Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,240
- 44,480
Mwanakijiji,
..kama elimu ilidorora, ina maana tulikuwa tukielekea kwa kasi kubwa kwenye ujinga.
Nani alisema elimu ilidorora, tulipopata Uhuru tulikuwa na madaktari wazalendo 8 tu, Mwalimu alipoacha Urais unajua tulikuwa na wangapi? Shule za msingi zilikuwa ngapi wakati wa uhuru, ni wangapi na "umasikini" wetu waliweza kusoma. Unajua literacy level yetu ilikuwa over 90% under Mwalimu? Wengi unaowaona leo hii madarakani walisoma enzi za "umasikini" wa Mwalimu. Sijui hili wazo la elimu ilidorora una ushahidi gani.
..kama huduma za afya zilidorora basi maradhi yalianza kutuzingira tena.
Duh, una msingi gani wa kusema huduma za afya zilidorora? Unakumbuka kampeni ya "Mtu ni Afya" na "Chakula Bora" jinsi zilivyokuwa na mafanikio. Mara nne katika utawala wa Nyerere hatukuwahi kuishi kwa njaa kiasi kama cha 1994 na 2004. Hata njaa ya 1984 tuliposhindia Yanga na RTC watu wetu hawakufa kama ilivyotokea Ethiopia at the same time. Kwanini?
..kama viwanda viliacha kuzalisha na kilimo kilianguka ina maana umasikini nao uliongezeka.
Viwanda gani viliacha kuzalisha wakati wa Mwalimu? Mutex, Mwatex, Urafiki, Bora, n.k ?
..Mwalimu aliazimia kupigana na ujinga, maradhi, na umasikini.
Hakuazimia tu, alijitahidi kupigana navyo. Na kwa kiasi kikubwa alifanikiwa sana.
..Mwalimu alielekeza kwamba maadui hao watatu walitufanya tuwe WANYONGE, na kusababisha TUNYONYWE, TUONEWE, na KUPUUZWA.
Mwalimu alijua tatizo, na hata leo watawala wetu hawajaja na tatizo jingine. Leo hii wameongezewa tatizo la nne, Ufisadi.
..Tukubali kwamba Jemedari wetu alishindwa kutuongoza ktk vita ya kuondoa Umasikini,Ujinga, na Maradhi. Pamoja na hayo alituachia lulu nzuri ya umoja na mshikamano.
Si kweli, jemedari alipigana kwa ajili ya uwezo wake wote, alijeruhiwa vitani, na alikubali kumpa jemedari mwingine. Alifanya yote aliyoweza na aliposhindwa kuwaingiza wananchi wake kwenye ile nchi ya ahadi, akaweka manyanga chini akitumaini Mungu atamuinua Yoshua!! Bado tunasubiri Yoshua ainuke kutuongoza kupambana na Yeriko ya Ufisadi, na kuwavamia wananchi wa Kanaani na kuwanyang'anya vitu vyetu.
Kama Martin Luther kabla yake, Mwalimu alitambua bila ya shaka asingeweza kuingia kwenye ya ahadi pamoja nasi, lakini kwa mbali aliona zile tambarare za nchi ile imiminikayo "maziwa na asali"!!