Phillemon unayosema ya kweli. Mbunge mmoja wa jimbo jirani na kwetu ambaye ni mwislamu na ni profesa (siku hizi nasikia wakimwita "alhaji profesa"),
sasa mbona unaona taabu KUMTAJA wewe mtaje au kuna dhambi kumtaja kwa jina? Huoni kama huko ni kupoteza Mwelekeo wa Mjadala?
Kwani kuna sehemu gani imeandikwa eti ni DHAMBI mtu kuitwa Alhaji Profesa? hiyo wewe inakuuma nini? na inaumuhimu gani kwako au katika mjaladala huuu?
Wewe ungemtaja MBUNGE FULANI..that simple sasa umeanza kujibu hoja kwa connotation za kikejeli unategemea nanai atakuchulia serious?
aliposikia habari za awali za chuo hicho (kabla ya Mkapa kukizindua), alikuwa anawakejeli wenzake wanaounga mkono wazo hilo.
Aliwakejeli wenzake ambao ni akina nani?
Lini?
ushahidi uko wapi?
Niliwahi kumsikia akimwambia mwenzie mmoja "na wewe na elimu yako unashabikia university ya wajahidina? nitashangaa sana nikiona unapeleka mwanao huko!". Kumbe si peke yangu niliyemsikia, ijumaa iliyofuata maneno yake yakakemewa vikali katika tahariri ya gazeti la Annuur, bila kumtaja jina.
Bado tuko kule kule kwenye maswali ya hapo awali.
Ajabu huyu tu asiye na na JINA anaendelea kumuongelea na sasa hivi umejitahidi kulitaja gazeti la Annur lakini naona bado una matatizo katika kuthibitisha ushahidi wako at least ungeweka:
TOLEO LIPI NA ANNUR:
LA LINI?
NA KICHWA CHA HIYO TAHARIRI KILIKUWA KINASEMAJE?
Hiki ni chuo kikuu cha waislamu au cha kiislamu? Swali hili bado gumu kulijibu practically. Wengi wanaona kama ni cha waislamu na pa ni cha kiislamu. Uongozi wote ni wa waislamu na ni wa kiislamu. Wanafunzi karibu wote ni waislamu. Wapo wachache wenye majina ya kikristo na yasiyo ya kidini.
Unaonekana ni mtu makini sana katika kutengeneza hoja lakini vile vile haiondoi ukweli kuwa unaonekana kuwa hoja zako hazipangiki kwani umeshindwa kufanya simple research kujua:
CHUO KIKO CHINI YA NANI?
UONGOZI WAKE NI AKINA NANI?
JE CHUO NI CHA KIISLAM AU CHA WAISLAM
unaposema wengi wanaona ni cha kiislam na cha waislam , je kwa research gani iliyofanyia au kura ipi ya maoni au hata ushahidi wa KIIMANDISHI
mwisho unasema wapo "wanafunzi wachache wakikristo" sasa kama umeweza kujua hilo umeshindwa vipi kupata majibu ya maswali hayo hapo juu?
Unaposema swali Gumu kulijibu Politically unamaana gani tafadhali FAFANUA hilo
Majuzi nilikuwa Dar nikasikia jinsi hao wachache walivyojiunga huko. Ilikuwa mjadala miongoni mwa waliomaliza form six, na walikuwa wanajadili swali hili: ati "kipi bora kati ya kutokwenda chuo kikuu kabisa na kwenda chuo kikuu cha waislamu Morogoro?" Wapo waliodai kuwa kuliko kukosa kabisa cheti cha degree, bora kwenda huko MUM. Wengine wakasema wako radhi waanze na diploma mahali pengine kuliko kwenda huko MUM. Sikubahatika kujua dini zao. Mtu mmoja aliyekuwa anafuatilia mazungumzo ya wale vijana akawauliza huko MUM kuna ubaya gani? Wakajibu kwa pamoja "tutaajiriwa wapi, Afghanistan?"
Mwenzetu inaelekea masikio yako yanafanya kazi maradufu...kwani harari zako zinakuwa za "KUSIKIA" ambayo haikatazwi lakini matumizi yake katika kujenga hoja zako yanakuharibia kwani huwezi kujenga hoja based on hearsay.
Vile vile je Mazungumzo hayo yangekuwa yana husu CHUO CHA KIKRISTO kama LOYOLA au ST XAVIER wewe binafsi ungekuwa na maoni gani?
Na mwisho kabisa huwezi kuwakataza watu wasiwe na maoni sasa sioni shida yako wewe iko wapi na hao jamaa kutoa maoni yao
Kwenye prospectus yao (inapatikana kwenye mtandao),
HUREEEEE!!!!!!!!!!!!!!
Kumbe wewe unaweza kufanya utafiti mdogo mdogo kama huuu sasa ulishindwa vipi kutoa majibu niliyokuuliza hapo juu?
ohhh by the way TUNAOMBA LINK ya hiyo PROSPECTUS tafadhali
wanasema ndani ya chuo kuna msikiti (ninavyofahamu yale majengo ya TANESCO hayakuwa na msikiti ndani), lakini watu wa dini nyingine wanashauriwa wafuate ibada nje ya campus.
TUNAOMBA EVIDENCE YA MANENO HAYO HAPO JUU
KAMA UNAYOPICHA TUTASHUKURU ZAIDI.
Je ni wapi wanafunzi wa KIKRISTO ambao so far hujatutajia idadi yao wamelalamika kuhusu KANISA ndani ya chuo cha morogoro...mheshimiwa kwenye karne hii huwezi kuniambia kuwa hakuna aliyesikia malalamiko hivyo nakuomba ufanye utafiti wako na ikiwezekana waulize hao vijana wa kikristo wanaosoma pale wakupe majibu
Lakini mimi niliwahi kwenda Uholanzi nikakuta msikiti ndani ya chuo kikuu cha kikatoliki (kulikuwapo pia na chapel kwa ajili ya wakristu).
Naona sasa tunaelekea UHOLANZI sasa bosi nataka nikufahamishe kuwa si uholanzi tuu bali UK vyuo vyote vina PRAYER ROOM, kwenye CONGRESS NA SENATE kule states kuna PRAYER ROOM
heathrow airport zipo prayer rooms... hata hiyo MISIKITI unayozungumzi ipo pale sasa sijakuelewa hoja yani ni ipi haswa?
Nadhani kuna mambo mengi bado ya kurekebisha ili kiweze kuwa secular kweli na kiweze kuvutia pia wanafunzi wa dini nyingine.
Kwanza kuna sheria gani inawalazimisha wawe secular?
Pili kwani ni lazima kiwavutue wenye dini zingine?
why is it so important kwako watu wenye dini zingine kujiunga na hikio chuo wakati vyuo sasa hivi vimetapakaa kila kona?
Hata hivyo sidhani kwamba kikitangaza rasmi ni cha kidini kutakuwa na ubaya wowote, ni haki yao.
naona unaendelea kujijibu safi sana!
Majengo yale walipewa bure kama taasisi ya kiislamu, kwa hiyo sioni ubaya wakiyatumia kama taasisi ya kiislamu.
ambayo hiyo haihusiani
Na pia nadhani si lazima watu wa dini nyingine wakasome huko, kwani siku hizi kuna choices nyingi.
unaendelea kujijibu....
Na pia si lazima waislamu wakasome kwenye chuo hicho pekee, nao pia wana choices nyingi.
once again...
Ila kama kuna wanaotamani chuo hicho kiwe secular kweli, basi kuna changamoto nyingi kama hizo.
J e watu hao ni pamoja na wewe au ?