Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Habari wana Bodi?

Nimerudi baada ya kuwekwa kifungoni na admin bila sababu. naona mkono wa Mzee Mengi ulitumika kunihukumu.

wanaopinga hoja za Mohammed Said watupe ukweli wao?
nimewahi kuuliza huko nyuma na narudia tena kuna kanisa gani au kuna kiongozi gani wa kanisa, alifanya ibada ya kuwaondoka wakoloni?
ulizeni Dua ngapi ?zilifanywa na waislam kuwaondoa wakoloni na hata Nyerere mwenyewe alikiri kusaidiwa sana na waislam.
nawaomba kabla ya kuchangia pitieni kitabu kwanza sio kubwata tu.

Ni mimi mswahili a.k.a Mandera.
 
Wewe umetoka nje ya mada sasa; in fact ndio huu udini unaoongelewa ambao unapotosha mambo.Inawezeakna baada ya kifungo chako, umeingia humu bila simile. Tafadhali nakushauri usome posts zote kabla ya kujibu.

Swala linaloongelewa hapa ni tofauti kabisa na wewe ulivyolirukia kichwa kichwa.
 
Mwanakijiji

Hiki kitabu kinaandikwa kwa ushirikiano wa watu wengi na kutumia record zilizopo US state department, UK Foreign Office, Germany East Africa archieve na hata Nyaraka kutoka Archieve ya Serikali.

Hiki hakitakuwa kitabu cha kupiga blah blah au kuonesha mwelekeo wa mwandishi bali kitakuwa ni kitabu kinachotumia report za wakati huo na kuhoji watu waliokuwepo. Kuna mahojiano yaliyopo kwenye mfumo wa maandishi, mfano yale ya Nyerere na Kawawa wakiwa mafichoni.

Pamoja na jitihada za kumtaka Kawawa aseme walikimbilia kujificha wapi wakati wa majaribio ya kupindua Serikali mpaka leo hii hajasema na hamna anayejua walikwenda wapi. Hata mama Nyerere ambaye ndiye aliyemwomba Nyerere kwenda kujificha baada ya kukataa hajui walijificha au wapi. Kuendana na habari za kijasusi za wakati huo zilishindwa kujua ni wapi walikuwa na hata Kambona hakujua, bahati mbaya aliyekuwa mlinzi wa Nyerere wakati huo hakujua walielekea wapi baada ya Nyerere na Kawawa kutokea mlango tofauti na ule waliotarajia.

Narudia tena swala la dini halikuwepo kabisa kwenye harakati za uchaguzi, kilichokuwa mbele ni Utanganyika na uongozi.

Kuna report nitaiweka hapa baadaye kidogo inayoelezea namna Nyerere alivyochaguliwa kuwa kiongozi wa wapigania uhuru.
 
Mzee Al-jeeeeeeee!

Bravo, maneno yako mazito yaani huna haja ya kuleta kitabu hayo uliyoweka hapo juu yanatosha, bro! ni yanaeleweka,

Ndugu zangu watanzania wakati umefika tuachane na issues za dini maana haizna mwisho wenye maendeleo, wazungu walifanikiwa pale tu walipoweza kutofautisha dini na uchumi, na ndiyo iliyokuwa message ya Luther baada ya kutoka Roman Catholic, na alikuwa so seroius na message yake ya capitalism, kiasi kwamba wa-Jewish walipkataa kuachana mila za dini yao kama alivyowataka, ili wajiunge na capitalism, aliwapachika propaganda iliyokuja kutekelezwa na Hitler baadye, ndiyooooo!,

Sasa tuacheni mchezo tuanze kazi, hizi issue za udini hazitupeleki popote, muulizeni Pope mpya yaliyomkuta mpaka amebidi aende huko ma-Turuki kuswali msikitini, tuache udini,

na mzee Aljazeeera tafadhali ndugu yangu wakiendelea na hizi dini dini weka darasa hapa, tumechoka na udini, maana bado tunajaribu kutafakari jinsi Mungu alivyotupa rais ambaye ni nabii wake, halafu akauchukua umeme ghafla labda mtusaidie kuelewa hayo ya kuwa na nabiii na kukosa umeme!!
 
Mzee Es na Jasusi

Muda ndiyo tatizo kwangu, ningekuwa na muda, ningeweza kuandika mengi ambayo wengi hawataki kuyafahamu.

Kuanzia wikiend hii nitaanza kuleta maandiko yangu kuhusu ni kimetufikisha hapa tulipo kiuchumi na nini kifanyike.

baadaye
 
Mswahili,
Umerudi mkuu, karibu sana...
sasa unataka tukupe ushahidi upi?... hakuna anayepinga Kitabu cha Mohammed Said, ila tofauti inakuja tu pale anapotumia neno waislaam kama vile TAA kilikuwa chama cha waislaam.
Nimekwisha sema Viongozi wa ngazi za juu ya TAA walikuwa wazawa ama wenyeji wa Pwani ambao wengi walikuwa waislaam. Kwa maana hiyo hiyo ya madai ya Mohammed Said tunaweza kusema Nyerere aliwachukia ama kuwafanyia roho mbaya wakazi wa Pwani baada ya UHURU.
Tunasema Mohammed Said kaandika kitabu hiki akiwa ndani ya kabati lake la UDINI... kwa sababu ktk watu muhimu, kawataja waislaam tena wanaume. Malengo ya kitabu chake inajieleza kwa hiyo hakuna Ubishi hapa. Darasa lake ni mchango wa waislaam ktk harakati za Uhuru nothing more na hii haina maana hapakuwepo watu wenye imani nje ya Uislaam.
Kwa mtazamo wako wewe ama kuelewa kwako kwa kitabu hiki.. Je, tunaweza kudai pia wanawake hawakushiriki ktk harakati za Uhuru kwa sababu Mohammed Said hakuwa shirikisha?... hapana mzee, sidhani kama ndio lengo lake na kama kweli alikuwa amelenga hivyo nadiriki kumpa challenge huyo Mohammed Said kama anaweza kuja na hesabu ya wanachama wa TAA kati ya mwaka 1954 hadi 1959 tuangalie uuwiano wa kidini.. maana Uhuru umeletwa na Chama - (UMOJA wa watu wenye malengo sawa).
Unajua hata ukitazama ktk elimu, wakereketwa hawa wa kiislaam huwa wanatupa hesabu za kijinga sana. Utawaona wakisema kati ya watoto 100 ni waislaam ishirini tu walioweza kuendelea na masomo, hapa wakigawa kuwa pande lililobaki ni wakristu. Wakati wa uhuru na pengine hadi leo hii- mgawanyo ni 30 waislaam, 30 Wakristu na 30 Pagani waliobaki 10 ni dini nyinginezo. Sasa imekuwaje waislaam 20 ilinganishwe na 80 wakristu hali kuna Wapagani asilimia 30?...
Nitakwambia nani alikuwa kiongozi wa Kidini!... Kreist Sykes alikuwa kiongozi wa kidini na ndiye mwanzilishi wa TAA hizi habari za mzungu gani sijui hapo inahitaji ufafanuzi zaidi. Na inajulikana kabisa kuwa Abdoul Wahid Sykes na Mwapachu (kwa mtazamo wako - waislaam) waliivamia ofisi ya TAA na kunyakua madaraka (mapinduzi baridi) Mtoto kamuondoa baba yake (muislaam).. Na sababu kubwa ni hizi. TAA kilikuwa chama kinachojikongoja kwa siasa za kidini chini ya Kreist na wengi viongozi wake walikuwa wazee. Nguvu mpya ilitakiwa na yenye mtazamo tofauti, ndipo unawakuta akina Nyerere na vijana wengine kibao waliotoka Burma na India vitani wanaingia ktk picha. Hawa ndio walikuwa na malengo ya kuupata Uhuru wa kweli. Kama kweli kuna UDINI badi udini aliufanya Abdoul Wahid kwa baba yake kwani alipindua chama chenye ilani ya kidini. Usiniulize vipi udini hali wote ni waislaam... Tunayaona huko Iraq, it is possible.
Kichuguu,
Mshikaji yale maasi ya wanajeshi nayo mbali kabisa kuna kijihistoria kidogo hapa katikati ambacho hakizungumziwi kabisa. Kama nilivyosema inawezekana nimekosea mwaka wake lakini hii habari ilitokea kweli. Utawasikia waislaam Nyerere alikuwa mdini kwa sababu aliwafunga waislaam na majina yapo kibao tu. Hiki kisa kinatembea chini chini kama vile ile issue ya Mwinyi na Sheikh Kassim mwenyewe. Je, unafahamu kwa nini Kassim alikuwa wanted?
I mean wewe unakumbuka issue yeyote ya kidini wakati wa Mwinyi ambayo ilikuwa hatari kwa usalama wa nchi?...Sasa sana utaambiwa mihadhara hali akina Ngariba wameendelea hadi wakati wa Mkapa na wakaibuka evangelist kujibu mapigano.
Yale ya wanajeshi akina Sarakikya ilikuwa wanadai haki zao kwa sababu hadi 1964 walikuwa bado chini ya Uongozi wa kiingereza. Luteni wetu atalala chini lakini Mwingireza atapewa nyumba. Mishahara tofauti, chakula tofauti na maasi hayo ndiyo sababu ya kuundwa kwa TPDF. Hiyo habari ya Nyerere kufichwa na Kawawa ndio kwanza naisikia kwa sababu historia inasema wanajeshi wetu hawakutaka kuipindua nchi bali walikuwa wakidai haki zao. Ilikuwa kitu kama strike. hawakuchukua silaha na kufunga mitaa ama kwenda Ikulu tena kambi zilizoshiriki zilikuwa za huko bara mashambani.
 
Mkandara

Safi sana, bado naendelea kuleta vitu.

Hapo uliposema Mwapachu et al umegusa patamu kwani hiyo ndiyo nilikuwa niendelee kuileta. Pia la Army Mutiny umepatia kabisa, labda ulishindwa kunielewa, sikusema Nyerere alifichwa bali walimshauri aondoke baada ya kuona wanajeshi wanaelekea Ikulu kwani hawakujua kuna nini. Lakini walipofika pale wao wakasema hawamtaki rais bali Waziri wa Ulinzi ili wamweleze waliyokusudia. Haya hapa ni maneno aliyotoa Bhoke Munanka "Why don't you go to see your Minister (Kambona)" Pia Joseph Nyerere usiku huo alikimbilia Ikulu na walipomnyima asiingie na kumwambia "asiingie Ikulu imetekwa" aliwajibu "mnaweza kuiteka Ikulu lakini hamwezi kumteka mama yangu" baada ya hapo walimwachia kuingia ndani.

Majaribio ya Mapinduzi (MM) yaliongozwa na kikundi kidogo cha wanajeshi (mostly noncommissioned officers" ambao lengo lao lilikuwa na kuwaondoa Maofisa wa Kiingerea. Hiki kikundi kilijiita Army Night Freedom Fighter. Walikuwa na malalamiko haya 1. Ongezeko la basic salahiri kutoka shilingi 105 kwa mwezi hadi 260 (2) Maofisa wa Kiingereza kutokuelewa malalamiko yao (3)Kuuliwa na kunyimwa kufuga kuku kisa Ofisa wa Kiingereza alisema nyumba zao za kuku hazikuwa safi. Usiku huo mmojawapo wa wanajeshi hao waliamua kuteka Colito Barracks. Mwanajeshi mmoja Pius Francis aliwaambia wenzake "..today we shall give back Mr. Kambona's teachers".

Baada ya kuteka Colito Barracks waligawanyika kwenye vikundi na kuanza kuelekea Dar es Salaam (Colito ilikuwa 10km kutoka mjini Dar). Kikundi kilichoelekea Ikulu kiliongozwa na Sergeant Francis Hingo Ilongi. Baada ya kuingia Ikulu na kumkosa Rais walielekea kwa Kambona na walimleta Ikulu. Na baada ya kurudi na kambona Ikulu ndipo walipomwambia kuwa "We have locked up our officers. We don't blame you ministers, because you are civilians. You don't know a soldier's difficulties. If you willcome with us to hear the men's complaints, the officers will be released" Kambona alikubaliana kuandamana nao mpaka Colito Barracks akisindikizwa na Kamishna wa Polisi.
Walipofika ndipo Hingo akamwambia Kambona kuwa wanajeshi wanataka " we want the army Africanized immediately -and completely. Baada ya kupiga longongo Kambona aliwaambia wanamtaka nani awe commander wa Tanganyika Rifles" badala ya Brigadia Douglas (mwingereza) Kuna aliyependekeza -Alex Nyirenda. Huyu alikuwa na cheo cha ofisa baada ya kufundishwa Sandhurst. Huyu ndiye aliyeweka Bendera ya Uhuru kwenye kilele cha mlima Kilimajaro siku ya Uhuru wa Tanganyika Desemba 9, 1961. Wanajeshi wengine walimpinga kwa kusema "Nyirenda is a European" Baada ya hapo walimchagua Luteni wa Daraja la Pili Elisha Kavana, na alikubaliwa na wote.

Baada ya mazungumzo ya muda mrefu na baada ya riot ambayo ilifanyika hasa sehemu za magomeni. Kambona alikubali kuwaondoa maofisa wa Kiingereza (mkutano huu ulifanyika Education centre). Kambona baadaye aliomba msaada kutoka Kenya lakini baadaye kidogo ombi liliondolewa na Job Lusinde aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani. Baada ya hapo ndipo Kambona alilihutubia taifa ni hii hapa ni transcript
"This is your Minister of External Affairs and Defense. The government is still there... There has been some misunderstanding between the Africans and the British officers in the Tanganyika Rifles. At my intervention, the soldiers have now returned to Colito Barracks..." Katika hotuba yake yote hakumtaja Nyerere. Baada ya kumaliza ililazimu George Rockey, aliyekuwa press secretary alisisimama na kusema "Mwalimu is safe, well and in command.

Sehemu inayofuata itaelezea namna Mrisho S.H Sarakikya kuwa battalion commander...
 
Radio Butiama,

Ama kweli huu ni ukumbi ambao wengi hawapendi kuingia kwa sababu nyingi za kimsingi. Na hakuna upinzani mkubwa ktk maelezo ya Mohammed Said isipokuwa upeo wa swala zima ndio umepindishwa kutokana na pale mwandishi kasimama.
Nitaeleza maelezo yangu kutokana na jinsi nilivyoelewa mimi hiki kitabu na hasa historia nzima ya UHURU wetu.
Kwanza kabisa lazima nikubali kuwa Mohaamed said kafanya kazi nzuri sana ktk kuiweka historia sawa lakini kosa kubwa ambalo limejitokeza ni pale alipowatolea mfano watu kwa rangi zao (DINI)... badala ya kuwachukulia kama Watanganyika.
Kwa nini nasema hivi:-
Kwanza ukitazama uongozi mzima wa TAA hadi TANU ulikuwa ni wakazi wa PWANI... Obvious hapa utapata waislaam wengi. Na nafasi hizo hazichaguliwi na wanachama ama viongozi wa Tanganyika nzima. Kwa mfano baraza la mawaziri wa JK hawachaguliwi na raiaama wanachama bali rais mwenyewe.
Ndugu Mohammed Said hakueleza uongozi wa TAA ama TANU mikoani ulikuwa vipi... na nakuhakikishia kila mkoa kulikuwa na aidha wakristu wengi ama waislaam wengi kutokana na wakazi wake. Lakini kilichojitokeza zaidi ni kwamba kila mkoa ulikuwa na watu wenye kabila lkubwa la hapo kuliko makabila mengine. Yaani Kilimanjaro kulikuwa na wanachama wengi wa TAA na TANU wachagga na Tabora wengi walikuwa Wanyamwezi. Je, hapa tunaweza kusema kulikuwa na Ukabila?... Sidhani!
Swala la Kupata UHURU lilikuwa very complicated toka Ukoloni na waislaam wanajua kwamba haingewezekana kuupata Uhuru wetu bila kuwatumia Wakristu. It was the fact, na Nyerere alipolia baada ya kushutumiwa kwa UDINI alikuwa akishindwa kujieleza vizuri tatizo lililopo bila kuingiza dini. Reality ni kwamba wakristu wengi ktk madaraka UHURU ulikuwa rahisi kutokana na sheria za Muingereza ambao waliwafunga Waislaam.
Muingereza alijua kuwa waislaam wanatafuta UHURU na waislaam ni karibisho la Ukommunist - kiuchumi. Sasa hapa utamwambia nini muislaam apate kukuelewa kuwa swala kubwa la nchi ni Uhuru wetu sio tofauti zetu ktk dini hali unapolianika swala zima juani (kwa Muingereza) lazima lionekane kuwa ni mahindi (Wakristu) ambao sio Wakommunist - Uhusiano wa kiuchumi na Wazungu.
Baada ya Uhuru, watu wengi wamejenga hoja ya Waislaam kutupwa nje na Nyerere lakini ukitazama kwa makini utagundua kuwa Nyerere alikuwa MBINAFSI. Mpenda madaraka kwa sababu alikuwa na dream yake. Wote ambao walikuwa tishio ktk azma yake (vision) waliondolewa bila kujali dini zao ama makabila.
UHURU kwa waafrika ulitafsirika kama kubadilisha watawala. Viongozi wengi wa Kiafrika walitegemea kuwa tukipata UHURU wetu basi wao watarithi nafasi za utajiri na Utawala wa Muingereza. Yaani hapa tunabadilisha rangi tu lakini bado wananchi watakuwa wametawaliwa na utajiri kuhama toka kwa mzungu na kushikwa na mswahili.
Nyerere was against that!.. alitaka Tanzania isiyokuwa na Wanyonyaji, Makabaila kama wazungu na pia kuondoa Ukabila na Udini. Na kukamilisha hayo lazima kuwepo na victims. Bahati mbaya msiba mkubwa uliwakuta waislaam kwa sababu ndio walikuwa ktk ngazi za juu - UONGOZI. Ukweli utasimama kuwa all politians wakati huo walikuwa na interest zao - dream ya Utajiri na madaraka na dream hii bado inaendelea hadi kesho. nani asiyependa madaraka kwa sababu ya Utajiri na madaraka ya kuwatawala watu!... That's what we have experienced for the long time.
Nyerere akawatupa Ma -chief wote nje ya nchi kuondoa influence yao ktk makabila kisha wale waislaam wenye siasa kali wakatupwa ndani BAADA ya kutumia dini kutofautisha Utawala mpya wa Nyerere.
Ni kweli Historia yetu imepindishwa sana na waandishi wetu kwa sababu ambazo sidhani kama Nyerere alitaka ziwe hivyo, kwa sababu vitabu vyote vinavyosomwa mashuleni ama University havipitishwi na Rais.
kama navyozoza siku zote kuwa ELIMU yetu waafrika imepangwa na mzungu na tunajifunza tu kile ambacho kinakubalika na mzungu hata iwe historia yetu wenyewe.
Hata mapinduzi ambayo hayakufanikiwa ya mwaka 1964 yalipangwa na waislaam na historia haisemi hivyo! - Na kama sio marehemu Sheikh Kassim Bin Jumaa kumshtua Nyerere kuhusu hayo mapinduzi leo hii Tanzania (Tanganyika) tungekuwa tunazungumza lugha tofauti. na ndio maana kuna watu wanaomchukia Marehemu Sheikh Kassim hadi alipokufa!...
Binafsi huyu Sheikh ni HERO kwangu kwa sababu azma ya Nyerere kuondoa Ukabila na UDINI ilikamilika na leo hii tunaweza kuzunguzia vitu ambavyo hakuna kati yetu anayeweza kutueleza - WHAT would happen if - Mapinduzi hayo yangefanikiwa. Ni makosa kutumia dini ya Kassim bin Jumaa badala ya kutumia Utanganyika wake kwa sababu hakuyafanya haya kwa sababu yeye ni Muislaam bali Mtanganyika.
Yes, kuna watu muhimu sana ktk kupigania Uhuru wetu wameachwa nje ya historia yetu lakini sio swala la Waislaam tu bali Watanganyika. Wapo watu mikoani ambao walishiriki kikamilifu kwa dini na kabila zao ktk mapambano yetu na tukianza kuwataja kwa kabila na dini zao utakuta mkorogano mkubwa. Kulikuwa na wanachama wengi wa TANU toka dini zote hata wahindi na waarabu walishiriki kikamilifu ktk nafasi zao kuupigania UHURU.
Nimesoma maelezo yako na ningependa sana kueleza khabari za Sheikh Kassim bin Juma kwani nina hakika si wengi wanafahamu historia yake. Ukishasoma khabari za Sheikh Kassim na uhusiano wake na Mwalimu Nyerere na Waislam labda tunaweza sasa tukaingia katika mjadala wa maana. Ila kwa kugusia tu hayo 'mapinduzi' ambayo uliyotaja Waislam wengi waliwekwa kizuizini babu yangu Salum Abdallah akiwa mmoja kati ya hao. Yeye wakati ule alikuwa Mwenyekiti wa Tanganyika African Railway Union (TRAU). Hata hivyo kesi ilipokwenda mahakamani hakuna hata Muislam mmoja alisimamishwa kizimbani kwa kosa la uhaini. Waliachiwa kimya kimya. Nina mada nilitoa Chuo Kikuu cha Kenyatta Agosti 2006 kuhusu maisha ya Sheikh Kassim. Nimemfahamu Sheikh Kassim toka utoto wangu hadi anafariki. Ikiwa wasomaji watapenda ninaweza nikaiweka katika mtandao huu kwa faida yetu sote.
 
Nimesoma maelezo yako na ningependa sana kueleza khabari za Sheikh Kassim bin Juma kwani nina hakika si wengi wanafahamu historia yake. Ukishasoma khabari za Sheikh Kassim na uhusiano wake na Mwalimu Nyerere na Waislam labda tunaweza sasa tukaingia katika mjadala wa maana. Ila kwa kugusia tu hayo 'mapinduzi' ambayo uliyotaja Waislam wengi waliwekwa kizuizini babu yangu Salum Abdallah akiwa mmoja kati ya hao. Yeye wakati ule alikuwa Mwenyekiti wa Tanganyika African Railway Union (TRAU). Hata hivyo kesi ilipokwenda mahakamani hakuna hata Muislam mmoja alisimamishwa kizimbani kwa kosa la uhaini. Waliachiwa kimya kimya. Nina mada nilitoa Chuo Kikuu cha Kenyatta Agosti 2006 kuhusu maisha ya Sheikh Kassim. Nimemfahamu Sheikh Kassim toka utoto wangu hadi anafariki. Ikiwa wasomaji watapenda ninaweza nikaiweka katika mtandao huu kwa faida yetu sote. Mohamed Said
 
Mwalimu,

Akina sisi wa juzi juzi inabidi tukae pembeni, mnamwaga data si mchezo jamani, ninajifunza.

Thanx

FD
 
Mkandara, maelezo yako ni mazuri na pia hayapingani sana na yale ya Mohamed Saidi. Kwa nlivyoelekwa mimi ni kuwa hata yeye anasema hivyo hivyo kuwa waislamu wale walifanya juhudi zile za uhuru bila kuwabagua watu kwa dini zao. Tofauti kubwa tu ni kuwa Mohamed Said was using the word waislamu prominently. The guy had a mission in writing his book, kwanza kuonyesha kuwa waislamu walitoa mchango mkubwa mno katika kuiletea uhuru nchi hii, lakini wengi wao sasa hivi hawanufaiki nao at the same level as wakristo. Ni kweli kuwa huko mikoa mingine vijitawi vilikuwepo .. and may be, just may be vilikuwa na wakristo wengi na watu wa dini nyingine. Nasema may be kwa sababu yajulikana kuwa makanisa yaliside na mkoloni. Ndio maana hata wewe hukuwataja majina.. na wachache walioongoza hata Mohamed Saidi kawataja. Ukweli ni kuwa kikawaida waanzilishi na viongozi wa juu, walio makao makuu ya chama ndio utatarajia watajike zaidi kuliko hao wa mikoani .. unless wawe walifanya vitu very exceptional.

Mission nyingine ni kupinga haya makosa kuwa zinapozungumzwa harakati za uhuru .. ni Nyerere tuuuu anaetajwa, wengine sio significant. Na hali wapo wengi walioshughulika pengine hata kuliko yeye na kisha wamesahauliwa au kuwa ignored kwa makusudi. Kwa hiyo ameandika kuwataja hawa forgotten heroes. Nasikitika kuwa hata Al-Jazeera nae, kwa dondoo alizoziweka hapa .. kitabu chake kinaelekea kufanya kosa hilo hilo .. la kufanya historia ya Tanganyika kuwa ni Historia ya Nyerere!.. ndio akaenda kutafuta mpaka maana ya neno Kambarage .. kwa nini alipewa jina hilo etc. as if hii ni biography ya Nyerere. Kwa mtindo huo mshkaji kitabu chako hakitakuwa na tofauti kubwa na vile vya akina Yusuf Halimoja tulivyokaririshwa mashuleni. Unless utuambie unafanya juhudi kama hizi kwa wagombea uhuru wengineo kutafuta mpaka sababu za wao kupewa majina waliyopewa .. maana ya hayo majina etc, that book will be more like Nyerere's biography.

Na of course another mission ya Mohamed Said ni kuuanika wazi udini wa Nyerere, ambao wengi wenu mnaupinga humu. Inabidi tukubali tu kutokubaliana, maana sie tumeelezwa mengi na wazee wetu about their disappointments kwa mambo waliyofanyiwa wao na Nyerere na mambo waliyoshuhudia Nyerere akiwafanyia madudu waislam bila sababu ya maana zaidi ya udini, tutabaki tukijua kuwa jamaa alikuwa mdini.. hata kama sio to the extent claimed by the likes of Njozi. Especially since akina Dr. Sivalon na wakristo wengine nao pia wameashiria hivyo.

Mwanakijiji, nakubaliana nawe kuwa mtu mwenye mission aliyoiweka wazi ni vigumu kuwa na conclusion iliyo neutral. Tatizo langu ni pale tunapotumia hoja hii kuashiria kukifanya kitabu hiki .. na hata kile cha Njozi .. kuwa reduced to nothing. There are valuable information that are very difficult to find elsewhere. Ntamshangaa Al-Jazeera ikiwa katika references zake kitabu hiki hakitokuwemo .. au hatokutana na Mohamed Said kujua baadhi ya mambo ambayo nae ameyaona katika nyaraka zilizoachwa na wagombea uhuru wengine, ili nae azione hizo Nyaraka au aelezwe pa kuzipata. Kama alivyokushauri Mwanakijiji na kuoffer financial support, for your book to be good .. shirikiana na wengine wenye mitazamo tofauti na hiyo ya kumuona Nyerere alikuwa Nabii wa uhuru wa Tanganyika.

Pia kusema kuwa kitabu hiki kimeandika historia kwa mwanga wa sasa baada ya kuingia notion ya kuwa waislam wanadhulumiwa duniani kote, especially Iraq, Afghanistan etc ... na hivyo wanaleta fikra hizo katika mazingira ya Tanzania, sijaikubali. Nafahamu kuwa Mwandishi kafanya utafiti wake miaka mingi sana. Na mengi aliyoandika alishakuwa akiyaandika katika magazeti ya wakati huo. Nishaelezwa kisa kimoja kuwa ilitolewa picha ya waanzilishi wa TANU katika gazeti either la Change au Africa Now, ikawa doctored kupunguza 'vikofia'. Mohamed Saidi aliwaandikia na kuwapa picha iliyo sahihi, toleo lililofuata yakafanyika marekebisho na ikatolewa picha sahihi.

Kuhusu kura tatu, Mohamed Said amejibu swali kuwa ilikuwa kuwa vipi mpaka waislamu waliokuwa ndio wameshika uongozi wa ugombeaji uhuru halafu wakatoka ikawa medani imehama. Ameeleza kuwa kura tatu was a turning point, hata kama hakukuwa na udini wakati huo,... the fact remains kuwa huo ndio mwanzo wa wakristo wengi kuingia katika hizo nafasi. Na kama Nyerere alisisitiza kushiriki uchaguzi ule with a hidden agenda in mind, which I personally doubt, sitarajii kuwa Aljazeera ataikuta hiyo katika hizo Nyaraka anazosema ana access nazo.

Kichuguu, sasa nshakuzoea kuwa unapokuwa na jambo hukubaliani nalo basi unaweza hata kudanganya na kuweka imaginary doubts kwa makusudi. Kwa mfano humu umedai: "Huyu Bwana Said anasema mambo aliyoandika amesimuliwa na baba yake. Inawezekana baba yake alikuwa upande wa waliopinga kura tatu kwa hiyo ndiyo maana akachukia yote yaliyoendelea baada ya uchaguzi ule." Namna hivi ndivyo uzushi unavyoanza, kwa lengo la kumdiscredit author, and by the way hicho kitabu kina references chungu nzima .. si maelezo ya baba yake tu. Na bado sijasahau siku zile nlipotoa reference ya Dr. Sivalon ukadai eti ni muislamu alietumia pen name ya kikristo .. mpaka nikakuonyesha biography yake iliyo online na yenye picha yake na kukueleza kuwa ni padre tena mzungu na alikuwa akifundisha UDSM. Leo unasema huelewi yule Padre alikuwa na nia gani .. jawabu ni kuwa aliandika aliyoyaona ni ukweli na kitabu chake kilidhaminiwa na kuchapishwa na kanisa .. na kopi za mwanzo za uzinduzi ziligaiwa bungeni... kwa sababu wanazozijua wao wenyewe. Na kaweka wazi ukaribu wa kanisa na nyerere na baadhi ya mbinu mbinu zao. Sasa tafuta conspiracy theory nyingine ulete doubts hapa kumdiscredit Dr. Sivalon na kanisa lake kuwa walitumiwa na Iran. Nakumbuka ulishawahi kudai humu kuwa mmoja wa hawa authors alipewa pesa na Iran ili aandike aliyoyaandika, nilipokuchallenge ukababika bila kutoa jawabu la maana. Ukiwa msomi wa aina yako inabidi uwe mwangalifu na unayoyasema.

Mkandara, do us a favor mshkaji. Hebu tuandikie kwa uwazi zaidi hayo mapinduzi ya waislam yaliyoshindwa. Wengi wetu umetuacha midomo wazi as ndio tunasikia kwa mara ya kwanza these serious allegations. Ukiwa na maelezo ya kukinaisha labda yatasaidia kutoa alternative reasons mbali na udini . as to why Nyerere aliwafunga masheikh na wengine kuwafukuza na kutuvunjia EAMWS yetu. Tupe mwaka na majina ya wahusika kama unayo .. na sababu zao za kutaka kupindua na walifikia wapi wakashindwa.. yaani any details mzee. Kama haziwekeki hapa nipe angalau kwa PM. Unaweza ukasaidia kunipunguzia hii brainwash kuwa Nyerere alikuwa mdini.
 
Kulikoni,

Nafurahi kuwa umenizowea; watu wanapozoweana huwa wanakuwa na maongezi mazuri kwani kila mmoja anakuwa anajua kona za mwenzie. Hata mimi nilishakuzowea na nakuomba kwa leo usahihishe yafuatayo:

(1) Kwenye forum hii sijawahi kujadili kitabu cha Sivalon kwani sina uhakika kama niliwahi kukisoma chote; ndiyo maana nikasema tu kuwa sijui alikuwa na ajenda gani. Nadhani umeshaangalia mwanahistoria mwingine Aljazeera naye akituhumu kuwa kitabu hicho kimepindisha ukweli. Kwamba kiliandikwa na padiri haina maana kuwa kina ukweli, inategemea sources zake za habari hizo.

(2) Kama utasikiliza mahojiano yote kati ya Bwana Said n mtangazaji wa radio Butiama bwana Deus Gunza, utamsikia mwenywe Bwana Said akisema kuwa habari zile alisimuliwa na baba yake, na ameongea kwa uchungu sana kuhusu mkutano uchaguzi wa kura tatu. Kwa kuzingatia kuwa nina historia pana sana kuhusu uchaguzi ule kwa vile mkutano ule ulifanyikia mjini kwetu Tabora, na kuna mnara wa kukumbukia uchaguzi ule ndio nikasema huyu bwana anapindisha ukweli hapa. Na kwa vile ameitaja kura tatu kama turning point ya Nyerere kuwavua madaraka wasilamu, na ndiyo inayomkera sana katika historia yote ya Uhuru, basi inawezekana mtu aliyemsimulia alikuwa yuko upande wa wale waliokuwa wakipinga ile kura tatu. Conclusion hiyo siyo uzushi hata kidogo. Mtaalamu mwingine wa historia ya uhuru, Mkandara, amemwaga data hapa kuonyesha kuwa pamoja na kwamba mlolongo wote ni sawa, huyu mwandinshi amepotosha kwa kudai kuwa matukio yale yalikuwa na lendo la kuondoa waislamu madarakani. Kwa bahati mbaya anasita kutuambia kwa uwazi zaidi kuhusu wale wasilamu waliokuwa wamepanga kumpindfua Nyerere. Mpango huo nadhani haukutangazwa sana kwa hiyo sikuwahi kuusikia. Na Kama ni kweli kuwa kuna waislamu walipanga kupindua serikali halali halafu wakakamatwa, unajua kabisa hilo ni kosa la uhaini na adhabu yake inajulikana, kwa hiyo inawezekana Nyerere akawa aliwaadhibu siyo kwa vile walikuwa waislamu, bali kama raia waliofanya kosa la uhaini.

(3) Najua mwelekeo wako katika mlengo wa udini na nadhani tulishajadili sana siku za nyuma. Unanishangaza zaidi unakurupuka na kusema kitabu cha Aljazeera kitakuwa biased hata kabla hakijatoka. Yeye amesema anaandika na jopoo la wanahistoria wengine kutumia research iliyokusanya documents mablimbali na zile za kijasusi kuotka kona zote zilizohusika. Unapopiga vita research project inayoendeleaikihusisha sources mbalimbali na researchers wengi na wala haijatoa conclusions zake, lakini unatetea kitabu kilichoandikwa na researcher mmoja unakuwa unajikosesha credibility katika mjadala wa namna hii.

(4) Mwisho, ni lazima ujue kuwa Nyerere alikuwa ni kiongozi mwasisi wa taifa, hakuna historia ya Tanganyika itakayoruka ukweli huo. Ni kweli Nyerere alisaidiwa na watu wengine wengi sana hasa pale Dar es Salaama alikokuwa akiishi, inawezekana wengine wasitajwe kwenye historia ya uhuru wa Tanganyika kutokana na ukweli kuwa hiyo itahitaji kurasa nyingi sana kwa vile walioshiriki katika mapambano yale walikuwa ni wengi mno. Kutokutajwa kwao isichukuliwe kuwa wameenguliwa katika historia kwa sababu ya dini zao. Inawezekana kuwa na biographies za kila mmoja wa walioshiriki kama vile ambavyo bwana Said amefanya ingawa baadaye focus yake imeelekea zaidi kwenye uislamu. In fact wewe mwenyewe unakiri indirectly kuwa ni wachache tu watakaotajwa unaposema "Ukweli ni kuwa kikawaida waanzilishi na viongozi wa juu, walio makao makuu ya chama ndio utatarajia watajike zaidi kuliko hao wa mikoani .. unless wawe walifanya vitu very exceptional."
 
Mkandara,

Hata mimi nilikuwa ndani ya box kuhusu mapinduzi. Sikuwa na taarifa zozote kuhusu mipango ya mapinduzi dhidi ya Nyerere kwa misingi ya kidini zaidi ya zilizotangazwa tatu (a) 1964 : maasi ya wanajeshi kutaka africanization kama ilivyoripotiwa, (b) 1969: Kambona, Chipaka, Titi Mohammedi & Company kwa hasira dhidi ya Azimio la Arusha kama ilivyojulikana, (c) 1982: Uncle Banyikwa, MacGhee, Kadege & Company kwa hasira dhidi ya uchumi mbovu baada ya vita ya Kagera kama tulivyoambiwa.

Ukipata nafasi tafadhali sana elaborate stori hiyo kusudi utusaidie kupanua uelewa wetu. Vile vile haitakuwa vibaya ukitumegea kisa cha mgongano kati ya Sheikh Kassim na Mwinyi.

Kuhusu madai ya udini wa Nyerere wakati wa kuogombea uhuru, na hasa kwenye kura tatu sikubaliani nayo kabisa. Unajua kweli kama Nyerere angekuwa mdini vile wakati huo, nina imani kabis kuwa Muungano wa Tanzania usingekuwapo; waislamu wengi wa Zanzibar wasingemkubali mkristo na mdini Nyerere awe rais wao hasa kwa vile vyama vya TANU na ASP vilikuwa vinashirikiana wakati wote wa uhuru. Nadhani unaweza kuwa na data kuonyesha kuwa ni Nyerere aliyemobilize Shiraz Party na African party kuungana na kuunda ASP dhidi ya ukoloni mwaka 1956 mara baada ya kutoka kwenye mkutano wa PAFMECA uliokuwa umeitishwa na Kwame Nkurumah kama sikosei.
 
Naam Mwl kichuguu,

Kwanza samahani if I appeared a bit harsh when I addressed you earlier. Then katika nukta zako:

1. Katika mada ya DrWHO ya Ukweli kuhusu Nyerere, ambayo sasa hivi iko katika kabrasha, katika uchangiaji wangu nlisema udini wa nyerere umeshakuwa documented by both muslims and christians, nikatoa reference ya Mohamed Said na ya Dr. Sivalon. Ulipokuja kucomment, ukaaandika: ".. Kwanza kabisa ni vizuri kuthibitisha credibility ya kila author; hawa wote hawawezi kupasi credibility test kwa vile siyo independent: wote ni waislamu ingawa wengine wametumia pen-names za kikristo...". Kwa hiyo hapa, indirectly ulimaanisha Dr. Sivalon hata kama hukumtaja jina.. maana ndio reference niliyoitoa. [Refer post yako: http://www.jamboforums.co.tz/showpost.php?p=5339&postcount=33 ya kwangu ilikuwa namba 26] Kwa hiyo katika point hii nahisi sina cha kusahihisha. Sana sana niseme tu kuwa hata kama kaandika Padre, si lazima kiwe 100% true, ingawa kuna dondoo na clues muhimu.

2. I was under the impression that you were statements indicates kuwa Mwandishi kaandika kitabu solely based on simulizi za babaake, which is not true. Kama hukumaanisha hivyo ni poa, chukulia hili ni sahihisho ulilotaka. Hata mimi katika hili la kura tatu bado sijalichukulia kuwa Nyerere alilikusudia kuwahujumu waislam.. ila nakubali kuwa ndipo turning point ya idadi ya waislam kushuka ghafla katika kilinge. Yaani si lazima kuwa zilikuwa ni njama.

Yap, Mkandara katuonjesha nyeti halafu hataki kutumalizia. Ni kweli kama waislamu walikula njama kumpindua Nyerere ndipo akawshughulikia, it will explain some of his actions that are perceived as udini.

3. Umeconclude kuwa mlengo wangu ni udini. What I know is that nnacknowledge kuwa tuna tatizo la udini, na kulisema wazi, na kuwaombeni mtakapokuwa na opportunity ya kulirekebisha mfanye hivyo pasi na kudhulumu wengine. Kwa hiyo kama mlengo huo ni udini basi sawa mie mdini. Lakini pia wale wanaofumbia macho ukweli huu, au kuenda extra step na kuzua uongo kuwadiscredit waandishi na wengine kuwasingizia wanatumiwa na wairani, sie tunapata hisia kuwa nao pia mlengo wao ni udini.

Kitabu cha Aljazeera, nampongeza kwa uzalendo na kumpa moyo, ila kwa dondoo alizozitoa hapa so far... binafsi naziona zimeelemea mno kurudia yale yale ya kuwa na biography ya Nyerere kuwa ndio historia ya uhuru. Especially pale alipoonyesha kuwa katika documents alizoziona, iliyomfurahisha zaidi ni ile iliyotoa sababu ya Nyerere kuitwa Kambarage! Kwa hiyo research yake siipigi vita .. bali natoa maoni yangu ili iwe bora zaidi na kukubalika na wengi.

Na pia sikitetei kitabu cha Mohamed Saidi kuwa ni infallible truth. The guy has a mission, and it is likely to slip along the way na kuweka chumvi za hapa na pale. Kwa hiyo tunaweza kuchukua data na kuuacha mtazamo wake.

4. Sipingi kuwa Nyerere alikuwa kiongozi na mwasisi wa Taifa, nnachopinga ni ile 'gape' au 'vacuum' inayowekwa katika jitihada zake na za wengine waliofanya kama yeye and possibly kumzidi. Kuna baadhi ya mambo huwa kidogo tunapata tabu kupata maelezo yake zaidi ya udini... kama vile mtu kuidoctor picha ya waanzilishi wa TANU ili kupunguza vikofia.

Mengineyo, Mh. Kichuguu, tunakubaliana ... au tunakubaliana kutokubaliana.
 
Kitabu cha Aljazeera, nampongeza kwa uzalendo na kumpa moyo, ila kwa dondoo alizozitoa hapa so far... binafsi naziona zimeelemea mno kurudia yale yale ya kuwa na biography ya Nyerere kuwa ndio historia ya uhuru. Especially pale alipoonyesha kuwa katika documents alizoziona, iliyomfurahisha zaidi ni ile iliyotoa sababu ya Nyerere kuitwa Kambarage! Kwa hiyo research yake siipigi vita .. bali natoa maoni yangu ili iwe bora zaidi na kukubalika na wengi.

Ndugu nasikitika sana kwako wewe kufanya hitimisho kwa kutumia sentensi moja katika kurasa kadhaa nilizoandika hapa bila kusoma ujumbe mzima.

Mimi nilimwelezea Nyerere pale watu walipoanza kusema Nyerere alikuwa mdini. Hii ni historia iliyopindishwa sana. Nyerere na hata baba yake hawakuwa wadini infact baba yake na Nyerere awali alikataa Nyerere kwenda shule kisa shule ilikuwa ya Kidini. Na kama siyo ushauri wa akina Oswald Marwa Nyerere angekuwa mtu mwingine leo hii. Mwenyewe alikataa hii dini ndiyo maana hata padre Walsh alipotaka kumbatiza aliogopa kwani alidhani Nyerere anaweza kurudi kuendelea na imani ya kizanaki. Ni mpaka 1942 baada ya babake Nyerere kufarki ndipo alikubali kubatizwa.
Kuelezea historia ya dini ya Nyerere ni muhimu, kwani huwezi zungumzia jambo hilo kama mtafiti bila kuanzia kwenye Background.

Pili mimi siandiki Biography ya Nyerere au wanasiasa wengine bali najaribu kusahihisha vile ambavyo tumekuwa tukilazimishwa au kufundishwa mashuleni na kila tulipohoji tukaambiwa ndiyo historia.

Mfano tumekuwa tukisikia waafrika walituletea uhuru, lakini ukipitia taarifa za kijasusi za mataifa mbalimbali (Nenda National Archieve kuomba clearance Certificate kuona baadhi ya documents) utaona kuwa kuna baadhi ya waliokuwa magavana wa Kiingereza ambao walisaidia au kuharakisha kupata uhuru chini ya miaka 25 ambayo tungetakiwa kuchukua. Kuna wahindi nk.

Vile vile unaweza kukaa chini na Mzee Kawawa na atakueleza historia tofauti kabisa na ile iliyoandikwa kwenye vitabu vya historia.

Mwisho napenda kukuambia nilichoandika hapa kwenye forum ni 0.0001% ya mambo ambayo tunayafanyia kazi.

Tuna zaidi ya kurasa 10,000 na audios za zaidi ya masaa 10 ikiwa ni pamoja na telephone conversations, personal diaries etc. Nadhani itachukua siyo chini ya miaka 2 kuwa na draft ya kwanza kwani kuna document za kufanyia tafsiri kutoka kwenye lugha za kigeni, ukizingatia kitabu kitakuwa kwenye lugha ya kiswahili.

nadhani ni muhimu kujadili hoja na siyo kujadili watu.
 
Aljazeera,

Asante kwa kunitoa wasiwasi kuwa kazi yako au niseme yenu haitorudia makosa ya kuifanya historia ya Nyerere ndio ya Tanganyika.

Kama wasiwasi wangu niliupresent in a way ukaonekana ni shutuma binafsi kwako, basi kwa heshima na taadhima, niwie radhi.. sio lengo.

I can understand that after de-classification of some documents.. hudhuhirika historia tofauti na 'iliyozoeleka'.

Mengineyo ya Nyerere kutokuwa na hata chembe ya udini ntasubiri kitabu chenu kitupe mwanga zaidi. Maana so far bado naona tatizo hilo alikuwa nalo.
 
Back
Top Bottom