno hili.

Fungu hili mbona ni Rahisi tu.

Kwanza ujue Mungu ashasema hakika tutakufa, na kweli tunakufa.

Hapo yesu alijua hili. Kikubwa uelewe kwamba. Amwaminie Yesu atapata uzima wa milele. Manaa yake ni kwamba hata akifa leo anakuwa amelala tu, siku ya mwisho atafufuliwa, ataapaa mbinguni, kisha atarudi kukaa kwenye nchi mpya milele na milele.
 
Uko makini sana na Neno big up. Hao wanataka kuficha uchafu wao kupitia Biblia Takatifu.
 
Ndugu BJC. DSM, hakika umenitoa machozi kwa uzi huu nadhani watanzania wengi watajifunza mengi kupitia bandiko hili Lucas mwashambwa naamini utasaidia kujibu hoja za BJC.
 
hivi hili sakata la vifaranga liliishaje ishaje mbona kama ilikuwa kashfa kubwa sana vifaranga kufia airpot
 
Natamani afufuke uwe mpinzani ufilwee e kwa maagizo yake kama waliyofanywa waliompinga afu uandike tena utoto wako hapa
 
Mbo

12) MUNGU IBARIKI TANZANIA!arty

BJC. DSM. 06.01.2023. 2023hrs.
Mbona uzi wenye umejaa uchochezi tu,kwani watoka wing ya sgang au mwana umoja party 🤔
 
Bandiko fupi sana, ongeza juhudi linalofatia liwe refu zaidi.

Kazi ya Mungu haina makosa.
 
Vimechomwa kwa kukosa solo.Je, baada ya kukosa soko ulidhani mwekezaji ilibidi afanye nini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom