Bin Maryamu, unaweza kuelezea hali ya Tanzania leo hususan umoja, utulivu na amani, bila kutaja jina la Mwalimu au vitu hivi tumeshushiwa na Mungu kwa sababu sisi ni watu wema zaidi ukilinganisha na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Msumbiji, Nigeria, Angola n.k ?
Kwanini Mungu atupendelee sisi?
Suala zima la Amani la TanzaniA ni complex issue. Na hakuna mtu anaweza kupata credit. Kwanza Tanzania ilikuwa ina njia tatu za utumwa. Na biashara hii ilifanya kuhamahama na kuchanganyikana. Ukienda Kariakoo kuna zaidi ya vizazi vitano vya wa kutoka Mwanza, Tabora au Kigoma. Na watu hawa wamechanganyika kabla mjerumani hajaja katika nchi yetu.
Vilevile wakazi wa mikoa ya kusini walishachanganyika toka miaka ya zamani sana. Na vita vya majimaji vilivyoua zaidi ya watu 300,000 katika mikoa hiyo vilifanya watu kusambaratika na kuzidi kuchanganyikana.
Vilevile utawala wa mjerumani ambao ulikuwa ni wa moja kwa moja haukuanzisha matabaka ya makabila yenye nguvu.
Tanzania ilikuwa sio koloni baada ya vita vya kwanza. Na hivyo wahamiaji wa kizungu ambao walichukua ardhi hawakuwa wengi. Mpaka tunapata uhuru kulikuwa na Wazungu kati ya 10,000 na 20,000. Wakati Kenya ilikuwa na zaidi ya wazungu 100,000. Kwa mtaji huu watanzania walibaki kwenye vipande vyao vya ardhi ambacho ni chanzo cha mahitaji yao ya kila siku na hawakuwa na sababu ya kudundana. Hiyo hali haikupatikana Kenya.
Lugha ya kiswahili ilikuwa imeenea nchi nzima. Hivyo watu tayari walikuwa na kitu kinachowaunganisha zaidi ya utaifa.
Makabila ya Tanzania ni vikundi vidogo vidogo na hakuna kabila linaloweza kubadili matokeo ya aina yoyote ya uchaguzi mkuu. Hivyo maasi au chuki ya kabila moja kwa kabila jingine, hayatingishi sehemu yoyote ya nchi. Kwa mfano kuna kabila moja dogo huko Singida lilikwenda kuiba ng'ombe na kufanya fujo huko Tabora. Na wakazi wa Tabora wakakusanya sungusungu wao na wakaenda kukomboa ng'ombe zao na mapigano makali yalitokea. Na haya yote yalifanyika kabla ya 1983. Ingekuwa mambo hayo yametokea kati ya mjaluo na mkikuyu ingekuwa ni matatizo ya nchi nzima. Kwa Tanzania ilitosha kupeleka kikosi kidogo cha FFU kutuliza ghasia.
Chanzo kikubwa cha migogoro Afrika kimekuwa EYES ON PRIZE baada ya uhuru. Prize yenyewe imekuwa kugawana mapato yanayotokana na uchimbaji wa madini. Tanzania haikuwa na prize yoyote hile ya kugombea. Amani unayoona wewe ni kwa sababu hatuna cha kugombania.
Hivyo amani ya Tanzania ipo kabla ya Tanzania kupata uhuru. Na kama unakataa lete mfano mmoja unaoonyesha watanzania walishajianda kupigana wenyewe kwa wenyewe baada ya kupata uhuru.
Na Tanzania ukilinganisha na Kenya:
Kenya kuna makabila makubwa ambayo hayakuwa na mahusiano yoyote ya karibu kabla na baada ya uhuru. Pamoja na nchi hiyo kuwa kubwa ni sehemu ndogo tu ya ardhi yafaa kwaa uzalishaji.
Na Tanzania ukilinganisha na Uganda:
Uganda kulikuwa na falme Tano za kikabila. Lakini waliopendelewa ni Baganda. Na migogor yao ina historia kabla ya kuja kwa wakoloni.
Na Tanzania ukilinganisha na Uganda:
Mgogoro wa Msumbiji ulianzia toka wao wakiwa katika vita vya mapambano ya kukomboa nchi yao. Na mgogoro huo ulianzia wakiwa Tanzania hivyo sina sababu ya kuuelezea zaidi.
Na Tanzania ukilinganisha na Nigeria, COngo:
Mgogoro wa Nigeria unafanana na wa Congo. EYES on Prize. Nchi hizi ziliachwa zikiwa tajiri kuliko nchi zozote za kiafrika ukiondoa SA. Na ufisadi uliopo Tanzania unaonyesha kabisa kuwa tungekuwa na vitu vya kugombea katika nchi hile urais wa Nyerere ungedumu kwa muda mfupi.
Na Tanzania ukilinganisha na Angola:
Pamoja na kuwa na mapigano ya kugombea mali. Mgogoro wa Angola ulitokana na ubaguzi. Moja ya tatu ya wa-Angola wanadamu ya kireno na hawa walikuwa na nafasi nzuri kuliko wasiochanganya. Hivyo mapigano kati ya walichanganya na waVimbundu yalianza.