eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 17,780
- 16,455
kwa kila mwanasiasa wa tanzania anaetaka kuungwa mkono na wananchi wengi amekuwa akijitahidi kujionesha kuwa ni mfuasi wa rais wa kwanza wa tzania mwl nyerere. Anasifiwa kwa kila kitu lakini kwangu mimi simkubali kabisa mwl nyerere. Siamini kama alikuwa na kipaji cha uongozi. Alikuwa ni dikteta. Alifinya uhuru wa habari, aliwafunga wapinzani wake, alileta umasikini mkubwa kwa taifa na wananchi wa tzania. Si kwamba alikuwa anapendwa bali alikuwa anaongoza wananchi wengi wasiojua dunia inakwendaje"wajinga".
Huyo ndio nyerere. Kwa miwani yangu namuona kuwa ana mabaya mengi kuliko mazuri kama tunavyolazimishwa kuamini. Kutojilimbikizia mali au kutoa huduma za jamii bure si kigezo cha kutokuwa dikteta maana hata pinnochet, hitler na mussolin walikuwa wanatoa huduma za jamii bora na bure kabisa kwa watu wao.
nenda kusini nenda kaskazini, nenda magharibi nenda mashariki, hakuna kiongozi dikteta ambaye ameacha madaraka kwa hiyari, huku wananchi wake wakimlilia. Kama Nyerere angewaumiza wananchi wake wangemchukia na katu wasingemkumbuka kama ilivyo sasa. Kama angekuwa dikteta asingelipigania usawa, vita dhidi ya mafisadi, kupigania mgombea binafsi, Kuifafanua katiba kuwa ni kama vazi la kijana ambalo huwa linamtosha kwa kipindi fulani. Lakini baada ya muda fulani vazi hilo halimtoshi tena, linambana. Hivyo anahitaji vazi lingine.
nenda uendako hakuna kiongozi kama nyerere. Ambaye alikuwa anahangaishwa na umaskini wa watu wake.