Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Sita huyu mwaka 1995 alimtete Lowass kwenye kamati kuu erti kuwa Lowass hakkuwa mla rushwa! na hiyo olikuwa mbele ya mwl Nyerere! Baadaya ya kuwa jina la Lowassa limeondolewa!

Na hapa mzanakai akachachamaa na kumwambia sita kama mnamtaka Lowassa rudisheni jima lake halafu siye na niye twende kwa wanachi ili waamue kama wanamtaka Lowassa au mtu Mwingine.

Bundi sita baada ya kuona hivyo aliamua kukaa kimya!

Kumbe hadi leo hii bado anamumeba Lowassa!

Inatakiwa mbunge mmoja atoe hoja ya kutokuwa na imani na sita kama spika.

CCM=CHAMA CHA MAJIZI
 
Anyaway!!! EL ni mlarushawa sikuanzia rmond tu..tangu zamani..Sioni akibakia kwenye uongozi kwa sababu yeyote ile!
 
Nyerere alisema Lowassa hafai kuwa Rais kwa sababu ni mla rushwa na mpenzi wa kujilimbikizia Mali.JK akaamua kukiuka maneno hayo na kumchagua kama waziri mkuu..Kumbe Mwalimu hakukosea..
 
kosa ni la nyani kama tungekuwa watu tusingechezewa
 
Nyerere alisema Lowassa hafai kuwa Rais kwa sababu ni mla rushwa na mpenzi wa kujilimbikizia Mali.JK akaamua kukiuka maneno hayo na kumchagua kama waziri mkuu..Kumbe Mwalimu hakukosea..

Huyo nyerere ndie alikuwa fisadi mkuu wa Tanzania, au haukuwepo wakati wake na unamsoma tuu kwenye historia za uwongo? Tuulize sisi tuliokosa bahati kwa kuwepo na kuonja joto na madhila ya uongozi wake.
 
mstahiki, nakuomba ingia kwenye post yako urekebishe ulipoandika "utabili" nadhani ulikusudia "utabiri". Samahani lakini nadhani ni wajibu wetu kuheshimu matamshi ya lugha yetu nzuri, na tusiwe mafisadi wa lugha.
 
Ndugu usiwe kishoka-nipunde tulitoka kwenye utawala wa Mkapa.
Nandio chaguo la Mwalimu-alotuamrisha tufunge mikanda wakati huyo kijana wake amekaribia kupasuka kwa kufura.
Inajulikana yakwamba yeye ni MJASIRI MALI nakajilimbikizia-Mh.Butiku anajaribu kumnasihi,jamaa utadhani mbuzi kagoma.
Vp,awe LOWASSA kujitetea hali yupo alotangulia-Mwanafunzi,Mwandishi na Chaguo la MWALIMU.
Hapa tumuunge mkono Rais wakati huu akifanya mabadiliko kwakuwa kadhamiria kutukomboa japo sisafi kiasi hicho.Ila tumuunge mkono maana huenda kaungama.
Ila MWALIMU naye ni mtu anaudhaifu wake-tena anapenda aonekane niyeye ndio kinara-tafadhali usitukumbushe huyu mtu-mwache huko aliko-tusije kupandwa nahasira.
 
Huyo nyerere ndie alikuwa fisadi mkuu wa Tanzania, au haukuwepo wakati wake na unamsoma tuu kwenye historia za uwongo? Tuulize sisi tuliokosa bahati kwa kuwepo na kuonja joto na madhila ya uongozi wake.

Watu wengi wamesahau ya Nyerere...yeye ndie aliwafuga wengi wa mafisadi kina Mungai,Msuya,Mkapa na wengine wengi.

Nakumbuka vijana ma seamen wamesota huko nje wakarudi bongo na vi peugeot 504 vyao..custom wakavichukua kwa ubabe kesho yake viko barabarani vinatumiwa aidha na mawaziri au makatibu wakuu kwenye miradi yao ya teksi.

Msitake kutumbusha enzi za serikali ya ki imla.At least siku hizi kuna angalau magazeti ambayo yanathubutu kuikosoa serikali.Nani aliweze kudiriki kumkosoa Kawawa enzi hizo? Alikiuwa akiamka vibaya anatoa amri za ajabu.."kuanzia leo nataka maduka ya watu binafsi yafungwe"...au "kuanzia leo sitaki kijana avae suruali ya kubana wala msichana kuvaa mini skirt"....jamani tumetoka mbali
 
..nyerere alikuwa na busara na uzoefu wake katika madaraka ulimwezesha kuona baadhi ya vitu ambavyo wengine hawakuona au hawakutaka kuona!

..sasa,maneno yake yalikuwa na maana nyingi kutokana na hali halisi ,wakati na mazingira!
 
Zomba una maneno ya chuki wewe na Mwalimu .Mwalimu kama mtu alikuwa na makosa yake lakini Mwalimu aliijali sana Tanzania na Watanzania .
 
Busara za kuwacha watu masikini wa kutupwa?, busara za kuwacha nchi inanuka rushwa?, busara za kuwacha viongozi wasiojali wananchi? busara gani njema uionayo wewe?, hebu tuelimishe, labda ipo, mimi siijuwi!
 
Angalau alifanya kama aliyosema. Hakuwa fisadi wala hakujilimbikizia mali, kama Mkapa aliyemchagua aligeuka hilo si kosa lake. Ndio tulikuwa maskini wa mwisho lakini hakukuwa na matabaka. Sasa kuna maskini wa kuzidi enzi za Mwalimu na kuna wanaoishi dunia ya kwanza.
Najua hakutufikisha mbali lakini matendo yake kama binaadamu yanaonyesha nia njema. Huwezi kufananisha na JK na wenzie wanaouza nchi.
 
Zomba una maneno ya chuki wewe na Mwalimu .Mwalimu kama mtu alikuwa na makosa yake lakini Mwalimu aliijali sana Tanzania na Watanzania .

Lunyungu, kweli kabisa nina mchukia sana kwa kutowa roho za watu wasio na hatia halafu anathubutu kupanda jukwaani na kujichekesha. KAUWA WATU WENGI SANA wa-Tanzania, kwa maamuzi yake mabovu, katutia kwenye umasikini mkubwa sana, Jee Lunyungu unataka nimpende mtu kama huyo?
 
Akina nani hao ndugu zangu ambao waliuawa na Nyerere? Mbona mimi sijawahi kuwasikia? Alipokuwa jukwaani mbona alipigiwa makofi nao hao aliowachekesha? Au kuna Tanzania mbili--moja ya Zomba na moja ya sisi wengine tunaomheshimu na kumwenzi Mwalimu?
 
Ilikuwa ni lazima ucheke alikuwa na jokes na wengi walikuwa wakilazimishwa kuhudhuria mikutano yake,uelewe kama Mzee akija mkoani kwetu siku hiyo ujue mashule maofisi yaani kazi zote zinasimamishwa mnajipanga barabarani kumgojea mnaweza kukakaa barabarani tokea asubuhi mpaka jioni mnasubiriHebu fikiria hoyo siku moja ni masaa mangapi ya kazi yamepotea?

Kumheshimu na kumwenzi Nyerere ni sawa lakini haimanishi kuwa Mzee was clean as people think.

Alikuwa na mapungufu mengi ambayo yameiva sasa yanajitokeza katika chama chake..his foundation was poor hence cracking.

Tabia ya kulindana ni mfumo uloshamiria ktk utawala wake kwa muda mrefu sana.
 
Akina nani hao ndugu zangu ambao waliuawa na Nyerere? Mbona mimi sijawahi kuwasikia? Alipokuwa jukwaani mbona alipigiwa makofi nao hao aliowachekesha? Au kuna Tanzania mbili--moja ya Zomba na moja ya sisi wengine tunaomheshimu na kumwenzi Mwalimu?

Haujawahi kusikia? ajabu sana, ngoj nikusikilizishe kwa kifupi tuu. Nyerere aliwahamisha zaidi ya watu million kumi kutoka vijiji, miji au sehemu zao za asili na kuwapeleka sehemu mpya, ya amma kulikuwa kuna vijiji vidogo vya asili na watu wapya wakabwagwa na kuwachwa hapo bila ya kuwa na facilities zozote za kuweza kukidhi mahitaji yao kila siku au walichukuliwa na kubwagwa maporini ambapo hakuna hata kijiji wala nyumba za kuishi, wengi wao walikufa kwa kuliwa na wanyama wa kali wa porini, wengine waligongwa na nyoka, wengine walikufa kwa njaa, wengine walikufa kwa kula mizizi ya sumu kwa njaa, wengine walikufa kwa kukosa matibabu. Ni wengi sana waliokufa na ilikuwa ni marufuku kuandikwa habari mbaya yeyote, waandishi wachache waliokuwepo wakati huo, ilikuwa ni lazima waandike inavyotaka serikali.

wengine walikufia jela kwa sheria yake ya ditenshen aliyoiweka, sijui kama imefutwa hii au bado ipo, watu wengi walikuwa wakionekana kupinga tuu siasa zake, walishikwa na kuwekwa vizuizini bila kuhojiwa wala kupelekwa mahakamani aidha mpaka wafie huko au mpaka nyerere mwenyewe awakumbuke na kuwawachia, hakuna mtu mwingine yeyote kwenye serikali aliyekuwa na ubavu wa kukutowa ditenshen isipokuwa nyerere mwenyewe.

Mbali ya hayo, mahospitali yalikuwa bure lakini huduma mbovu kabisa na ndio mpaka sasa hali imebaki hivyo-hivyo. Yaani alifisadi kila kitu.

KUCHEKA na kuchekesha watu, hilo ndio moja linalonishangaza mpaka leo, kwa yote aliyokuwa akiyafanya lakini bado alikuwa na uwezo wa kucheka na kuchekesha watu na aliupata usingizi. Hiyo ni dalili ya ukatili wa hali ya juu. Kumbuka wakati huo alikuwa akiweka masharubu yake kama hitler.

Ni mengi mabaya aliyoyafanya na ndio maana unaona ufisadi uliokithiri leo hapa nchini unatokana na hawa viongozi aliowarithisha yeye. Hawana huruma hata kidogo na wananchi kama alivyo yeye. Na aliyejaribu kumpinga kidogo alikiona. Abood Jumbe ni mfano mzuri, aliwachishwa umakamu wa rais akawekwa house detention akakatiwa umeme, maji, marupupu yake ya umakamu wa rais mpaka alipotubu kwa nyerere kuwa hatosema lolote na hatoingilia tena mambo ya siasa ndio akafunguliwa. Na toka wakati huo akawa kimya mpaka wakati wa mwinyi ndio akathubutu kuandika kitabu kilichogusia kidogo siasa za kidikteta za nyerere.

Ni wengi tuu aliowauwa nyerere kwa maamuzi yake mabovu, na umasikini uliokithiri ametutakia yeye, inasemekana kuwa kuanzia mwaka 1965, mpaka anaacha urais uchumi wa tanzania ulikuwa ukishuka kwa 0.03% kila mwaka. Hatari kubwa.
 
Naam, hapa kuna ukweli na ushahidi wa kutungwa(kama ukweli na ushahidi wa namna hiyo upo).

Na kwa watu waliokwishajiaminisha ukweli huo hapawezi kuwepo na ukweli mwingine.

Kwa wat wa namna hiyo,haijalishi, hata kama halaiki ya wananchi waliomuenzi Mwalimu wanapoendelea kumheshimu na kumtukuza; ni wao tu ndio wenye ukweli. Kwa maneno mengine, waTanzania walio wengi ni vichaa kwa kumwona Nyerere kuwa kiongozi aliyetukuka. Ni akina Zomba tu ndio wenye akili timamu. Sasa wanyo kazi ya kututibu ukichaa huu, nasi tufanane nao watu wenye akili timamu. But the reverse of this seems more plausible.
 
Ndugu yangu Kalamu afadhali wewe umesema. Sikujua Jumbe alikatiwa umeme pale Mji Mwema mpaka Nyerere alipomsamehe. Na mbona hilo hakuliweka kwenye kitabu chake? Au naye alikuwa anaogopa adhabu kubwa zaidi?
 
Back
Top Bottom