Rugemeleza
JF-Expert Member
- Oct 26, 2009
- 668
- 138
Ni kweli nyerere hakupigania uhuru bali alipewa tuu. Hata babaako kama angekuwa mstari wa mbele ktk chama angepewa huo uhuru. Kumbukeni kuwa kipindi hicho tulikuwa chini ya himaya ya waingereza baada ya mjerumani kushindwa ww2. Mkumbuke pia kuwa alikwenda UNO kwenye mkutano miaka ya 1958 akisindikizwa na baadhi ya wahindi (waliosponsor safari yake huko) . Maadhimio ya mkutano huo yalikuwa kwamba watanganyika wasubiri kidogo hadi 1961 ndo watapewa huo uhuru wanaodai. Kwa wale mtakaokumbuka, nyerere alipokuwa anarejea toka yuno akiwa eapot alikuwa ameshikilia bango lenye ujumbe wa kuwa "uhuru 1961'. Kwa hiyo ni kweli kabisa nyerere hakupigania uhuru. Kumbukeni kuwa wakati wa mkoloni kulikuwa na matabaka yaani wazungu(tabaka la juu) waasia(kati) na weusi(chini). Kwa maan hiyo waasia(wahindi) walikuwa wanaloby namna ambavyo watakuwa tabaka la juu na ndio maana walishadadia sana na kusupport move yote ya kuomba uhuru. Mtakubaliana na mimi kwamba wahindi ni wataalamu wa lobying.mtakubaliana na mimi pia kuwa katika wageni wote waliokuwapo enzi za ukoloni, ni wahindi pekee ndo hawakufukuzwa na ndo hadi sasa wako wanamiliki biashara nyingi na kuishi katika maeneo prime ya miji yetu mikubwa. Watu kama akina mtikira ndo maana walikuwa wanamchukia sana nyerere kwa kuwabeba "magabachori'
Kwa maana nyingine ni sawa na sasa ambapo matajiri (akina rostam na wengineo) wananyenyekewa kwa sababu ya kusupport chama. Hata enzi za mwalimu walikuwepo. Ninachoweza kusema ni kuwa Nyerere alikuwa na "stupidity innocense". Mkumbuke kuwa amepewa nchi akiwa a mere guy, hajui mambo ya uchumi,hana chochote yaani hakuwa na experience yoyote ya uongozi pamoja na kuwa kiongozi wa TAA na baadae Tanu. Ujinga na uppuuzi wake unakuja pale alipokuwa hataki ushauri toka kwa watu wataalamu kama akina mtei, kolimba nk. Mjue pia kuwa ndo maana uongozi wa Nyerere ulijaa viongozi ambao noi ma yes men/women. Yeyote aliyeonekana kuchallenge aliwekwa kizuizini au kupelekwa mbali mfano kuwa balozi.
Ukiangalia uchumi wa Tanganyika na baadae Tanzania utagundua kuwa wakoloni walituacha pazuri sana. Baada ya kupewa uhuru nyerere na wenzake walikuwa wakisherehekea tangu hiyo 61 hadi kuungana na zanzibar. Miaka yote hiyo no production at all. Kilichokuwa kinafanyika ni kuchukua kwenye hivyo viwanda. Kuja kutahamaki uchumi unaanza kuyumba na yeye kuja na arusha declaration(ujamaa na kujitegemea-african socialism) kama suluhisho la kurevive uchumi. Lakini kwa sababu ya mipango mibovu inashindwa. Come 1972 anakuja na villagilization anahamisha watu mahali ambapo walizoea kulima( kwa maana wanajua majira ya mwaka, udongo nk) na kupelekwa sehemu ngeni. Matokeo yake watanzania wakawa stranded. Hawajui cha kufanya. Unapita msimu wa kwanza na wapili kwani hawajui ni zao gani walime na majira hawayajui. Baati mbaya ukame unaikumba nchi miaka ya 1975 na kuleta disaster ya njaa. Kumbuka kuwa tangu 1972 uzalishaji wa chakula unayumba kwa sababu ya vilagisation, ukame unaikumba nchi, matokeo yake ni njaa. Kama mnakumbuka enzi za unga wa Yanga kama msaada toka marekani. 1978 vita ya kagera ambayo inaigharimu tanzania mamilioni ya shilingi. Kwa hiyo tanzania ikawa haina pesa hata kidogo.
Kuna tetesi kuwa baada ya vita na I'd amin nyerere alitaka kung'atuka lakini intellijensia ikamshauri asubiri na akaamua kusogea hadi hiyo 1985. Alipong'atuka na kuwa nje ya uwanja ndo akaanza kuhisi madudu aliyofanya na kuwa kama mshauri wa serikali.
Mkumbuke pia kuwa uchumi ulipoanza kuyumba miaka ya 1975 mataifa mbalimbani wakiwemo IMF walikuwa wakishauri nchi yetu kujiunga na stractural adjustment programs(SAPs) kama suluhisho la uchumi lakini nyerere alikataa kabisa. Baada ya nyerere kujiuzuru, haya mataifa yaliendelea kushauri serikali kwani hali ya uchumi ilikuwa mbaya sana. Sharti mojawapo kwenye hizo SAPs ilikuwa ni kuingia kwenye vyama vingi. Ilipofika mwaka 1992 kukawa hamna jinsi na nyerere akamshauri mwinyi akubaliane na hilo sharti. Lakini kwa sababu mwamko wa vyama vingi ulikuwa mdogo miaka hiyo ikabidi nyerere amuombe mrema(usalama wa taifa) aanzishe chama kama kiini macho kwa haya mataifa ili tuweze kuendelea kupata misaada. Mantiki ikiwa sio kukifanya kiwe chama kikubwa bali kiwe kama chambo kwa haya mataifa. Hapo ndipo nccr mageuzi ikazaliwa na vyama vinginevyo. Kama mtakumbuka nccr mageuzi ilipanda chati sana 1995. Mtakumbuka pia kwenye baadhi ya mahojiano ya nyerere aliwahi kusema hatuwezi kumuachia mwizi(mchaga),mbwa(askari) kwenda ikulu na ndipo nyerere akaingilia kati kufanya kampeni chafu dhidi ya mrema hadi nccr kukosa uraisi 1995. Mkapa akaingia ndani ya mjengo kwa mgongo wa mwalimu.
Naomba kuhitimisha kwa kusema kuwa nyerere kweli hakuwa kiongozi mzuri, na hakuwa anasilikiza ushauri toka kwa mtu yeyote. Laiti kama angeshaurika tusingekuwa hapa tulipo. Kwa hiyo haya yanayotokea sasa ni matokeo ya uongozi mbovu na wakidikteta aliokuwa nao nyerere.
I stand to be corrected.
Debe tupu haliachi kupiga kelele! Lakini kelele nyingine ni za kutia aibu!