Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

112007-10-13_220932.jpg


112007-10-13_221347.jpg


112007-10-13_221522.jpg


Hizi ni picha za Mama Maria za Hivyi Karibuni
 
112007-10-13_221649.jpg


112007-10-13_221700.jpg


112007-10-13_221708.jpg

Haya ndio yaliyokuwa magari ya TANU!

112007-10-13_221715.jpg


Hapa ni siku Mwalimu anapewa kuwa Mkuu wa TANU

112007-10-13_221732.jpg
 
112007-10-13_221737.jpg


112007-10-13_221744.jpg


112007-10-13_221750.jpg


Hii ndio jinsi ikulu ilivyokuwa kipindi hichoooooooooooo!

112007-10-13_221753.jpg


Hapa mwalimu alikuwa anakwenda China!
 
Familia ya Nyerere. Hizo number ni kutokana na mpangilio wa kuzaliwa..

112007-10-13_222428.jpg



112007-10-13_222430.jpg


112007-10-13_222446.jpg


112007-10-13_222449.jpg


112007-10-13_222451.jpg


112007-10-13_222453.jpg
 
Shukran Mkuu CMB kwa picha na clips zinazohusu kauli za Mwalimu,Ni vyema kumuenzi Mwalimu kwa kufuata yale yote mazuri aliyoanzisha.Mwalimu ni Kiongozi ambaye si rahisi kumsahau,Hekima na Busara zake bado ni Hazina kubwa kwa Viongozi wengi Afrika.

Kama majuma matatu yaliyopita nikiwa New York nilipata nafasi ya kuzungumza na Rafiki Mkubwa wa Mwalimu ambaye mwenyewe anamuita Mwalimu "Kaka",Mtu huyo si mwingine ni Mzee Kenneth Kaunda, Rais wa Kwanza wa Zambia,Ambaye kwa hivi sasa anaishi Boston (MA),Mzee Kaunda alisema kila siku anamkumbuka Mwalimu.

Nilijaribu kumuuliza Mzee Kaunda mambo mengi kuhusu Mwalimu,lakini kwa kauli yake aliniagiza nimuone Mama Joan Wicken,ambaye alidai kuwa anamfahamu vizuri Mwalimu kikazi labda kuliko Watoto na mkewe,nilipewa contacts za Mama Wicken lakini sikuweza kumpata.

Nilimwambia Mzee Kaunda kwamba nae anamfahamu vizuri Mwalimu,lakini akakataa na kuniambia Mwalimu hakuwa Rafiki yake bali alikuwa KAKA,na kumtaja Samora kama Mdogo wao,Alinitajia majina 17 ya Marafiki wa karibu wa Mwalimu,Naomba niyaweke hapa labda yatatusaidia kujua Mwalimu alikuwa Mtu wa namna gani;
1.- Kwame Nkrumah.
2.- Chou En-Lai.
3.- Nelson Mandela.
4.- Indira Gandhi.
5.- Patrice Lumumba.
6.- Gamal Abdel Nasser.
7.- Fidel Castro.
8.- Josip Broz Tito.
9.- Yasser Arafat.
10.-Siaka Stevens.
11.-Petreaus Pappandreaus.
12.-Mengistu Haille Mariam.
13.-Augustino Neto.
14.-Robert Mugabe.
15.-Omari Bongo.
16.-Milton Obote na
17.-Anwar Sadat.
 
baathi ya marafiki wa Mwalimu ni hawa hapa kama Mmoja wa MwanaJF alivyosema hapo juu.


112007-10-13_224726.jpg


112007-10-13_224732.jpg


112007-10-13_224733.jpg


112007-10-13_224740.jpg


112007-10-13_224751.jpg


112007-10-13_224754.jpg


112007-10-13_224757.jpg


112007-10-13_224801.jpg


112007-10-13_224804.jpg


112007-10-13_224807.jpg


112007-10-13_224810.jpg
 
Shukran Mkuu CMB kwa picha na clips zinazohusu kauli za Mwalimu,Ni vyema kumuenzi Mwalimu kwa kufuata yale yote mazuri aliyoanzisha.Mwalimu ni Kiongozi ambaye si rahisi kumsahau,Hekima na Busara zake bado ni Hazina kubwa kwa Viongozi wengi Afrika.

Kama majuma matatu yaliyopita nikiwa New York nilipata nafasi ya kuzungumza na Rafiki Mkubwa wa Mwalimu ambaye mwenyewe anamuita Mwalimu "Kaka",Mtu huyo si mwingine ni Mzee Kenneth Kaunda, Rais wa Kwanza wa Zambia,Ambaye kwa hivi sasa anaishi Boston (MA),Mzee Kaunda alisema kila siku anamkumbuka Mwalimu.

Nilijaribu kumuuliza Mzee Kaunda mambo mengi kuhusu Mwalimu,lakini kwa kauli yake aliniagiza nimuone Mama Joan Wicken,ambaye alidai kuwa anamfahamu vizuri Mwalimu kikazi labda kuliko Watoto na mkewe,nilipewa contacts za Mama Wicken lakini sikuweza kumpata.

Mwawado,

Nafikiri unajua kwamba mama Joan Wicken ni marehemu, alifariki 2004 hapa UK na Watanzania mbalimbali walihudhuria mazishi yake.

Alikuwa ni mwumini wa Nyerere namba moja.
 
Mwawado,

Nafikiri unajua kwamba mama Joan Wicken ni marehemu, alifariki 2004 hapa UK na Watanzania mbalimbali walihudhuria mazishi yake.

Alikuwa ni mwumini wa Nyerere namba moja.

Shukran Mkuu, Habari mpya hii,sikuwa nafahamu!
 
Shukran Mkuu, Habari mpya hii,sikuwa nafahamu!

Wakati watawala wetu wa sasa wanahamisha mali na kuishi kifahari, mama kama huyu na elimu yake yote alijitolea kuisaidia Tanzania. Watanzania tunamtumia tu Mwalimu, sidhani kama tunamkumbuka kwa mioyo yetu.

January 1, 2005 at 12:23 am · Filed under Issue 80, Obituaries

JOAN WICKEN (79) former Personal Assistant to the late Mwalimu Julius Nyerere, died on December 5th of pneumonia after six weeks in hospital.

The funeral ceremony at Keighley in Yorkshire was presided over by Maggie Blunt, a Funeral Officiant of the British Humanist Foundation – Ms Wicken did not want a religious ceremony. Mrs Blunt spoke of Joan's unique character and how she had faced death in a calm and philosophical manner. Her father had been a strong trade unionist. After school she joined the ATS and worked during the Second World War on anti-aircraft radar. At Oxford University she had studied politics, philosophy and economics and later, wisely for her future career, became proficient in secretarial skills. She was a dedicated socialist all her life and spent 30 years as a member of the Labour Party
Tanzanian High Commissioner in London H.E. Mr H O Gumbo Kibelloh. said: "We have learnt with profound sadness of the untimely demise of Ms Wickham, a friend of Tanzania. She went to Tanzania when she was a young energetic lady in the early fifties, sent by the Labour Party at the request of the prominent nationalist political party, TANU, struggling to lead its people to freedom….. Ms Wicken worked hard with exemplary commitment and dedication. She was dependable, reliable and a remarkably efficient worker with a strong sense of international socio-economic justice…… The demise of Ms Wicken is therefore a big loss……to Tanzania as a whole. On behalf of the President, the Government and people of the United Republic, my family and on my own behalf, I wish to convey our heartfelt condolences to the members of the bereaved family and friends. May God rest her soul in Eternal Peace. Amen."
Emeritus Professor Lionel Cliffe said that her life should be celebrated. It was essentially unsung. She had had four major commitments – to Tanzania, to Africa and the Third World, to the late President, with whom she had an incredibly creative working relationship (they had had only one serious row – about women's position in society) and to socialism. She became an actor in the making of history.
She had worked first in 1960 for the Tanganyika Education Trust whose main purpose was to create a college for adults like Ruskin College in Oxford. She spent several weeks touring many of the remotest villages in the country collecting funds (often only a few shillings or, on some occasions, just a chicken – Editor) - to build what became the Kivukoni Ideological College in Dar es Salaam.
Her final major job had been to assist the President in setting up the South Foundation. With him she visited 31 countries in less than six months and met Heads of State all over the world. Later she helped in setting up the Nyerere Foundation in Dar es Salaam.
She retired in 1994 as her health began to deteriorate. She stayed for five years in Keighley with old friends Mike and Maureen Yaffey who organised the funeral ceremony.
Speaking to TA afterwards, former Tanzanian Attorney-General (1961-65) Roland Brown, who still works on various legal matters in Tanzania, said that Joan was a ‘mirror of Julius Nyerere's mind' and, in dealing with his correspondence, had a marvellous ability to write things for him which sounded like him. She drafted innumerable letters to other Heads of State and many of his speeches on the basis of only brief conversations with him. She was never indiscreet. In her retirement, she worked on transcribing the detailed shorthand notes she had taken during her time with the President.
Several speakers referred to her unassuming and modest nature in spite of her strong character and strong beliefs. Photographs were circulated of the simple thatched roof hut, in the Salvation Army compound in Dar es Salaam, where she lived for many years.
The ceremony ended with an example of New Orleans revival jazz music – ‘Panama Rag'.
 
Ms Wicken (RIP) alifanya kazi kubwa nilimuona early 1990's wakati alipokuwa na mwalimu kwenye mikutano yake mingi na alikuwa anaonekana kuwa na kazi nyingi sana na wakati wote makini katika kuchukua details.
 
Wakati leo tunaadhimisha???/tunakumbuka miaka 8 toka kufariki kwa Mwalimu Nyerere, mambo si shwari kimasiha ktk familia ya mwalimu huko kijiji, pata habari zaidi...


Ukoo wa Mwalimu Nyerere sasa taabani



*Yatima, vitegemezi wake wakosa msaada
*Dada yake afariki kwa kukosa nauli ya Dar
*Kikwete,Museveni wafichwa ukweli wa mambo


Waandishi wetu Dar na Butiama

AKIZUNGUMZA kwa hisia huku wakati fulani akionekana dhahiri kulazimika kusita na kuvuta pumzi nzito, mpwa wa Mwalimu, Bw. Anhthony Nyerere, amelithibitishia Majira Jumapili na Watanzania kwa ujumla kuwa pamoja na wanasiasa wengi kujisifu hadharani kuwa wanamuenzi Mwalimu Nyerere, halisi halisi ya ukoo wake ni taabani na inasikitisha.

Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti hili nyumbani kwake, Dar es Salaam juzi, Bw. Anthony ambaye pia kwa mujibu wa mila za Kizanaki ndiye mrithi wa mali za mjomba wake (Mwalimu Nyerere), anasema miaka nane sasa ndugu wa Mwalimu walioko Butiama, yatima aliokuwa amewachukua na kuwalea, jamaa wengine na watu wengi waliokuwa wakimtegemea Mwalimu wana hali mbaya kuliko ambavyo jamii inaweza kuamini.

"Nimeamua kuvunja ukimya na kuyaeleza haya kwa Watanzania si kwa nia mbaya bali kuielewesha jamii kuwa tofauti na hisia zao, tangu Mwalimu alipofariki ukiondoa wanafamilia chini ya Mama Maria, wana ukoo wengine ambao walikuwa wakilelewa na Mwalimu na ambao hakuwaachia mali zozote, wako taabani, hali zao kimaisha zinatisha," alisema Anthony ambaye ni mtoto wa Nyakigi Nyerere, mdogo wa Mwalimu.

Akifafanua hali ilivyo sasa Bw. Anthony alisema kwa ujumla ukoo wa Mwalimu hata mwenyewe alipokuwa hai haukuwa na maisha ya kifahari kwa sababu Mwalimu alikuwa si tajiri, lakini alikuwa akijitahidi kuwasaidia shida ndogondogo huku akilea yatima kadhaa.

"Mwalimu aliweza kutoa vjifedha kila alipopata kuhakikisha kuwa anawatunza watoto wengi yatima aliowachukua sehemu mbalimbali, kuwasaidia ndugu zake wengine ambao wana umasikini mkubwa kwa kusaidia gharama kama vile za maji, umeme na chakula.

"Kwa mfano Mwalimu alikuwa akilipa ankara za maji na umeme kwenye nyumba ya Mama Nyakigi lakini tangu alipofariki,huduma hizo zimesitishwa katika nyumba hiyo na hakuna aliyeweza kujitolea kusaidia," alisema.

Akasisitiza: "Huyu Nyakigi ambaye ndiye mama yangu yeye ni wa tano wakati Mwalimu ni wa nne kuzaliwa. Ni mmoja wa ndugu waliokuwa wakipendana sana na Mwalimu kiasi kwamba Mwalimu alikuwa siku zote akimwita dada yake huyu kwa jina la shangazi.

"Lakini tazama Mama Nyakigi aliyekuwa akilipiwa gharama hizo na kupewa fedha za kujikimu na Mwalimu mwenyewe, aliishi kizani kuanzia Mwalimu alipofariki akiwa hana maji pia hadi mwaka 2002 alipofariki."


Akizungumzia kifo cha Nyakigi, Bw. Anthony kwa masikitiko alisema mama huyo alikosa japo nauli ya kusafirishwa kwenda hospitali ya Muhimbili kwa matibabu.

"Tulikosa fedha za kumsafirisha kwenda Muhimbili na akafariki mwaka 2002. Hata kwenye maziko yake, hatukupata hata senti ya mtu," alisisitiza.


Kuhusu yatima waliokuwa wakilelewa na Mwalimu, Anthony alisema kwa sasa wengi wamesambaratika, huku waliopo wakiendelea kuishi katika nyumba ya mama yake Mwalimu ambayo hata hivyo ni chakavu na haina umeme.

"Sina pesa kwa sasa, mimi kama mkuu wa ukoo inanilazimu kuikarabati lakini siwezi, hata nyumba ya mama Nyakigi imebaki ina nyufa na jiko lake la nyuma limebomoka. Aliishi maisha ya shida sana,"alisema.

Bw. Anthony alisema kuna watoto wa mjomba wa Mwalimu aitwae Salim Nyakomge, mtu ambaye ndiye Mwalimu alitumia ngo'mbe wake kupata fedha za kwenda Chuo Kikuu Makerere, hao nao maisha yao ni taabani na sasa wanaishi kwenye vibanda vya tope vilivyoezekwa kwa nyasi.

Alimtaja mtu mwingine ambaye anataabika kuwa ni mpishi wa Mwalimu, Mzee Mohammed Sheikh ambaye amekuwa na Mwalimu tangu alipokuwa Waziri Mkuu mwaka 1960 hadi na kuendelea na kazi hiyo hadi alipostaafu mwaka 1983.

"Huyu Mzee ana matatizo makubwa. Ameunguliwa na nyumba yake huko Tanga na yuko hapa Dar es Salaam kwa wajukuu zake nako anapata shida tu. Hana pa kuishi, hana pa kwenda, hana pa kujishikiza," aliongeza.

Kielelezo kingine cha matatizo yanayoukabili ukoo wa Mwalimu kwa sasa ni hali ya sasa ya Kiboko Nyerere, mdogo wa mwisho na mmoja wa vipenzi wake.

Kiboko kwa mujibu wa Bw. Anthony hivi sasa yuko kitandani akiwa mgonjwa, msaada pekee alionao ni kijana wake mmoja wa kiume anayemsaidia na pia kipato chake cha sh. 15,000 anachokipata kwa mwezi kutokana na wapangaji wa nyumba yake.

"Tumejitahidi kuchanga fedha wakati fulani tukampeleka Mwanza kupata matibabu, lakini hivi sasa amerudishwa nyumbani hatuna fedha. Bahati nzuri ana nyumba aliyojengewa na marehemu Sokoine, ina vyumba vinne. Kwa sasa amepangisha vyumba vitatu kila kimoja sh. 5,000 kwa mwezi hivyo anashukuru Mungu kuwa na sh. 15,000 kwa mwezi lakini hali ya afya yake ni mbaya,"alisema.

Bw. Anthony alisema kitu kinachomuuma zaidi kuliko umasikini huo ambao yeye anasema "tumeuzoea na Mwalimu alishatuandaa kuishi hivyo," ni kubaini kuwa kuna viongozi ambao hufika na kuahidi kuwasaidia wanaukoo hao lakini wanakwazwa na watu aliowataja kuwa ni warasimu.

"Mama Nyakigi aliwahi kuomba msaada kwa Rais (mstaafu) Benjamin Mkapa ambaye alikuwa tayari kusaidia lakini akaambiwa 'Mzee fedha za kuwatunza hawa mbona zipo.' lakini hazikuonekana,'," alisena na kuongeza:

"Kuna wakati alikuja Rais (Joseph) Kabila wa DRC, akakutana na Mama Nyakigi akaliliwa shida naye akaahidi kuleta fedha. Najua alileta fedha nyingi sana, lakini zilikokwenda hazikuwafikia wanaukoo wa Mwalimu."


Bw. Anthony pia alisema alikasirishwa na kitendo cha hivi karibuni, Rais Yoweri Museven wa Uganda na Jakaya Kikwete walipokuwa Butiama, ambapo watu aliowaita 'vimbelembe' hawakudirika hata kuwafahamisha viongozi hao kuwa mmoja wa vipenzi vya Mwalimu; Kiboko, alikuwa mahututi kitandani.

"Hili jambo mimi lilinikera sana na kila ninapolitafakari naona ulikuwa ni unyama mkubwa sana. Kama Museveni na Kikwete wangefahamishwa kuwa kuna kipenzi cha Mwalimu alikuwa kitandani mahututi sijui ingewapunguzia nini hao waliokuwa na viongozi hao," alionesha kukerwa.

Kutokana na shida hizo, baadhi ya vijana, waliokuwa wakiishi na Mwalimu kwa muda mrefu na kusaidiana naye kazi za shamba kule Butiama, sasa wamekimbia kutokana na hali hiyo, kama anavyothibitisha mmoja wao, Bw. Hamis James Kiberiti, alipofanya mahojiano na Mwandishi Gladness Mboma, jijini Dar es Salaam wiki hii.

"Najua watanzania wengi hawataamini, lakini naomba waamini kuwa toka alipofariki Mwalimu Nyerere ukoo wake kwa sasa uko taabani ukiishi katika mazingira magumu kimaisha," alisema Bw. Kiberiti.

Alisema ukoo wa Mwalimu Nyerere umekumbwa na hali ngumu ya maisha na hata kufarakana kutokana na kumtegemea Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake kwa kila jambo.


"Sikufichi Mwalimu alikuwa akilima na kisha mazao anayopata anayagawa kwa ndugu zake yaani kaka, dada zake na wengineo pamoja na kuwasaidia pia kwa mahitaji mengine ya muhimu.

"Lakini baada ya kifo chake, vitu hivyo vyote vilikosekana,hivyo baadhi ya vijana walikimbilia mijini na maisha yao bado yanatisha kama unavyoniona mimi, huwa naona aibu kumweleza mtu kuwa mimi niliishi karibu na Nyerere," alisema kijana huyo ambaye anafanya kazi za 'deiwaka' na pia kulinda kiwanja cha mtu eneo la Kimara, Dar es Salaam huku akiishi kwenye kibanda kilichojengwa kwa mabati chakavu.

"Kama mnataka kuamini hilo ninaomba Watanzania wenye uchungu na ukoo wa Mwalimu siku moja waende kutembelea Butiama wajionee wenyewe.

"Mkifika ombeni kuonana na ndugu zake Mwalimu Nyerere aliozaliwa nao tumbo moja mjionee maisha wanayoishi, nyumba zimechoka wao wenyewe wamechoka wako hoi taabani, mimi ni kijana nina nguvu lakini nina waonea huruma wazee wangu hao," alisema.

Alitoa mfano wa mdogo wa Mwalimu, Bw. Kiboko kuwa sasa yupo hoi kitandani, anaumwa ni wa kugeuzwa na hana msaada wowote anaoupata.

Kijana huyo anakiri kuwa aliamua kukimbilia mjini kutafuta maisha kutokana na ugumu ulioibuka kijijini.

Majira Jumapili pia lilizungumza na wakazi wa Butiama ambako mwandishi wetu, Joyce Mabiti, anathibitisha kuwa wazee waliokuwa marafiki wa Mwalimu, nao 'wanalia njaa.'

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hilo kijijini hapo wiki hii umeonesha kuwa pamoja na hali inayowakabili wanaukoo wengi wa Mwalimu kuwa tata, wazee waliokuwa marafiki wakubwa wa Mwalimu, walisema shida zimeongezeka.

Akiongea kwa niaba ya wazee wenzake, Bw Marwa Ihunyo (82) alidai kuwa enzi za uhai wa Mwalimu, walikuwa wakipata misaada mbalimbali ikiwemo pesa kwa ajili ya kujikimu jambo ambalo amedai kuwa hivi sasa halipo kabisa.

Mzee Ihunyo ambaye alisoma na Mwalimu mwaka 1933 katika Shule ya Msingi Mwisenge iliyoko mjini Musoma pamoja na misaada hiyo waliokuwa wakipata kutoka kwake alikiri pia kuwa Mwalimu alikuwa akiwaelimisha mambo mbalimbali ya kisiasa, kilimo na maendeleo kwa ujumla.

Alisema kuwa inasikitisha kuona viongozi wa Serikali wamewasahau wazee hao na badala yake wamekuwa wakiwakumbuka katika kipindi cha maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Nyerere pekee.

Aliwashauri viongozi wa Serikali kuwa na tabia ya kuwatembelea wazee hao mara kwa mara ili kujua matatizo yao na kuweza kuwasaidia.

"Unajua Mwalimu alipenda sana mshikamano kati ya viongozi na wananchi hivyo nawashauri viongozi wa serikali kuendeleza tabia hiyo ili kuweza kuondoa matatizo yanayowakabili wananchi hasa sisi wazee," alisisitiza.

Akihitimisha kuhusu hali iliyoukumba ukoo wa Mwalimu miaka nane baada ya kifo chake, Bw. Anthony amewataka Watanzania kujua kuwa wanaukoo hao hawalilii kuwa na maisha ya gharama, wanajua Mwalimu aliwafundisha uvumilivu lakini wameamua kuweka bayana ili jamii na hasa wahisani wanaotoa fedha zao nyingi pia wajue haziwafikii walengwa

Can we do something on this?
 
...Mpwa wake anena:Ubovu wa viongozi umemuua.....

*Atoboa siri kuwa aliomba afe mapema zaidi
*Pia Mwalimu ameacha deni la 50,000/- za spea

Na Hassan Abbas

MWALIMU Julius Kambarage Nyerere, ambaye miaka nane iliyopita, siku kama ya leo, alililiwa sana kiasi cha watu wengi kuzimia na hata sasa majonzi yakiwa hayajawatoka, imebainika kuwa kifo chake kimechangiwa kwa kiasi kikubwa na viongozi wabovu wa kisiasa ambao walimfanya akate shauri la kutoendelea kuishi, Majira Jumapili limeelezwa.

Siri hiyo na matukio mengine ya ndani zaidi katika siku na nyakati za maisha ya Mwalimu, zimewekwa bayana na mpwa wake, Bw. Anthony Nyerere alipofanya mahojiano na gazeti hili juzi nyumbani kwake Sinza, Dar es Salaam.

Akieleza suala la kifo cha Mwalimu, Bw. Anthony ambaye alibahatika kuishi kwa Mwalimu tangu akiwa na umri wa miaka sita, alisema kila anapokaa kuzikumbuka siku za mwisho za mjomba wake, kauli zake na mwenendo wa mambo katika kuelekea mauti yaliyomfika siku kama ya leo, alisema, "Kama Watanzania wangelijua hili, naamini wasingehuzunika sana kwa kifo cha Mwalimu.

"Leo nimeona niseme ukweli nilioujua kwa miaka mingi sasa kuhusu siri za kifo cha Mwalimu.Kwa kweli Mwalimu aliomba mwenyewe ni heri afe mapema," alisema.

"Nakuthibitishia kuwa katika nyakati zaidi ya tatu tofauti Mwalimu alinisisitizia siri hii kuwa amekuwa akiomba afe mapema. Kwa kuwa nilimjua Mwalimu alikuwa mtu wa maono, ilinitisha sana alipokuwa akisema hivyo," alisema.

Akifafanua suala hilo, Bw. Anthony alisema cha kwanza kilichomfanya Mwalimu aombe kufa mapema ni suala la maisha magumu ya Watanzania na maono yake kuhusu ubabaishaji wa viongozi wengi waliomzunguka.

"Mwalimu alianza kutoa kauli hii hata kabla hajaanza kuumwa na kuirudia tena na tena alipokuwa ameanza kuumwa. Nakumbuka aliniita na kuniambia: 'Anthony, kama Mungu angenipa nafasi ya kuchagua niishe au nife, ningechagua kifo.

"Neno hili mwanzo nililishangaa, lakini akalisisitiza zaidi ya mara tatu katika nyakati tofauti. Alisema alikuwa akiomba afe mapema kwa sababu alichoka kuona watu wake wanavyopata shida huku viongozi waliopaswa kuwasaidia wakiwa hawana msaada. Mwalimu aliwaona viongozi wake wengi waliomzunguka, walikuwa wabovu," alisema na kuongeza:

"Jambo jingine lililomtisha na kuomba afe mapema ni woga wa kuwa mzigo atakapokuwa mzee sana. Aliniita siku moja na kuniambia: 'Sipendi kuishi kama bibi yenu. Unajua ukiwa mzee unasaidiwa kila jambo wakati huna faida yoyote kwa wanaokusaidia.'"

Aliongeza kuwa hata alipokuwa akipelekwa London, Mwalimu alijua kuwa hatarudi akiwa mzima.

"Nakumbuka siku alipokuwa akichukuliwa Butiama kwa safari ya Dar es Salaam na kisha London kwa matibabu, kuna mdogo wangu anaitwa Nyakwaka alimuaga akimwambia Mwalimu kwa kizanaki aende salama.

"Lakini Mwalimu alijibu kwa kizanaki 'ndora magya otandora makyora.' (Nione nikienda, hutaniona nikirudi). Kweli Mwalimu alirudi akiwa kwenye jeneza!" alisema.

Mbali na hilo, Bw. Anthony alisema hadi mauti yanamfika Mwalimu alikuwa kiongozi aliyeishi maisha ya kawaida, akiwa hana fedha kiasi cha kuacha deni la sh. 50,000.

"Hadi sasa tunamtafuta huyo mtu anayemdai Mwalimu ili tulilipe deni hilo,lakini hajajitokeza. Mwenyewe kabla hajasafiri kwenda Uingereza alituambia kwamba alikuwa amenunua spea za trekta lililokuwa bovu akiwa mjini Arusha.

"Akatuthibitishia kuwa hakuwa na fedha za kutosha hivyo akaaminiwa achukue na kuacha deni. Hadi sasa tunaendelea na utafiti alikopa watu gani ili tufanye utaratibu wa kulipa," aliongeza.

Akihitimisha maisha ya Mwalimu aliyemfahamu, Bw. Anthony aliliambia gazeti hili akisema: "Yule Bwana alikuwa kiongozi wa aina yake. Kama ni peponi basi atakwenda huko kwani alivumilia mengi."

ooh poor Mwalimu....
 
Back
Top Bottom