ninawasilisha sehemu ya tamko la serikali ya Tanzania kuhusu kuiunga mkono Biafra, pamoja na sababu za kufanya hivyo. Tamko hilo lilitolewa 1968 na C.Y.Mgonja, aliyekuwa waziri wa mambo ya nje.
The world has taken it upon itself to utter many ill-informed criticisms of the Jews of Europe for going to their deaths without any concerted struggle. But out of sympathy for the suffering of these people, and in recognition of the world's failure to take action at the appropriate time, the United Nations established the State of Israel in territory which had belonged to the Arabs for thousands of years. It was felt that only by the establishment of a Jewish homeland, and Jewish national state, could Jews be expected to live in the world under conditions of human security. Tanzania has recognised the State of Israel and will continue to do so because of its belief that every people must have some place in the world where they are not liable to be rejected by their fellow citizens.
But the Biafrans have now suffered the same kind of rejection within their state that the Jews of Germany experienced. Fortunately they already had a homeland. They have retreated to it for their own protection, and for the same reason - after all other efforts had failed - they have declared it to be an independent state.
In the light of these circumstances, Tanzania feels obliged to recognise the setback to African Unity which has occurred.
We therefore recognise the State of Biafra as an independent sovereign entity, and as a member of the community of nations. Only by this act of recognition can we remain true to our conviction that the purpose of society and of all political organisation, is the service of man.
hotuba nzima inapatikana hapa. hoja zilizojengwa ni nzito na hakuna UDINI hapo.
http://www.biafraland.com/biafra_recognized_by_tanzania.htm
Unajua kuna kikundi cha Waislamu wa Tanzania waliamua kusoma hitma kwa heshima ya Iddi Amin Dada. Kitendo hicho kinasikitisha ukizingatia kwamba kimefanywa na Watanzania wenzetu. Kikundi hicho ndiyo kinaleta madai kwamba vita ya kumuondoa Nduli Amini ilikuwa ya kidini.
Jamani, Gadaffi alikuja kumuomba radhi Nyerere na Watanzani kwamba alipotoshwa na Iddi Amini kuhusu ugomvi wake na Tanzania. Sijui ni kwanini watu wanaendeleza hoja hii hata baada ya kukanwa na wahusika wake wakuu.
Hoja ya kudai Uhuru, pamoja na kwamba waasisi wake wengi walikuwa ni waislamu, haikuwa hoja ya KIDINI au UDINI. Ilikuwa ni hoja ya KITAIFA. Hoja ile ilitaka kurejesha heshima ya MWAFRIKA ndani ya nchi yake.
Kwamba hakuna Kanisa lililounga mkono waziwazi hoja ya kudai Uhuru, si suala gumu kueleweka. Mkoloni alikuwa Mkristo, kuna ugumu ktk hilo? Pamoja na hayo kulikuwa na mbinu za chinichini za Wamisionari/Kanisa kumuunga mkono Mwalimu na Tanu katika kudai Uhuru.
Ziko taarifa kwamba wamisionari wa Maryknoll walikuwa wakimsaidia Mwalimu kifedha wakati wa harakati zile. Ziko fununu kwamba alipokuwa UNO Mwalimu alifikia katika misheni ya Maryknoll.
Pamoja na hayo hiyo siyo hoja ya msingi. Waislamu wenyewe waliojitoa mhanga kuanzisha harakati za Uhuru walimkataa kila aliyejaribu kuziteka nyara harakati zile na kuzipa sura za Kidini--Uislamu. Waislamu walimkataa Mtemvu alipotaka kuleta Udini katika kudai Uhuru.
Kinachonishangaza mimi ni kwanini Waislamu wa miaka ya 1980/1990/2000 wadai harakati zile zilikuwa za dini yao, wakati waasisi wenyewe, wengi wao wakiwa Waislamu, walishakataa kuhusishwa na UDINI? Kwanini?