Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

mtaogopa kuzungumza hadi lini...??? zungumzeni msikike.. ila kama kuna matusi hapo ingilieni lakini kama tu hoja inawaudhi kwa sababu haifurahishi huo ni ufinyu wa mawazo!! Sitaki kusikia hoja zinazofurahisha tu, nataka nisikie na zile ambazo zinaudhi na kusikitisha!!!
 
Hapo you have a point Mzee, hii tabia ya kuogopa kuongea tutaiacha lini? I mean zile enzi zilishaisha za usalama kila mahali mpaka kuhesabu visoda vya bia sasa watu wanaogopa nini? Yaani tunakuwa kama viongozi wetu tunaojaribu kuwasahhihisha?

Acheni hiyo, watu waseme tena waachwe waseme freerly!
 
ndugu modireta ili kuweka usawa tungaliomba zile mada zingine ulizo zihamisha hapa maana hazina tofauti na hii uzirudishe watu wasemee hapa hapa .Mimi sijaona sababu ya kuziondoa na kuziweka kule ukaicha watu wanaendeleza udini na kejeli juu ya Mwalimu wetu . Ama zifute ama zirudishe hapa tuelewe moja maana naona kuna mbinu chafu dhidi ya Mwalimu na kukejeri dini zingine
 
Fine understood. Ila let's keep it for a while then nayo tutaihamishia chini kwenye UCHAFU (which means itaendelea ingawa ni thread ya zamani kidogo). Suala la udini ni fikra za mchangiaji na inakuwa ngumu kumrekebisha kila mmoja. Fine, umeeleweka kaka
 
wewe Invisible, Una maana gani kutaka hii topic indelee? na wakati huo huo kufuta zile nyingine?

Mimi ninashauri kaka huyo hapo juu kuwa iondoeni hii.

kwanza ukisoma kwa makini utagundua kuwa kuwa hii topic ndiyo ilikuwa kuwa chanza cha vurugu na labda ndiyo iliyozaa hizo topic mbili zilizofutwa!

Topic na majadiliaono ya mswahili na dr WHO et al wajirekebishe tuwe waungwana sasa wewe Invisible ninona unaanza kuwa selective! tukueleweje?

Au na wewe umeamua hiki kiwe kijiwe cha umbeya na udini na kukashifu wazee wetu kama akina JM na JKN? na pia kutuletea toipc za dini kwenye siasa?
 
Haha, dah Mkira jama!

Nilisema:- "....let's keep it for a while then nayo tutaihamishia chini kwenye UCHAFU..."

Anyway nimekuelewa na kesho naahidi kuihamisha hii thread. Itahama at 00:00 usiku huu (East African Time).
 
Invisible!

kumbe UCHAFU MAANAKE WATU WANAENDELEA KUCHANGIA HUKO?!

NI KWANI USIZIONDOE JAMANI?

KAMA UCHAFU MAANAKE NDIYO HIYO NILIYOONA HUKO BASI NI AFADHALI ZIAJE HAPA ILI SASA TUENDELEZA MASHAMBULIZI HADII WATU WAKIMBIE KWENYE HII FORUM!
 
Haha, Mkira hapo nimekubali NIMESHINDWA. YES, sehemu ya Uchafu tutafunga kuendeleza postings ila client ambaye anataka kufanya reference anaweza kuchukua mawazo kule.

Nimeona nikumbushie kitu hapa. Moja kati ya Rules ambazo tuliweka ili zituongoze inasema hivi:

1 - Flaming, Bashing, and Trolling:
Hate posts and personal attacks will not be tolerated on the boards. Treat others on these message boards as you would expect them to treat you. Posting topics specifically designed to provoke a negative response from someone (aka trolling) is also asked to be avoided.

Sasa nadhani iko clear kabisa na inakidhi kinachoongeleka hapa.
 
Nakubalian na hili la kuheshimian na kujibizana kupitia HOJA na sio personal attacks

Sikubaliani na kufunga kila threa kwa sababu kuna mtu kasema kitu ambacho ni sensitive kwa watawala na hii itakuwa kinyume na hiyo motto ya JAMBO FORUM which is "WE DATE TO TALK OPENLY" sasa kama kuna mtu anataka kukaa katika mstari ni bora atumie maneno kama 'allegedly' nk

Mfano ni kuwa its "ALLEGED"kuwa mtoto wa Lowasa ndie front wa kampuni ya Richmond ilio peleka umeme bongo

Au its ALLEGED kuwa mtoto wa APSON alipewa tenda ya kussuply vifaa vya security kule OFISI KUBWA...

Sasa hiyo tayari ishamweka mtu katika safe side ya mambo
 
Yes,

Nadhani language ya aina hiyo itafaa katika threads zozote ambazo mchangiaji anaona hajafurahishwa la mchango wa mwenzake au anachukizwa na utendaji wa kiongozi flani.

Ahsante DrWHO kwa kutupa hekima zako za namna ya kuwasilisha mawazo yetu ambayo twahisi ni hasi kwa wale wayaonayo hasi kwao.

Regards
 
Mkandara,

Nilikwishasema kuwa hili darasa nimelifunga kwani uchache wako haurekebishiki kwa kuangalia haya unayoandika ambayo nimeyanukuhu hapa. Labda itakusaidia kama utakaa na kutafakari ili ujuwe mtu aliyekufuru huwa anaisabika vipi mbele ya Mwenyezi Mungu na tofauti yake ni nini na huyo mtu unayesema hakukufuru kwa sababu haja amini kamwe. Pengine fikara hizo zinaweza kukuamsha ukichukulia kuwa tunaongelea mtu aliyekufuru kwa kipimo cha Uislam na dhamira yake kuhusu imani atakiwayo kuwanayo kila binadamu kiasili. Hapa hatuongelei neno kufuru kama neno la Kiswahili tu linaloweza kutumiwa na mtu yeyote, la hasha, hapa tunaongelea neno kufuru katika context ya Uislam ambayo kama wewe ungekuwa Muislam basi ungeielewa.

Mkandara said:
Jizaledo,
Kufuru inakuja baada ya KUAMINI.. ikiwa wewe huamini ama huna IMANI huwezi kutumia neno kufuru isipokuwa kwa dini yake. .
 
Jizaledo,
Vipi bro, mbona waitafuta na kuishupalia sana imani yangu!..wewe nani hasa wa kutafuta kunihukumu kama sii mchawi!... eboooo.

Umesema mada hii imekwisha na bado warudi na zako za kuleta. Umeyasema mwenyewe haya hapa nanukuu kipande ulichoanza nacho...ati kunikosoa na kusema Kufuru!

Niliandika - Tunapoambiwa waislaam tujitahidi tupate kufanikisha kitu haina maana kwamba JK karudi nyumbani na atawafunga kamba wengine ili sisi tupate urahisi wa safari yenu....Mimi nimeukubali Uislaam na hasa Sunni kwa sababu moja tu kubwa sana. Nayo ni - Hakuna binadamu yeyote kati yangu na Mungu! yaani hakuna mbora kwa Mungu kati yetu isipokuwa yule mwenye kufanya ibada. Huyo Sheikh I can challenge him/her. Lakini imani hii pia imekuja na madhara yake. Hii kkt maisha ya kuviziana kama mafisi ni hatari kubwa sana. Till today bob sunni hatuna mwongozo Hii ndio sababu tumepewa chombo cha Bakwata kuweza kutusimamia kama tulivyokuwa tukisimamiwa na TMWS.

Mtu yeyote mwenye upeo mkubwa wa dini ataelewa mambo yote uliyoyapinga ni uzushi wako mwenyewe...Hasa yale maneno uliyo-highlight..

1. YENU:- Ukisoma sentesi nzima utaona ya kwamba nimesema SISI kabla ya makosa madogo ya YENU na haiwezi kuwa kiswahili safi kama hapakutokea makosa ya uandishi.....ilitakiwa kuwa YETU.

2. Hakuna mtu yeyote kati yangu na Mungu:- Hapa nikasema ktk dhehebu la Sunni hakuna MUNGU MTU...wote hapa tunaelewa nini maana ya MUNGU MTU.. wewe ukaja na Muhammad kuwa ni mtu kati yetu kwa sababu ana daraja zaidi...Wala haihusiani kabisa, sielewi hii kufuru yako kwangu inatoka wapi hali sote humu tunafahamu kuwa mitume wetu wote wana daraja kuliko sisi. Mbali na hayo nikakupa hata vielelezo vya akina Ayatollah, Aga Khan na Papa Paul..bado umeg'ang'ania kufuru!

Na ikiwa swala ni Mungu mtu basi nadhani kama kuna kufuru basi wewe ndiye umekufuru. Muhammad sii Mungu mtu. ..

3. Her - hapa sijui ulikuwa na maana kuwa sunni hatuna Her kama Sheikh?.. Hata kama nimesema hivyo baso sijui kuna kufuru gani?

4. Sunni hatuna mwongozo:- Mwongozo unaozungumziwa ktk hoja hii ni ule unaotufahamisha mrithi wa UONGOZI. Wakristu wanao jinsi ya kumchagua Papa, Shia wanao, Ismailia na kadhalika... Sunni hatuna na hakuna Sunni anayeweza kunambia wapi panasema jinsi ya kuchagua kiongozi wetu. (mwongozo).

5. Tumepewa Chombo cha Bakwata:- Hapa sijui umefikiri kuwa namaanisha Mungu ndio katupa bakwata au kitu gani.. bado siioni hiyo kufuru unayozungumzia ikiwa ulifuatilia hotuba ya JK.

So, ni wewe ulokuja na hayo ya kufuru baada yangu kusema naamini kabisa kuwa kufuru yangu itakuwa tu pale napomshirikisha Mungu. Yaani nimezua/ kugeuza ama kuondoa baadhi ya aya za Quran na kupindua hadithi.
That was an open for You...

Wewe ukaja na lako kuwa sio lazima kufuru iwe kumshirikisha Mungu tu hata yule asiyekuwa na imani sita. Well, mimi sioni wapi imani hizo sita zimepotoshwa ktk maelezo yangu.

Madai yako:-
1. Quran ni mwongozo wetu:- madai haya hayahusiani kabisa na maelezo yangu kwani hakuna sura wala aya inayosema jinsi ya kuchagua kiongozi ktk dhehebu la Sunni.

2. Muhammad ni Kiongozi:- Nimesema Muhammad ni Mtume KWANZA.. Na ndivyo imani ya kiislaam inavyosema. Pili, kiongozi tunayezungumzia ni kufuatana na mwongozo wa kuchagua viongozi wa dhehebu. i.e Ayatollah, Papa na kadhalika. Bado umeshupalia neno Kufuru kama vile it's your invention.

-------------------------------------------------------------------------------
 
Mzee Invisible,

Haya mambo ya kufuta na kuhamisha thread, I mean what are the standards? Halafu where do you draw the line? Yaani sasa pole pole ninaona kuna baadhi ya wanaotaka wote tuwe na msimamo mmoja, na wewe huonekani kuelewa ila kuwafuata tuuuuu, what is goin on bro?

I mean hii forum imefikia hapa kwa watu kuweka mawazo yao tofauti, ninakumbuka the first week nimeingia hii forum ilikuwa ni baada ya siku mbili mpaka tatu ndio unakuta posting mpya, leo nimakuta watu 120, wana-view kwa wakati mmoja,

sasa inakuja wanaotaka kui-control hii fourm na maneno mengi ya ujanja kumbe tu ni kutaka matakwa yao, what is it now bro, kila kukicha ooh sogeza hii rudisha hii na wewe umo tuuuuu! No! man lazima tuwe watu wazima kukubali mawazo tofauti na yetu, na kuendelea na program, watu waweke hoja sio directions wote hapa ni watu wazima kusiwe na udikteta hapa,

Mimi mambo yangu futa sogeza lakini nitaweka na wala sitalia hata siku, moja isipokuwa sasa you are going too far, mtu anaanza kejeli zikijibiwa oooh hamisha na wewe umo tuuu, vipi bro? Kama watu hawawezi vita vya kisiasa basi wasije hapa, sisi tunataka malumbano tuu bro ili tupate msimamo wa kweli, lakini msitufundishe kuwa bendera hapa, Mzee Invisible sifurahishwi kabisaa na hii tabia ya kuchezeana, na kututaka wote tuwe na akili moja, na ninakuhakikishia kuwa sasa ni wewe ndiye unakivunja hiki kijiwe taratibu na hivi vilio vya kitoto, kama watu hawawezi mawe watoke lakini msituharibie forum, wemngine sisi hatuwezi kuishi bila malumbano ya siasa jamani, wasioweza waondoke waanzishe forum yao huko ya kubembelezana, sio hapa
 
mimi nilidhani mada hii pamoja na zile 2 ama 3 ilikuwa zifutwe kabisa mbona hii imebakia na ina muongelea mwalimu ? Modireta ama futa na hii ama lete na zile zingine watu waendelee kuchangia badala ya kuleta mkanganyiko hapa .
 
Hussein,
Binafsi, nadhani Invisible anatakiwa kuondoa michango iliyojaa matusi kwani matusi hayawakilishi mawazo tofauti ya mtu...Ni bora sisi wenyewe tuache mpango wa kumsakama mchangiaji badala ya wahusika wa mada yenyewe. Pia matusi kwa viongozi wetu hayafai ila zipo njia bora zaidi za kueleza mapungufu ya kiongozi kiasi kwamba watu wataelewa.

Mada hii sioni makosa kabisa tunapomzungumzia Nyerere, isipokuwa pale tunapotukana. Haisaidii kitu kutukana kwani matusi hayabadilishi uzito wa hoja isipokuwa huongeza karaha kwa wasomaji.
 
Mkandara,

Hata mimi toka jana nimeona acha tuu iendelee ili watu wamalize dukuduku zao.

Mwishowe watasema wananyimwa uhuru.


hii ndiyo demokrasia ila lakini wana jambo tukumbuke ni watanzania wachache wanapta hii bahati ya kuchangia mawao yao kwa ajili ya kujenga taifa letu. Na kama inavyosemekana message zinafika.

Kwa hiyo tuitumie hii nafasi kwa busara zaidi. Ili michango yetu siku za baadaye ichangie kuamusha hamasa kwa viongozi wetu kujirekebisha na kusukuma gurudumu la maisha ya wanachi. Sasa sis tulio na hii bahati tukianza matusi na malumbano/kugombana inakuwa ni kichekesho!

ALUTA CONTIUNUA.
 
Mzee MENGI amekamilisha kazi yake kwani hakuna mada hata moja yenye jina lake. ADMIN tutafika?
Tuliambiwa kuwa Kapuya kalalamika huku ukweli ni Mzee Mengi, na ushahidi mada zake zote zimefutwa, Wizi wa mabilioni ya UN, na Hongo yake aliyowapa Bakwata kupitia kwa Khalifa Hamis ili apewe tunzo huku hajafunga na kaenda kuzamia futari ya waislam.
Inaonyesha JAmbo forum wanahadiliwa wanyonge tu wenye milungula hawajadiliwi?
kwanini asikanushe shutuma? kama hazina ukweli?
 
Wazee tukubaliane kuwa hakuna anyeweza ku-control mawazo ya wengine, tunaweza ku-control matusi lakini sio mawazo, sasa ninaomba niwaulize nyinyi mnaolilia mawazo ya wengine yafutwe ambayo sio matusi tofauti yenu na Mahita asiyetaka maandamano against CCM ni nini?

Tofauti yenu na huyu tajiri anayetaka kuifunga hii forum ni nini? Tofauti yenu na viongozi wa serikali yetu tunaowapiga mawe hapa kila siku ni nini? Wote mna mawazo sawa ila ni katika vitengo tofauti, wao serikalini, utajirini na nyinyi kwenye forum, Yes! kubalini kuwa hata mkipewa madaraka yatakuwa ni yale yale tu, hamtaheshimu haki za wananchi kusema yanayowakera, si hapa mnaonyesha udikteta wenu, kama wa akina Kingunge!

Siasa ni siasa, ni mchezo mchafu hata uuseme vipi ukweli unaendelea kuwa pale pale kuwa nyie ni madikteta sasa msishangae huyu tajiri akidaihii forum ifungwe maana hata mngekuwa nyinyi mngedai hivyo hivyo, WANAFIKI wakubwa, hebu niambieni mtu kama tafiti akipewa urais ataiacha hii forum? Kuuulizwa tu kidogo kuhusu RO basi imekuwa chuki tu na hasira na wala watu humu hawajui je angewajua siu atawaua huyo? Sasa akiwa rais au tajiri ingekuwaje? Sasa tunalalamika nini?

Tuache unafiki, kama tunalilia mada kufutwa humu kwa sababu zinasema ukweli kuhusu watu wanaotuhusu, basi tusishangae matajiri wakidai mada zinazo wahusu zifutwe, tabbia ni ile ile u-ARROGANT, Yes, arrogance na ushamba ndani yake, na ulimbukeni wa mtandao, hii ni burudani tu ndugu zangu kuna watu wanapafanya hapa ni mahali pa kugombea ubunge au urais, au mahakama, NO! hii ni bulogu tu ya burudani, ukimaliza kusoma yameisha, waacheni wanachi waandike wanavyotaka as long as hawatukani, uongo na ukweli wananchi hapa sio wajinga wanajua ukweli uko wapi na uongo uko wapi!

Halafu tumegundua kuwa kuna watu wanatumwa hapa kuja kuchafua hii forum, ili watu hapa wakahamie kwenye forum zao huko vichochoroni, wewe mzee tunakujua unayetumia majina mengi kumbe ni mpuuzi mkubwa wewe unafikiri unazo akili sana kuliko watu hapa? Ninakuonya uache ujinga wako tumekushitukia kuwa una bulogu yakko huko porini haina watu, kule una majina mengi na hapa unaingia na majin mengi mpuuzi mkubwa wewe, mimi nilikuwa ninaku-chek tu nikuone utaishia wapi, ulifikiri ukirusha maneno mengi ya Malecela ndio ninatatoka nije huko chooni, nyama mkubwa weee, sitoki ng'o na hatoki mtu hapa na usipoacha ujinga wako nitakusema wazi hapa wewe ni nani na nitatoa ushahidi hapa hapa, acha ujinga wako,

Wanachi waruhusiwe kuandika hapa, matusi hapana lakini mambo yajadiliwe bila huruma hata kama ni nani anajadiliwa, hata u-China Mao siku hizi anajadiliwa jinsi alivyokuwa hapendi kuoga, lijaama hukaa hata wiki mbili hlijaoga, sasa hiyo inampunguzia nini uwezo wake kikazi, kama huamini tafuta kitabu kilichoandikwa na daktari wake,

Wacheni burudani hii iendelee jamani! Ndio mimi ni Es the man ninasema watu waweke ukweli let the chips fall where they may, lakini hatutaki akili ya uniform hapa!
 
Mzee ES.
pole sana kinachofanyika hapa ni kama PCB ambao kila siku wanakamata hakimu wa mahakama ya mwanzo kaomba rushwa ya elfu moja, au mwalimu wa primary school kaiba box la chaki akapate chochote, huwezi kusikia judge fulani kafikishwa mahakamani kwa rushwa au matajiri fulani wamefikishwa makamani kwa kukwepa ushuru au PCB wanafuatilia mkataba feki wa madini n.k,

sasa watu wanapenda mijadala ya Maumba kambaka mtoto,au Kifimbo cha Nyerere kilikuwa na dawa za kuona wachawi, suti ya Mwl ilikuwa ya kijivu n.k

Tunakuja humu kujadili agenda nzito zitazoleta changamoto kwa nchi yetu si mwl kuwa mtakatifu then what?
 
Back
Top Bottom