Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Typical watanzania tulivyo...sasa jamani, itawezekana kutunza UKOO wote wa mwalimu? lazima tufike sehemu tutambue aliyekuwa kiongozi ni JULIUS na sio ukoo wake wote. watu wanaostahili kusaidiwa au kulipwa pension ni primary depandants wake ambao ni Mama MARIA NA WATOTO WAKE WALIO CHINI YA MIAKA KUMI NA NANE! No this is unfir kuona kwamba kila mtu as long as ana ukaribu na Nyerere bas anastahili kutunzwa na serikali. Hiyo serikali itawatunza wangapi? yenyewe ndo hiyo tunaipigia kelele kwa rushwa nk. Angelalamika mama Maria ningeelewa lakini hawa extended families? Iam sorry!

Infact watoto wa Mwalimu wote, hakuna anayestahili kusaidiwa na serikali! wameshakuwa watu wazima wastruggle kama watanzania wengine. Mama Maria ndo anastahli pension ya mumewe na si vinginevyo. Tuache huu "ujamaa" uliopitiliza mipaka! Jamaa wafanye kazi na sio kulia lia..oohh sisi ni ndugu wa mwalimu tumetelekezwa. This is nonsese kabisa.
 
Masanja umeongea!Mwalimu alisisitiza kujitegemea na aliupinga sana uzembe!haiwezekani ukoo wote wa nyerere pamoja na ndugu na majirani wake wapate fadhila kutokana na jina la mwalimu huu upuuzi!watu wazembe kama hawa mwalimu aliwatandika mikwaju!
 
"Kama mnataka kuamini hilo ninaomba Watanzania wenye uchungu na ukoo wa Mwalimu siku moja waende kutembelea Butiama wajionee wenyewe.

Mbali na hilo, Bw. Anthony alisema hadi mauti yanamfika Mwalimu alikuwa kiongozi aliyeishi maisha ya kawaida, akiwa hana fedha kiasi cha kuacha deni la sh. 50,000.

hizi paragraph mbili zimeniacha hoi.
 
...sipendelei malumbano ya kisiasa, lakini jamii nilozaliwa, kukulia na ninayoishi inanifanya ama kwa njia moja ama nyingine kuathirika na 'mavuno' ya fikra za wanasiasa na viongozi wetu. Ckeck these facts;...

Economy - overview: Tanzania is one of the poorest countries in the world. The economy depends heavily on agriculture, which accounts for about half of GDP, provides 85% of exports, and employs 80% of the work force. Topography and climatic conditions, however, limit cultivated crops to only 4% of the land area. Industry traditionally featured the processing of agricultural products and light consumer goods

Population below poverty line: 36% (2002 est.)

Tanzania Rural poverty

Rural poverty in the country has been halved in the period from 1985 to 2001. At present about 38 per cent of people living in rural areas are classified as poor. This progress is reflected in the United Nations Development Programme's Human Development Index for Tanzania, which rose from 0.3 in 1991 to 0.4 in 2002. Nevertheless, poverty is still widespread and acute, and is generally a rural phenomenon: about 85 per cent of the country's poor people live in rural area and rely on agriculture as their main source of income and livelihood. According to the Household Survey of 2000/01, some 20 per cent of rural people live in extreme poverty and about 39 per cent are considered poor.

...hayo yote yalitokana na sera za viongozi wetu. Pamoja na mengi mazuri waloyafanya, lakini maisha ya wananchi wa Tanzania yetu ni matokeo ya Sera za Viongozi walopita na wa sasa, kiasi kwamba hizo shida zinazowakabili familia ya Mar. Mwl JK Nyerere (RIP), ni kioo tu cha hali za mamilioni ya wazee, ndugu, jamaa na watanzania wenzetu (Est 36%-39%) wanaoishi below poverty line.

Binafsi namshukuru sana Mzee (Ruksa) Alhaj Ali Hassan Mwinyi, pamoja na mapungufu yake, lakini angalau aliweza kupunguza kasi ya umaskini katika kipindi cha utawala wake, 1985-1995, japo kuna wataopinga kwa sababu za Vita vya Kagera 1978-1979. Bado nataka kuamini Azimio la Arusha ndilo lilotusababishia umaskini huu, ambao hata familia ya Mwl inakumbana nao.

Nachelea kujiuliza uliza swali hili; iweje ndugu hao hawakutumia wakati 'wao' kujiendeleza kielimu, ukulima na kibiashara (kipindi Mwl akiwa madarakani), badala ya kumtegemea mzee wa watu hata kwa pesa za kulipia umeme?, ...ingawa, mwanya wa 'Golden opportunity' hiyo inatumiwa vibaya na ndugu wa viongozi wengine wengi tu duniani kujitajirisha, kwa Mwl ingelikuwa kuna unafuu kidogo.
 
...sipendelei malumbano ya kisiasa, lakini jamii nilozaliwa, kukulia na ninayoishi inanifanya ama kwa njia moja ama nyingine kuathirika na 'mavuno' ya fikra za wanasiasa na viongozi wetu. Ckeck these facts;...





...hayo yote yalitokana na sera za viongozi wetu. Pamoja na mengi mazuri waloyafanya, lakini maisha ya wananchi wa Tanzania yetu ni matokeo ya Sera za Viongozi walopita na wa sasa, kiasi kwamba hizo shida zinazowakabili familia ya Mar. Mwl JK N yerer (RIP), ni kioo tu cha mamilioni ya wazee ndugu jamaa na watanzania wenzetu (Est 36%-39%) wanaoishi below poverty line.

Binafsi namshukuru sana Mzee (Ruksa) Alhaj Ali Hassan Mwinyi, pamoja na mapungufu yake, lakini angalau aliweza kupunguza kasi ya umaskini katika kipindi cha utawala wake, 1985-1995, japo kuna wataopinga kwa sababu za Vita vya Kagera 1978-1979. Bado nataka kuamini Azimio la Arusha ndilo lilotusababishia umaskini huu, ambao hata familia ya Mwl inakumbana nao.

Nachelea kujiuliza uliza swali hili; iweje ndugu hao hawakutumia wakati 'wao' kujiendeleza kielimu, ukulima na kibiashara (kipindi Mwl akiwa madarakani), badala ya kumtegemea mzee wa watu hata kwa pesa za kulipia umeme?, ...ingawa, mwanya wa 'Golden opportunity' hiyo inatumiwa vibaya na ndugu wa viongozi wengine wengi tu duniani kujitajirisha, kwa Mwl ingelikuwa kuna unafuu kidogo.

Mchongoma,

Hizo statistics za UN ni utumbo mtupu. Mimi nilizaliwa na kukulia kijijini na mpaka leo ni mwumini wa siasa za vijijini. Nikiwa nyumbani nashinda huko vijijini.

Utalilaumu Azimio la Arusha, sawa lakini miaka hiyo watu wengi kule vijijini walikuwa sio ombaomba wala walikuwa hawafi njaa.

Hali ya sasa inasikitisha, unaona watu wengi wanashindwa hata kutunza familia zao. Miezi minne baada ya mavuno tayari ni njaa kubwa. Wazee wanaomba bila hata aibu. Halafu mtu anasema umaskini huko vijijini umepunguzwa kwa nusu?

Wakati mimi nasoma msingi na sekondari, kulikuwa na wafanyakazi wa kilimo mpaka vijijini, mabwana mifugo nk. Sasa nawaona mabwana mifugo tu wanaoenda kukagua nyama kwenye vilabu ili wapate kitoweo, au wanaoenda kudunga ng'ombe sindano ili walipwe.

Mabwana shamba hawana kazi ya kufanya na wanashinda ofisini wakisubiri semina na wenyewe wafaidike na kujaza forms.

Sera za Nyerere zinaweza kuwa zilikwamisha baadhia ya wananchi wenye elimu na hasa mjini, lakini kwa wananchi wa vijijini Mwalimu alisaidia mno.

Sawa tungebadilisha yale mabaya ya mwalimu na kuendeleza mazuri yake, kama alivyosema mwenyewe sisi tunachukua mabaya na kuacha mazuri.

Priorities zetu Tanzania zimeenda kushoto mno!
 
Hapo wanaJF siyo kulalamikia mfumo wa siasa za viongozi wetu wa zamani. Kitu cha msingi kama mdau hapo juu alivyonena, serikali haiwezi kumtunza kila mtu as long as alikuwa analelewa na Nyerere.

Huo ndiyo ule uzembe ambao yeye Mwalimu alikuwa anaupigia kelele. Hata huyo Anthony ambaye ni mpwa, ninamshangaa anaposema yatima wameachwa bila msaada, sasa alitaka nani awalele hao watoto kama siyo jukumu lake. Otherwise wawapeleke hao yatima kwenye nyumba za kulelea watoto yatima, lakini siyo jukumu la serikali kuwalea eti kwa sababu wanamajina ya ubini ya NYERERE.

Nawasilisha.
 
.....BAADA ya maziko ya mwalimu mama maria na wanawe waliwaambia wana ukoo kuwa business cannot be as usual...uwezo wa kuwasaisia pesa na mavuno utakuwa mdogo ..na wangefanya tu pale watakapoweza..

mama maria amesikika akisema zile pesa za rambi rambi kwa miaka karibu saba amekuwa akizitumia KUSOMESHA WAJUKUU WAO[nafikiri yeye na mwalimu wanategemea mmoja wao atafanikiwa huko mbele]..ambao mwalimu alimwagiza wasomeshwe kwa kadiri ya uwezo wao..na ndio zimeisha...museveni pia anawalipia baadhi...
 
Kwani Mwalimu hakufanya investment yoyote?

Je Salim Ahmed Salim wa Mwalimu Nyerere Foundation anajua haya?

Sikubaliani kuwa kodi za waTanzania ziwa subsidize familia ya Nyerere kwani hata mimi babu yangu alipigania uhuru na ukoo wetu ulisacrifice kama wa Nyerere sasa kwa nini akina Nyerere wapewe preferential treatment?

Kama wanataka hizo pesa za kulipa madeni wauze yale magari aliyokuwa anatumia mwalimu, ile nyumba ya mwalimu pale Butihama, Msasani nayo wakiuuza wanaweza kumaliza madeni bila kusahau ardhi kubwa waliyonayo.Vile vile wanaweza kuachana na hizi gharama za kumkumbuka mwalimu kila mwaka. Hizo zote ni un necessary expenditures na wao kama wanafanmilia wanapweza kufanya shughuli zao in private.Ya nini kungangania kuomba misaada serikalini wakati hakuna mwenye nia ya kuwasaidia?




Naamini wakiuza vyote hivyo hawashindwi kulipa deni la hospitali, umeme na matatizo mengineyo kisha kila mmoja aangalie ustaraabu wake.


Nadhani this should be a wake up call...na wajue kuwa Mzee Kwawawa na Mzee Kingunge wakishavuta tu basi wao hawatokuwa na lao.




Thats life na desperate times call for desperate measures, najua wengine mtakuja kusema kuwa dozi yangu ni kali mmno lakini lets be real, hatuwezi kubabysit ukoo mzima wa Mwalimu.

 
!
Yes, kuna watu muhimu sana ktk kupigania Uhuru wetu wameachwa nje ya historia yetu lakini sio swala la Waislaam tu bali Watanganyika. Wapo watu mikoani ambao walishiriki kikamilifu kwa dini na kabila zao ktk mapambano yetu na tukianza kuwataja kwa kabila na dini zao utakuta mkorogano mkubwa. Kulikuwa na wanachama wengi wa TANU toka dini zote hata wahindi na waarabu walishiriki kikamilifu ktk nafasi zao kuupigania UHURU.

Mkandara,

Heshima yako kaka. Uchambuzi makini kabisa huu, na natamani watu wengi wangepata nafasi ya kuusoma na kuuelewa hivi. Nimenukuu hayo hapo juu kwa sababu nimeona ni hitimisho murua la maelezo yako.

Watu wengi wamekuwa wakisahau kwamba kilichokuwa kinawatuma watu kupigania uhuru si dini wala kabila zao bali ni kusukumwa na uzalendo kwa nchi yao. Na hakika ni kweli kwamba ukianzisha chama Dar au Tanga au Zanzibar na kikakubalika kwa sera zake na wenyeji wa maeneo hayo, wakijiunga nacho, wengi wao watakuwa waislam, si kwa sababu chama ni cha kidini, bali kwa sababu hao walioko maeneo hayo ndio sifa (demographic characteristic) yao. Vivyo hivyo ukitaka mbunge au diwani kutoka eneo kama hilo, uwezekano (probability) mkubwa ni wa mtu huyo kutoka katika kundi lenye watu wengi. Si kwamba mtu wa kundi lenye wachache hatachaguliwa, la hasha, aweza akachaguliwa, lakini probability ni ndogo. Sasa hapo sidhani kama kuna ubaguzi, unless kuwe na jitihada za wazi za kulisakama kundi fulani.

Nadhani wakati umefika sasa wa watanzania kuwekana sawa kuhusu njia muafaka za kudai uwiano sawa wa fursa za kimaendeleo kwa kuzingatia zaidi yale yanayotuweka pamoja (ubinadamu na utanzania) kuliko yale yanayotutenga (kabila, dini, rangi n.k). Nina uhakika yakipatikana maendeleo eneo fulani, watafaidika wenyeji wa pale bila kujali tofauti zao. Chukulia kwa mfano kuwe na university kila mkoa. Na pia ubora (standard) wa elimu katika ngazi zote uwe katika viwango fulani vizuri vya kitaifa. Unadhani itawezekana university of Rukwa iwe ati hakuna mwanafunzi mfipa? Au eti wanafunzi wagogo hawaendi university? Sidhani. Kwa hiyo hebu tupiganie usawa wa fursa za maendeleo kimgawano (distributive equity) tuone kama hatutasonga mbele kwa pamoja kama taifa.
 
hata hivyo kuna malalamiko kama ,jina la chuo linawakwaza watu kuingia pale ,hata waislamu wenye uwezo hawapendi kuwapeleka watoto wao pale au hata shule za misimamo mikali .

Phillemon unayosema ya kweli. Mbunge mmoja wa jimbo jirani na kwetu ambaye ni mwislamu na ni profesa (siku hizi nasikia wakimwita "alhaji profesa"), aliposikia habari za awali za chuo hicho (kabla ya Mkapa kukizindua), alikuwa anawakejeli wenzake wanaounga mkono wazo hilo. Niliwahi kumsikia akimwambia mwenzie mmoja "na wewe na elimu yako unashabikia university ya wajahidina? nitashangaa sana nikiona unapeleka mwanao huko!". Kumbe si peke yangu niliyemsikia, ijumaa iliyofuata maneno yake yakakemewa vikali katika tahariri ya gazeti la Annuur, bila kumtaja jina.

Hiki ni chuo kikuu cha waislamu au cha kiislamu? Swali hili bado gumu kulijibu practically. Wengi wanaona kama ni cha waislamu na pa ni cha kiislamu. Uongozi wote ni wa waislamu na ni wa kiislamu. Wanafunzi karibu wote ni waislamu. Wapo wachache wenye majina ya kikristo na yasiyo ya kidini. Majuzi nilikuwa Dar nikasikia jinsi hao wachache walivyojiunga huko. Ilikuwa mjadala miongoni mwa waliomaliza form six, na walikuwa wanajadili swali hili: ati "kipi bora kati ya kutokwenda chuo kikuu kabisa na kwenda chuo kikuu cha waislamu Morogoro?" Wapo waliodai kuwa kuliko kukosa kabisa cheti cha degree, bora kwenda huko MUM. Wengine wakasema wako radhi waanze na diploma mahali pengine kuliko kwenda huko MUM. Sikubahatika kujua dini zao. Mtu mmoja aliyekuwa anafuatilia mazungumzo ya wale vijana akawauliza huko MUM kuna ubaya gani? Wakajibu kwa pamoja "tutaajiriwa wapi, Afghanistan?"

Kwenye prospectus yao (inapatikana kwenye mtandao), wanasema ndani ya chuo kuna msikiti (ninavyofahamu yale majengo ya TANESCO hayakuwa na msikiti ndani), lakini watu wa dini nyingine wanashauriwa wafuate ibada nje ya campus. Lakini mimi niliwahi kwenda Uholanzi nikakuta msikiti ndani ya chuo kikuu cha kikatoliki (kulikuwapo pia na chapel kwa ajili ya wakristu). Nadhani kuna mambo mengi bado ya kurekebisha ili kiweze kuwa secular kweli na kiweze kuvutia pia wanafunzi wa dini nyingine. Hata hivyo sidhani kwamba kikitangaza rasmi ni cha kidini kutakuwa na ubaya wowote, ni haki yao. Majengo yale walipewa bure kama taasisi ya kiislamu, kwa hiyo sioni ubaya wakiyatumia kama taasisi ya kiislamu. Na pia nadhani si lazima watu wa dini nyingine wakasome huko, kwani siku hizi kuna choices nyingi. Na pia si lazima waislamu wakasome kwenye chuo hicho pekee, nao pia wana choices nyingi. Ila kama kuna wanaotamani chuo hicho kiwe secular kweli, basi kuna changamoto nyingi kama hizo.
 
Bw. Anthony alisema kuna watoto wa mjomba wa Mwalimu aitwae Salim Nyakomge, mtu ambaye ndiye Mwalimu alitumia ngo'mbe wake kupata fedha za kwenda Chuo Kikuu Makerere, hao nao maisha yao ni taabani na sasa wanaishi kwenye vibanda vya tope vilivyoezekwa kwa nyasi.

MWE!!...Mswahili,Samvulachole,Nungwi...mpooooo!!!


Kiboko kwa mujibu wa Bw. Anthony hivi sasa yuko kitandani akiwa mgonjwa, msaada pekee alionao ni kijana wake mmoja wa kiume anayemsaidia na pia kipato chake cha sh. 15,000 anachokipata kwa mwezi kutokana na wapangaji wa nyumba yake.

"Tumejitahidi kuchanga fedha wakati fulani tukampeleka Mwanza kupata matibabu, lakini hivi sasa amerudishwa nyumbani hatuna fedha. Bahati nzuri ana nyumba aliyojengewa na marehemu Sokoine, ina vyumba vinne.

..Sokoine alimjengea nyumba mdogo wake Nyerere? Nyumba hiyo iko wapi? Mwaka huu tutajifunza mengi jamani.

Kwa upande mwingine Raisi wa Jamhuri ya Muungano anapata fedha na marupurupu kiasi gani? What did Mwalimu do with all the money he was getting? Kuwa Raisi wa Tanzania miaka 25 siyo jambo dogo jamani.

..nakumbuka kusoma kuhusu Thomas Jefferson Raisi wa tatu wa USA. Baada ya kufariki watumwa wake, na mali zake, zilipigwa mnada. Hata yeye alikuwa na watu wengi tu waliokuwa wakimtegemea.
 
It is an amusing story na a sad one pia, lakini I am going with Masanja, sasa some where ni lazima tu-draw the line,

Taifa limtunze mke tu wa Mwalimu, wengine watuonyeshe mfano wa waliyojifunza kutoka kwa Mwalimu, ya self-reliance, wao walijionea first hand, sisi ni kuwaiga wao,

Anyway, it was a good story kwa kuburudisha tu wananchi na taifa kwa ujumla, lakini nothing serious kwa taifa! Yaaani I am shocked jinsi Mwalimu alivyokuwa akitutaka wananchi tujitegemeee, huku akiwaweka watu wa ukoo wake mwenyewe bure tu na kuwalipia!

I hope hii haikuwa a double standard!
 
Kwani Mwalimu hakufanya investment yoyote?

Je Salim Ahmed Salim wa Mwalimu Nyerere Foundation anajua haya?

Sikubaliani kuwa kodi za waTanzania ziwa subsidize familia ya Nyerere kwani hata mimi babu yangu alipigania uhuru na ukoo wetu ulisacrifice kama wa Nyerere sasa kwa nini akina Nyerere wapewe preferential treatment?

Kama wanataka hizo pesa za kulipa madeni wauze yale magari aliyokuwa anatumia mwalimu, ile nyumba ya mwalimu pale Butihama, Msasani nayo wakiuuza wanaweza kumaliza madeni bila kusahau ardhi kubwa waliyonayo.Vile vile wanaweza kuachana na hizi gharama za kumkumbuka mwalimu kila mwaka. Hizo zote ni un necessary expenditures na wao kama wanafanmilia wanapweza kufanya shughuli zao in private.Ya nini kungangania kuomba misaada serikalini wakati hakuna mwenye nia ya kuwasaidia?




Naamini wakiuza vyote hivyo hawashindwi kulipa deni la hospitali, umeme na matatizo mengineyo kisha kila mmoja aangalie ustaraabu wake.


Nadhani this should be a wake up call...na wajue kuwa Mzee Kwawawa na Mzee Kingunge wakishavuta tu basi wao hawatokuwa na lao.




Thats life na desperate times call for desperate measures, najua wengine mtakuja kusema kuwa dozi yangu ni kali mmno lakini lets be real, hatuwezi kubabysit ukoo mzima wa Mwalimu.


Investment Nyerere alio acha ni Mtu kwenda Shule, na kufanya kazi au kuwa mkulima Bora.
 
hii inawezekana ikawa sababu moja ya viongozi wetu kujilimbikizia mali kwa familia zao na watoto zao ! its just ze beginning !
 
hii inawezekana ikawa sababu moja ya viongozi wetu kujilimbikizia mali kwa familia zao na watoto zao ! its just ze beginning !

Haitosaidia kama akili hakuna au Mngt Skills hakuna, au wanabwia unga
 
Kama Anthony Nyerere ndiyo mrithi (kimila) wa estate ya Mwl. basi ni yeye ndiye aliyetakiwa aangalie familia/yatima wananoongelewa hapa.

Speaking of Nyerere Foundation kama alivyouliza Game Theory. Pale yupo Jeseph Butiku ambaye ninadhani ni ndugu ya Mwl. MNF inafahamu haya matatizo lakini sidhani kama wanaweza kusaidida. Kwenye ile foundation kuna pesa nyingi sana inamiminika lakini kuna ubadhirifu mkubwa sana wa pesa. Na ukithubutu kufungua mdono wako umekwisha.
 
Back
Top Bottom