Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

1. Those who make things happen
2. Those who complain when things happen
3. Those who watch things happen
Sijui watanzania wengi tunaangukia wapi?

Watanzania bado hatujaondoka kwenye siasa za kijamaa, viongozi wetu wanahubiri siasa nyingine, raia wengi bado wanaishi kijamaa.
Mwalimu alikuwa na mapungufu yake na alikosea kama kiongozi sasa imefikia wakati Watanzania tukayaweka yote nyuma na kusonga mbele kuendeleza Taifa, mambo ya kukaa na kusema tusingeenda vita ya Kagera or isingekuwa sera hizi na zile za Mwl tungekuwa mbali kimaendeleo.
Imeshapita miaka 22 tangu ang'atuke nadhani sasa itakuwa aibu kuendelea kulalamika wakati hatufanyi chochote kurekebisha makosa yake, muda umefika mimi, wewe na yule tupiganie taifa letu.
Well said ndugu yangu lakini huko Nyambiti na Nyakalilo bado maradhi yapo ya woga na umbumbumbu.Kile kirusi cha mwalimu bado hakijapata tiba.
 
WanaJF,
Naomba nijue ukweli tu kuhusu kile kifimbo cha Baba Wa Taifa, Mwl. Nyerere (RIP).


6tk55cn.jpg

Wakati niko shule ya msingi, nilisikia stori kibao kuhusu hicho kifimbo, lakini sikuwa na uhakika nazo mpaka hii leo hii ninaposema haya.

Je, yafuatayo ni ya kweli:

--yakuwa, kilikuwa kizito na akikiacha pahali hamna aliyeweza kukinyanyua.

--yakuwa, aliachiwa na bibi yake (sijui mzaa baba au mama)

--yakuwa, ikizuka safari, alikuwa akikinyosha kuelekea kule anakotaka kwenda, na kikipinda na ku-point chini alikuwa anaghaili safari yake hiyo.
 
Come on people, what does it have to do with our national interests, hii haifai hata kwenye udaku!
 
Come on people, what does it have to do with our national interests, hii haifai hata kwenye udaku!

Bongolander, heshima yako ndugu. Kuna thread kibao zenye national interests ndani yake, kama hutaziona naomba ukaanzishe zako.

Last time I checked, this was still JamboForums! Baadae ndugu, ahsante kwa mawaidha yako katika national interest threads.
 
Nyerere alikuwa na kifimbo, Kenyatta alikuwa na kifimbo chenye manyoya, Kaunda yeye kitambaa cheupe, Mobutu alikuwa na kifimbo vilevile...

My take: Zote mbwembwe tu hamna kitu...
 
Nyerere alikuwa na kifimbo, Kenyatta alikuwa na kifimbo chenye manyoya, Kaunda yeye kitambaa cheupe, Mobutu alikuwa na kifimbo vilevile...

My take: Zote mbwembwe tu hamna kitu...

Mwakilishi, hilo kweli linawezekana kabisa, mbwembwe tu za hawa waasisi wa mataifa yetu... Je kule Ghana, Nkurumah naye alikuwa na kifimbo?
 
Inawezekana mzee ni kama viongozi wetu alikuwa anakesha kwa Karumanzila.Kwani nani anajua hilo.Yaweza ukawa uzushi na ukawa ukweli ambao vilevile hautakiwi kubezwa.
Lamsingi je hilo ni muhimu kwa wasaa huu wa leo?
 
Inawezekana mzee ni kama viongozi wetu alikuwa anakesha kwa Karumanzila.Kwani nani anajua hilo.Yaweza ukawa uzushi na ukawa ukweli ambao vilevile hautakiwi kubezwa.
Lamsingi je hilo ni muhimu kwa wasaa huu wa leo?

HAM, yawezekana kabisa ikawa siyo muhimu, ila ni swali na dukuduku lililonikaa toka nikiwa mtoto, na nimeamua kuuliza leo hii. Basi kama kuna anayejua ni either naambiwa hayo si kweli au oooh, hilo ni kweli. Mambo ya umuhimu yatatokana na atakaye kuwa anataka kujibu na anayejua. Ila ni swali tu ndugu yangu, natumaini umenielewa. Ahsante.

SteveD.
 
HAM,...ila ni swali na dukuduku lililonikaa toka nikiwa mtoto, na nimeamua kuuliza leo hii. Basi kama kuna anayejua ni either naambiwa hayo si kweli au oooh, hilo ni kweli. ....Ila ni swali tu ndugu yangu, natumaini umenielewa......SteveD.

Now, where is Mwanakijiji when we really need him!
 
---same question here, inaanza kuonekana kama kisa cha nahodha kutosa meli.... yaani wewe acha tu! lol
 
Nina imani kuwa ile ilikuwa ni fimbo tu aliyotaka kutumia mzee wetu kama trade mark yake. Kama alivyosema Mwakilishi hapo juu, wanasiasa wengi wa wakati ule walikuja na mtindo wa kuwa trade marks zao. Najua kuna kiongozi mmoja huko Kenya yeye alikuwa na rungu kabisa, sijui ni Mzee Jaramogi Oginga Odinga au nani. Wengine walikuwa na vifimbo vyenye mikia ya ngo'mbe ilhali kila mtu na trade mnark yake.

Inasemekana kuwa Nyerere alinunua kifimbo kile huko Dodoma akiwa kwenye treni pamoja na rafiki yake Oscar Kambona ambaye inasemekana kuwa alikuwa mwalimu wa Mazengo (sina uhakika sawasawa). Baada ya hapo wafuasi kadhaa wa Nyerere nao walikuwa na vifimbo vya aina hiyo na waliendelea kuvitumia pamoja na kuvaa mashati ya Chou En-Lai kama dalili ya kuongoza mapamabo ya uhuru na kujenga ujamaa hadi kunako mwanzoni mwa miaka ya sabini ambapo Nyerere aliibuka na vazi jingine lililojulikana kama Nyerere Suit sambamba na mavazi yaliyokuwa na umaarufu fulani wakati huo ya Kaunda Suit na Ngouabi Suit. Ujio wa hii Nyerere Suit ndiyo ulifanya wanasiasa wengi waachane na Chou-En-Lai na hivyo kuacha kutumia kifimbo. Pamoja na Nyerere ku-transision kutoka kwenye Chou-En-Lai hadi kwenye Nyerere Suit, yeye hakuachana na kifimbo hicho ambacho kilibaki kuwa trade mark yake. Inasemekana kuwa alikuwa na vifimbo vya aina hiyo vingi sana kiasi kuwa ilikuwa kama mojawapo ya mavazi yake.

Sidhani kama kifimbo hicho kilikuwa na jambo lolote zaidi ya madoido tu.
 
Kile kifimbo kuna wakati kilinadiwa na kuuzwa kwenye fund raising moja hivi, sikumbuki vizuri nani alikinunua, lakini baadae kada maarufu Mustafa Jaffer Sabodo akaamua kukinunua tena toka kwa huyo mtu na kumrudishia Mwalimu. Nadhani sasa kiko mahali fulani huko kwenye Makumbusho ya mwalimu. Angekuwa kabila letu, sisi mzee kama huyo akifariki ile fimbo yake inakabidhiwa kwa mwanae mkubwa wa kiume, ndio symbol ya authority juu ya nduguze.
 
Hata Chacha Wangwe pia anatembeaga na kifimbo chake, huwa kinampa confidence sana akikishika!
 
kadiri ya maelezo ya Maria Nyerere, Mwalimu alianza kutembea na kifimbo baada ya kuacha kuvuta sigara.
 
Niliwahi kusikia eti kuna wakati Nyerere alipokutana na Malkia Elizabeth II katika kusalimiana Malkia hakuvua gloves kwa hiyo Nyerere naye akampa kifimbo badala ya mkono, ya kweli hayo au ndio danganya toto zenyewe hizo?
 
Niliwahi kusikia eti kuna wakati Nyerere alipokutana na Malkia Elizabeth II katika kusalimiana Malkia hakuvua gloves kwa hiyo Nyerere naye akampa kifimbo badala ya mkono, ya kweli hayo au ndio danganya toto zenyewe hizo?

same here nshawahi sikia once kuwa alifanya hivyo kwa malkia!!
 
Niliwahi kusikia eti kuna wakati Nyerere alipokutana na Malkia Elizabeth II katika kusalimiana Malkia hakuvua gloves kwa hiyo Nyerere naye akampa kifimbo badala ya mkono, ya kweli hayo au ndio danganya toto zenyewe hizo?

Hilo swala nasikia ni ukweli na kuna makumbusho moja ipo london sumwea called richmond i think,hio picha imewekwa but mm binafsi sijaiona
 
Back
Top Bottom