who unachekesha ,mwalimu hakupata kuwa na upendeleo wala kuwaonea waislamu,mnasahau historia,mwalimu aliwanyanganya wakatoliki,wakristo wengine na wahindi shule ili waislamu nao wasome ,leo mnakosa shukrani,serikali haikuwa na shule za kutosha,mwalimu angeweza hata kutengwa na kanisa kwa kulirudisha nyuma,kumbukeni utamaduni wa wakristo ulikuwa kuhakikisha kila kanisa linajengwa na shule ,hospitali na chekechea,,baada ya mwalimu kutaifisha shule na hospitali zao waligoma kujenga nyingine hadi mzee mwinyi alipokuja kuwaomba wasamehe.
msisahau kati ya hospitali nne za rufaa nchi hii ,tatu kutoa mohimbili ni za wakristu waliojenga,bugando [wakatoliki],kcmc[walutheri] nk hospitali hizi zingekua mbali sana kama si kutaifishwa ili tu waislamu wasikwezwe kuzitumia,nazo pia mzee mwinyi ndie alizirudisha,.
kwa hiyo hili la udini siliubali,,nyerere alitaka tofauti kati ya wananchi isiwe kubwa ,kuna msemo wake "inabidi wengine msimame kimaendeleo ili muwasubiri wengine.." kama si nyerere kuna jamii nchi hii zingebakia manamba,wakati tunapata uhuru tayari mikoa kama kilimanjaro na wakristo walikua mbali.
tena kwa hili wala tusilaumu wakoloni ,,tulaumu utamaduni wa walioleta dini zetu wengine walifundisha elimu ya dini ,kutibu na elimu wakati wengine walileta dini tu,tiba zikabaki za waganga na elimu ikabakia ya dini tu...
tuwe na shukrani,,,,