Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Mzee Joka,

Tumewahi kuwa na ma-PM wafuatao,

Kawawa, Sokoine, Salim, Msuya, Warioba, Malecela, Msuya, Sumaye, na sasa Rich-MonduliLowassa, ninakuomba unitajie kati ya hawa nani aliyekuwa na uwezo wa uongozi kuliko Sokoine?

Under Sokoine, angalau kulikuwa na the political feeeling kwamba serikali ipo, je do you think that is the case leo? Katika muda mchache aliokaaa kwenye power, pamoja na mapungufu yake lakini aliweza kuelewa kwamba tatizo la bonbgo mpaka leo ni viongozi wabovu! Ninarudia kuwa tatizo la bongo kwanza ni viongozi wabovu, ukisha litatua hilo basi the rest yatajipa yenyewe, kwanza ni viongozi wabovu,

Mzee Joka, hebu niambie Sokoine angekuwa PM, halafu zije issue za IPTL na Richimond si ingekuwa kiama? Mzeee wangu siku Sokoine alipopewa u-PM, alienda Msasani kwa Mwalimu akiwa na list ya viongozi wala rushwa na madhambi yao yote na alikuwa tayari ku-take them down, Mwalimu kuangalia list akakuta washikaji wake wote wamo, akamwambia no way!

Mimi siku moja nilimuona the man pale posta enzi zile UDA haina mpango, yakaja maaa-Ikarus kumba kumba na dala dala, baadaye zikaja pick-up, yote haya katika kipindi kifupi cha uongozi wake, halafu bongo agenda huwa zinawekwa na rais, sio waziri mkuu, ndio maana mimi ninasema kwamba Rich-MondLowassa, ndiye waziri mkuu wakwanza mwenye full power bongo, lakini sio waliopita.

Mzee Joka, bongo haitakuja kupata kiongozi mwenye calliber ya Sokoine tena, ninakubali kuwa alikuwa na mapungufu yake, lakini hakuwa na tatizo la kupambana na adui wa bongo nambari moja, then and now, yaani Rushwa!
 
kwa kweli chuo kikuu cha waislamu morogoro ,ni challange kwa waislamu na wasiokua waislamu kukichangia,kupewa majengo na ardhi ni hatua kubwa sana ,kuna vyuo vingi vimeshindwa kwa sababu ya kukosa facilities hapa nadhani watu wa bukoba wananielewa ..
hata hivyo kuna malalamiko kama ,jina la chuo linawakwaza watu kuingia pale ,hata waislamu wenye uwezo hawapendi kuwapeleka watoto wao pale au hata shule za misimamo mikale[ie al haramain],nafikiri MDF wangefikiria hili kwani hata ukikiita MOROGORO UNIVERSITY,bado wamiliki watabaki kuwa waislamu,na hii itawapa fursa wanafunzi wanaomaliza pale kutonyimwa ajira kwa sababu tu ya kuonekana wanatoka kwenye chou kinachoweza kufundisha propaganda ets waajiri wengi wa nchi za magharibi au wabaguzi wanaogopa sana neno ISLAMIC.pia hii ndio inafanya pia wakiristo wengi wanapofungua vyuo vya umma huviita majina ya kawaida kabisa sio CHRISTIAN UNIVERSITY,angalia IRINGA UNIVERSITY.,MAKUMIRA,,TUMAINI,,ST AUGUSTINO,,na huwa naangalia vyuo hivi vinachukua dini zote ,juzi pale st augustino njegezi wanachuo waislamu wamechagua viongozi wao ,they are free to religion na wana sehemu saafi ya kuswalia.
pale morogoro hawajaweza kuwavutia sana wakiristo kujiunga ,,,likini nimegundua hata wao hata baadhi ya walimu wao ni so liberal mfano academic chancellor wao prof msonda[correct me],juzi alipata tatizo ,alimtoa darasani mwanafunzi aliyevaa hijab[ile inayofunika hadi mdomo,gloves mikonono na soksi miguuni] akamtoa nje ,wanafunzi wakagoma wakitaka warudishwe,bahati akaja prof iddi akawasihi ,so yule binti hadi leo anaingia darasani na hijab kali[nafikiri wengi kuacha wanaokaa nae room moja hawamjui sura]
pia wanafunzi wale wanalalamikia kukosa mabweni kwani MDF imekodisha mabweni Kwa PCB ambao wanatoaga mafunzo kwenye kambi jirani pale ili kikiongezea mapato,wanafuzi wao wanapanga uraiani,sasa tatizo mabinti na vijana wa pcb damu inachemka wanavaa mini na mabo mengine ya vijana tena wanawaharibia udhu wanafunzi wanaomhofu mola wao...
 
Naona Mkandara ametuona karibu wote tulipo hapa ni wadini. Mdini ni mtu anayetumia ubaguzi wa kidini katika uongozi au mtazamo wake. Kuhimiza makundi yote ya jamii, ikiwa ni pamoja na yale ya kidini, kuongeza juhudi katika Elimu sio udini.

Nawashukuru wale wote waliokubali kunielewesha kuhusu uongozi na curriculum ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro. Hiki ni chuo kinachotuhusu wote, kwani kikitoa matunda mazuri basi taifa zima litanufaika. Na kikitoa matunda ya chuki za kidini basi wote tutahusika vile vile.

Nakubaliana kabisa na wazo kwamba kwa sasa, kuna hisia za kuogopa neno "Islamic" katika baadhi ya jamii duniani. Ni bahati mbaya kwamba chuo hakikuitwa jina kama Chuo Kikuu cha Morogoro.

Ni tumaini langu kwamba kutakuwepo na exchange programs nyingi kati ya hicho chuo na UDSM, St.Augustine University, Mzumbe University, Tumaini University, na vyuo vingine vya ndani na nje ya nchi.

Ni muhimu Wakristu wajisikie wanakaribishwa kwenye hicho chuo. Wapewe uhuru wa kuabudu na kuwa na vyama vyao vya wanafunzi. Ujengwe ushirikiano na upendo kati ya wanafunzi wote, na viongozi wa kidini wanaohubiri chuki wasikaribishwe hata kidogo chuoni.

Augustine Moshi
 
Augustine Moshi,
kama utakumbuka toka Bsc,nimekuwa na msimamo mmoja tu. Kupinga mgawanyo wa makundi ya watu kwa rangi zao. Nimepinga kitendo cha Mkapa kuwapa Waislaam majengo - University kwa sababu za makusudi ambazo zinaficha ukweli kuwa watu wake wanapendelewa kwa kupewa viwanja na vibali zaidi kujiendeleza. Leo hii elimu imegawanyika kwa makundi ya dini na hakuna uuwiano wa kitaifa hata kidogo. Elimu inazidi kuwa fake, watu wanaitwa educated hali knowledge yao ni zero kisha tunanyoosha vidole na kusema -aaaah waislaam hao bwana!...
Waislaam nao wanasema wakristu shule zao ni biashara tupu hakuna elimu yeyote.,,blaaa blaa bla. at the end of all this?
Kiwango cha elimu nchini kimeshuka vibaya sana kwani wana takwimu hawatenganishi waislaam na wakristu. Rudia kusoma mahojiano ya Nyerere utakuta vipengele vinavyojieleza makosa kama haya.
ELIMU ni swala la TAIFA zima halina kabila, dini wala gender. Nitapinga sana kuona wti wanawake wanapewa chuo Kikuu chao hali kinachotakiwa kuwepo ni nafasi sawa kwa wanawake kushiriki ktk hivi vyuo tulivyokuwa navyo.
Nikirudi ktk msemo wako kuwa nawaona nyie nyote kuwa wadini na umeitoa tafsiri yako....
Augustine, huku majuu hata kauli inamsuta mtu ktk ubaguzi. Mzungu akisema hata kwa nia nzuri kuwa - Watu weusi wote warudi kwao Afrika!
Hii huchukuliwa kama kauli ya ubaguzi...Kisha tenga kundi la watu kwa rangi zake! hata kama inahimiza kundi moja kufanya kitu fulani kwa manufaa yao ni kauli isiyokubalika. Huyu mzungu kwa upeo mkubwa ana maana -Nchi hii sii ya watu weusi waondoke!.
Hapa labda wewe unashindwa kuelewa nini maana ya UTAIFA, watu tunapewa pasi za uraia na kuhakikishiwa haki sawa, Haki sawa haipatikani kwa kuyaweka mafungu ya watu ktk utawala kwa kabila, dini wala jinsia zao bali kitaifa tarafa, wilaya, na majimbo ndiyo hutumika. Ktk msemo huo ndio maana tumeweza kuyaona mapungufu ktk Kitabu cha ndugu yetu Mohammed Said... Na sote tumekubaliana!
Katika hoja zenu za nyuma mmetumia kauli hizo. Tazama maelezo yanayotumiwa na wachangiaji akina Mzee Es, Kichukuu, Jokakuu na Dua ni kauli ambazo zinatujenga sisi sote kuwa kundi moja, tofauti na kundi lako ambalo linazungumzia issues kwa makundi ya dini.
Nitamalizia kwa kukupa mfano mdogo sana,
Mimi hapa naishi nje, lakini hata siku moja hutanisikia nikisema:-
'Nitapenda kuona kuwa Watanzania mnapata rais kiongozi ambaye atawaendeleza mnapata maji, Umeme na huduma zote muhimu, maendeleo yenu ni maendeleo yetu na vizuri zaidi kama tutaweza kuingia nchini bila visa.'
Augustine, bila shaka mtashangaa kwa kauli hiyo ya mimi kujiweka nje hali nikidai haki za Utanzania. Mnayo kila haki ya kukosoa mchango wangu unaowahusu Watanzania wanaojisikia kuwa they are part of the family. Wewe mwenzangu unajitoa, waislaam ni jirani zako na sijui hiyo mipaka yao iko wapi!
Sometimes I wonder kuwa inawezekana hata JK anapata upinzani kutokana na rangi yake ya dini!...sababu ambayo nimeiona kwa Nyerere ktk mjadala huu.
 
Viongozi wa kidini wanaohubiri chuki kama Pope Benedict, wanahitaji dialogue kama huyu mzee aliyoifanya kule Turkey majuzi, na hata kwenda msikitini kuswali na baadaye baada ya kufahamishwa deeply kuhusu asichokifahamu katika dini ya wenziwe ali-denounce maneno yake ya chuki aliyoyatoa mapema,

Kwamba sio Waisilamu wote ni wakorofi, na kwamba sio Wakristo wote zamani kazi yao ilikuwa kwenda Africa kuwapa waafrika biblia, na kuchukua ardhi zao, Mkandara is right watu wengi kwenye hii mada ni wadini, maneno tu yanajionyesha, wadini wadini tu, ndio maana nchi haiendelei, kazi kumsifia tu muungwana JK huko miskitini, kama ilivyokuwa enzi za Mwinyi, na hata wale mapadri walioesma kuwa JK ni nabii nao ni wadini wakubwa pia, maana ni rais gani wa zamani au wa sasa ambaye aliweza kuutumia unabii wake wa mungu ku-deliver?

Tuangalie mfano wa Botswana, ni nchi poa na sisi siku zote tunakimbilia huko kutafuta ajira, je umewahi kusikia watu wa huko kwamba rais wao ni nabiii?
Tuache udini, tena haya mambo ya udnini huwa yanaletwa na watu wa bara wakuja kwa treni hapa mjini, kina Moshi, mwalimu mzima wa elimu babu kubwa, lakini wamejaaa udini tu, Moshi acha udini ndugu yangu wewe ni mtu baaabu kubwa lakini hiii dini yako ya Mkapa inakurudisha nyuma ndugu yangu!
 
Maneno mazito haya ndugu zanguni Mzee ES, Mkandara na wengine. Very soothing indeed!
 
Naona Mkandara anasema mtu akizungumzia makundi ya dini na yeye hayumo kwenye hayo makundi basi ni mdini. Sitabishana kwenye logic ya namna hiyo.

Mzee ES; naona umenitupia madongo bila sababu na bila mpango. Sitajibu. Hata hivyo, unapomshambulia Baba Mtakatifu bila ukweli, inaudhi. Nilishakujibu siku za nyuma kuhusu hotuba aliyotoa Baba Mtakatifu Regensburg. Kama ungeisoma, ungegundua wazi kwamba usemayo ni uongo. Inapatikana hapa: http://www.ewtn.com/library/PAPALDOC/b16bavaria11.htm

Augustine Moshi
 
Now with all this said, the great leader Mwalimu, kwa nini hakukuwa other greats karibu yake? Na kwa nini hakuliona hili? Maaana look China, the great leader Mao alikuwa na wafuasi ambao ni greats too, hebu angalia kina Guo-Feng, Deng, Chuo, ukirudi hapa Africa, kina Mandela wameacha hawa kina Mbeki, Zuma, ndugu yangu hawa wafuasi nao ni moto wa kuotea mbali, sasa sisi bongo ilikuwaje?

I mean look at Mwinyi, Mkapa na sasa Muuungwana JK, hili ni balaaa gani hili? Please Mzee Jasusi help me kuelewa? What is this mess? A great man aliwezaje kuzungukwa na hawa wasaniii? Hebu angalia Martin Luther King kule ma-US, akawaacha kina Jesse Jackson, Andrew Young, Al-Sharpton wote wakali, sasa sisi bongo WHY? Ninasema WHY? Akatuachia kina Ditopile?



ES

I beg to differ with you
Namjua personally huyo Andy Young na nakuhakikishia kuwa as much as Mkapa kumweka karibu lakini alikuwa na mitikasi mingi tu ya ajabu ajabu

mfano wa Mbeki na Zuma ni vichekesho na huyo Obasanjo nadhani akakuwa on the same basket hivyo i wouldnt rate them as great men

As far as Martin Luther King is concerned have you ever asked yourself on why White America loved him so much?

and lastly on Mandela...personally i wish he would just keep his mouth shut as he make's us Africans look like cartoon characters

if you need further info plse dont hesitate to ask.
 
Augustine Moshi,
Mzee Es anapozungmzia baba mtakatifu inakuudhi kwa nini?..
 
Dua,Mzee ES,
someni makala ya kanku gambile wa tanzania daima kuhusu edward sokoine[r.i.p]. sokoine alikuwa na nia nzuri, na mchapakazi hodari. he came at a wrong time. tulikuwa na matatizo ya kiuchumi na hakuwa na slightest clue ya jinsi ya kuyatatua.

NASIKITIKA kwamba Edward ni kama Edward. Mbio kali, kuhema, kutopata muda wa kutafakari yaliyopita na ya sasa. Nasikitika kwamba Edward wa leo ni kama Edward wa jana. Kutokuwa mvumilivu hata kwa aliyeanza kazi jana. Kutaka kila kitu kiwe tayari jana badala ya leo au kesho. Kutokuwa na subira.

Ndivyo alivyo Edward Lowassa. Ndivyo alivyokuwa Edward Sokoine. Ni mtindo wa fanya lolote, potelea mbali matokeo yake kesho. Hivyo ndivyo Waziri Mkuu Edward Lowassa alivyojitambulisha hadi sasa.


*Wakati fulani Edward Sokoine, akiwa Waziri Mkuu wa Tanzania, alitembelea Australia na Newzealand. Aliona farasi walionona. Alifurahi sana. Aliwatamani.


Sokoine alitamani farasi hao waletwe Tanzania ili watunzwe, wazae na kuongezeka ili baadaye wasaidie, pamoja na mambo mengine, kupunguza "tatizo la usafiri."


Amri ilitolewa. Wataalamu wakaagiza farasi. Farasi wakapelekwa Chuo Kikuu cha Kilimo, Morogoro ambacho baadaye kimekuja kuitwa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA).


Hapo ndipo kimbunga kilianza. Magonjwa yalianza kuwaandama. Farasi wakaanza kufa mmoja baada ya mwingine. Wataalamu walisema kabla na baada ya kuagiza farasi, kwamba mazingira ya Tanzania yatakuwa magumu kwa farasi hao.


Aidha, kulikuwa na ugonjwa unaoua farasi na wanyama wengine wa kufugwa ambao wataalamu waliutambua kwa jina la "African horse disease."


Ugonjwa huu huwamba sehemu zote za mafuta mwilini na kusababisha yasiyeyuke. Wataalamu walieleza kwamba ugonjwa huo, husababisha hali kama ile ya binadamu aliyeugua ugonjwa wa "njano" – jondisi.


Sokoine hakusikia. Kama alisikia hakuelewa. Kama alielewa hakuamini. Kama aliamini, basi alikaidi tu. Farasi waliendelea kufa, mmoja baada ya mwingine.


Nilipata fursa ya kuonana na mtaalamu wa mifugo katika Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro kabla ya kuitwa Sokoine, Dk. Kavishe. Wakati huo alikuwa amebaki farasi mmoja tu.


Mtaalamu huyo aliniambia kwa ufupi tu akisema: "Wasingeweza kuendelea kuishi. Kulikuwa na makosa…" Na farasi huyo wa mwisho alikufa baada ya kupagawa kwa kipindi cha siku nne au tano na hatimaye "kufunga" mradi wa Sokoine.


Ya Sokoine sasa huenda yakawa yaleyale ya Lowassa. Lowassa amekwenda nchi za Mashariki. Amekutana na wanaoitwa wataalamu. Amewalilia kwamba nchi inarudi kwenye ujima. Kiza kimetanda hata mchana.


Wataalamu ‘wasamaria' wameguswa na kilio hicho, wameonyesha moyo wa huruma. Wakamwambia wana uwezo wa kuleta mvua. Hii siyo ile ya "waleta mvua" ya miujiza wa Sumbawanga au Kigoma.


Lowassa ameambiwa kwamba hii ni mvua ya kitaalamu ya kuweza kunyesha katika bwawa la Mtera, likajaa na kutoa maji ya kutosha kusukuma mtambo wa kuzalisha umeme.


Waziri Mkuu amerudi na kicheko kipana usoni. Anaona mvua itanyesha, itajaza bwawa la Mtera lililojaa matope na maji kidogo yatakayoongezeka yatasukuma mtambo na umeme utapatikana.


Ni hivi: Mvua itanyesha kwenye bwawa lenye nafasi ndogo ya kuhifadhi maji. Maji yatasukuma mashine. Maji yataisha haraka kwa kuwa ni machache. Mvua itaendelea kutengenezwa.


Hii ina maana utaalamu huu ni kama ule wa kuangalia mgonjwa aliyeko chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Hebu vinjari katika maelezo haya yafuatayo:


"Kuna daktari. Mgonjwa ni mahututi. Anapewa dawa. Dawa haziondoi ugonjwa. Mgonjwa anaendelea kukaa ICU. Daktari analipwa kila mwezi. Mgonjwa anadaiwa gharama za dawa na huduma nyingine. Ugonjwa unaendelea. Mgonjwa haponi. Daktari analipwa" (Rudia kusoma aya hizo mbili ugundue mzunguko ulivyo).


Hiyo ndiyo mvua ya Lowassa ambayo pia ni ghali. Zaidi ya shilingi milioni mbili zitakwenda kwa mtaalamu kila siku. Kwenye malipo hayo ongeza deni la IPTL, lile dondandugu waliloleta wanasiasa wa awamu ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.


Kwenye madeni hayo ongeza pia gharama za TANESCO na wataalamu wake kutoka Afrika Kusini katika Kampuni ya Net Group Solution (wengine wanaita Net Group Problem).


Huyo ndiye Edward wa leo. Anahamaki. Ni kama Edward Sokoine wakati wa kile kilichoitwa "vita dhidi ya walanguzi!"


Ukikutwa na mche mmoja wa sabuni utajuta kwa nini ulizaliwa. Ni mhujumu. Ukikutwa na dawa mpya ya mswaki utajuta kuwa Mtanzania. Ni mhujumu. Ukikutwa na shilingi 500,000 utajuta kuwa na fedha. Ni mhujumu.


Tofauti ilikuwa ndogo kati ya mwananchi masikini na jambazi la biashara lililoficha vyakula na kusababisha upungufu mkali na njaa.


Edward wa wakati huo alisimamia hilo kwa nguvu zake zote. Ilifikia wakati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, yule rais wa kwanza wa Tanzania, akamwambia apunguze kasi.


*Mwalimu Nyerere akamweleza Sokoine; "Ukiwa unaendesha gari huwezi kwenda kwa kasi ileile eneo la tambarare, na kasi hiyohiyo mlimani na kasi hiyohiyo kwenye kona. Sharti ufike mahali useme kasi hii siyo ya hapa…" Lakini Sokoine hakusikia.


Sokoine na Lowassa walikwenda nje ya nchi. Wakaona. Wakakurupuka kumaliza kiu ya mshangao wao. Sokoine alikwama. Lowassa anaelekea hukohuko.


Ukizingatia maji yaliyomo nchini Tanzania – ya mito na maziwa. Ukizingatia uwezekano wa kuvuna na kuhifadhi maji kutokana na mvua kubwa zinyeshazo nchini.


Ukizingatia uwezekano wa kutumia maji kwa "mrudio" – kwamba yaliyopita yarejeshwe kwenye mtambo; na ukizingatia uwezekano wa kusafisha mabwawa na kuyaondolea matope, utagundua hivi:


Maji yaliyomo nchini yanatosha kuzalisha umeme kwa matumizi yanayotakiwa hivi sasa. Nadiriki kusema kwamba iwapo watawala hawayaoni, basi giza limekaa kwa muda mrefu na mboni imechakaa.


Mvua ya Lowassa italeta kashfa, siyo kwake tu bali kwa taifa zima. Na mvua ya Mtera haiwezi kukidhi mahitaji ya umeme kwa nchi nzima kwa kuwa umeme wote wa gridi hautegemei Mtera peke yake.


Hiki nacho ni kiroja katika utawala wa Jakaya Kikwete. Lakini pia ni njia ya kuweka jina la mhusika katika historia ya kudumu kwamba kulikuwa na "mvua ya fulani."


Wakati hakuna sababu ya kutaka kuonekana mtu anamzibia mwanasiasa mashuhuri fursa ya kupalilia umaarufu wake, hakuna sababu pia ya kutumia fedha za walipa kodi kwa ajili ya maigizo ya filamu za sayansi.

kankugambile@yahoo.com
 
After Sokoine death the system crumbled kwa sababu waliokuwa wanakula rushwa walianza kushamiri tena. Sokoine was the man lakini hakupewa ulinzi wa kutosha.



dont even go there

Sokoine was more of a pseudo socialist who thought of human beings as tools than anything else.In otherwords he was a Leninist who was way dangerous than Lenin himself especially when he introduced mini-GULAGS-in Tanzania which were called OPERESHENI VIJIJI



I am glad he didnt stay long.
 
Naona Mkandara ametuona karibu wote tulipo hapa ni wadini. Mdini ni mtu anayetumia ubaguzi wa kidini katika uongozi au mtazamo wake. Kuhimiza makundi yote ya jamii, ikiwa ni pamoja na yale ya kidini, kuongeza juhudi katika Elimu sio udini.

Nawashukuru wale wote waliokubali kunielewesha kuhusu uongozi na curriculum ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro. Hiki ni chuo kinachotuhusu wote, kwani kikitoa matunda mazuri basi taifa zima litanufaika. Na kikitoa matunda ya chuki za kidini basi wote tutahusika vile vile.

Nakubaliana kabisa na wazo kwamba kwa sasa, kuna hisia za kuogopa neno "Islamic" katika baadhi ya jamii duniani. Ni bahati mbaya kwamba chuo hakikuitwa jina kama Chuo Kikuu cha Morogoro.

Ni tumaini langu kwamba kutakuwepo na exchange programs nyingi kati ya hicho chuo na UDSM, St.Augustine University, Mzumbe University, Tumaini University, na vyuo vingine vya ndani na nje ya nchi.

Ni muhimu Wakristu wajisikie wanakaribishwa kwenye hicho chuo. Wapewe uhuru wa kuabudu na kuwa na vyama vyao vya wanafunzi. Ujengwe ushirikiano na upendo kati ya wanafunzi wote, na viongozi wa kidini wanaohubiri chuki wasikaribishwe hata kidogo chuoni.

Augustine Moshi



WE NEED MORE PEOPLE LIKE YOU WHO SEE THINGS N DIFFERENT PERSPECTIVE

THUMBS UP!
 
Tuangalie mfano wa Botswana, ni nchi poa na sisi siku zote tunakimbilia huko kutafuta ajira, je umewahi kusikia watu wa huko kwamba rais wao ni nabiii?



LAKINI SERIKALI HIYO HIYO YA BOTSWANA ILIWANYANGANYA MA BUSHMEN ARDHI YAO KWA AJILI YA KUWAPA WACHIMBA ALMASI WA KUBWA DUNIAN 9DE BEERS) MPAKA JUZI SUPREME COURT IKAWARUHUSU KUBAKIA KATIKA HIYO ARDHI

Mjoma huko Africa kila serikali lina zimwi lake
 
DrWHO,

nakuomba tembelea site hii ya chuo cha Tumaini. http://www.elct.org/tumaini.html
Kisha jiweke wewe pembeni kama Muislaam then nambie utajisikia vipi?... the same Augustine anavyoona kuhusu hiki chuo cha Tanesco lakini kashindwa kutazama nguoni mwake.
Mkapa kaharibu elimu nchini kwa kuiga nchi za wenzetu ambao hata katiba zao zimeundwa kutokana na imani zao za dini. Huu ndio ufugaji wa Farasi wa Sokoine...
 
DrWHO

Check your facts when Sokoine was in government before calling him names?

jokaKuu

What you gave me is a litany of Edward Lowasa – a corrupt leader by any definition. Mwalimu warned us in 1995 and nobody took him seriously hence the problems of today.

I asked you simple questions and none of them was answered, it shows that you do not want facts, you are interested in majungu I assume or …………………. I haven’t denied that Sokoine thought bringing horses in Tz was good idea – By the way do you know how much was the cost?
 
DrWHO,

nakuomba tembelea site hii ya chuo cha Tumaini. http://www.elct.org/tumaini.html
Kisha jiweke wewe pembeni kama Muislaam then nambie utajisikia vipi?... the same Augustine anavyoona kuhusu hiki chuo cha Tanesco lakini kashindwa kutazama nguoni mwake.
Mkapa kaharibu elimu nchini kwa kuiga nchi za wenzetu ambao hata katiba zao zimeundwa kutokana na imani zao za dini. Huu ndio ufugaji wa Farasi wa Sokoine...



Chonde chonde mheshimiwa

mimi siy muislam wala mkristo na sijawahi kumuambia au kujitambulisha kama mwislam humu

kwanza rekebisha hilo kwanza kabla hatuajendelea
 
DrWHO

Check your facts when Sokoine was in government before calling him names?

jokaKuu

What you gave me is a litany of Edward Lowasa – a corrupt leader by any definition. Mwalimu warned us in 1995 and nobody took him seriously hence the problems of today.

I asked you simple questions and none of them was answered, it shows that you do not want facts, you are interested in majungu I assume or …………………. I haven’t denied that Sokoine thought bringing horses in Tz was good idea – By the way do you know how much was the cost?




what fact do you need?
the man was responsible for implementing some weirdo socialist policies of Nyerere after the Azimio la Arusha

which in turn were counter productive

and the rest is History

he was a failure and history will/ have judged him as such
 
Can you tell me which mini-GULGS in Tanzania opened during his premiership?
 
operesheni vijiji where people were forced to work on government owned Ujamaa farms which they softened by calling them villages


that to me equates to some form of Gulag since the order came from a Leninist Prime minister who adored other dictators such as Mao and of course Vladmir Lenin

I know its a dirty past that most do not want to tak about but it was forced labour
 
Back
Top Bottom