Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,219
- 44,316
Huo ni muono wako nami sina uwezo wa kuuingilia wala kukubadilisha mawazo. Isipokuwa, facts zijibu kama unaweza:
Jee, nyerere hakuhamisha watu takriban millioni kumi kutoka makazi yao ya asili?
Kasome historia vizuri na facts kuhusu Operesheni vijijini. Hivi unajua ni Watanzania wangapi leo wanaishi kwenye vijiji ambavyo ni matokeo ya kazi ile. Mwalimu alikuwa na jukumu la kujenga Taifa siyo kujenga vijiji! Anayejua mapungufu tunajua ni jinsi gani operesheni ile ilishindwa kutekelezeka jinsi ilivyopasa, lakini leo nenda uangalie ni jinsi gani nadharia yake ya "vijiji" ndio imeunda msingi wa Taifa leo hata leo hii. Ushawashi kusikia mahali kunaitwa "Geza Ulole"?
Jee, nyerere hakusababisha kati ya aliowahamisha wafe kwa, kuliwa na wanyama? kugongwa na majoka? kukosa chakula? kula mizizi yenye sumu kwa njaa? kukosa matibabu?
Yaani wewe unataka kutuambia wananchi wangeendelea kukaa nyumba moja hapa nyingine kule katika makazi ya kijima halafu wapate maendeleo? I'm glad tuliweza kuunganishwa katika vijiji. Mapungufu yake ni gharama ya maendeleo. Watu kufa n.k yote ni gharama. Tungeweza kupunguza au kuzuia vivyo na matatizo mengine ingekuwa bora zaidi, lakini ndivyo ilivyokuwa.
Jee, nyerere hakuanzisha sheria ya "ditenshen" amabyo hakuna aliyeweza kukutowa isipokuwa yeye?
wewe umewahi kuisoma hiyo sheria au unasikia "detention" tu.? Haya nimekubandikia hapa ili utuoneshe hapo mahali panaposema kuwa mtu hakuweza kuachiwa isipokuwa kwa Nyerere amuachie.
Jee, watu aliowa-"ditenshen" nyerere wengine hawakufia jela?
Hoja nyingine bwana, sasa unajua wafungwa wangapi hufia jela? Unajua wangapi huwa wanafia rumande?
Jee, nyerere, hakuzuwia habari kuandikwa isipokuwa inazotaka serikali yake tuu?
Una uhakika? alizuia lini, kwa tangazo gani, na vipi....? Nyerere alikuwa anajukumu la kujenga Taifa, baadhi ya maamuzi lazima tuyaelewe kwa mwanga wake halisi siyo kutumia darubini ya muda kuanza kuyahukumu.
Nadhani hizo ndio hoja na hoja si mimi wala si wewe wala si mtanzania yeyote kuwa ni mwendawazimu. Wendawazimu ni maradhi kama maradhi mengine yeyote na si tabia njema kujumuisha watu na kuwatusi kama unavyotaka ieleweke. Naomba jibu facts.
Nakubaliana na wewe hapo kwani hoja hujibiwa kwa hoja, siyo vioja wala vi-hoja!
kama kuna kikundi hicho mimi nakuhakikishia sikijuwi, msimamo wangu ni facts zisizopingika na nilikuwepo wakati wa nyerere na nimeyaona na si ya kusikia. jee hujuwi kuwa wakati wa nyerere tulikuwa kwenye dimbwi la umasikini?
hoja zinapingika! KUhusu dimbwi la umasikini ambalo tulikuwemo wakati wa Nyerere naomba ututangazie tulitoka lini?
Usemayo swadakta na yanaingia akilini, lakini huwezi kuwa ni chanzo cha kuuwa halaiki ya watu na si kwa ajali bali kwa maamuzi ya makusudi kabisa na ya muda mrefu, halafu ujitetee kwa kukubali nimefanya makosa lakini "nilikuwa na nia njema" Ambayo ndiyo argumente kubwa ya kutetea dhambi za nyerere. Haaa.
Hii "halaiki" ya watu waliouawa iko wapi!? Jamani naomba mtu yeyote ambaye wazazi wake, kaka zake, au ndugu zake waliuawa wakati wa Operesheni vijijini wajitokeze na tuanze kuhesabu. Kusikia "fulani aliuawa" hatukubali, tuko wengi hapa JF nina uhakika angalau mtu mmoja atakuwa amepoteza shemeji, dada, au kaka wakati wa ile Operesheni ya vijiji. Binafsi wazazi wangu walihama kule toka mabonge ya Peramiho na kusogezwa karibu na Misheni, na ingawa walitusimulia jinsi walivyoondoka kwenye makazi yao, lakini hakuna hata mtu mmoja aliyekufa au kuliwa na simba! Sasa nyinyi mliopoteza ndugu zenu mauaji ya "halaiki ya watu" naomba mnyoshe mikono.
Ukienda leo Baghdad na ukiuliza kama kuna mtu anamjua mtu yeyote aliyeuawa na vitendo vya ulipuaji kule usishangae karibu kila mmoja anajua mtu, na hata hapo nyumbani ukiuliza kama kuna mtu anamjua aliyekufa kwa Ukimwi usishangae karibu kila nyumba inamjua mtu, sasa wale walioishi miaka ya sabini (nikiwemo wenu mtiifu) nimejaribu kukumbuka ni kina nani waliuawa na Mwalimu katika operesheni vijijini.
Zomba kwa vile unasema ulikuwepo naomba tuanze na wewe, ni ndugu zako wangapi na wapi walikuwa wakihamishiwa? ili tuanze kuhesabu tuache kuandikia mate...
Kuhusu la Lowassa, argument yangu ni kuwa, si huyo tuu ni mfumo mzima wa kukubali kuwa nyerere hajafanya makosa ndio wenye tatizo na iwe kikwete, lowassa, pinda au pinduwa, kama hawa viongozi hawatakubali kosa na kulirekebisha basi tutabaki na kosa mpaka watapopatikana viongozi wataokiri kosa limeanza wapi na ndio walirekebishe. simply, kama mtu hujuwi kosa nini, utatatuwa nini? If you dont know what the problem is, how do you solve it?
point nzuri, tatizo huwezi kuumba kosa lisilokuwepo ili ulijaribu kulisolve!
Problem ni kutokukubali nyerere ndie aliyetutia kwenye ufisadi wa hali ya juu, kwa kuwa mwenyewe alikuwa fisadi.
wenzio walienda mbali zaidi walimuita nyerere Dikteta, kama Nyerere alikuwa fisadi, basi miye naupenda ufisadi wake! Kwa sababu,
> Nyerere hakuanzisha mgahawa Ikulu
> Nyerere hakuuza nchi yetu kwa wawekezaji
> Nyerere hakusujudu kwenye madhabahu ya Mataifa makubwa na kudhalilisha utu wake. n.k n.k
naomba ieleweke, ufisadi si kuiba kwenye mikataba tu, hata kutowa roho za watu wasio na makosa ni ufisadi, kudhulumu mali za watu pia ni ufisadi. jee, nyerere hakuuwa watu wasio na makosa? jee nyerere hakudhulumu mali za watu? Tukubali kulijuwa tutatizo ndio tuweze kulitatuwa bila hivyo, bure tu.
Hiyo mali aliyoidhulumu Nyerere aliipeleka wapi? Hao watu ambao Nyerere aliwaua makaburi yao yako wapi? Lazima kuna mtu anajua. Nyerere alishaondoka siku nyingi na kufa, sasa hakuna haja ya kuogopa tena, watajeni wale waliouawa na Nyerere ambao ni halaiki!! Halafu tulinganishe kama idadi yao inafikia wale waliouawa wakati wa Mkapa, au Mwinyi!