Ni kweli nyerere hakupigania uhuru bali alipewa tuu. Hata babaako kama angekuwa mstari wa mbele ktk chama angepewa huo uhuru. Kumbukeni kuwa kipindi hicho tulikuwa chini ya himaya ya waingereza baada ya mjerumani kushindwa ww2. Mkumbuke pia kuwa alikwenda UNO kwenye mkutano miaka ya 1958 akisindikizwa na baadhi ya wahindi (waliosponsor safari yake huko) . Maadhimio ya mkutano huo yalikuwa kwamba watanganyika wasubiri kidogo hadi 1961 ndo watapewa huo uhuru wanaodai. Kwa wale mtakaokumbuka, nyerere alipokuwa anarejea toka yuno akiwa eapot alikuwa ameshikilia bango lenye ujumbe wa kuwa "uhuru 1961'. Kwa hiyo ni kweli kabisa nyerere hakupigania uhuru. Kumbukeni kuwa wakati wa mkoloni kulikuwa na matabaka yaani wazungu(tabaka la juu) waasia(kati) na weusi(chini).
Yaani hapa ndio tuna tatizo mnageuza kabisa historia ili kujenga hoja inayofuata hapa chini na mnataka tukubali kuwa ndivyo uhuru ulivyopatikana. Kwanini Nyerere aliacha kufundisha Pugu? Alipokuwa Makerere alikuwa kiongozi wa nini na kwanini? Unayajua maandishi ya Mwalimu alipokuwa Uingereza masomoni na ni kitu gani alikuwa anakifanya au unataka tuamini tu alikuja akakaa na wahindi (wanaojua sana kulobby) na wakasema nenda kachukue uhuru!?
waasia(wahindi) walikuwa wanaloby namna ambavyo watakuwa tabaka la juu na ndio maana walishadadia sana na kusupport move yote ya kuomba uhuru. Mtakubaliana na mimi kwamba wahindi ni wataalamu wa lobying.mtakubaliana na mimi pia kuwa katika wageni wote waliokuwapo enzi za ukoloni, ni wahindi pekee ndo hawakufukuzwa na ndo hadi sasa wako wanamiliki biashara nyingi na kuishi katika maeneo prime ya miji yetu mikubwa. Watu kama akina mtikira ndo maana walikuwa wanamchukia sana nyerere kwa kuwabeba "magabachori'
Hatukubaliani na wewe! kwanza unapotosha hoja kuwa "wahindi pekee ndo hawakufukuzwa" nani alifukuzwa mgeni?
Kwa maana nyingine ni sawa na sasa ambapo matajiri (akina rostam na wengineo) wananyenyekewa kwa sababu ya kusupport chama. Hata enzi za mwalimu walikuwepo. Ninachoweza kusema ni kuwa Nyerere alikuwa na "stupidity innocense". Mkumbuke kuwa amepewa nchi akiwa a mere guy, hajui mambo ya uchumi,hana chochote yaani hakuwa na experience yoyote ya uongozi pamoja na kuwa kiongozi wa TAA na baadae Tanu.
yaani, hata huoni self-contradiction humo humo!! What is "mere guy"? Kwanini hawakumpata mtu mwingine ambaye alikuwa "a mere guy". Mnasema hakuwa anajua mambo ya uchumi - yaani mtu anashahada ya pili ya uchumi mnasema alikuwa hajuii mambo ya uchumi?
Ujinga na uppuuzi wake unakuja pale alipokuwa hataki ushauri toka kwa watu wataalamu kama akina mtei, kolimba nk. Mjue pia kuwa ndo maana uongozi wa Nyerere ulijaa viongozi ambao noi ma yes men/women. Yeyote aliyeonekana kuchallenge aliwekwa kizuizini au kupelekwa mbali mfano kuwa balozi.
Na hawa waliokubali ushauri wa mawaziri wao wa fedha (basil Mramba) na kina Mgonja na wengine "upuuzi wao na ujinga wao" uko wapi? Yaani, mnaamini kabisa kuwa kama Nyerere angekubali hoja zote za Mtei nchi isingekuwa hapa ilipo? Really? Mtei si yupo hai hadi leo hii kwanini serikali haijaa kumuuliza ushauri wake na tuone kama wataufanyia kazi? Mtei si ameandika mara kadhaa na kutoa ushauri hata hadharani amesikilizwa na nani?
Na kama wengine mnapotosha ukweli ati "yeyote aliyeonekana kumchallenge" aliwekwa kizuizini? Really? Embu tutajieni watu waliowekwa kizuizini kwa kumchallenge Nyererer. Na kupelekwa Ubalozini kuwa balozi ni adhabu? ! Hivi mnajua madikteta wa kweli hufanya nini na watu wanaowachallenge kiukweli - mnioneshe dikteta aliyempa mtu kazi ya kuwakilisha taifa lake nje baada ya kumpinga na mimi nikutaonesha waliowasindikiza makaburini waliowapinga!
Ukiangalia uchumi wa Tanganyika na baadae Tanzania utagundua kuwa wakoloni walituacha pazuri sana. Baada ya kupewa uhuru nyerere na wenzake walikuwa wakisherehekea tangu hiyo 61 hadi kuungana na zanzibar. Miaka yote hiyo no production at all. Kilichokuwa kinafanyika ni kuchukua kwenye hivyo viwanda. Kuja kutahamaki uchumi unaanza kuyumba na yeye kuja na arusha declaration(ujamaa na kujitegemea-african socialism) kama suluhisho la kurevive uchumi.
Yaani hadi najihisi mzee! ati Wakoloni walituachia uchumi mzuri? TAfuta takwimu za uchumi wetu kati ya miaka kumi baada ya uhuru (1961 -1971) na ulinganisha na miaka 50 kabla ya Uhuru! Halafu utuambie ni upi ulkuwa bora.
Lakini kwa sababu ya mipango mibovu inashindwa. Come 1972 anakuja na villagilization anahamisha watu mahali ambapo walizoea kulima( kwa maana wanajua majira ya mwaka, udongo nk) na kupelekwa sehemu ngeni.
Hapa ndio inaonekana watu hata hamjui historia yetu. Swali la kuuliza ni kwanini ulikuja mpango wa kutengeneza vijijini vipya na kuachana na vile vya asili? Leo hii kama nilivyosema hapo nyuma Tanzania imeundwa na vijiji vilivyoundwa wakati wa Nyerere na vichache ambavyo viliachwa. Ikumbukwe si vijiji vyote vilihamishwa kulikuwa na sababu za kiutawala, usalama na huduma ambazo ililazimisha kuleta watu karibu. Lakini vile vile watu wanachukulikia kirahisi rahisi tu kujenga taifa. Hivi, mnafikiri Marekani ya leo watu walijikuta tu wanahamia kwenye miji ya kisasa? Hivi mnafikiri China ya leo isingetengenezwa na kina Mao (kwa gharama kubwa sana) ingekuwa na nguvu tunayoiona nayo leo?
Kati ya vitu ambavyo historia itamhukumu Nyerere vizuri zaidi ni kuleta wananchi pamoja katika muundo wa vijiji vya kisasa. Tatizo kubwa ambalo leo tunajua vizuri kwanini ni kuwa hakukuwa na mfumo mzuri wa kusimamia na kama tatizo la watendaji wa leo ambao ni wasomi sana tunaliona katika mambo mbalimbali fikiria mwaka 1972 watendaji wetu walikuwa na elimu na uzoefu gani kukamilisha mradi ule mkubwa.
Matokeo yake watanzania wakawa stranded. Hawajui cha kufanya. Unapita msimu wa kwanza na wapili kwani hawajui ni zao gani walime na majira hawayajui. Baati mbaya ukame unaikumba nchi miaka ya 1975 na kuleta disaster ya njaa. Kumbuka kuwa tangu 1972 uzalishaji wa chakula unayumba kwa sababu ya vilagisation, ukame unaikumba nchi, matokeo yake ni njaa. Kama mnakumbuka enzi za unga wa Yanga kama msaada toka marekani. 1978 vita ya kagera ambayo inaigharimu tanzania mamilioni ya shilingi. Kwa hiyo tanzania ikawa haina pesa hata kidogo.
Tatizo unataka kukwepa historia; matatizo ya mwanzoni ya miaka ya sabini ilikuwa ni pamoja na kuyumba kwa uchumi wa dunia na vile vile bei ya mafuta kupanda sana mwaka 1970. Kama tunavyoona leo hii baada ya kuyumba uchumi wa dunia jinsi gani hata mataifa yaliyokuwa yako yamesimama yaliyoumba. Sisi tuliyumba kidogo lakini guess what? Nyerere hakuona aibu kuomba msaada wa chakula na baadaye kuhakikisha tunalima chakula cha kutosha sana. Hata leo hii miaka karibu 40 tangu wakati ule Tanzania bado inahangaika na tatizo la njaa! Kama tatizo lilikuwa Nyerere kwanini leo bado watawala wetu wameshindwa kulitatua tatizo hilo?
Kuna tetesi kuwa baada ya vita na I'd amin nyerere alitaka kung'atuka lakini intellijensia ikamshauri asubiri na akaamua kusogea hadi hiyo 1985. Alipong'atuka na kuwa nje ya uwanja ndo akaanza kuhisi madudu aliyofanya na kuwa kama mshauri wa serikali.
Haikuwa tetesi, Nyerere alitaka kustaafu mapema zaidi. Na siyo alitaka tu alishawahi kujiuzulu uongozi serikalini (na kumuachia Kawawa)! Lakini upotoshaji mwingine wa historia ni kudai kuwa ni baada ya "kuwa nje ya uwanja ndo akaanza kuhisi madudu". HIili nalo si kweli. Labda tafuta kijitabu kiitwacho "Tujisahihishe" utaona kuwa Nyerere alifanya kitu ambacho hakuna Rais mwingine wa Tanzania amewahi kukifanya nacho kujiangalia kiuongozi na kusahihisha makosa! Hakusubiri atoke madarakani kama Mwinyi, au Mkapa walivyofanya.
haya mengine ni recent histori nitawaachia wengine.
and corrected you are.