kichwamaji
JF-Expert Member
- Dec 1, 2006
- 232
- 13
Historia mliyosoma ndiyo tuliyosoma. Nyerere hakuandika kitabu chochote cha historia. Hakuwahi kusema mahali popote kwamba alipambana peke yake katika harakati za uhuru. Tena, alipoweza alikuwa akiwasifia aliokuwa nao, wale wazee - na diyo maana alijenga utamaduni wa kulihutubia taifa kupitia wazee wa Dar es Salaam. Zaidi, hakuwandika hata historia yake mwenyewe. Hivyo, wakati tunatafuta kujenga majina yetu kwa kurekebisha historia, ni bora tukaepuka makosa ya kumsingizia kwa yale ambayo hakuyafanya.
Ninachojua ni kwamba wana historia wengi wa wakati huo, tena wengi wakiwa wageni, ndio walioandika historia yao. Walitazama matakwa ya wakati huo, wakandika kinachosomeka na kukubalika wakati huo, katika enzi za kujenga utaifa na kusifia viongozi waliokuwapo. Hawakuandika historia yote.
Walichofanya ndicho kinafanyika sasa Afrika Kusini. Kiwewe cha uhuru na umaarufu wa Mandela kinawafanya wasomi na wanahistoria kuandika kumbukumbu nyingi za mapambano kuhusu Mandela, kana kwamna aliteseka peke yake, alipambana peke yake na kuleta uhuru. Hata wazungu wengine hawakupenda manyanyaso ya waafrika. Walisaidia kupata uhuru wa Afika Kusini.
Hadi sasa wanamuimba shuleni na katika miktano kadhaa Mandela..Mandela...Lakini hakuwa peke yake. nadhani mnajua. Si haki wasomi wa baadaye wakianza kumalumu yeye kwa sehemu ya historia iliyoandikwa kumsifia Mandela. Hiyo ni sehemu tu ya historia. Wanaojua sehemu nyingine waandike. Mataifa yote ndiyo yamekua. Hakuna taifa lililoandika historia kwa vitabu vichache na kwa wakati mfupi hivyo.
Hata katika dini mambo ni yale yale. Yesu hakuandika vitabu vyote unavyosoma leo kuhusu Ukristo. Wala yeye hakuagiza viandikwe. Na havikuandikwa vyote wakati mmoja. Na havikuwa na ujumbe ule ule. Ndiyo maana historia inaendelea kufunua vingine katika karne za leo.
Kuna watu walicheza n Yesu akiwa mtoto. Kuna watu walikuwa rafiki za familia yao. Kuna watu walimsikia akifundisha. Kuna watu wanakumbuka mengi waliyoona na kusikia ambayo hayakuandikwa katika Injili. Wapo na wameandika (kwa taarifa yenu). Si vema kumlaumu Matayo, Luka, Marko au Yohana au Yesu mwenyewe kwa kila kilichoandikwa kwenye vitabu hivyo, huku baadhi ya mambo muhimu kama tarehe ta kufa kwake, alipofia Maria mama yake, alipofia Yosef na hata mitume wenyewe, yakiachwa!
Walipoandika, hilo halikuwa lengo lao. Yaani haikuwa angle ya stori waliyoandika. Wakati huo huo, huwezi kusema walichoandika ni uwongo. Ni kama waandishi wanapoandika habari kila siku. Yapo mengi wanayokuwa wameyaona siku hiyo, lakini wanayaacha na kubakiza yale tu yanayouza magazeti yao, au waliyotumwa na wakubwa wao...yale wanayoona ni habari kwa kesho yake au siku hiyo. Sasa akitokea mtu akasema 'mbonahawajaandika kile au kile' anakuwa hajui maana ya angle. na Wakati mwngine hicho walichokiacha watakitumia baadaye katika stori zijazo, iwap litatokea jambo lililo relevant au wataandika makala.
Kwa sababu hiyo, tunafanya makosa kumlaumu Nyerere kwa historia iliyoandikwa kuhusu juu yake. Kama binadamu ana mengi aliyokosea - kama mimi na wewe - lakini si hili la historia yetu. Halimhusu. Na kama sisi tunajua vinginevyo, basi tuandike. Tusiishie kulalama nakujidaidai tu kana kwamba kunajipya tumegundua. Kuandika historia ni kazi ya kila mmoja anayeweza, hasa wanahistoria. Si ya wanasiasa.