Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Acheni kumdhalilisha Mwalimu, udikteta, mnajua maana ya udikteta nyie? Mwalimu alimwua nani? Mwalimu alitoa orders zipi ili watu wateswe?

Angalia marais waliomzunguka Mwalimu, wote walikuwa wanachinja watu labda ukiondoa rafiki yake Kaunda.

Mwalimu alikuwa kama baba ambaye alitaka kuwajengea wanawe kwa faida ya baadaye, lakini bahati mbaya mitoto yenyewe imekuwa mijinga na sasa badala ya kuangalia ujinga wao inaanza kumlaumu mzee wa watu ambaye alifanya kila kitu kuwajengea misingi mizuri ya maisha.

Nyerere alikuwa anapambana na watu kwa hoja na sio kwa mtutu wa bunduki. Sawa kuna watu wachache aliwaweka ndani, au kuna watu wachache ambao alipunguza speed yao wasiwe matajiri zaidi lakini huwezi kumwita Nyerere dikteta kwasababu ya kutetea misingi na mambo ambayo alikuwa akiyaamini?

Nyerere alitutengenezea misingi mizuri ya kusimama sisi wenyewe na kuendelea mbele kama binadamu lakini tulivyowajinga tumerudi kule kule. Tunaua elimu na kupeleka wanetu Ulaya, Kenya, Uganda na kwingineko, tumeua hospitali zetu na huduma za afya mpaka watu wanafumuliwa vichwa badala ya miguu. Tumeanza kuua mshikamano wa Kitanzania na sasa hata maofisini ukabila unaanza kujionyesha waziwazi. Sera kama za mtu ni afya zimekufa, leo mitalo ya vinyesi mpaka milangoni, kipindupindu kimekuwa donda ndugu katika karne hii ya 21.

Kibaya zaidi tumeanza kuwa watumwa kwenye nchi yetu. Tunauza nchi kwa kila anayetaka kununua kipande ili mradi ni mzungu. Tunajifanya tuna middle classs wengi ambao hawana uhuru wowote maofisini, wananyenyekea makaburu utafikiri hawajasoma, wanalipwa mishahara kidogo kuliko makaburu na hawawezi hata kulalamika. In fact wanaona furaha kuhudumia Wazungu kuliko Watanzania wenzao, huo ndio uhuru mnaotaka?

Mwacheni mzee wa watu apumzike salama huko aliko, ndio maana alivyokufa hata wale wapinzani wake wakubwa wa magharibi hawakuthubutu hata kutoa neno. Jamaa alikuwa kichwa na hicho kichwa ndio kilimjengea marafiki na maadui.

Lazima ujue Mwalimu alikuwa kiongozi wa miaka ya 60 na 70, miaka ambayo viongozi wengi walitakiwa wawe na misimamo, walikuwa na nguvu kubwa waliyopewa kikatiba na information ilikuwa haba, hivyo mambo mengine ambayo watu walikuwa wanatendewa huku chini ilikuwa sio rahisi kwa mtu wa juu kuyajua. Ni tofauti na sasa ambapo inatosha kuja JF kujua nani katembea na mke wa nani.

Sawa kuna makosa ambayo Nyerere alifanya kama binadamu yeyote anavyofanya lakini athari zake ni kidogo sana. Nyerere aliachia madarama miaka 22 iliyopita, je nini kimekuwa tofauti pamoja na hii demokrasia yetu? Watu wameuawa Zanzibar, tumepata Watanzania wakimbizi wa kwanza, nchi imeuzwa, vyuo vyetu havina watu wenye hoja tena badala yake wanavaa magwanda ya kijani utafikiri punguani. Nyerere hakuingilia uhuru wa wasomi na ndio maana hata watu waliotoka pale walikuwa wanajua kujenga hoja, nenda leo, kazi yao kubeba wanasiasa. Sio kazi ya mwanafunzi wa chuo kikuu kubeba wanasiasa utafikiri Machingas Kariakoo.

Mwafrika wa Kike huna hoja hapa kabisa, kama umekosa cha kuandika kaa kimya na mwache mwalimu wetu apumzike salama.

Nenda Tanzania leo, nenda Sheraton pale kama hujatolewa mkuku, eti changudoa, Mzungu sio changudoa lakini dada zetu ndio Changudoa. Uhuru ambao Nyerere aliamua kuacha kazi yake ya maana ya ualimu na mshahara mnono na marupurupu kibao ili atutetee Watanzania, leo tunaupoteza kijinga kijinga. Hiyo inatofauti gani na Apartheid ambako kama mweusi ilitakiwa ujue kikomo chako cha maeneo ya kwenda? Leo nenda kwenye Beaches zetu, kama Mwafrika kuna sehemu huwezi kufika.

Acheni kumkashifu Mwalimu bila hoja. Kama unataka andika hoja za maana ili tupambane kwa hoja. Huwezi kuandika mistari miwili eti unataka kujua athari za udikteta wa mwalimu. Nenda google na search jina la Mwalimu pamoja na dictator angalia utapata articles ngapi, why? Kwasababu watu walio wengi sasa wanakubaliana kwamba Mwalimu hakuwa dictator.
[/SIZE]

...Mtanzania, naunga mkono hoja zako nyingi katika hii post.
 
yes, but is Nyerere who did it not any other she/he so why not cherish him?

Rwabugiri. Katika hili la uhuru nadhani wanaopingana na wewe wana hoja za kihistoria. Hata kama nyerere asingelikuwepo uhuru ungepatikana. Inawezekana isingelikuwa mwaka 1961.
 
Mtanzania,

Asante kwa post nzuri.
Mimi hapa simpondei mwalimu ila naandika kile ambacho kimesemwa.

Kama umekuwa umesoma post zangu mimi ni mtetezi mkubwa wa mambo mema aliyofanya Nyerere. Hotuba yake kwa wafanyakazi aliwaomba watanzania kuacha mabaya aliyofanya na kufata mema ila imeonekana kuna watu hapa wanadai kuwa mwalimu ndio anazuia hata sasa hivi tusiendelee (sijui kwa namna gani labda tuwaulize).

Kuna wengine pia wanapondea JF kuwa mambo ya Nyerere hayajadiliwi (hasa mabaya - na sijayaona bado) kama vile walivyoanza kuwa Mengi na Mbowe hawajadiliwi hapa kwa hiyo nimeanzisha hii kusahihisha kuwa Nyerere anaweza kujadiliwa anytime.

Mimi nasubiri kusoma tu hayo mabaya yakiwekwa hapa. Wasipoyaweka nitayatafuta popote walipoyaandika ili niyaweke hapa kwa niaba yao.

Thanks!
 
Mtanzania, nami naungana nawe. Nakala yako imetulia.

SteveD.
 
that is what I thought in the beginning then I thought.. madikteta huwa hawafanya vitu kunufaisha watu wao kwao kila wanachofanya ni katika kunufaisha kikundi cha watu wachache na mifuko yao. Sasa, kama Nyerere alikuwa Dikteta, tutajuaje kuwa hakuiba fedha na kuziwekeza huko Uswisi n.k? Maana kama kila kisemwacho kuhusu ubaya wa Nyerere why can't we believe in this.. binafsi naona ina mantiki sana ukiunganisha Udikteta wake na wizi wa fedha za Tanzania. Otherwise, utaelezaje umasikini wetu chini ya Mwalimu? Leo hii viongozi hawaibi fedha na wanajali wananchi ndio maana tumeendelea sana.

Umaskini chini ya Mwalimu ulisababishwa na kutegemea mazao ya biashara tu kama ndio chanzo cha mapato yetu ya kigeni. Wakati wa Mwalimu pia ukusanyaji wa kodi ulikuwa ni mdogo sana ukilinganisha na sasa.

Sasa hivi tuna rasilimali zetu kama dhahabu, tanzanite, mbao, gesi n.k. pamoja na kuwa mikataba iliyosainiwa haina maslahi kwa Tanzania, imeongeza kwa kiasi pato la fedha za kigeni, lakini wananchi hawaoni tofauti yeyote katika maisha yao ya kila siku kutokana na ongezeko hili la pato la fedha za kigeni na ongezeko kubwa la makusanyo ya kodi kupitia TRA.

Inakuwaje pamoja na kuongezeka pato letu la fedha za kigeni na makusanyo makubwa ya kodi, bado wananchi hawaoni kupanda kwa ubora wa maisha ukilinganisha na wakati Mwalimu Nyerere (RIP) alipokuwa madarakani? inakuwaje wengine wanaona ubora huo wa maisha unazidi kushuka?
 
Hivyo ndivyo tulivyo! Mtake msitake. Mwalimu hahusiki kabisa na umaskini wetu. Afrika nzima kusini mwa Sahara iko maskini (ukiondoa makaburu). Ina maana umaskini wa huko kwingine umesababishwa na Mwalimu? Jamani eeh...tuweni fair ktk kutoa lawama kwani zingine hazina msingi kabisa.
 
Mtanzania yaani unasema Nyerere hakuua watu.. hujasikia ya Kassim Hanga sijui na nani mwingine? Tumeambiwa watu walikuwa wanatupwa kizuizini kama utitiri; sitashangaa kuna mtu anajua makabuli ya halaiki za watu waliouawa chini ya utawala wa Nyerere. Hivi tukiuliza ni watu wangapi ambao hawajulikani walipo tokea wakati wa Udikteta wa Nyerere? Na ni wangapi ambao Mwalimu alitoa idhini anyongwe maana dikteta mzee hakopeshi.

Yaani Dikteta anawapeleka mahakamani watu waliotaka kumpindua? Ati leo viongozi wetu ni waoga kwa sababu ya Mwalimu, uoga wao ndio wa kitoto na bila ya shaka ndio wao walikuwa wa kwanza kuimba nyimbo za "zidumu fikra za mwenyekiti".

Mwaka 2010 karibu miaka thelathini tangu Mwalimu awaaachie nchi viongozi wetu watazidi kushindwa kutimiza ahadi zao kwa sababu ya Mwalimu! Labda kuna kile ambacho mwalimu wangu wa historia alikiita "colonial legacy" ambapo mojawapo ya athari zake kubwa ni utumwa wa kifikra.

Mwanamuziki Bob Barley aliandika ule wimbo wa "Redemption Song" na mojawapo ya sehemu ya utenzi wa pili unasema hivi kuhusu huu utumwa wa fikra "Emancipate yourselves from mental slavery
None but ourselves can free our minds".. Yes sir, not Mwalimu, not Kambona, no one can free an enslaved mind but an act of pure defiance to those who hold our minds into captivity just like those "ol'pirates"

Ni jitihada hizi ndizo tunazoziongoza na matokeo yake tumeanza kuyaona. Kuzifungua fikra za kila Mtanzania kuweza kuwaza zaidi, kutamani zaidi, na kufanya kazi zaidi kufikia malengo yanayoeleweka. Wale ambao bado wamefungwa na pingu za historia na mbele zake wanaabudu wakiweweseka ndio hao ambao leo hii tunataka watambue ya kuwa; kuna mazuri ya kujifunza kutoka kwa Mwalimu, Kambona, n.k lakini kuna mambo ambayo hatuna budi kuyaachilia.

Mwalimu mwenyewe alisema hivi: "Sisi kuna mambo mazuri tuliyoyafanya, na kuna mambo mabaya tuliyoyafanya. Jukumu za awamu zinazokuja ni kuyaacha yale mabaya na kushikilia yale mazuri. Tatizo mlilonalo ni kuwa hata mazuri mnayatupa!". Ndio ndugu zetu wanaofikiri kuwa Amani, Umoja na mshikamano ni vitu ambavyo vimeshushwa tu. Kuna watu walihenyeka kuvidumisha na sisi leo tunakula kutokana na jasho lao; shukrani yetu tunamuita kiongozi wa hoja hizo "dikteta".
 
Duh! Yaani Mwanakijiji anavyomjua Nyerere utadhani sijui nini vile....maana anajua karibu kila neno alowahi kusema Nyerere. Kweli unampenda Nyerere....nadhani kisirisiri undependa mchonga awe mdingi wako....kwikwikwiiiii......hey it's friday...so don't get mad
 
Mimi binafsi sidhani kama mabaya aliyofanya Nyerere yanakaribia kiwango cha kumfanya aitwe dikteta. Nyerere hakuwa dikteta na wala matendo yake hayakuukaribia udikteta. Nilichokuwa napinga ni vitendo vya baadhi ya watu kupinga kila baya litakalosemwa kuhusu Nyerere, hawa watu wanataka mazuri tu yatukuzwe na tusahau yote mabaya. Kama mnapenda mazuri yake yatajwe na kutukuzwa, basi pia muwe tayari kuyakubali mabaya yake bila ya kuanza kutoa ngonjera zenu za kuwanyamazisha watu kuwa Mzee wa watu ameshafariki mwacheni apumzike.

Mungu Amlaze Mahala Pema Peponi.
 
Duh! Yaani Mwanakijiji anavyomjua Nyerere utadhani sijui nini vile......weli unampenda Nyerere....nadhani kisirisiri undependa mchonga awe mdingi wako....kwikwikwiiiii......hey it's friday...so don't get mad

Kwi!Kwi!Kwi!kwi!!!
Kweli JF kuna mambo, no wonder watu wanakuwa addicted
 
Vipi....kwani nimeongopa? Jamaa anampenda Nyerere kikweli kweli. Hivi umewahi kumsikia anavyoongeaga kwenye podomatic? Yaani anasound kama Nyerere...sitashangaa na yeye kukata mitaa ya huko Detroit na kifimbo chake na kibaragashia. Hehehehehe....

Ngoja niwape stori. Kuna siku moja hivi...imekuwa kitambo kidogo. Jamaa alikuwa na podcast ya Nyerere akiongea na Watanzania....mimi nikaharakisha kusikiliza nikitegemea kumsikia Nyerere mwenyewe....sasa guess what? You guessed it....it was yours truly!! Yaani alimpatia kishenzi utadhani sijui nini....sikuwa na mbavu tena
 
hahahahahahaha this is funny.
 
Mazee tupate burudani bana...Ijumaa leo au sio?
Vipi weekend hii kutakuwa na old school session? Maana nikitoka hapa warehouse nataka nipitie Heineken halafu nikachukue tako la mbuzi...
 
Nyani, man you are now killing it for real!! ha ha ha

But remember,
6onpgjt.gif
, won't his baragashia cover his eye then? !

SteveD.
 
Mazee tupate burudani bana...Ijumaa leo au sio?
Vipi weekend hii kutakuwa na old school session? Maana nikitoka hapa warehouse nataka nipitie Heineken halafu nikachukue tako la mbuzi...
Tufanye basi Leo kuanzia saa mbili ya usiku ya kwenu hapo yaani itakuwa ni Old School tupu na Slow Jamz. Kwa kuanzia tu kuna jamaa mmoja pale EastAfricanTube kashusha mambo ya Old School si kawaida. Check it out at Old School Jamz
 
Mtanzania:
I hear you loud and clear in that posting #20.

Huyu Nyerere inaelekea alikuwa ni mchawi wa ajabu sana kuwakoma waTanzania wote roho zao kiasi hiki kinachosemwa siku hizi ikiwa ni pamoja na haya yafuatayo.

Qeeque: ...."Kuongelea mabaya ya Nyerere hasa katika ukosekanaji wa demokrasia nchini mwetu, hali tunayoiona leo pale Tanzania ambapo wananchi n waoga na pia wako kama mazezeta wanakubali kufanyiwa madudu yoyote ni kutokana na legacy ya Nyerere,Watanzania hata waone ubaya gani unafanywa na viongozi wao wanakuwa ni watu wa kunyamaza tu......." Ni Nyerere aliyekuwa na system ya kutumia dola kudhibiti wale wote waliokuwa wanampinga kiitikadi ......Alitumia dola kunyamazisha wengi, na hii ilifanya wananchi wengi wawe na waoga wa kwenda kinyume na matakwa ya serikali au viongozi wa nchi." (Queeque)

Kitila Mkumbo:
"Tatizo moja tu alilotuachia ni kujenga roho ya uwoga, urahisi wa udanganyifu, unafiki na UNDIO bwana/bibi miongoni mwa watanzania kwa kutumia mzimu wa CCM" (Kitila Mkumbo)

Tutumie mifano michache ya viongozi wa wakati wa Nyerere na tuangalie walivyowafunga midomo wananchi , na jinsi wananchi hao walivyo leo, tukiwalinganisha na waTanzania:

Kenyattaa - Hakuwa dikteta na hakuwafunga watu midomo daima, kama akina JM Kariuki, na akina Tom Mboya na wengineo. Kwa sababu hizo hizo waKenya leo wako huru na wameneemeka sana kuliko walionyamazishwa na kuogopeshwa waTanzania.

Iddi Amin - Waganda walipata uhuru sana kiasi kwamba hawakuwa na sababu ya kujenga tabia ya woga inayowasumbua hadi hii leo.

Africa Kusini chini ya Kaburu yeyeote yule - hawa ndugu zetu hawakujengewa mazingira ya woga wowote yanayoendelea kuwadhuru hadi leo hii, miaka zaidi ya kumi na ushee, ukilinganisha na woga unaoendelea kuwasumbua waTanzania miaka ishirini ya legacy ya Nyerere.

Tito wa Yugoslavia, Nkrumah wa Ghana, Mao wa China, Nasser wa Egypt, Kaunda wa Zambia na wengine wengi tu waliokuwa katika ongozi za viongozi wenye misimamo imara, wote hawa hawakuacha legacy za watu wao kuwa waoga, isipokuwa Nyerere tu, kwa sababu labda za uchawi wake mkali kuwazidi wote hao!

WaTanzania walimwelewa na kumwamini Nyerere; lakini hiyo isiwe sababu ya kuendelea kumlaumu Mwalimu kwa haya makosa mengi yanayofanyika nchini mwetu.

Mwalimu was a visionary, he was a thinker, he was an architect of the independence struggle. He obviously did not do all that single handed; but he was the leader, and others followed.

Kitila: Nyerere nadhani aliwahi kusema CCM si mama wala baba. Sijui alikuwa na maana gani hapo!
 
mmh.. miye niko hapa nafanya interview.. Nyani.. yaani nitembee na fimbo kwenye wheel chair...? now that is funny!
 
Inawezekana bana...si unaiweka kwenye kwapa au kwenye lap
Si nilidhani wheelchair yako electric au...?
 
Mtanzania,

Asante kwa post nzuri.
Mimi hapa simpondei mwalimu ila naandika kile ambacho kimesemwa.

Kama umekuwa umesoma post zangu mimi ni mtetezi mkubwa wa mambo mema aliyofanya Nyerere. Hotuba yake kwa wafanyakazi aliwaomba watanzania kuacha mabaya aliyofanya na kufata mema ila imeonekana kuna watu hapa wanadai kuwa mwalimu ndio anazuia hata sasa hivi tusiendelee (sijui kwa namna gani labda tuwaulize).

Kuna wengine pia wanapondea JF kuwa mambo ya Nyerere hayajadiliwi (hasa mabaya - na sijayaona bado) kama vile walivyoanza kuwa Mengi na Mbowe hawajadiliwi hapa kwa hiyo nimeanzisha hii kusahihisha kuwa Nyerere anaweza kujadiliwa anytime.

Mimi nasubiri kusoma tu hayo mabaya yakiwekwa hapa. Wasipoyaweka nitayatafuta popote walipoyaandika ili niyaweke hapa kwa niaba yao.

Thanks!

Utakapokuwa tayari kuyatafuta hayo mabaya ya Nyerere usisahau ya ...mabaharia waliolazimika kutoa rushwa ili wapate shule, pale wapi? Nasaco au? Yote hayo ni kwa sababu walitumwa na Nyerere, na pengine hata huko walipo leo ni rushwa hizo hizo alizowafundisha huyo mzee ndizo zimewafikisha huko.

Na usisahau 'colgate' za pale Namanga, na misururu ya foleni za mikate, kumbe ni za saruji! Wakati hizo colgate zinapatikana huko kwa majirani, wenzetu pale Turkana na Mandera walikuwa wakifa kwa njaa, huku wakubwa Nairobi wakinepa tu kwenye mabenzi. Wakati Nyerere anahangaika kutafuta yanga na maharage ya funza ili wananchi wake pale Idodoma wasife njaa, mabaharia wetu hawakutaka udhia wa kunyimwa mafuta ya kuvinjari na mabenzi yao club Billicana.
Huyu Nyerere alikuwa ni mshenzi kweli kweli kunyima watu raha.
 
Kalamu, kumbe na wewe kuna mambo unayajua.

Nyani, mzee hii ya electric na snow hii si 'ntachezea sakafuni. hapa natumia ya kawaida tu maana nikijaga na ya umeme watu wanataka wadandie.. hii ya mikono inabeba kasympathy ka "aina" fulani...
 
Back
Top Bottom