Mmeuza vyote alivyoanzisha mwalimu leo mnaona hata hafai, hao ndio watanzania wa sasa wa kizazi cha bongo freva, hamjui hata mlikotoka. Wewe unaamini kiswahili unachozungumza kutoka Mtwara, Pemba, (Kalya) Kigoma, mpaka Bukoba kimekuja hivihivi. Hospital za Bugando,Maweni Kigoma, Rufaa Mbeya, Mhimbili, Moshi.....n.k na Viwanja vya michezo kila mkoa wa Tanzania, vililetwa hivihivi. Muanzisha thread inaonekana either umri wako ni mdogo na hujui historia ya Tanzania na Dunia kwa ujumla au una lako jambo, au umetumwa au unapima bongo za Watz. Nyerere aliongoza katika vipindi vizuri na vibaya kabisa kwa historia ya Dunia. Wakati mfumo wa Kidunia unabadilika kutoka Vita baridi kuja hali ya sasa yenye Unitary super power nchi ilikuwa chini ya Nyerere. Nyerere ameongoza nchi during world oil crisis. Mwalimu kaongoza Tanzania wakati wa vita na Uganda.Hujui nchi hii imetoka wapi. Ni kweli Nyerere alikwa na mapungufu yake lakini huwezi kufananisha utawala wake na Kiongozi yoyote aliyefuata. Kama unaamini Nyerere aliacha nchi katika hali mbaya, basi kwa taarifa yako kama umri wako mdogo mpaka Mwinyi anaondoka mwaka 1995, ofisi za Serikari zilikuwa hazina hata karatasi, mahakamani kama umemshitaki mtu, tulikuwa tunanunua karatasi wenyewe. Mkapa alichofanya ni kuuza viwanda na mashirika, na alikuwa makini kidogo kukusanya kodi na alifanya vizuri muhula wa kwanza. Muhula wa pili alianza kujilimbikizia mali na fedha nyingi alizokusanya alijigawia vya kutosha. Huyu mkwere ndio hamna kitu kabisa. Alivyoingia madarakani alikuta mabaki ya fedha aliyoacha Mkapa. Akachanganyikiwa akaanza kuzigawa, kwa kubuni utaratibu kama Mabirilioni ya JK, akagawa anavyojisikia, kwa kuwa Mkwere masikini hakuzoea kuona hela nyingi kama ile, wala hajui kama ni fedha za selikari na wala kwa sasa hatujui yeye alikwapua ngapi. Na sasa selikari haina akiba ya kutosha.
Tusubiri mkwere amaliza muda waka ila kwa mwendo anaokwenda wala hata hamfikii hata punje Mwalimu. Mwalimu mwache apumzike kajenga Taifa la Tanganyika, hilo namkubali ila ukichanganya na Zanzibar hapo nakubali kuna kasoro kwenye muungano na ni changamoto ya viongozi wa sasa kuweka mambo sawa.