Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,162
- 137,242
That's a good one!! I got me a good laugh....
Wakati Nyerere anahangaika kutafuta yanga na maharage ya funza ili wananchi wake pale Idodoma wasife njaa, mabaharia wetu hawakutaka udhia wa kunyimwa mafuta ya kuvinjari na mabenzi yao club Billicana.
Jamani na hii mi email ya mitaperi ya Nig. nayo mnaihusianisha na Nyerere?
-Bila Nyerere uhuru tungeupata wapi?
Utakapokuwa tayari kuyatafuta hayo mabaya ya Nyerere usisahau ya ...mabaharia waliolazimika kutoa rushwa ili wapate shule, pale wapi? Nasaco au? Yote hayo ni kwa sababu walitumwa na Nyerere, na pengine hata huko walipo leo ni rushwa hizo hizo alizowafundisha huyo mzee ndizo zimewafikisha huko.
Na usisahau 'colgate' za pale Namanga, na misururu ya foleni za mikate, kumbe ni za saruji! Wakati hizo colgate zinapatikana huko kwa majirani, wenzetu pale Turkana na Mandera walikuwa wakifa kwa njaa, huku wakubwa Nairobi wakinepa tu kwenye mabenzi. Wakati Nyerere anahangaika kutafuta yanga na maharage ya funza ili wananchi wake pale Idodoma wasife njaa, mabaharia wetu hawakutaka udhia wa kunyimwa mafuta ya kuvinjari na mabenzi yao club Billicana.
Huyu Nyerere alikuwa ni mshenzi kweli kweli kunyima watu raha.
Tufanye basi Leo kuanzia saa mbili ya usiku ya kwenu hapo yaani itakuwa ni Old School tupu na Slow Jamz. Kwa kuanzia tu kuna jamaa mmoja pale EastAfricanTube kashusha mambo ya Old School si kawaida. Check it out at Old School Jamz
JK naye ni binadamu ana mapungufu yake, kwa nini mnamzodoa kila kukicha?. mwacheni atulie ikulu afanye vitu vyake kwani umesikia wapi kwamba JK hana uchungu na tanzania?.
Kwa kumalizia nawaombeni mumwache kumsema vibaya Mwalimu ili apate mapumziko ya amani ya milele, alikuwa na mapungufu yake mengi tu, lakini mazuri aliyoyafanya kwa Tanzania siku zote yatashinda mabaya.
Mkuu Bubu,
Thank you kwani article yako ni educative na fair enough, kuhusiana na ishu at hand! Na sina objection kabisa na hoja zako maana ni very clear na to the point! Ingawa ninatka kusema tu kuwa hatumsemi vibaya Mwalimu, mkuu Martin Luther alipojitoa kwenye dini ya Catholic, aliyasema wazi yiliyomtoa kule, na inaaminika kwamba moja kati ya idea zake za revolution katika dini mpya aliyoianzisha, ndio kilikuwa kiini haswa cha kuzaliwa kwa Capitalism, lakini kwanza aliyaweka bayana yale aliyoyaona kuwa ni mapungufu ya kanisa la Catholic,
Kuyazungumza mapungufu ya Mwalimu, kwa ni aya kujirekebisha sio kumsema vibaya Mwalimu, wewe kuna mapungufu umeyasema hapo kwenye article yako sio kweli kwamba umemsema vibaya Mwalimu, umeyasema mapungufu ambayo tukiyakalia kitako as a nation tunaweza kujisaidia na kutoyarudia tena na ku-move forward, lakini tatizo ni pale tunapokataa, kwa mfano Mwalimu siku zote alipenda sana kuamua ishu za kisheria kwenye vikao vya CCM, I mean that was wrong na ndio mana sasa kina Kingunge bado wanajaribu kutaka ishu ya mafisadi iishie kwenye vikao vya CCM wanaposema wanataka suluhu na wapinzani, sasa hivi kweli ni kumsema vibaya Mwalimu?
Kuna tofauti ya kumsema vibaya Mwalimu, na kujifunza mapungufu ya Mwalimu kwa faida ya taifa letu, kujitawala miaka 22 baada ya Mwalimu kuondoka, haibadilishi the fact kuwa mpaka leo bado kuna trace za Mwalimu kila kona, kwa mfano Mkapa alimpa urais Muuungwana, exactly kama yeye alivyopewa na Mwalimu, sasa we need to address ishu kama hizi ili naye Muungwana asizirudie, maana Muungwana naye akifanya kama Mkapa basi taifa letu halitakuja kujinasua na haya matatizo sugu!
Umaskini chini ya Mwalimu ulisababishwa na kutegemea mazao ya biashara tu kama ndio chanzo cha mapato yetu ya kigeni. Wakati wa Mwalimu pia ukusanyaji wa kodi ulikuwa ni mdogo sana ukilinganisha na sasa.
Sasa hivi tuna rasilimali zetu kama dhahabu, tanzanite, mbao, gesi n.k. pamoja na kuwa mikataba iliyosainiwa haina maslahi kwa Tanzania, imeongeza kwa kiasi pato la fedha za kigeni, lakini wananchi hawaoni tofauti yeyote katika maisha yao ya kila siku kutokana na ongezeko hili la pato la fedha za kigeni na ongezeko kubwa la makusanyo ya kodi kupitia TRA.
Inakuwaje pamoja na kuongezeka pato letu la fedha za kigeni na makusanyo makubwa ya kodi, bado wananchi hawaoni kupanda kwa ubora wa maisha ukilinganisha na wakati Mwalimu Nyerere (RIP) alipokuwa madarakani? inakuwaje wengine wanaona ubora huo wa maisha unazidi kushuka?
Vipi....kwani nimeongopa? Jamaa anampenda Nyerere kikweli kweli. Hivi umewahi kumsikia anavyoongeaga kwenye podomatic? Yaani anasound kama Nyerere...sitashangaa na yeye kukata mitaa ya huko Detroit na kifimbo chake na kibaragashia. Hehehehehe....
Ngoja niwape stori. Kuna siku moja hivi...imekuwa kitambo kidogo. Jamaa alikuwa na podcast ya Nyerere akiongea na Watanzania....mimi nikaharakisha kusikiliza nikitegemea kumsikia Nyerere mwenyewe....sasa guess what? You guessed it....it was yours truly!! Yaani alimpatia kishenzi utadhani sijui nini....sikuwa na mbavu tena
Jamani na hii mi email ya mitaperi ya Nig. nayo mnaihusianisha na Nyerere?
Hakuwa malaika huyu mzee, kuna aliyokosea mengi, lakini mazuri aliyo yafanya kwangu mimi naona yanazidi mabaya aliyo yatenda.
-Bila Nyerere uhuru tungeupata wapi? Kumbuka alikubali kuacha kazi yake ya mshahara, akaishi kwa misaada ili atupatie uhuru wetu.
-Elimu ya bure kwetu sie walala hoi tungeipata wapi?
-Madini yetu tunayo yalilia wezi hawa wanayo kimbilia yauza na kugawana kama njugu si yangeisha isha?
-Bila Nyerere umoja na undugu wa kitanzania (ambao huwa hatubaguani kwa misingi ya dini na ukabila) alio tujengea tungeupata wapi?
Udikiteta wake ulikuwa wa maana sana ili nchi iweze kuungana, ni kama sasa hivi ili tuendelee tunamuhitaji dikiteta mwingine ambaye atatupilia mbali maamuzi ya kijinga yaliyo fanywa na walafi kina Mkapa/Yona/karama/ na wengineo ili tuanze upya!
Tunahitaji dikteta ambaye ataweza jisimamia katika maamuzi yake siyo hawa tunao waona wajasiriamali ikulu, na vascodagama kwa kodi za walala hoi!
Tunahitaji raisi amabye atakuwa na guts za kusema No, palipo na No! siyo blabla.. bila utendaji!
Misingi mizuri aliyo tuwekea ya kusomesha vijana wenye uwezo ili waje walitumikie Taifa yote tumeipiga chini, sasa hivi elimu ni kwa wateule waliobarikiwa kuwa na njuruku, kazi nzuri zinazo lipa ni kwa majina ( rejea BOT)
Tunaona misingi hiyo inavo zidi kufukiwa tunapoletewa sheria za ajira za serikalini kuwa za teuzi?? siyo za ushindani wa qualifications!
Am out of this, leave Nyerere alone, Mwacheni apumzike kwa Amani, kiumbe wa Mungu!
Mazuri mengi mno katufanyia MUNGU MPUMZISHE KWA AMANI.