Bin Maryamu, kuna nchi duniani ambazo sera za nyuma za nchi hiyo zilikuwa mbaya na viongozi wapya wakaingia na kubadilisha. Na yote yametokea katika kizazi chetu:
a. Uganda:
Nchi ya Uganda imepitia matatizo mengi, mapinduzi ya kijeshi, vita vya wenyewe kwa wenyewe na maamuzi mengine ya kibabe ya viongozi wake huko nyuma. Musevenni alipoingia madarakani 1986 aliikuta nchi imeporonyoka na majengo kadhaa hadi pale Kampala yalikuwa na matundu ya risasi! Ukifika maeneo ya Luwero (njia ya Bombo) kwenye msitu wa jirani mabaki ya watu waliouawa na final push ya 1986 yalikuwa yamezagaa. Ndani ya miaka 22 Uganda imeweza kufanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi tena bila kubadilisha sana mfumo wake wa kisiasa. Waliingia na mfumo walioubuni wao wenyewe wakauita "Movement" ambapo NRA (baadaye NRM) ilikuwa ndiyo "chama tawala pekee" na kimsingi kilikuwa ni Udikteta wa kijeshi. Guess what, leo hii Waganda wanashukuru hatua ambazo Museveni alichukua mwanzoni ili kuliokoa Taifa lake. Leo hii wanatengeneza Uganda than ever before, leo hii Uganda wameanza kuchimba mafuta, wanatembea kwa nyuso za kkujiamini na waliokimbia wanarudi na waliobakia wanaendelea kubakia. Lakini kuna mambo ambayo Museveni hakuinama chini kukubali. Alimwacha Amin afie ugenini, na alimwacha Obote afie Ugenini ingawa alitumia hekima kuuleta mwili wake ulazwe nyumbani. Wao waliweza na hawakuwa wafungwa wa historia yao; iweje viongozi wetu washindwe?
b. Rwanda
Mfano huo tena ni mwingine mzuri. Historia ya nchi himaya ya Watutsi na kuvunjika kwa himaya hiyo na maumivu ya historia ya nchi hiyo yanaeleweka. Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1950 na mwanzoni mwa miaka ya sitini na baadaye hadi wakati wa mauaji ya ya 1994 Rwanda ilikuwa inaelekea kwenye kujiangamiza yenyewe kama Somalia. Akaingia Kagame, na yeye kama Museveni (a contemporary and a friend os his) akaingia madarakani. Akafanya maamuzi ambayo were uniquely Rwandan. Akapitia changamoto nyingi na akaongozwa na lile la roho ya Taifa. Walioasamehewa wakasemehewa ilioshindikana wanasota Arusha na kwenye mahakama zile za kijadi. Wao wenyewe wa Rwanda pamoja na historia yao ya machozi, dhuluma n.k wakaweza kukaa pamoja kama Taifa. Kuna ambao hawakuridhishwa na maamuzi ya Kagame huko mwanzoni lakini leo hii wanafurahia matnda ya maamuzi hayo. Na ilipo Rwanda sasa imeanza kung'aa duniani. Muda si mrefu watakuwa ni kituo cha teknolojia katika eneo letu!
Sisi hatujapigana, hatujuana, hatujawa na mapinduzi ya kijeshi n.k bado ati tunamlalamikia Nyerere; aidha sisi ni watu duni kabisa duniani kifikra au tumelaaniwa katika eneo letu. Vinginevyo hakuna jinsi nyingine ya kuelezea hali yetu. Kujaribu kutaja jina la Nyerere kuwa ndiyo chanzo cha matatizo yetu mtu ambaye aliiachia nchi miaka 22 iliyopita ni kututukana akili zetu. Lawama za hali yetu remains squarely on the people in power today! Period. Lazima tuwawajibishe viongozi wetu kwa makosa yao badala ya kuwatengenezea huu udhuru usio na mantiki (illogical excuse) kuwa Nyerere ndiye amesababisha tuingie mikataba ya kijinga, sheria mbovu, rushwa, n.k ! Mkiendelea hivi hata watoto wa watoto wetu wataendelea kumlalamikia Nyerere wakati majirani zetu wote wanayoyoma kimaendeleo. We got to stop this and hold the people in power accountable.
Kama huu ungekuwa mwaka 1985 basi hali ya Tanzania hadi mwaka huo ingekuwa moja kwa moja imefungamana na utawala wa Nyerere na lawama zote tungembebesha Nyerere, lakini miaka 22 baadaye kuendelea kumbebesha Nyerere ni kukubali uduni wa kifikra na hicho nakikataa na ndio maana naongoza mapambano haya ya kifikra kuwa hadi sisi wenyewe tubadilike, tujiamini kuwa tunaweza, tutambue kuwa tunastahili vitu vyema na tukubali nafasi yetu katika kujenga taifa tulitakalo. Vinginevyo, nyinyi wenzetu endeleeni kumlalamikia Nyerere mkifungwa na historia milele, wakati wengine kama vile Nabii Samson tunasimama katikati ya watawala wetu tukizitingisha nguzo za majengo yao na kumwomba Mungu kuwa atupe nguvu "just this time" ili waangushwe na kutokomea ili hatimaye viongozi wapya wasimame katika ardhi yetu!!
Sasa angalau umeleta mifano yenye nguvu na ambayo itajibu kile tunachozungumza hapa.
Pilika zote za vita vya Uganda ilikuwa ni kumrudisha Obote madarakani. Lakini Museveni hakuona umuhimu wa kurudisha old guards madarakani. Na Nyerere alimuita Museveni MROHO WA MADARAKA.
Na Obote aliporudi madarakani alifanya yale yale aliyofanya zamani (OLD HABIT DIE HARD) na kuongezea mengine aliyojifunza Tanzania kulazimisha watu kuanzisha vijiji. Matokeo yake mambo hayakuwa mazuri na vita vya wenyewe vikaendelea mpaka pale Museveni alipochukua nchi. Museveni alikuja na framework mpya ya mawazo ambayo ilibadilisha muundo mzima wa kiserikali kwa kuanzia na katiba na kuleta watu wake wapya kuendesha nchi.
Kagame vile vile alipochukua nchi, cha kwanza ni kubadilisha nchi na alianzia na katiba na kuendelea na mambo mengine ya kiuchumi na kuleta sura mpya kuendesha uchumi.
Mabadiliko ya kisiasa katika nchi za Ulaya mashariki yalipofanyika, kitu cha kwanza ilikuwa ni kuvunja vyama vya kijamaa, kubadilisha katiba na kuleta sura mpya kuendesha nchi.
Kwa upande wa Tanzania, mabadiliko hayakubadilisha muundo wa serikali, kasoro ya katiba ya chama kimoja na hayakuleta sura mpya katika ngazi zote za utawala.
Muundo wa chama kimoja ulikuwa na maana ya kudumisha amani na kuleta umoja. Lakini miongoni mwa athari zake ni kuwa na kundi la viongozi walioacha taaluma zao na kujiingiza ndani ya chama kupata ULAJI. Kikwete alisomea uchumi lakini hakufanya kazi za kiuchumi.
Watu hawa hawana jipya na utendaji wao wa kazi ni sawa na waliyofanya miaka 30 iliyopita. Nyerere aliaga dunia miaka 8 iliyopita lakini muundo wa serikali na watendaji wake bado wamo madarakani.
Kitu cha kuwafanya hawa watu waondoke madarakani haraka na kuleta mabadiliko yasio na EXCUSE ZA NYERERE ni kutumia ya KAGAME au MUSEVENI walichotumia - MTUTU wa bunduki. Hivyo usilete mifano ya Museveni na Kagame kama hauko tayari kushika mtutu wa bunduki kwa jinsi unavyopenda amani.
Mwaka 1995, kulikuwa na uwezekano mkubwa wa mabadiliko ya muundo mzima wa serikali na katiba nchi nzima. Yazilipoonyeshwa Video za mauaji ya Rwanda, watu wakataa mabadiliko.
Kama hatutaki mabadiliko ya mtutu wa bunduki au kutumia nafasi chache zinazopatikana kuchagua sura mpya basi itabidi tusubiri mabadiliko ya vizazi kwani kundi lililopo madarakani litaendelea kuzeeka na kufa.