Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Jasusi:
Si jambo la kuficha kuwa kuna kikundi chenye mlengo na kusudio maalum la kumchafua Nyerere tokea siku nyingi. Lakini juhudi zao hazifui dafu kila wanapopambana na kivuli cha mwanamapinduzi huyu.
 
Haujawahi kusikia? ajabu sana, ngoj nikusikilizishe kwa kifupi tuu. Nyerere aliwahamisha zaidi ya watu million kumi kutoka vijiji, miji au sehemu zao za asili na kuwapeleka sehemu mpya, ya amma kulikuwa kuna vijiji vidogo vya asili na watu wapya wakabwagwa na kuwachwa hapo bila ya kuwa na facilities zozote za kuweza kukidhi mahitaji yao kila siku au walichukuliwa na kubwagwa maporini ambapo hakuna hata kijiji wala nyumba za kuishi, wengi wao walikufa kwa kuliwa na wanyama wa kali wa porini, wengine waligongwa na nyoka, wengine walikufa kwa njaa, wengine walikufa kwa kula mizizi ya sumu kwa njaa, wengine walikufa kwa kukosa matibabu. Ni wengi sana waliokufa na ilikuwa ni marufuku kuandikwa habari mbaya yeyote, waandishi wachache waliokuwepo wakati huo, ilikuwa ni lazima waandike inavyotaka serikali.

wengine walikufia jela kwa sheria yake ya ditenshen aliyoiweka, sijui kama imefutwa hii au bado ipo, watu wengi walikuwa wakionekana kupinga tuu siasa zake, walishikwa na kuwekwa vizuizini bila kuhojiwa wala kupelekwa mahakamani aidha mpaka wafie huko au mpaka nyerere mwenyewe awakumbuke na kuwawachia, hakuna mtu mwingine yeyote kwenye serikali aliyekuwa na ubavu wa kukutowa ditenshen isipokuwa nyerere mwenyewe.

Mbali ya hayo, mahospitali yalikuwa bure lakini huduma mbovu kabisa na ndio mpaka sasa hali imebaki hivyo-hivyo. Yaani alifisadi kila kitu.

KUCHEKA na kuchekesha watu, hilo ndio moja linalonishangaza mpaka leo, kwa yote aliyokuwa akiyafanya lakini bado alikuwa na uwezo wa kucheka na kuchekesha watu na aliupata usingizi. Hiyo ni dalili ya ukatili wa hali ya juu. Kumbuka wakati huo alikuwa akiweka masharubu yake kama hitler.

Ni mengi mabaya aliyoyafanya na ndio maana unaona ufisadi uliokithiri leo hapa nchini unatokana na hawa viongozi aliowarithisha yeye. Hawana huruma hata kidogo na wananchi kama alivyo yeye. Na aliyejaribu kumpinga kidogo alikiona. Abood Jumbe ni mfano mzuri, aliwachishwa umakamu wa rais akawekwa house detention akakatiwa umeme, maji, marupupu yake ya umakamu wa rais mpaka alipotubu kwa nyerere kuwa hatosema lolote na hatoingilia tena mambo ya siasa ndio akafunguliwa. Na toka wakati huo akawa kimya mpaka wakati wa mwinyi ndio akathubutu kuandika kitabu kilichogusia kidogo siasa za kidikteta za nyerere.

Ni wengi tuu aliowauwa nyerere kwa maamuzi yake mabovu, na umasikini uliokithiri ametutakia yeye, inasemekana kuwa kuanzia mwaka 1965, mpaka anaacha urais uchumi wa tanzania ulikuwa ukishuka kwa 0.03% kila mwaka. Hatari kubwa.

Population yetu wakati wa Operation hiyo ilikuwa ni watu wangapi?
 
Huyo nyerere ndie alikuwa fisadi mkuu wa Tanzania, au haukuwepo wakati wake na unamsoma tuu kwenye historia za uwongo? Tuulize sisi tuliokosa bahati kwa kuwepo na kuonja joto na madhila ya uongozi wake.

Hizo enzi zako unazosema, tungelikuwa na viongozi hawa tulionao kwa wakati huo, leo hii tusingeonana hapo JF. Nakuachia utafakari au ni chuki binafsi au ni nini????
 
Haujawahi kusikia? ajabu sana, ngoj nikusikilizishe kwa kifupi tuu. Nyerere aliwahamisha zaidi ya watu million kumi kutoka vijiji, miji au sehemu zao za asili na kuwapeleka sehemu mpya, ya amma kulikuwa kuna vijiji vidogo vya asili na watu wapya wakabwagwa na kuwachwa hapo bila ya kuwa na facilities zozote za kuweza kukidhi mahitaji yao kila siku au walichukuliwa na kubwagwa maporini ambapo hakuna hata kijiji wala nyumba za kuishi, wengi wao walikufa kwa kuliwa na wanyama wa kali wa porini, wengine waligongwa na nyoka, wengine walikufa kwa njaa, wengine walikufa kwa kula mizizi ya sumu kwa njaa, wengine walikufa kwa kukosa matibabu. Ni wengi sana waliokufa na ilikuwa ni marufuku kuandikwa habari mbaya yeyote, waandishi wachache waliokuwepo wakati huo, ilikuwa ni lazima waandike inavyotaka serikali.

wengine walikufia jela kwa sheria yake ya ditenshen aliyoiweka, sijui kama imefutwa hii au bado ipo, watu wengi walikuwa wakionekana kupinga tuu siasa zake, walishikwa na kuwekwa vizuizini bila kuhojiwa wala kupelekwa mahakamani aidha mpaka wafie huko au mpaka nyerere mwenyewe awakumbuke na kuwawachia, hakuna mtu mwingine yeyote kwenye serikali aliyekuwa na ubavu wa kukutowa ditenshen isipokuwa nyerere mwenyewe.

Mbali ya hayo, mahospitali yalikuwa bure lakini huduma mbovu kabisa na ndio mpaka sasa hali imebaki hivyo-hivyo. Yaani alifisadi kila kitu.

KUCHEKA na kuchekesha watu, hilo ndio moja linalonishangaza mpaka leo, kwa yote aliyokuwa akiyafanya lakini bado alikuwa na uwezo wa kucheka na kuchekesha watu na aliupata usingizi. Hiyo ni dalili ya ukatili wa hali ya juu. Kumbuka wakati huo alikuwa akiweka masharubu yake kama hitler.

Ni mengi mabaya aliyoyafanya na ndio maana unaona ufisadi uliokithiri leo hapa nchini unatokana na hawa viongozi aliowarithisha yeye. Hawana huruma hata kidogo na wananchi kama alivyo yeye. Na aliyejaribu kumpinga kidogo alikiona. Abood Jumbe ni mfano mzuri, aliwachishwa umakamu wa rais akawekwa house detention akakatiwa umeme, maji, marupupu yake ya umakamu wa rais mpaka alipotubu kwa nyerere kuwa hatosema lolote na hatoingilia tena mambo ya siasa ndio akafunguliwa. Na toka wakati huo akawa kimya mpaka wakati wa mwinyi ndio akathubutu kuandika kitabu kilichogusia kidogo siasa za kidikteta za nyerere.

Ni wengi tuu aliowauwa nyerere kwa maamuzi yake mabovu, na umasikini uliokithiri ametutakia yeye, inasemekana kuwa kuanzia mwaka 1965, mpaka anaacha urais uchumi wa tanzania ulikuwa ukishuka kwa 0.03% kila mwaka. Hatari kubwa.

Naomba idadi ya Watanzania wakati wa hiyo operation.
 
ana mapungufu yake kama binadamu yoyote lakini he was much better kuliko mifisi iliyopo madarakani saivi
.
 
samahani,mwana JF kama kuuza nchi ilikuwa ni ajenda yakutosha ya Kaka Ben Mkao Wahapa-ameuza mpaka kachukiza.Aliweka mikataba mibovu mfano wake hakuna.Kwani watu wamesahau wale makaburu walokuja kuwekeza kwenye maji jijini kama hujui muulize huyo mchumba wa msanii jafarai maana alikuwa meneja mahusiano.
Huko AFGEM na KAHAMA-yote hayo ni Mkapa.Angalia nyumba zetu za ILALA jamaa alikuwa akimfurahisha Mke-maana asingempatia angemvunja mguu wa pili.Hebu mwacheni JK kama uchungu nanchi ndio sasa kaupata nategemea hatorudia makosa.
 
Naam, hapa kuna ukweli na ushahidi wa kutungwa(kama ukweli na ushahidi wa namna hiyo upo).

Na kwa watu waliokwishajiaminisha ukweli huo hapawezi kuwepo na ukweli mwingine.

Kwa wat wa namna hiyo,haijalishi, hata kama halaiki ya wananchi waliomuenzi Mwalimu wanapoendelea kumheshimu na kumtukuza; ni wao tu ndio wenye ukweli. Kwa maneno mengine, waTanzania walio wengi ni vichaa kwa kumwona Nyerere kuwa kiongozi aliyetukuka. Ni akina Zomba tu ndio wenye akili timamu. Sasa wanyo kazi ya kututibu ukichaa huu, nasi tufanane nao watu wenye akili timamu. But the reverse of this seems more plausible.

Huo ni muono wako nami sina uwezo wa kuuingilia wala kukubadilisha mawazo. Isipokuwa, facts zijibu kama unaweza:

Jee, nyerere hakuhamisha watu takriban millioni kumi kutoka makazi yao ya asili?

Jee, nyerere hakusababisha kati ya aliowahamisha wafe kwa, kuliwa na wanyama? kugongwa na majoka? kukosa chakula? kula mizizi yenye sumu kwa njaa? kukosa matibabu?

Jee, nyerere hakuanzisha sheria ya "ditenshen" amabyo hakuna aliyeweza kukutowa isipokuwa yeye?

Jee, watu aliowa-"ditenshen" nyerere wengine hawakufia jela?

Jee, nyerere, hakuzuwia habari kuandikwa isipokuwa inazotaka serikali yake tuu?

Nadhani hizo ndio hoja na hoja si mimi wala si wewe wala si mtanzania yeyote kuwa ni mwendawazimu. Wendawazimu ni maradhi kama maradhi mengine yeyote na si tabia njema kujumuisha watu na kuwatusi kama unavyotaka ieleweke. Naomba jibu facts.
 
Hizo enzi zako unazosema, tungelikuwa na viongozi hawa tulionao kwa wakati huo, leo hii tusingeonana hapo JF. Nakuachia utafakari au ni chuki binafsi au ni nini????

Ni kweli kabisa, na ndio maana kila jema alilofanya kikwete nimemsifu na nnadhani anaelewa mapungufu ya nyerere na anaelewa kuna viongozi wasiotaka kuamini kuwa nyerere ana mapungufu na ndio sababu JK alipigwa chini na nyerere mara ya kwanza alipowania urais na akapandikizwa mkapa, au umesahau?
 
Ndugu yangu Kalamu afadhali wewe umesema. Sikujua Jumbe alikatiwa umeme pale Mji Mwema mpaka Nyerere alipomsamehe. Na mbona hilo hakuliweka kwenye kitabu chake? Au naye alikuwa anaogopa adhabu kubwa zaidi?

Wewe si jasusi? ingia kazini utafute ukweli utaupata tu. Jumbe ni muungwana na muungwana "akitafunwa na mbwa hatangazi kidonda".
 
It's true kama zilivyo serikali nyingine zote, serikali ya JKN ilikuwa na mapungufu, LAKINI ni vema ikafahamika kuwa Mwalimu alikuwa akifanya yote hayo kwa maslahi ya taifa, tofauti na hawa wengine wanaofanya madudu kwa maslahi binafsi.
 
Huo ni muono wako nami sina uwezo wa kuuingilia wala kukubadilisha mawazo. Isipokuwa, facts zijibu kama unaweza:

Jee, nyerere hakuhamisha watu takriban millioni kumi kutoka makazi yao ya asili?

Jee, nyerere hakusababisha kati ya aliowahamisha wafe kwa, kuliwa na wanyama? kugongwa na majoka? kukosa chakula? kula mizizi yenye sumu kwa njaa? kukosa matibabu?

Jee, nyerere hakuanzisha sheria ya "ditenshen" amabyo hakuna aliyeweza kukutowa isipokuwa yeye?

Jee, watu aliowa-"ditenshen" nyerere wengine hawakufia jela?

Jee, nyerere, hakuzuwia habari kuandikwa isipokuwa inazotaka serikali yake tuu?

Nadhani hizo ndio hoja na hoja si mimi wala si wewe wala si mtanzania yeyote kuwa ni mwendawazimu. Wendawazimu ni maradhi kama maradhi mengine yeyote na si tabia njema kujumuisha watu na kuwatusi kama unavyotaka ieleweke. Naomba jibu facts.

Zomba, mi nadhani naelewa argument yako,lakini nahisi kwamba kuna a big amount of bitterness, wakati hakuna haja. Inaeleweka kwamba Nyerere alifanya kosa kubwa na vijiji vya ujamaa, na wakati ule alitaka kujenga jamii ya kishosalisti, lakini also lazima tukubali kwamba despite it all he was honest, hakujilimbikizia mali.
Nadhani tunaweza kuanza thread nyingine kuhusu Nyerere ingawa tayari imeshajadiliwa, but katika hili la Lowassa he was right!
 
Jasusi:
Si jambo la kuficha kuwa kuna kikundi chenye mlengo na kusudio maalum la kumchafua Nyerere tokea siku nyingi. Lakini juhudi zao hazifui dafu kila wanapopambana na kivuli cha mwanamapinduzi huyu.

kama kuna kikundi hicho mimi nakuhakikishia sikijuwi, msimamo wangu ni facts zisizopingika na nilikuwepo wakati wa nyerere na nimeyaona na si ya kusikia. jee hujuwi kuwa wakati wa nyerere tulikuwa kwenye dimbwi la umasikini?
 
Zomba, mi nadhani naelewa argument yako,lakini nahisi kwamba kuna a big amount of bitterness, wakati hakuna haja. Inaeleweka kwamba Nyerere alifanya kosa kubwa na vijiji vya ujamaa, na wakati ule alitaka kujenga jamii ya kishosalisti, lakini also lazima tukubali kwamba despite it all he was honest, hakujilimbikizia mali.
Nadhani tunaweza kuanza thread nyingine kuhusu Nyerere ingawa tayari imeshajadiliwa, but katika hili la Lowassa he was right!

Usemayo swadakta na yanaingia akilini, lakini huwezi kuwa ni chanzo cha kuuwa halaiki ya watu na si kwa ajali bali kwa maamuzi ya makusudi kabisa na ya muda mrefu, halafu ujitetee kwa kukubali nimefanya makosa lakini "nilikuwa na nia njema" Ambayo ndiyo argumente kubwa ya kutetea dhambi za nyerere. Haaa.

Kuhusu la Lowassa, argument yangu ni kuwa, si huyo tuu ni mfumo mzima wa kukubali kuwa nyerere hajafanya makosa ndio wenye tatizo na iwe kikwete, lowassa, pinda au pinduwa, kama hawa viongozi hawatakubali kosa na kulirekebisha basi tutabaki na kosa mpaka watapopatikana viongozi wataokiri kosa limeanza wapi na ndio walirekebishe. simply, kama mtu hujuwi kosa nini, utatatuwa nini? If you dont know what the problem is, how do you solve it? Problem ni kutokukubali nyerere ndie aliyetutia kwenye ufisadi wa hali ya juu, kwa kuwa mwenyewe alikuwa fisadi. naomba ieleweke, ufisadi si kuiba kwenye mikataba tu, hata kutowa roho za watu wasio na makosa ni ufisadi, kudhulumu mali za watu pia ni ufisadi. jee, nyerere hakuuwa watu wasio na makosa? jee nyerere hakudhulumu mali za watu? Tukubali kulijuwa tutatizo ndio tuweze kulitatuwa bila hivyo, bure tu.
 
Angalau alifanya kama aliyosema. Hakuwa fisadi wala hakujilimbikizia mali, kama Mkapa aliyemchagua aligeuka hilo si kosa lake. Ndio tulikuwa maskini wa mwisho lakini hakukuwa na matabaka. Sasa kuna maskini wa kuzidi enzi za Mwalimu na kuna wanaoishi dunia ya kwanza.
Najua hakutufikisha mbali lakini matendo yake kama binaadamu yanaonyesha nia njema. Huwezi kufananisha na JK na wenzie wanaouza nchi.

sasa ina maana Nyerere alimsifia mkapa bila kumjua kama naweza kumgeuka?
nyerere alikuwa apingwi na abishiwi, sasa hiyo ni nia njema?
aliwafukuza matajiri na kutuongezea umaskini, nia njema?
kwangu nyerere ni mpenda sifa na mjuaji aliyefanywa kuonekana mtakatifu na vyombo vyake vya habari
 
Watu wanatania ndoto. Mimi siwezi kuitania maana nafahamu meni ambayo nimewahi kuyaota na yakatokea kweli.
Nakuunga mkono hasa kwa maneno ya mwisho kwamba JK wakati wa kuwatosa marafiki na maswahiba wasio safi, ni sasa. JK unapaswa kuelewa kuwa si kila rafiki na si kila ndugu anafaa kuwa kiongozi. Kamwe usimteue mtu kuwa kiongozi kwa sababu tu ni rafiki yako au ni ndugu yako, angalia uwezo na uadilifu wake. Umepata nafasi sasa ya kuteua mawaziri wapya - achana na marafiki wafisadi, Tanzania imejaa watu safi na waadilifu, nafikiri sheria ya kuwa mawaziri lazima wawe wabunge imekufunga mikono na kukupunguzia wigo wa kuchagua. Nakushauri chagua kwanza baraza dogo halafu peleka muswada bungeni kubadili hiyo sheria, halafu malizia kwa kuteua wengine toka wale wasio wabunge.
Sheria hiyo ni mbaya pia kwani imesababisha mawaziri kuacha kuhudumia taifa na kuhudumia zaidi majimbo yao ili waweze kuchaguliwa tena
JK, FUATA NDOTO HIYO NA UTAFANIKIWA VINGINEVYO MZIMU WA NYERERE UTAKUTAFUNA. Na hicho kikao cha Halmashauri kuu mnachotaka kufanyia Butiama, ni kama kwenda kumkejeli Nyerere, hakika mtakiona cha mtema kuni kama mtaenda kuenedeleza ufisadi kwa kulindana.
 
Wewe si jasusi? ingia kazini utafute ukweli utaupata tu. Jumbe ni muungwana na muungwana "akitafunwa na mbwa hatangazi kidonda".

Interesting. You make the allegation and you want me to seek the evidence? Tupe ushahidi wewe, na majina ya wale waliouawa detention na walioliwa na wanyama.
BTW sheria ya detention bado ipo. Tuliirithi kwa Waingereza.
 
kama kuna kikundi hicho mimi nakuhakikishia sikijuwi, msimamo wangu ni facts zisizopingika na nilikuwepo wakati wa nyerere na nimeyaona na si ya kusikia. jee hujuwi kuwa wakati wa nyerere tulikuwa kwenye dimbwi la umasikini?

Kama moja ya maneno uliyoweka hapa dhidi ya Nyerere yakithibitishwa kuwa ni ya uongo basi kila kitu hapa ulichosema ni uongo tupu....

Tuanze na hili la kuhamisha watu milioni kumi!

Je, sera ya kuhamisha watu kwenye vijiji vya ujamaa ilifanyika lini? na wakati ikifanyika Tanzania ilikuwa na jumla ya watu wangapi? na kati ya watu hao, ni wangapi walihamishwa?

Ukijibu hili swali utagundua kuwa waliohamishwa ni chini sana ya namba unayoitaja hapa (kitu kinachokufanya uonekane muongo tu na mzandiki)!
 
Interesting. You make the allegation and you want me to seek the evidence? Tupe ushahidi wewe, na majina ya wale waliouawa detention na walioliwa na wanyama.
BTW sheria ya detention bado ipo. Tuliirithi kwa Waingereza.

Jasusi mpe shule huyu zomba AKA.....

Labda hana taarifa kuwa hata marekani "Eminent Domain" inaruhusu serikali kuhamisha watu toka maeneo yao na kuwapeleka maeneo mengine ili kupisha uendelezi wa maeneo husika. Wamarekani wamejaribu kupingana na hii sheria lakini supreme court ya Joji Kichaka imekubaliana na serikali na watu wanahamishwa kila siku kupisha ujenzi wa mabarabara na viwanda na makampuni binafsi wakati mwingine bila hata "kulipwa fidia"!
 
Zomba chuki hizi zinakushusha Mwamba .Ongea ukweli hapa JF longo longo hutafika mbali .Walikuja hapa akina Kada Mpinzania sasa hata majina yao wameyakimbia utaweza kweli JF kwa mwendo wa kuokoteza maneno ?
 
Back
Top Bottom